Home
Unlabelled
gwaride
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Duh hili gwaride linafanyika porini? si ndio mwanzo wa kuliwa na Simba huku?
ReplyDeleteKusema kweli huyu mzee nimemchoka, yaani bado yupo tu. Uzee wote badala ya kutulia nyumbani bado linaqwiba tu!
ReplyDeleteKwenye malumbano ya maana, tafadhali sana tutii nguvu ya hoja; sio hoja ya nguvu na matusi!
ReplyDeleteUfuatao ni upande mwingine wa hoja kuhusu huyo Ngombale-Mwilu:
Mara yangu ya kwanza kumwona Ngombale-Mwilu ilikuwa mwaka 1962 wakati nikiwa sekondari Bwiru, Mwanza. Wanafunzi wa shule za sekondari mjini Mwanza, na mazingira yake, tulitayarishwa kumpokea Rais Sekou Toure wa Guinea alipotembelea Tanganyika.
Wakazi wa Mwanza wengi wasingeweza kumwelewa Rais Toure akizungumza kwa Kifaransa, wakati wa mkutano wa hadhara, hapo Uwanja wa Nyamagana, karibu na Posta.
Rais Nyerere alisimama kutoa hotuba fupi ya kumkaribisha Rais Toure. Rais Toure alikuwa mhutubiaji bingwa na wa haraka haraka. Mkalimani alikuwa huyo huyo Ngombale-Mwilu.
Ngombale-Mwilu blew the minds za umati kwa umahiri wake na spidi ya kufuatilia kile alichokuwa akizungumza Rais Toure, ingawa that was not interpreted instantaneously!
Baadaye, enzi zetu za Mlimani (1967-1970), tulikuwa tunapenda kukutanisha "vichwa" (sijui niseme intellectuals) kutoka TANU, Magazeti ya Chama, Kivukoni College, Mlimani, Vyama vya Ukombozi, na kadhalika, ili vitupige msasa kidogo na kuelezea mambo mengi mengi ya nchini na duniani.
Kutoka TANU na magazeti walikuwa wakina Mapunda (sasa marehemu), Mkapa, na huyo huyo Ngombale-Mwilu. Again, Ngombale-Mwilu always blew our minds!
Wale wanaomjua Ngombale-Mwilu seriously na vizuri, watakubaliana nami kuwa Ngombale ni "kichwa" kinachojua mengi, kisiasa, kiitikadi, kimantiki na kifalsafa. Hicho "kichwa" kimeongoza TANU hadi CCM mpaka sasa!
Serious individuals wenye kutaka ku-discern deeper down kumjua Ngombale-Mwilu, watakubaliana nami ‘mzee” huyu is endowed with rich analytical mind. Ndio maana Ngombale-Mwilu ame-survive toka awamu ya kwanza hadi sasa; and wajao wataendelea ku-seek his invigorating guidance until...
Mwalimu Nyerere alikiheshimu
"kichwa" cha Ngombale-Mwilu!
Wenye “kumchoka” Ngombale-Mwilu wanayo haki ya kudai hivyo. Lakini the mere ujana is never a panacea to all Tanzanian ills.
Sometimes playing ones part in national building is never ujana-determined; it transcends chronological age. Tusiwatupe ovyo wazee wenye busara kwa sababu ya chronological age. La sivyo, tutakuwa walilia vipya, kama watoto wadogo ambao the utility za toys zao ni transient: Baba/Mama, ninunulie puto mpya!
Ninapendekeza mbele ya vijana waendao shule (hasa vyuo vikuu na wanaochukua mafunzo ya siasa - digrii za masters au doctorates), kufanya utafiti wa thesis au dissertations kuhusu viongozi wetu wa siasa, kwa mfano, wakina Rashid Mfaume Kawawa, Ngombale-Mwilu, au Maspika wa Bunge.
