
kwa idhini yenu wadau naomba leo nianzishe mada mpya.
ni kwamba, hivi tunavyoongea mchakato (process) wa kujadili kuanzishwa kwa shirikisho la nchi za afrika mashariki unakaribia kuanza nchi nzima, na tayari mkuu wa mkoa wa dar mh. abbass kandoro keshatangaza kuwa utaanzia bandari ya salama tarehe 10 mwezi huu ambapo wabongo wote wanaoishi humo wamekaribishwa kushiriki kwa kutoa maoni yao juu ya dhati juu ya hilo.
baada ya hapo jopo maalum la kukusanya maoni litahamia mkoa mwingine na kuendelea hivyo hivyo hadi mwisho. naomba ieleweke kwamba mada ya faida/hasara ya uraia wa nchi mbili haujakoma. wenye michango waendelee kuitoa tu sehemu husika.
wadau naomba maoni yenu juu ya kuanzishwa kwa shirikisho la afrika mashariki ama kwa ung'eng'e east african federation...
nawasilisha
pia si vibaya ukiwa unachangia huku ukiburudika hapa na muziki huo chini:


Kaka Michuzi na watanzania wenzangu, Mimi naafiki kwa kauli moja hili swala la muungano wa Afrika mashariki. Lakini, ninachoona hapa ni kwamba hatujawa makini kabisa katika namna tunavyoweza kulitekeleza. Maoni yangu, twende hatua kwa hatua, tusiwe na papara kwani tuliyaona yaliyotokea mwaka 1977 lilipovunjika. Huu muungano inabidi uwe wa watu na sio wanasiasa kwenye maconference Arusha na Nairobi..babu yangu kule kijijini aweze kuuza kahawa yake popote kwa bei anayoitaka...na wala si vinginevyo, kama ni kupeleka bidhaa Burundi iwe open na sio kuogopa uhamiaji na custom pale boarder ....Kwa hiyo tungeanza na shirikisho la uchumi kwanza (tuachane na fast trucking) tujipe nafasi hata ya miaka kumi au zaidi, tuangalie tumefaidika vipi na shirikisho la KIUCHUMI kwanza. Na mimi nina imani watu (naongelea wakulima na wafugaji ambao ndo wengi wa baba zetu huko vijijini) wakifaidika watalisupport hili shirikisho...Amini nakuambieni....Na baada ya hapo tuanze kufanya kura ya maoni "referendum" unajua hapa tunaongelea nchi tano Kenya Uganda Tz, Rwanda na Burundi. Tunaongea SWALA VERY SERIOUS kuuza uhuru wetu..ceding of our sovereign!! sio kitu cha kukusanya maoni pale Karimjee au ukumbi wa Anatouglo..pale mnazi mumoja..hapa kila raia inabidi ashirikishwe kwa kura ya SIRI!!! Na kama tunavyojua binadamu na waafrika especially tuna tamaa ya madaraka..na kama wote ni maskini si rahisi kufanikisha shirikisho la kisiasa maana kila mtu anataka kivyake... Tuache papara, shirikisho sio lazima alilete Kikwete au Museveni, la hasha.....waweke mazingira na misingi ya kupata shirikisho lenye manufaa. Lakini tukifanya mambo kwa haraka haraka kama tunavyofanya kwa ajili ya watu wachache kukumbukwa kwenye historia...., tutajikuta tunarudi kule kule. Kuna vitu vingi vya kurekebisha kama sheria za ardhi, mfumo wa elimu, ulinzi nk. Tuchukue mfano wa TZ tumeungana na Zanzibar takribani nusu karne sasa, ila bado malalamiko ni mengi mno.(mpasuko wa kisiasa Zanzibar) na kumbuka zanzibar in raia chini ya Milioni moja hivi...sasa wewe fikiria nchi tano na zote zina historia ya vurugu...TWENDE TARATIBU KAMA KWELI TUNA NIA YA KUUNGANISHA NGUVU ZETU KWA FAIDA YA WATU WETU. Hata Europe wameanza hiki kibarua tangu 1950s na leo bado wanaenda mbele taratibu!! TUJIFUNZE.
ReplyDeleteTanzania na wengine pale East Africa tusidanganyane..hatujawa tayari (morally, economically or otherwise) kuwa na shirikisho la kisiasa (sio kwamba nakuwa na mawazo hasi sana) ila kama Mkapa alishindwa kuelewana na akina Mrema na Lipumba wanaoongea lugha moja, wamesoma wote, wamefanya kazi wote..leo ndo JK ataelewana na akina Nkurunziza na Kagame? Twende taratibu, wanasiasa wasituuze tena.
Najua faida za muungano ni nyingi sana kuanzia uchumi, labour mobility nk, ila waungwana twende taratibu. maskini na maskini hamuwezi kuwa marafiki, urafiki ukadumu!!!
