UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU WAZIRI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE, amefanya uteuzi wa Mawaziri wawili na Naibu Mawaziri wawili kama ifuatavyo:-
1. NDUGU BERNARD MEMBE (Mb)., kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ndugu Membe alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dr. Asha-Rose Migiro ambaye ameteuliwa kuwa NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA.
2. DR. BATILDA SALHA BURIAN (Mb)., kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu). Dr. Burian anajaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha Mhe. AKUKWETI. Kabla ya uteuzi huu, Dr. Burian alikuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji.
3. NDUGU WILLIAM MGANGA NGELEJA (Mb)., kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Ndugu Ngeleja ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema.
4. NDUGU GAUDENCE CASSIAN KAYOMBO (Mb)., kuwa Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji. Ndugu Kayombo ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki.
5. Mawaziri na Naibu Mawaziri hao wataapishwa siku ya Ijumaa, tarehe 12 Januari, 2007, saa 10.00 jioni IKULU, Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Rais pia amemteua BIBI AMINA MRISHO SAIDI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mjini. Uteuzi huu unaanza mara moja.
IKULU (Phillemon L. Luhanjo)
DAR ES SALAAM KATIBU MKUU KIONGOZI
Kwa B. Membe Rais kapatia haswaa. Huyu jamaa yuko fit na ni mchapakazi kwelikweli. Hongera kwa Rais na Membe.
ReplyDeleteHao wengine siwajui...ni wale wale...lakini kafanya vizuri kuibua watu.
Profeshenali, sawa!
ReplyDeleteWaropokaji sasa semeni msinyamaze, hao mawaziri walioteuliwa wa dini gani? maana mumemsema sana raisi kuwa anapendelea. "Mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu."
ReplyDeleteMIMI NIMEFURAHISHWA NA MUHESHIMIWA AL HAJI KIKWETE KUTEUA MIKRISTU MINGI THIS TIME MAANA WAMETUCHOSHA KULALAMIKA OOH ALHAJI KIKWETE ANAJAZA WAISLAMU TUUU, SASA HIYO ILIYO CHAGULIWA YOTE NI MIKRISTU SIJUI MTAONGEA NINI SASA, INASIKITISHA KUONA MIKRISTU MINGI NI MALALAMIKO KUJA KWENYE KAZI RUSHWA! SASA CHAPENI KAZI MSIENDEKEZE KUPOKEA NA KULA RUSHWA!
ReplyDeleteNaona Wanaharakati wa Kikristo leo wote wamefunga midomo yao maana wanaongoza kwa kulalamika kuhusiana na teuzi mbalimbali za Raisi kuwa zina mlengo wa kupendelea Dini ya Kiislamu.
ReplyDeleteOngeeni sasa leo maana mnajifanyaga mahodari wa kuongea pumba zisizo na kichwa wala miguu. Ndio maana siku zote nasemaga nyinyi mnaongoza kwa kuwa na udini wa hali ya juu, si unaona leo pamoja na teuzi zote nne za mawaziri na manaibu mawaziri hakuna mtu wa Kiislamu hata mmoja aliesema Rais Kikwete ni mdini na anapendelea wakristo.
Dr. Amour kama unavyojiita sijui ni Dr.wa uganga wa kienyeji au ni dakitali wa elimu,lakini kwa kulingana na kauli zako naona wewe ni daktari wa uganga wa kienyeji maana huhitaji kuambiwa kwamba ungekuwa na kisomo lugha yako ingekuwa ya kistaarabu hata kama unachuki za binafsi zidi ya watu kadha.
ReplyDeleteWewwe unyejiita Dr Amour --- sijui kama kweli ni Dr,kwani kutokana na maoni yako inaelekea wewe ni Dr wa MITISHAMBA na wala si vinginevyo.Kwa taarifa yako rushwa haichagui dini,uadilifu wa mtu na jamii aliyomo huchangia sana ktk rushwa.
ReplyDeleteNDUGU WANA MARUMBANO.....
ReplyDeleteIngawaje JK anajitahidi kubadili kidogo system lakini bado mambo ni yale yale.Mbona hatuoni new faces kwenye cabinet , ma graduate wangapi na wataalamu vijana hawapewi nafasi kama hizi matokeo yake ni kuvutana huyu alikuwa hapa kapelekwa kule.. thus why we cant be stable wezentu wanachagua mtu kutokana na taharuma aliyo nayo ,sisi kwetu mtu anawekwa kwasababu........(time is over now )umefika wakati wakuwa na uchungu na nchi yetu halafu Tanzania inawasomi wa kutosha sasa hivi amesema mwenyewe JK siku ya miaka 45 ya uhuru.. wapeni nchi vijana wasomi ..(nguvu mpya ,hali mpya na kasi mpya by JK).........
Doctor.
Ni kweli sijui huyu waziri aliyekua kwenye nishati anajua chochote kuhusu mahusiano ya kimataifa? Au huko kwenye nishati CV zake zilikua sio kamili? Mimi nilidhania viongozi wanapewa shunguli kutokabna na background career yao. Kama ni nishati na madini lazima vitabu viwe vimepanda sana kwenye physics, geology etc. Na huku kwenye international at least mwenye legal pro. alinipa moyo. Au hawa viongozi wetu wa Tz ni multitalented sana? Kwasababu naona rahisi wetu anawashuffle tu. Toka huku nenda huku, rudi huku. Hiyo ingetakiwa ifanyike miaka ya 60 ambako kulikua hakuna wasomi wa field mbalimbali na watu hawana choice. Ina maana basi tu kwa vile mtu ana PHd anaweza aka tackle kila angle ipasavyo? That is not true.
ReplyDeletedu kiswahili cha Anoni huyo hapo juu wa Jan 12, saa 10:41:29 pm kimeniacha hoi, at taharuma, jamaani hata lugha hii nyepesi nyepesi inatushinda. duu
ReplyDeleteLingine namnukuu .... nguvu mpya, hali mpya(arimpya)....
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha
Mbavu sina
akiambiwa aongee kingereza ndo yatakuwa yale yaleeeee
WE ANON WA SATURDAY 13 JAN, 1:35:07 AM ACHA UJINGA.
ReplyDeleteSIO LAZIMA WAZIRI AWE AMESOMEA FANI YA WIZARA ANAYOONGOZA, KINACHOTAKIWA AWE NA REASONABLE UNDERSTANDING OF ISSUES. UNACHOJIFUNZA CHUO KIKUU SIO SPECIFICS PEKE YAKE KAMA BIOLOGY AU ECONOMICS, BALI PIA ABILITY TO THINK SYSTEMATICALLY....UKIWA UMESOMA VIZURI UNAWEZA KU-RELATE ISSUES AND GET BIG PICTURE, SIO SPECIFICS IN A NARROW SENSE, UMENIPATA?. UNACHOTAKIWA NI KUONGOZA WATU WATAALAMU WA NYANJA MBALIMBALI KUFANYA KAZI KUFIKIA COMMON OBJECTIVES.
Wewe 2:14 nyie ndio mnaokimbia shule na kutaka uongozi wa bure. How can you lead people if you don't much about that field. ndio maan hatutaendelea if we need only the ability to think systematically. Kila mtu anayo ability hiyo. So don't be that dumb. Ukweli ni kuwa kushuffle na kushuffle watu itaturudisha nyuma forever...Ndio maana mgao wa umeme hauishi....think systematically then...
ReplyDelete