Ahasante Born again pagan
ReplyDeletekwa kutupatia dodoso ya Kingunge. Mie binafsi sijawahi kuelewa kwa nini huyu jamaa amekaa sana kwenye siasa.
lakini kila nchi huwa inahitaji mawazo mapya-kwa hiyo huyu Kingunge,Kawawa,Malecele etc nafikiri muda wao umepitwa na wakati.
Ahsante sana Born Again Pagan kwa maelezo yako. Nina hakika wengine tujifunze jinsi gani tunaweza kuongea kwa kutoa reference au kuegemea kwenye ushahidi hasa. Mimi binafsi huyu mzee ninamkubali, hunivutia sana anapoongea hususan kama ikiwa anajenga hoja, si mbishani wa hovyo bali ni mtu mpenda kuchukulia mambo kwa subira kubwa sana, anauvumilivu katika usikivu na mpenda kuelimisha sana. Si vyema tukawaponda wazee au hata watu wengine bila ya sababu za msingi. Hebu fikiria wazee wote wangeondolewa katika kufanya shughuli za leo wakaachiwa vijana nini kingetokea? Je, mnakumbukumbu ya yule mzee wa Ilala (Mzee Kitambi) aliye hitimu juzijuzi degree yake kutoka chuo kikuu huria? Kuna vijana wangapi ambao wameshindwa kufanya hivyo? Tuwaenzi wazee wetu, tutumie fursa hii kujifunza kwao halafu na sisi tufundishe watoto wetu. Wazee hongereni, hongera Born Again Pagan!
ReplyDeleteTatizo la vijana wanapenda sana kuzarau wazee.Usimzarahu mzee hata siku moja.Nanimeona watu wengi waopiga "tararira" hapa shule haijapanda.SHULE NZURI SANA JAMANI, ITATO TONGO TONGO ULIZOKUWA NAZO ZA UMASIKINI WA FIKIRA.Thanks born Again Pagan kwa hoja yako nzuri.
ReplyDeleteHatukatai kwamba Ngombale na wanasiasa wengi tu wa bongo ni VICHWA vya kuaminika. But the fact still stays the same, these guys have been abusing our resources, wameiba hela ili kujinufaisha wao, watoto, vijukuu, vitukuu and the family list goes on while our people are still struggling. Kabla hawajapata vyeo serikalini wanakuwa wazuri [they talk about not taking shit from anyone, they will work hard for the people]. Wakishapata hicho cheo, wanasahau walichokisema and take advantage of their position and don't tell me you have not seen this and if you have not you are BLIND!
ReplyDeleteKuna nini cha kujifunza kutoka kwa hawa wazee wa serikalini. Mimi binafsi sijaona walichokifanya zaidi ya kujaza vitambi vyao na kulala bungeni.
ReplyDeleteKusema kweli pamoja na kuipenda sana nchi yangu, hawa wazee wameiharibu sana nchi. Kila siku wanakuja na schemes mpya za kuiba hela za wananchi from Parking tickets to radar to minerals. Nasikia huyu huyu mzee amepata tender ya mambo ya usafiri [Now this country is just a joke kusema kweli Michuzi].
Mimi bado sijamuona kiongozi ambaye ana uwezo wa kuokoa hii nchi yetu. Kuna mifano ya nchi ambazo zilikuwa maskini huko ASIA sio chini ya miaka kumi iliyopita kupita nchi yetu zinazobadilika kiuchumi haraka sana [wana viongozi wachapakazi, they are doing something for their country and not for GREED] wakati nchi yetu bado imelala, hebu niambie ni miaka mingapi sisi hapa toka tupate mapinduzi au ngoja nipunguze toka Mwinyi atawale nchi [this is a disgrace].
Kazi yetu sasa kumpigia makofi Kikwete katika ziara zake duniani na kila anachosema everyone goes NDIO MZEE. He is another character under the little fingers of these so-called wazee. Kila siku story ni hizo hizo, amebadilisha mawaziri, mara analichukulia hatua tatizo fulani mara amesimamisha miradi iliyochukuliwa na wa South Africa wakati hiyo miradi tena wanapewa hao hao wa South Africa kupitia makampuni yao mengine. Kwa kuongea tu ndo wenyewe, put ur fckn WORDS into ACTION!