Tutafute masoko na mianya mingine ya biashara kwa ajili ya nchi zetu. Otherwise tutajikuta hata hatua moja ambayo tungepiga, tunarudi nyuma. Wabinafsi ni wengi na hili ni kwetu wote....
Muungano wa Kiuchumi kwa sasa ndo ufumbuzi wa matatizo yetu, na baadaye tukifanikiwa..tutafanya referendum tukubali mganda au mkenya awe raisi wetu..but after seeing and analysing the costs and benefits.
Mungu Ibariki Tz na watu wake, na viongozi wake wafanye maamuzi sahihi kwa ajili ya Tanzania ya leo na kesho!! JK,you and me we might be dead tommorrow, but Tanzania should and will remain forever!! so tufanye maamuzi tukiwa tunafikiria implications zake in 100 years to come!!!
Ukiona US leo tunakeba box tunapata mshahara wa waziri Africa, si bure..kuna watu walihangaika kuifikisha hapa ilipo ingawa walikufa maskini ila walikuwa wanafanya yote kwa vizazi vijavyo na ndo maana leo we are here where we are si kwa sababu ya Bush au Cheney ni sababu ya akina Rosa Park, G Washington na wengineo.
Naomba kutoa haka kamchango kangu.
Michuzi, ziweke hizi kwenye blog yetu ili watu waburudike.
ReplyDeleteMadilu
http://www.youtube.com/watch?v=WyWbHoWfyIA
Franco Luambo Luanzo Makiadi na T.P.OK Jazz
Unanikumbusha mbali sana wimbo huu
http://www.youtube.com/watch?v=itzTgp39NaY
Koffi Olomide
http://www.youtube.com/watch?v=ecwlEx8o9uk
Huyo anony wa kwanza kasema ukweli mtupu. Muungano wa kiiuchumi, kitu kama free trade zone, ni wa muhimu kwanza, kuliko kuwa na federation, ambayo inatafsiri kuwa na kiongozi mmoja wa federation yote, kama ilivyo U.S., au Germany, au Nigeria. Tatizo linakuja, wenzetu jirani zetu wote waliotuzunguka ambao ni members wa East African Community ni wenye ukabila sana, kiasi kwamba wanabaguana hata wakiwa nje. Mimi binafsi niwewahi kufananishwa na mkenya, ambapo mkenya huyo aliniuliza kama mimi ni kabila gani. Nilimjibu kuwa mimi ni mTanzania, na baada ya hapo aliona aibu, kwa kuwa anajua kuwa sisi waTanzania hatuna ukabila. Wakenya wanatengana kwa makabila wakiwa nje, kwa mfano, mkikuyu, anatumia muda wake mwingi na wakikuyu wenzake. Mkalenjin, anakuwa na wakalenjin wenzake pia. Inafikia point wao kwa wao hawaelewani kiasi cha kutoongea kabisa. Sasa cha kushangaza, lakini ni kizuri, wote hao wanashirikiana vizuri na waTanzania, kila mmoja kwa wakati wake, na ukiwa nao kwa wakati tofauti, wanakueleza matatizo yao ya ukabila. Mimi binafsi nimeshaelezwa zaidi ya mara moja jinsi ambavyo wanamsifu sana Nyerere kwa kutuunganisha, na wanajutia viongozi wao kwa kudumisha ukabila. Wanasema ukabila umewarudisha nyuma. Tukirudi kwenye federation, sasa Mkukuyu akawa president, au Mtutsi akawa president, hao raia kutoka makabila mengine watapumua kweli? Au ndio ofisi itajaa kabila moja tu? Kwa maoni yangu, bado hatujafikia hatua ya kuwa na federation, kwa sababu hata hiyo Nigeria tunaona ukabila, na udini jinsi vinavyoleta mauti kwa raia.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteWhy would we collect comments from wananchi now, while the contract to formulate EAC was signed way back?
Si mazingaombwe hayo? Why are political leaders in Tanzanian treating regular wananchi like dummies?
Huu ni mjadala mzuri, lakini hauna kichwa wala miguu kutokana na ukweli kwamba Mkapa na wenzake walishafanya maamuzi.
Namuunga mkono Jaduong hapo juu kwa kusema: Ero Kamano, Nyasai Akonyi!
ReplyDeleteNapenda kukumbusha kuwa hapo awali mjadala huu ulitundikwa na tukachangia, ikiwa ni pamoja na sehemu iliyopima maoni yetu kwa mizani ya ki-% kujua kwa wastani ni wangapi wanapenda ama kukataa muungano huo wa kuzijumuisha nchi za Burundi na Rwanda!
