Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huu mbuyu una umbo la aina yake. Unajua mibuyu ni miti ina heshima fulani kwenye tamaduni za Afrika. Huenda umbo lake hilo lina maana fulani (au mtasema ushirikina huo?)
ReplyDeleteDuh!, Ama kweli wabongo Pombe ni URITHI wetu. hata miti inabidi ichukue shepu za Chupa za Lager ikiwa ni namna ya kuwahamasisha wabongo tuitunze na kuijali kama tufanyavyo kwa Ze Lager.
ReplyDeleteMichuzi, hivi ndio vitu vya kutuletea wanablogu. mambo mazuri ya nchi yetu ambayo wengi wetu hatuyajui. nimeenda kigamboni mara kadhaa na beach kadhaa lakini sijauona huu Mbuyu Bia. upo sehemu gani huu mbuyu? au ndio Mbuyu wa SAFARI Lager???
siku ukienda Lushoto piga Snepu mandhari nzuri ya lushoto. Milima mabonde na Misitu iliyopo kule ni mizuri kinoma especially sasa ambapo mvua zinanyesha nchi nzima na rangi ya kijani ikiwa imetamalaki kila kona ya upeo wa macho yako...
Mbuyu Chupa upo katika kisiwa kidogo kiitwacho Sinda. Ukitaka kufika kisiwani- nenda Mjimwema Kigamboni ambako wavuvi watakupekela kwa gharama ndogo, ni mwendo dakika 15 kutoka pwani ya Mjimwema-Kigamboni.
ReplyDeleteOk, Kisiwa cha Sinda nakifahamu. ila sijawahi kukanyaga huko. siku nikitia maguu huko, nitautafuta huo mbuyu BIA. shukran kwa Anony wa hapo juu kwa details.
ReplyDeleteMichuzi, tupe snepu nyingine za maajabu yaliopo nchini kwetu.
kule Tanga kwenye Mapango ya Amboni nako kuna maajabu kweli kweli. niliwahi tembelea huko one time na kuona mambo ya ajabu. kuna njia za chini kwa chini toka Amboni hadi ktk miinuko ya Kilema-Kyaro (Mlima Kilimanjaro). Na mambo mengine kibao.
ajabu jinginge la huko amboni ni sanamu ambayo inafanana na sanamu ya Bikira Maria ambayo imetengenezwa naturally kwa chumvi itokanayo na maji ya mvua yanapopenya ktk miamba. Stalactites na Stalagmites kwa wale tunaokumbuka Physical Geography ya Form 3 au Form 4
MIBUYU SI NDIYO INAAMINIKA KUFANYA KAZI NA WAGANGA WA KIENYEJI? MAANA KUKU LAZIMA AKACHINJWE CHINI YA MBUYU, ILI LIPATIKANE JIBU ANAPOKATA ROHO KUKU ANAPEPERUKIA UPANDE GANI ILI MGANGA ATOE TAFSIRI.
ReplyDeleteAina hii ya miti iko nyingi tu Tanzania. Kule Mafia kuna mnazi uliopinda kama nyoka. Kama unavyosema, uhitaji kwenda Hawaii kuona, kila kitu kiko bongo humu.
ReplyDeleteMichuzi ulikwenda kurenew kibali chako huko nini? Tuambiane basi....Huu mti!!!!!!Tusije tukakuletea hela zetu zote bila kuwaza kitu. Kwasababu hata hii blog yako utazania nicotine vile...Wengi tumeshakua addicted hatuelewi sababu. Thanks men for your good pictures and news. Keep it up and God bless.
ReplyDelete