Sio kwamba napenda kukandia tu bila sababu bali nina uchungu na nchi ambayo mpaka leo hii the INFRASTRUCTURE + DEVELOPMENT in all departments is still Ffff'd up!
Ndio corruption is everywhere, mpaka huku ughaibuni ma-ministers wanaQWIBA lakini nchi wanajenga. Bongo it's vice versa, wanaqwiba na hawajengi!
Na kabla sijamaliza, Michuzi usipoweka hii comment. Itakuwa mara yangu ya mwisho kutoa comment hapa.
Anonymous hapo juu 12:52:00
ReplyDeleteUmeandika tumesoma na tunaheshimu mawazo yako, Je, unaweza kusema ni jambo gani umeifanyia nchi yako kabla kutupa ushahidi wauliyoyaeleza hapo juu?
Jamani kuna watanzania hamweeleweki. Kama hakuna la kuandika si usome tu halafu uache?Born again amesema vizuri sana na amewafahamisha wengine yale ambayo hawakuyajua. Hapa ni mahali pia wengine wanajifunza mengi. Viongozi wetu wengi wamefanya kazi nzuri tu kwa taifa, nie mnaolia kila siku eti wanaaiba sijui nini nie mmefanya kitu gani kwa taifa? kuna ubaya gani wazee wakiendelea kufundisha vijana ili wao pia wakati wao wafundishe wengine? eti wakati wao umepita! kama bado wana nguvu na wanaweza kufanya kazi hamna cha wakati kupita halafu wafanyeje wakati nie mnaosema ndo wazalendo halisi na ni vijana mmekalilia ulaya eti nyumbani kubaya? angalau wao wamebaki huku hata kama ni kubaya. Kila siku kulinganisha Tz na US au UK, hatukatai watu watoe mawazo yao lkn kuwe na tofauti ya kujadili, kutoa mwazo na sio kudharau kila kitu!Tembeleeni mataifa mengine ya kiafrika maana hao ndoo tunaweza linganisha mtaona tz tuko mbele kwa mengi hasa AMANI.
ReplyDeleteTanzania kuzuri, viongozi wanajitahidi, matatizo yapo kila mahali, tafuteni nchi yakufagilia mimi na tanzania mpaka kufa maana ndoo kwetu!!
Born again pagan,
ReplyDeleteUnaweza kuongea maneno matamu kuwa Kingunge anakichwa kizuri, lakini matendo hayaonyeshi hivyo. Nyerere aliliishi Azimio la Arusha mpaka siku ya kufa na akazikwa nalo. Unataka kusema kuwa Kingunge alikuwa mshauri wa Nyerere katika hilo? Mwinyi alikutana na mawaziri wake Zanzibar, wakalifuta Azimio la Arusha na kuja na Azimio la Zanzibar, ambalo linatajirisha viongozi na marafiki zao. Unataka kusema Kingunge alikuwa mshauri wa Mwinyi kwa hilo? Mkapa akaja na sera ya kuuza mali za umma, pamoja na kuliingiza taifa katika mikataba yenye utata. Makaburu wamepora madini yote bila kulipa kodi kwa mgongo wa utanda wazi. Mpaka Raisi mpya anaangalia uwezekano wa "kunegotiate" upya hiyo mikataba. Unataka kusema Kingunge alikuwa mshauri wa Mkapa? Amekuja Kikwete na ulimbukeni wa kushinda anatembeza bakuli la umasikini dunia nzima akiamini kuwa fedha za mikopo ndio msingi wa maendeleo. Unataka kusema Kingunge anamshauri Kikwete kwa hilo? Born again pagan, tatizo la wazee wetu hawakuandika vitabu ili tusome mawazo yao na kujua wanacho amini au kusimamia. Kila mtu anajua Nyerere alisimamia nini mpaka anakufa kwa sababu aliandika mawazo yake na kuyaweka kwenye vitabu. Misimamo yake ilikuwa haibadiliki kutokana na upepo. Si vibaya mtu kubadilisha msimamo, lakini ni bora watu wakajua ni lini umebadilika na kwa nini umebadilika. Maraisi wetu wanne wanaamini vitu tofauti sana, yaani kutoka Azimio la arusha mpaka "wahisani" na "wajomba", bado mshauri ni yuleyule Kingunge? Labda, wewe anayemjua Kingunge unisaidie, je huyu mzee wetu anaamini nini? sera na itikadi yake ni ipi? ni kitu gani alichoshindwa kufanya baada ya miaka arobaini na kitu madarakani anaweza kukifanikisha katika umri huu?
