
kocha milutin sredojevic ‘micho’ wa serbia, aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa na wanachama na wapenzi wa klabu ya yanga, aliwasili nchini jumatatu tayari kufundisha wana-jangwani.
Micho, ambaye aliongozana na msaidizi wake, Dusan Kondic, pamoja na wakala wao, Ivica Stankovic, tayari ameshamwaga wino leo ofisini kwa mfadhili mkuu wa yanga yusuf manji, na atakuwa kocha mkuu na kuisaidiwa na mmalawi jack chamangwana. shoto ni yusuf mzimba na kulia ni prezoo wa yanga kifukwe
Hatma ya kocha wa simba mbrazil bado kujulikana hadi tunaenda mitamboni….


Hongera Kifukwe,kazi yako tumeikubali!!!!
ReplyDeletehapa micho huku kondik hapa chamangwana..... kudadek! yanga mshindwe wenyewe
ReplyDeleteHivi huyu mzimba anahusika vipi? au ni 'kamati ya ufundi'
ReplyDeleteNasikia atakuwa analipwa milioni 36 za madafu!!!
ReplyDeleteHapo hakuna kocha, Yanga wameliwa tu!!! Wa-Serb hawa hawana utaalamu wowote wa soka, bora kina chamangwana na chambua au minziro. tumezoea sana kupapatikia weupe.
ReplyDeleteNimewaona Les Ferdinand na John Barnes wakiwa Tanzania. wote ni wataalamu wa soka. Simba au Yanga wangeweza kuongea nao kwa ajili ya kufundisha timu zao.
Barnes ni mchambuzi wa masuala ya soka ktk kituo cha TV cha channel Five (dada wa Skynews/sports UK) na Les yuko BBC Match of the day.
Michuzi tafadhali kumbuka haya maoni yangu...Yanga wameliwa! (Niulize Januari ya mwaka kesho 2008)
Ni kweli hayo maoni yako huyu Barnes kafundisha timu gani ikapata mafanikio? Huyu jamaa CV yake inajiuza, waswahili tukae kimia kama hatuna cha kuongea
ReplyDelete