watangazaji hodari wa luninga ambao awali walikuwa tvt mariam komanya (shoto) na saida mwilima pia wako wanabukua hapa ukerewe...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. JK: Urais si kujifungia ndani
    Asema nchi ina sura mbili
    Na Mwandishi Wetu
    RAIS Jakaya Kikwete amesema Urais maana yake sio kujifungia ndani na wananchi.
    Kikwete alitoa kauli hiyo alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mjini London, na matangazo hayo kurushwa jana.
    Alisema nchi ina sura mbili; ya ndani na nje hivyo kiongozi mkuu anapaswa kutembelea nchi nyingine ili nchi ijulikane na yeye afahamike na “sio kujifungia ndani na umaskini wenu na kula mihogo na wananchi”.
    Akizungumzia ziara yake nchini Uingereza ambayo aliianza mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema alialikwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tony Blair.
    Alifafanua kwamba, alipokuwa Marekani miezi michache iliyopita Rais George Bush aliomba akutane naye na kuhoji, “je wakubwa hawa niwakatalie?”
    Rais alitoa majibu hayo baada ya kuulizwa na BBC sababu za yeye kusafiri kila mara nje ya nchi kuliko wanavyofanya viongozi wa Kenya na Uganda.
    Kuhusu swali kwamba anajionaje kuwa Rais, Kikwete alisema mtu anapokuwa rais ina maana kufanya kazi saa 24 kwa sababu ndiye mwenye uamuzi wa mwisho katika nchi.
    Rais Kikwete alitoa mfano kwamba mwaka jana alipewa taarifa saa tano usiku kuwa kesho yake Levy Mwanawasa wa Zambia alikuwa anaapishwa kuwa rais.
    Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, alimtaka msaidizi wake afuatilie kuhusu safari ya kwenda kwenye sherehe hizo.
    Alisema msaidizi huyo akarudisha jibu kwake saa saba usiku kwamba kila kitu ni sawa na safari ilifanyika kesho yake.
    Kuhusu ni mambo gani hupendelea kuyafanya wakati wa mapumziko baada ya kazi, Rais Kikwete alisema hupendelea kusikiliza muziki hasa hu wa kisasa kwani hufungua televisheni na kusikiliza.
    “Zamani nilikuwa siuelewi, lakini sasa ninauelewa,” alieleza Rais na kuongeza kwamba, ule muziki wa zamani wa rhumba siusikii sana,” alisema.
    Jambo lingine ambalo analifanya akipata nafasi, alisema ni mazoezi hasa kwa kutembea, na kusema kwamba kukimbia hawezi sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...