Wewe anon wa 1:01, acha kuongea pumba eti nchi ina AMANI ndo kitu kilichokaa kichwani mwako wakati maendeleo ni namba ZERO. Yaani serikali imekupumbuwaza namna hiyo, wewe kazi kufikiria nchi yetu ina AMANI (drop some constructive lines in here please).
ReplyDeleteNa wewe Isaac hapa tunaongelea vigogo katika serikali, tunachokifanya bongo sisi is out of the question [FYI tumefanya mengi sana, mengine utakuwa umeyasikia na mengine yanaendelea mpaka sasa hivi]
Mimi bado naendelea na mahojiano hapa: Ngoja nikupe kisa kingine, katika msafara wa Rais UK, alipata kuhojiwa Basil Mramba na Ayub Mzee wa Ben TV. Yaani hayo majibu aliyotoa huyo minister ni kama vile yuko nyumbani anaongea na wajukuu zake yaani ni katuni [you don't expect such answers to come from a minister who was in an entourage that was supposed to promote Tanzania].
Halafu mnasema wamefanya kazi kweli katika nchi hii
Pole sana anon hapo juu. Kwanza kabisa hakuna haja ya lugha kali hapa toa mawazo yako tu. (hunijui kwahiyo huwezi jua yaliko kichwani mwangu na ni mengi sana wala haiwezekani niaandike yote hapa).
ReplyDeleteMaendeleo ni nini kwako? basi labda hujui AMANI ni kiini cha maendeleo. Kama kwako maendeleo ni kufanya biashara basi utafanyaje biashara kama hakuna amani? au utatengenezaje barabara, utajengaje mashule, mahosiptal, nk kama hakuna AMANI?
Mimi nataka sikia mtu hapa aseme mimi fulani nimefanya hili kwa tz sio kudharau kila kitu wengine wafanyapo. Well Tanzania ni yetu wote so kila mtu aitumikie pale anapo weza lkn sio kutwa kuona ya wengine (nyani haoni k*le)
Ungesema maswali aliyo ulizwa waziri na majibu aliyotoa tungejua kama kweli usemayo au tu ndoo hivyo tena "one things he knows everything better than others poor tz kama ndoo hizo points unasema ni za maana kwako basi bado tuko mbali sana. Mungu ibariki tz viongozi na hasa watu wake!
Aurely
Ina elekea huju n
Aurely nakupongeza kwa mchango wako. Hawa watu wanaonalalamika sasa bado na mimi nakazia uzi palepale kwamba watueleze wameifanyia nini Tanzania kwani kila mtu anawajibika kuifanyia kitu nchi hii kwani ni yetu sote. Jamani tuambieni basi na yale mazuri mliyoifanyia nchi hii.
ReplyDeleteWewe Aurely,
ReplyDeleteHivi unaishi ulimwengu gani wewe? Unapomuuliza mtu kaifanyia nini Tanzania una maana gani. Kwa taarifa yako hao unaowauliza wamefanya nini jibu ni kuwa WAMELIPA KODI. Mwananchi wa kawaida hana cha kufanya zaidi ya kulipa kodi na hao waliojidai kuomba uongozi wazitumie kuleta maendeleo. Sasa hawa akina Kingunge na genge lao wanafuja hizi kodi halafu tunaambiwa eti ni vichwa. Vichwa my**
Wamefanyia nini tanzania? Wamelipa kodi eboo!
