jk akiongea na wabongo ukerewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. michuzi usidanganye bwana kuna wengine hawajawahi fika huko london sasa unawazingua hapa.hapo j.k alipokutana na wabongo london

    ReplyDelete
  2. kikwete ni mwisho nakwambia, kiboko yao, mpaka ukerewe watu matumbo joto.

    ReplyDelete
  3. Kikwete hana lolote ni Msanii tu. Nasikia amekimbia maswali ya wananchi na kuwahi mechi ya Arsenal na Totenham halafu anawaongopea watu kuwa eti yeye kuhudhuria hiyo mechi ilishapangwa toka zamani. Nini muhimu kuzungumza na wananchi wako au kwenda kuangalia mpira????

    Halafu hao wapenzi wa CCM waliovalia kofia na fulana za CCM wamezidi upambe, pamoja na kujua uchafu unaofanywa na viongozi wa CCM kuhusiana na rushwa na uchumi wa nchi yetu lakini bado mpo tu vigwanda vyenu kama vikaragosi. Nilitegemea mko UK na mnakuwa exposed na scandals zote za viongozi wetu wanazozifanya kuihujumu nchi yetu basi mngepunguza upambe wenu kwa CCM lakini bado mpo tu kama mmeshushwa leo kutoka bushi.

    Najua Michuzi hutotoa haya maoni kutokana na kuwa kada wa CCM na mpambe wa Kikwete.

    ReplyDelete
  4. Raisi wetu kavaa koti hilo hilo toka Dar..ingawa alivua tai na kuongezea sweta!

    ReplyDelete
  5. Wewe anonymous wa hapo juu acha ulimbukeni,Kikwete hakwenda kuangalia mechi ya Arsenal na Tottenham,ilikuwa Newcastle na Tottenham.Isitoshe tiketi za mechi zilishanunuliwa mapema kabla hata ya mkutano na Watanzania iweje useme eti alikwenda kuangalia mechi badala ya kuzungumza na Watanzania?
    Kwanza hukuwepo kwenye mkutano na wala ratiba huzijui zilikuwaje,hakukimbia maswali bali muda wa kuyajibu haukuwepo kutokana na msafara wake kuchelewa kuwasili jambo ambalo Abdul "Sisco" Mtiro ndiye anayepaswa kulirekebisha akiwa kama mratibu wa taratibu za Rais.
    Jaribu kuwa na busara,usiongee vitu usivyovijua.

    ReplyDelete
  6. you guyz r sick bus**** huyu ni raisi wetu mnatakiwa kumueshimu kama inshara ya kuiheshimu nchi yetu hamuwezi kila mtu kumkashifu kama vile hamkufundishwa heshima NA WAZAZI wenu huyu ni MTUKUFU RAISI yeye kuja huku london ni moja ya upendo wake kwa wananchi wake walio mbali na nyumbani. mlicho takiwa kufanya ni kumuunga mkono kwa safari yake ya london. kwenda kuona mpira ni baada ya kazi he still got his life to leave apart from being presedent.
    HESHIMA YAKO RAISI. NA AKHASANTE KWA KUJA KUTUTEMBELEA.
    KK
    ESSEX

    ReplyDelete
  7. kikwette yupo UK kumsupport blair na scandal lake na madili yaliyofanywa na serikali ya Mkapa kuusu radar na mambo mengi ya ministry of defence..wabongo kazi kumshabikia kikwette wakati hela zenu za kodi watu wanatafuna...ari mpya njia mpya za kuibia wananchi...

    ReplyDelete
  8. Wewe anon wa Tue 12:54 kama hujui kitu basi funga domo lako.
    Hebu tutolee pumba zako hapa. Huyo Cisco Mtiro si ndio mpambe wa Rais. Sasa kuchelewa kwa Rais sio tatizo la Watanzania walioacha shughuli zao kibao waje kumsikiliza na kumuuliza maswali Rais wao. Tena kuna wengi walitoka nje ya London ili kuja tu kwa shughuli hiyo lakini matokeo yake Rais akachelewa. Hivi huoni umuhimu wa kuwa on time???? Hivi huoni inaonyesha picha gani kwa Rais kuchelewa kila mara. Na hii sio mara ya kwanza kwa Kikwete kuchelewa. Nakumbuka alichelewa Minnessota, USA kwenye kupokea degree yake ya heshima, ilibidi Rais atoke mbiombio awahi kwenda airport pale MN maana ndege ingemuacha na hakula hata Lunch aliyokuwa ameandaliwa na wenyeji wake. Akaja akachelewa tena pale kwa Balozi New York. Huyu jamaa au watu wake ni wachovu sana.

    Kikwete amechemsha kuacha kujibu maswali ya wananchi na kukimbilia mpirani. Iwe Arsenal au Newcastle zote ni timu kwa hiyo hakuna tofauti hapo, watu wengine kama hamna vya kuongea bora mnyamaze maana mnachemsha kama ma-goigoi wa kifikra. Kama walishanunua ticket za mechi toka zamani ndio nini kwani?? Wananchi waliomuweka madarakani ni muhimu kuliko hiyo mechi au huyo Lord wa Kingereza. Majukumu yake kwa wananchi wa Tanzania ni muhimu kuliko mambo mengi sana binafsi.

    Si walishajua toka mapema kutakuwa na watanzania wengi kwenye mkutano, kwa nini wasipange mkutano uanze mapema ili wajipe muda wa kuwahi mpirani?? Tatizo la viongozi wengi wa Kiafrika hawana nidhamu ya muda na hawachelewi kujiona miungu watu wakijiamulia mambo wanavyotaka bila ya kufikiria wananchi waliokusanyika pale wameacha mambo yao waje kumuona.

    Kikwete umechemsha na hiyo February uliyoahidi utaenda usije ukatoa sababu nyingine ya kukimbia maswali. Tumeshasikia scandal ya Radar iko hewani na viongozi kuhongwa $12million. Kuna scandal ya Richmonduli ambayo watu wamekula. Kuna Scandal ya Prof. Mahalu kuachiwa pamoja na kuiibia nchi. Kuna mambo mengi kweli ambayo watu wanataka wakuulize lakini ukaingia mitini.

    Michuzi usinibanie hakikisha unaweka kwenye mtandao wako haya maoni yangu hata kama nimempiga madongo mshikaji wako Kikwete. Hii ni zama ya uwazi na ukweli.

    ReplyDelete
  9. Hivi J.K anafikiri angali waziri wa mambo ya nje pia? Mbona safari za nje zimezidi?
    MICHUZI J.K ana mpiga picha wake na Mwanadishi wake wa habari kwanini unatumia pesa za umma kusafiri kwenye safari zisizo na maana kama hizi? ( Kukutana na wana CCM London?)
    Rais ana waandishi wake wa habari Michuzi stay home and do your work?
    We are tired of this B.S

    ReplyDelete
  10. HAPO HAKUNA HATA MTANZANIA MMOJA WOTE WA KIMBIZI.WATANZANIA HALISI NA WA PASSPORT ZA KIJANI TUPO STATES.RAIS KAISHIA KUHUTUBIA WARUNDI HAPO LONDON.

    ReplyDelete
  11. Wewe sina Makosa ni mshamba sana. Watanzaia walioko London sio wote wakimbizi. Kama kweli una uchungu na nchi yako, mbona unakaa marekani bila papers. husafiri wala kutoka nje ya state. zaidi ni kutoka kwenye kijichumba unachokaa kwenda kazini. Bora hawa arundi wanapata maisha bora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...