TANZANIANS IN UK: DON’T MOURN ORGANIZE!!

For far too long our Tanzanian UK COMMUNITY has been a laughing stock from our neighbours as we are leading separate lives in this country and hence missing out on benefits that belonging to a community brings.

Our friends Kenyans in UK recently organised the first ever investment conference in London and nearly 1500 Kenyans attended the occasion. Several institutions that stood to benefit from such an event attended including Barclays who came with a theme ‘’LETA MALI HOME’’ a scheme devised by Barclays Bank Kenya Ltd to encourage Kenyans in Diaspora to invest in their motherland.

Now coming back to our TZ community, we haven’t got anything in UK in the form of unity/organisations that can unite us. Now help is at hand….

ARISE MAMA MWANAIDI SINARE MAAJAR!

She has shown the way, for the first time ever in the history of ubalozi since I have been here, the high commission has prepared a meeting for all Tanzanians. This is a welcome move in the right direction. I am very excited I can’t wait.

This commendable initiative from Mama Balozi needs the support from all of us. As the agenda suggests, we will hear from Mama Maajar on her plans to unite us under the new to be formed TANZANIAN COMMUNITY.

My recent interview with Mama Balozi immediately when she presented her credentials to the queen, she told me that she is very concerned about the community of Tanzanians in UK and she is planning to organise her diary so that she will have a day set free from her diplomatic duties so she can meet and chat with Tanzanians in UK and help solve any problems they may have.
I know that for a lawyer like Mama Maajar who has a lot of pro bono work experience, the Tanzanian community can only stand to benefit from this commendable scheme.

It is now down to all of us to give her moral support and encourage her initiative, we now have to come out of the comfort zone and challenge our conscience.

If we truly need to develop ourselves, the time is now!

I look forward to see all of you my country folks on Saturday at Holloway Road Resource Centre.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. naomba mtuma ujumbe uandike kwa kiswahili mana nna hakika 99% ya watanzania wote mwaka huu wa 2006 wanajua kiswahili nani asilimia ndogo inayojua kingereza kwahiyo ndugu kua mzalendo tumia lugha yako vinginevyo utumwa huo!

    ReplyDelete
  2. Wisen up Anony of 2:41:56PM. I know majority of us Tanzanians can read, write and speak the english language pretty well. Why do you want to stoop so low!?

    ReplyDelete
  3. asilimia 99.9 ya wanaoishi uingereza wanaelewa nini kinazungumzwa hapa.achana na porojo za aina hiyo.

    ReplyDelete
  4. ASANTE MAMA BALOZI. wewe umetualika kwa kiswahili (na nukuu BANGO la rang - picha), lakini huyu mchemshaji mwingine anatoa matongotongo yake kwa KINIGERIA. Hivyo wewe jamaa, kipindi kijacho ujumbe kama huu wa UTAIFA tumia lugha yako ya TAIFA.

    ReplyDelete
  5. Kama ni Hujumbe unaolenga Watanzania, tumia Kiswahili, ndio Lugha inayoeleweka na wengi.Msituludishe nyuma katika kukuza lugha yetu duniani.Tuachane na utumwa wa kupenda lugha za kigeni.

    ReplyDelete
  6. nakubaliana nawe. na hata mualiko umetumia kiswahili kwa asilimia 90, iweje mtuma ujumbe atubague ambao hatujisikii huru tukiongea kiingereza. au ndio anatufukuza ili waende wanaojiona wasomi?

    ReplyDelete
  7. Good thing the mama is doing. Ila aliyeandika hii piece ana kiingereza kibovu. It does not do justice to the good work of those involved. Siku nyingine andika kiswahili tu.

    ReplyDelete
  8. Sioni tatizo la kutumia kiingereza hapa. Ndio maana watanzania walio nje hawawezi ku form simple sentence ya kiingereza kwa sababu ya kung'ang'ania kiswahili. English ni muhimu sana, hasa pale unapoishi nje kama U.K., au U.S.. Bila english utawasiliana vipi na wenyeji wako?, au utawezaje kufuata directions ukiwa kazini. Kuna watanzania kadhaa wameacha kazi nzuri zenye kulipa hela ya maana kwa sababu hawawezi kutoa report in english. Ikifika wakati wa kuongea, wanabaki wanajiumauma. Hakuna sababu ya maana ya kufanya watanzania washindwe kuongea kiingereza zaidi ya UZEMBE. English tunajifunza toka darasa la tatu, kwa nini ushindwe kuongea kiingereza. Ndio maana wakenya wanakuwa na maendeleo zaidi ya watanzania huku nje kwa sababu wenzetu wakenya wanatilia mkazo english.
    Inapokuja kwele swala la ku invest Tanzania, ikumbukwe kuwa watanzania wengi walio nje ni wanafunzi. Kwa hiyo unapotegemea mwanafunzi a-invest, wakati anafikiria lini atamaliza shule,kidogo unakuwa umekwenda off-the-course. Ni nani hapo Dar anayekwenda UD, au IFM, au CBE, akategemewa ai-invest wakati anafikiria jinsi ya kumaliza shule. Tuwe wakweli japo mara moja. Pia ujambazi umezidi mno, hata kama mtu ana uwezo wa ku-invest, anafikiria mara mia kabla ya kuamua. Tatu, watu wa bandarini, (COTECNA na TRA)wakishirikiana, wanakatisha tamaa wananchi wanaotaka kuleta vifaa vyao Tanzania. Ku clear mizigo Dar Port, paper work inaweza chukua zaidi ya mwezi, mbali na kuhonga. Sasa nani anataka arudi Tanzania alafu aanze kuzungushwa bandarini akijaribu kutoa mizigo yake. KAMWE HATUTAENDELEA KAMA URASIMU WA BANDARINI HAUTAISHA.

