mzee wetu simba wa vita rashidi mfaume kawawa leo amepewa tuzo ya 'martin luther king jnr.
drum major for justice award na balozi wa marekani nchini michael retzer. waliowahi kupata tuzo hiyo hapa bongo ni dk.jaji sinde warioba (1999), mwalimu nyerere (2000 - alipokea mama maria kwa niaba), jaji francis nyalali (2002) profesa geofrey mmari ( 2003), mama justa mwaituka (2004), mama mongella (2005) na dk. salim ahmed salim (2006)
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mzee Kawawa kweli anajua kwa nini amekabidhiwa picha hiyo ya King?Ukiwa mweusi na ukabidhiwe picha ya mpiganaji wa haki za weusi sio mambo ya kuchukua kiurahisi,ni mambo makubwa mno.Ila kwa mzee kama huyu ataishia kuibandika ukutani bila kuijadili na kujiuliza kwa nafasi aliyo nayo yeye je?Amefanya kitu gani katika mapambano hayo au atajihusisha vipi kumwenzi M.L.T?

    ReplyDelete
  2. Kwa nini umpe award kama hiyo mtu kama Kawawa wakati amefanya kazi hata kabla ya MLK kujulikana kwenye civil rights movement? Huu ni uzandiki na upumbavu. Ninamuheshimu sana MLK, lakini ninasikitishwa kuona jinsi serikali yao ilivyotake over legacy yake, kwanza kwa kile alichokuwa anapigania hasa, na pia hata at the expense ya legacy ya Malcolm X.

    ReplyDelete
  3. ur rigth anony hapo juu,,malcom x was a "field negro" na dr king was a mere "house negro"........pfffff

    ReplyDelete
  4. Anony 11.20 hapo juu
    Hawa wote yaani malcom x na martin luther king walikuwa ni wanaharakati za kudaiwa haki za weusi huko marekani. Tofauti kati yao ni kwamba kila mwanaharakati alitumia njia tofauti. Sikumbuki ni nani alisema "There was a slave who lived in the house and there was a slave who lived on the farm". Sidhani kama ni sahihi kusema dr martin luther king "was a mere house negro" huku ni kumdhalilisha. Kwa kweli huyu mtu ana heshima yake na ndiyo maana ya tuzo hili.

    ReplyDelete
  5. Wewe ANYONY wa Wednesday, January 24, 2007 9:02:43 AM pamoja na ANYON wengine wagumu kuelewa.
    ACHA DHARAU ZA KISHAMBA, WEWE MWENYEWE HUELEWI PIA. Kwani award nyingine mbona zinatolewa hata kwa watu ambao ni marehemu kwakutambua michango yao kwa jamii? Hata mzee Kawawa kama alifanya mambo mazuri na sasa ni mzee, hata kama uelewa wake ni mdogo kwa sasa kwa sababu ya uzee, unataka asipewe heshima yake? Be smart kuelewa mambo usichangie tu ilimradi.

    ReplyDelete
  6. USHAURI: MICHUZI REKEBISHA KIDOGO HII AUTOMATIC DISPLAY YAKO KAMA INAVYOSOMEKA HAPA 'Your comment has been saved and will be visible after blog owner approval' Sahihisho badala ya owner approval weka owner's approval. Ila siotatizo sana unaweza kuacha hivyo inaeleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...