Mbona tupaiga maki taimu, maki taimu! Ama hii inatokana na brifu za serikali kwa waandishi wao wa vyombo vya habari (kama Michuzi) kuhamasisha mchakato wa shirikisho; pamoja na kuwaonya wasizungumzie ama kuandika ya Dito?
TOFAUTI YA SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI (EAC) YA SASA NA ILE JUMUIA ILIYOVUNJIKA
ReplyDeleteWatanzania wengi hivi sasa, ikiwemo wale walioko vijijini, wanatakiwa kutoa maoni yao kuhusu shirikisho la afrika mashariki. Kwa walio wengi, bado hawaelewi tofauti kati ya shirikisho la afrika mashariki pamoja na jumuia ya afrika mashariki vya sasa, na ile ya zamani iliyovunjika. Maelezo yafuatayo hapa chini ni ufafanuzi wa tofauti hizo.
1. Ile jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika, misingi yake ilikuwa ni ya kiuchumi, usawa katika mchango na manufaa, na ushirikiano wa kijamii uliolenga kupambana na nguvu za wakoloni. Hili jumuia / shirikisho la sasa hivi (EAC) ni tofauti kabisa. Lengo lake kuu ni kufuta Taifa la Tanzania, pamoja na mengine yatakayokubali, na kuanzisha taifa moja litakaloitwa EAC. Jakaya Kikwete ndiye mtu wa mwisho kuwa Rais na Amirijeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ifikapo Januari 01 2010, Jamhuri ya Afrika Mashariki itachukua nafasi ya zilizokuwa jamhuri ndogondogo, na kutengeneza Taifa Kubwa litakaloweza kupambana na utandawazi. EAC ya sasa ni mradi unaofadhiliwa na nchi za magharibi.
2. Katika nchi hiyo (tuiite EAC) kutakuwa na jeshi moja (tuliite JWEA), litakalotokea kwa kufuta Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kuliunganisha na lile la Uganda lililovamia Kongo na kusababisha mauaji makubwa ya watu, na lile la Rwanda lililovamia pia Kongo, la Kenya na Burundi. Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi hilo wa kwanza ameshajitangaza kuwa ni Mhe. Yoweri Museveni.
3. EAC itakuwa na Polisi moja itakayozaliwa kutokana na kufuta Jeshi la Polisi Tanzania, kwa kuliunganisha na Polisi wa Kenya, Polisi wa Uganda, Polisi wa Rwanda, Polisi wa Burundi ili kutengeneza Jeshi moja la Polisi la Afrika Mashariki.
4. Idara ya Uhamiaji ya Afrika Mashariki itaanzishwa, nayo ndiyo itakuwa na majukumu ya kuwafahamu nani ni raia wa EAC, ikiwemo wale wananchi ambao (wakati huo tutasema, 'zamani walikuwa raia wa Tanzania') kuwa ni kina nani. Yaani Waganda walioajiriwa "Idara ya Uhamiaji ya EAC" wanaweza kuwa ndio maafisa waliopangiwa kazi ya kudhibiti uhamiaji wa watu toka nje ya EAC kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam au wa Kilimanjaro. .. na Watanzania walioko idarani humo wakafanya kazi Burundi au Rwanda. Hakutakuwa tena na mipaka wala mipanya baina ya zile ambazo zamani zilikuwa nchi. Mipaka ya Tanzania haitakuwepo kwa Wanyarwanda, Warundi, Wakenya na Waganda. Wahutu na Watutsi, Waluo na Wakikuyu wataingia na kutoka wapendavyo kwenye jimbo ambalo zamani ilikuwa inaitwa nchi ya Tanzania, bila kuulizwa na mtu, kama ambavyo Wamakonde na Wasafwa watakavyopewa ruksa ya kuingia zilizokuwa nchi zile nyingine. Vituo vya uhamiaji baina ya nchi zanachama vitafutwa -- na vitabakia vile tu ambavyo ni vya kimataifa -- vya kushughulika na nchi za nje jirani na Jamhuri ya EAC. Vitambulisho vya Taifa vitakuwa vya EAC. Viza itakuwa ya EAC. Mtalii atakayewasili uwanja wa ndege wa Entebbe, na kuingia EAC, atakuwa na ruksa ya kwenda popote EAC -- Mtwara, Kigali, Gulu, Naivasha, Bujumbura -- bila kuulizwa na mtu.