    ReplyDelete
  9. Tatizo wa Tz\wengi wa UK hawajasoma wala nini hawana elimu. Wengi wanakata masomo yao ya chuoni na kubaki kufanya kazi za kishenzi kama kuwa chamba wazee wakizungu n.k...ndio mana kufanya mambo flani yalio enda shule inakua tatizo.

    ReplyDelete
  10. Allah akubariki daima mama maajar na napenda kutoa mkono wa rambi rambi kwako.

    ReplyDelete
  11. walio UK hawasomi kwa sababu hakuna aliyewalipia shule. Kulipa ada ya malkia siyo mchezo ati.

    ReplyDelete
  12. jamani Betyy anataka kumsue Michuzi wa watu,kwanini kila siku tunasikia mahali pameungua moto bongo and then unasikia tatizo la umeme kama hili soko Dodoma why don`t we fucking sue this umeme corparation kwa kusababisha matatizo.Nchi zingine hakuna umeme unaosababisha moto na kucompromise miasha ya jamii.I hate Tennesco and TTCL but no doubt their days are numbered.

    ReplyDelete
  13. Hongera mama Maajar kuanzisha mshikamano wa watanzania uingereza.Mshikamano uliokuweko Uingereza ulikuwa ni wa wapemba tu ukihusisha kuchangishana Pesa kwa ajili ya CUF na kuandamana London kupinga chaguzi za Zanzibar.Na kuendesha harakati za kidini uingereza.

    Tunaomba utumie nafasi hiyo pia kuwashauri kuwa pamoja na hali ngumu walizo nazo wasome sana kama wakenya,wanigeria,wahindi na waghana halafu watafute kazi za maana za pesa nyingi na zenye hadhi kubwa kimataifa huko uingereza na mataifa mengine kwenye nchi nyingine zilizoendelea badala ya kutoroka shule na kwenda kuchamba wazungu na kubeba mabox viwandani na kufanya kazi za ulinzi (sungusungu) kama wamakonde hapo zamani.Balozi zingine huita raia wake na kuwashauri hata ni fani gani wasome.Ni aibu mtu kwenda uingereza aende kuuumia asome kwa bei kubwa kwenye mazingira magumu kidegree au kidiploma kinachopatikana Dar es salaam kwenye hata vyuo vya vichochoroni ambacho hakina ushindani wowote kimataifa au hata akirudi nacho Tanzania anaweza ishia kukosa kazi vilevile sababu watu kibao wanacho.

    Mwisho

    ReplyDelete
  14. Anony hapo juu inaonekana una ufinyu wa kuelewa. Hata siku moja usilinganishe elimu ya UK (Dunia ya kwanza) na TZ (Dunia ya tatu). Watu tumeisoma elimu ya TZ mpaka level ya Degree na ya UK elimu ya juu, tumeona tofauti kubwa. Inaonekana ulikosa visa ndio maana una donge "sizitaki mbichi hizi". ktk maisha ni kawaida kuna watu wanaosoma na wasiosoma si ajabu, kwa hiyo usi generalise kuwa wa TZ wa UK hawasomi. Na hili suala la kufanya kazi unazoziona ni za ovyo ni "means to an end" ili wapate kumudu maisha wakati wanasoma na hii ni kawaida hata kwa wenyewe wanafunzi wa kizungu, siyo hapo TZ mwanafunzi hajishughulishi wanasubiri pesa kiduchu za serikali kwa kuandamana.

    ReplyDelete
  15. Hivi jamani naomba kuuliza maana sisi wengine tunachangabywa humu ndani kabisaaaaa!!

    Kwanza huku ndani kuna ANONYMOUS wangapi?maana naona majina yao yanatuchanganya,kama wapo tofauti plse unaweza kutumia majina tofauti?

    Pili Anonymous msg ya mwisho naona kidogo akili zako zina fikra na zimekuwa tofauti na wa juu,anafikiri watu wote hapa ni KULA KULALA kama yeye ndiyo maana amefikia kusema maneno kama hayo.

