madenti wa chuo kikuu cha sokoine wakiandamana kupinga asilimia 40 wanayotakiwa kulipia kwenye ada zao, kwa mujibu wa mkataba wa masomo waliokwisha tia saini wakati wa kujiunga na chuo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Choka mbaya !
    sasa nyinyi mlitaka msilipe ? mbona sisi huku mtoni tunalipa ?

    ReplyDelete
  2. hakuna elimu ya bure, huku marekani tunalipa vibaya mno. Tunasoma na kufanya kazi kusudi tuweze kulipa. Bongo mnasoma tu hamfanyi kikazi cha aina yoyote. Kila kitu bure serikali yetu ni maskini haiwezi kuwalipia kila kitu nyie wote. Mlipe japo kidogo that is just 40% haijafika hata nusu ya ada jamani! Mtakapolipa na nyinyi kidogo hizo hela zitasaidia kuendeleza chuo, jamani naelewa ni umaskini lakini mjitahidi sio kujiendekeza! Kila siku mnasema maskini kila kitu mpewe bure kutoka WAPI? hata madawati ya kukalia hapo chuoni hayatoshi wengine wanakaa chini, hizo hela zenu zitasaidia kuongezea visivyokuwepo hapo chuoni. Marekani imeendelea lakini kila kitu watu wanalipia ndio maana serikali inapata pesa ya kuiendeleza nchi yao. Hata ukinunua maji ya kunywa unalipa na Tax. Bongo watu hawataki kulipia chochote hata ELIMU ndio kabisaaaaa!
    Kibaya BONGO watu wakilipa hizo hela zinaliwa na viongozi wa juu na hakifanyiki chochote.

    ReplyDelete
  3. sasa wewe anon wa 11:53:26 AM mbona unajichanganya mwenyewe? hiyo sentensi ya mwisho inaji contradict na maelezo ya kwanza kuhusu USA!! Kumbe wakilipa pesa zinaliwa, kwa hiyo ni bora wasilipe, si ndiyo????? Maana hata wakilipa hakuna kitakachoboreshwa, tofauti na wenzao wa USA.

    ReplyDelete
  4. Asante kidume na anony wa juu yako. Hao wanaosema ati Marekani wanalipa sasa kwanini usilipe wakati umeenda huko ukijidai unayo fedha ya kulipia? Marekani watu hawalipi bali wanakopeshwa au mwenzetu unasoma chuo gani hicho wanachotoa mifukoni? Ndio kuna watu hawachukui hiyo mikopo lakini gharama zao ni ndogo ukilinganisha na wewe uliyejidai babako ni mkurugunzi wa TANESCO. Mfano term moja gharama kwa Mmarekani inaweza ikawa dola mia saba kama anasoma Jimboni kwake hizi mtu anamudu hata asipochukua mkopo. Ni watanzania wangapi wanaweza kumudu millioni na nusu kwa mwaka?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...