5. Taasisi nyingi za serikali zitakuwa za shirikisho: Ukusanyaji kodi EARA (vunja ka-TRA kenu), EAoT (BoT baibai)... na kadhalika. Pana fikra potofu kwamba japokuwa umeunganisha nchi hizi za EAC, bado zitabaki kama zilivyo hivi sasa (TRA yetu 'ishirikiane tu' na patna wake wa KRA, URA,RRA na BRA). Maandishi ya shirikisho la EAC yanaonyesha itakuwapo EARA itakayopatikana kwa mwendo uleule kama wa Uhamiaji. Waziri wa Mambo ya Nje atakuwa wa EAC (kama ambavyo Zanzibar haina Waziri wa Mambo ya Nje, ndivyo itakavyokuwa kwa Tanzania). Tanzania haitakuwa na balozi nchi za nje -- bali ubalozi wa EAC. Ila Watanzania watakaoteuliwa na Mheshimiwa Rais Museveni au Kagame (rais wa EAC) kuwa mabalozi wa EAC ndio watakuwa mabalozi wanaowakilisha EAC nzima.
6. Uraia utakuwa ni wa Afrika Mashariki. Siyo tena uraia wa Tanzania. Paspoti ya Tanzania ya nini? Itafutwa, na kuanzishwa ile ya pamoja ya Afrika Mashariki itakayokuwa inatumiwa pia na Wakenya, Wanyarwanda, Warundi na Waganda.
7. Baada ya yote hayo, mchakato wa kujiondoa kwenye shirikisho la afrika mashariki ni karibu sawa na kusema haiwezekani. Kwa yule atakayefanikiwa kujiondoa, anatakiwa aache EAC kama ilivyo -- aondoke kama alivyokuja -- hana chake tena.
8. Japo hivi sasa Watanzania wakulima na wafugaji wanatoana macho kwa kugombea ardhi -- matatizo yao yataisha kwa kuwaleta Wakenya, Waganda, Wanyarwanda na Warundi wanaouana shauri ya shida ya ardhi, tukawapa ruksa ya kutamba kwenye ardhi ya Tanzania, na Watanzania nao watakuwa na ruksa ya kwenda kujimegea ardhi Kenya na Rwanda, Burundi na Uganda!
9. Wengi wa Watanzania wanazo ajira serikalini na mashirika binafsi kwa vile nafasi za kazi zinasema "Tunataka MTANZANIA mwenye sifa zifuatazo... " Kwenye EAC na 'soko la pamoja', tutatakiwa kusema "Tunataka mtu, hata awe Mkenya, Mganda, Mnyarwanda au Mrundi mradi mwenye sifa..." kwenye matangazo ya kazi za polisi, jeshi, ualimu wa shule za msingi na sekondari, kazi zozote zile -- mesenja, dereva, sekretari, mhasibu, mhadhiri, profesa, mwanasheria, afisa kwenye halmashauri, serikalini, migodini na popote ajira zinapotangazwa. Hii inategemewa itawezesha Watanzania kuwa na Maisha bora kutokana na kuwa na watu wenye sifa stahili toka EAC yote wakiwahudumia serikalini, jeshini, polisi, mashuleni, hospitali na kadhalika.
10. Wapo Watanzania wengi wanaopata ugali wao wa kila siku kutokana na sekta binafsi na ile isiyo rasmi. Kwenye EAC tutawapambanisha na Wakenya, Waganda, Wanyarwanda na Warundi watakaotaka kuja Tanzania kuwa Mama lishe, kuchuuza magengeni na sokoni, kuuza madukani, kulima, kufuga, kuchimba madini, kukata mbao, kuwa makonda na madereva wa daladala, kuwa madereva teksi, kuuza magazeti, kuwa waandishi wa habari, wamiliki vyombo vya habari, wachome mkaa, wavue samaki, waongoze watalii, wafagie barabara, wawe maseremala, mafundi ujenzi, wachoma nyama, wauza vocha za vilongalonga, wawe mgambo, wawe askari makampuni binafsi ya ulinzi, wasukume mikokoteni na maguta, na kufanya kazi yoyote inayofanywa na Watanzania wasio na ajira rasmi, au wale walioko sekta binafsi. Hii inatazamiwa itawezesha Watanzania waliolala usingizi siku nyingi waamke na kutafuta rizki itakayowapa maisha bora kabisa. Wale Watanzania watakaoshindwa kuhimili ushindani huo hawatakufa njaa. Wana ruksa ya kwenda Uganda, Rwanda, Kenya au Burundi, bila kuulizwa na mtu, wakatafute rizki zao. M-EAC yeyote ataweza kufanya kazi popote na kuondoka na mtaji, mali, faida na chochote atakacho kutoka popote na kwenda popote EAC. Unaweza kuja kuvuna mbao Rwanda, ukaja kutengeneza fenicha Tanzania. Au ukachimba almasi Kenya, na kuikata Burundi. Utaswaga ng'ombe toka Rwanda na kuwachinjia Tanzania. Ukachukua mchanga Uganda, au Burundi Ukajenga barabara ya Tanzania, au ukachukua ardhi kubwa Kenya ukalima mashamba ili kupunguza makali ya bei za vyakula Tanzania.
ahmad kombo
xi'an jiao tong university
china