    Hata hao maproffessor bongo kama wamesoma ulaya maisha ya mzeto ni lazima ili mradi tuu usisahau nini kilichokulete huko,hizi Ulinzi,kufanya kazi viwandani yote ni pass way siyo ya kudumu

    Hivyo kijana shule muhimu kwani huko kichwani 0 unayo kwa mtazamo wa maneno yako hapo juu Anonymous wa KWanza juu1!

    ReplyDelete
  16. WATU WALA HAWAKUWA WENGI KWENYE HUU MKUTANO. NA WALA IT WAS NOT ALL THAT. THAT IS WHY WATU WA MAANA WOTE HAWAKWENDA KUACHA SHUGHULI ZAO ZA MAANA KUSIKILIZA HUU MKUTANO. I WAS THERE AND I CAN TELL YOU PEOPLE WHO DID NOT GO.....YOU DID NOT MISS A THING. KAMA ATAWEZA KULETA MAENDELEO MAMA MAAJAR.....BASI WE AWAIT TO SEE. MAANA MABALOZI WOTE WALIOPITA WALIKUWA CHOO SANA KAZI YAO KULA PESA ZA SEREKALI TU. NA HAWAJALI WANANCHI. NDIO MAANA EMBASSY ZA NCHI NYINGINE WANANCHI WAO WAKIFIKA TU WANARIPOTI KWENYE BALOZI ZAO, WANATOA ANUANI ZAO N.K. LAKINI HAPA UBALOZI WA LONDON HAKUNA ANAYEONA KWENDA NI VIZURI, MAANA HATA WAFANYAKAZI WENYEWE WANAJIONA SANA NA NYODO NA KUDHARAU WATU, UKIFIKA UNAONEKANA KAMA UNA SHIDA NA UNATAKA MSAADA AU NINI SIJUI.
    HATA KAZI WANAPEANA WENYEWE KWA WENYEWE, FAMILIA NA MARAFIKI ZAO. NI KWA KUJUANA TU HAPO, NA WAISLAMU NDIO WANATAWALA.

    ReplyDelete
  17. Asante Michuzi kwa jitihada zako zako za kuwa daraja la mawasiliano miongoni mwa Watanzania huku duniani.
    Nilikwenda kwenye huu mkutano na yaliyotokea si mageni sana miongoni mwa watanzania.
    Mhe Balozi alikuja na ajenda zake ambazo hazitofautiani sana na za Mhe Rais wetu, kasi mpya tena mpya kwelikweli!!,Viongozi aliwo wataka kuwa miongoni mwa watendaji wa kamati hii walikuwepo na wapendekezaji wakaandaliwa na ndipo kazi ikaanza Wajumbe tisa wakateuliwa kwa kupendekezwa na wenyewe, humu wamo Watanzania/Waingereza, humu wamo jamaa wenye Visa za miezi sita, wamo jamaa wenye kesi za kutokuwepo kihali hapa Uingereza, wamo jamaa wasioruhusiwa kupata ajira hii kufuatia maombi yao ya kuishi hapa uingereza kuwa na migogoro na Serikali ya hapa.katika orodha hii tuma Waislam nane! na MKristo mmoja!!!!

    ReplyDelete
  18. Huyu Mhe Balozi atachemsha tena haraka sana, kwani inaelekea anapenda kufanya kazi kwa mipango ya zima moto!
    Ilitakiwa kwanza kupata usajili wa Watanzania wote waishio hapa na kupata wasifu wa kila mmoja kabla hajaingia katika kuomba kuongoza, yaani kwa kuwa baadhi ya watu walijitolea sana kuwa karibu naye wakati wa msiba basi hawa wanahaki ya kuwa viongozi wa wa-watanzania! baadhi yao hawana hata uwezo wa kujenga hoja nyepesi kabisa achilia mbali kuwaongoza watanzania ugenini! hapa unataka mtanzania mwenye hadhi ya kujenga hoja zihusuzo utamaduni wa nchi mbili, mchambuzi wa hoja mtaalamu wa mawasiliano na muelewa wa mambo ya kidunia kwa kina na si ubabaishaji, kwa kuwa nina namba ya simu ya Balozi au huwa naonana na Balozi kila siku nyumbani kwake basi nitakuwa kiongozi wa Watanzania!, pia Mhe Balozi jaribu kuchagua hafla za kwenda hao jamaa wanaojaribu kukuonyesha jiji la London watakuharibia sasa hivi, yetu macho, mwenzio Kibelloh alikuwa anafanya kivyake vyake!!, wanukupatia Umaaufu rahisi kwa vyombo vyao finyu vya mawasiliano nawe unawakaribisha mpaka uani, jamani tuwache ushwahili na Udini tujenge Taifa huku ugenini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...