ReplyDeleteUkitaka mahojiano yaliyofanywa na Ayub, mtafute katika website yake www.swahilidiaries.co.uk
ReplyDeleteWatu wamesema mengi,kuhusu Kingunge na Viongozi wengi waliopita na waliokuwepo madarakani.Mi binafsi naona ukweli upo palepale,hata msemeje nyie manotetea huu uozo wa viongozi wetu nchi ina amani sawa,lakini nchi ni maskini pia????. Mi nahisi nyie manaotetea viongozi hawa mnamahusiano nao,na kwa kifupi mnafaidika na wizi wanaoufanya kwenye maliz za uma,ivo hamuwezi wapinga hata siku moja.Watu wanamsifia Nyerere,kwa mambo mengi,wakati wake nchi ilikuwa na amani,nchi ilikuwa inaongoza kwa kuwa na watu wanaojua kusoma na kuandika katika sub saharani africa,rushwa ilikuwa katika kiwango cha chini kabisa,viongozi walitambua miiko ya uongozi. Sio leo watu hajui hata miiko ya uongozi,wameingia wameuza madini yetu,wamesaini mikataba ya ajabu,inayotuleta matatizo kila siku,nawakiondoka madarakani ni matajiri kuliko hata mwaziri wanaotoka katika nchi zinanozotoa misaada. Ebu angalia nchi kama Ghana,mabazo zilipishana na Tanzania miaka 4,kupata uhuru zikowapi sasa???zimetuacha mbali mno.Halafu mnasema eti sisi tumeifanyia Tanzania,kumbuka hawa watu wameanza kuongoza kupitia wakiwa na umri wa kuanzia miaka 20 kwenda juu,napaka sasa wapo madarakani karibu miaka 40,na hakuna cha maana,Jerry Lawrings wa Ghana ameoongoza kwa miaka mingapi nasasa Ghana ipo wapi???ndio maana tunasema hawana jipya waachie nchi yetu,tuiongoze nasisi. Sanasana wanachofanya ni kuchukua pesa kujenga majumba ya kifahari,kuwaanzishia watoto makampuni ambayo yanapewa tenda za serikali kupitia vifua vya baba zao,nani asiye jua habari za Mkapa na mwanae,nani asiyejua Kingunge na mwanae, nani asiyejua habari za akina Kigoda,na wengine wengi,zote awamu hizi kingunge ni mshauri,je Nyerere angeamua kufanya hivo familia yake ingekuwa wapi,ukizingatia ameongoza kwa miaka 24,acheni kutufanya mazuzu bwana,hamna hoja hapa,hata nchi zilizopitia vita zinamaendeleo kuliko sisi???nyie mnasema wanawunza amani,sasa tunapenda amani,lakini pia na maendeleo,nchi inanuka rushwa,na Kikwete anasema nawajua,eti anawapa muda wajirekebishe.Sisi tuanamachungu sana na nchi yetu kuliko nyie mnafaidi pesa za ndugu zenu wanaoibia nchi,nadhani mnalitambua hilo,na mnajua ipo siku mwisho wenu utafika, na mungu atawaadhibu kwa matendo yenu hata vijukuu vyenu.
ReplyDeleteNachukua nafasi hii kusema nilicho gundua humu ndani kuna vita baridi kati ya watanzania walioko bongo na wa nje ya nchi.
ReplyDeleteNobody is better than the other. Tupende tusipende we make a big family called NATION. THE ROOTS!
Hakuna haja ya kuvunja keyboards kwa kuandika kwa hasira tujadili ka watu wenye busara.
Tuwe na approch nzuri wakati tuna jadili kitu kinacho tu husu sisi wote mfano hapo juu huyo Nyati anaponiuliza naishi dunia gani na wakati tunakutana hapa michuzi haoni kwamba tuko dunia moja?! tena tunaandika kiswahili hehehe lol.
Hay bac nikujibu, zaidi ya kodi kila mtanzania pale alipo awe mwalimu, daktari au nani basi hiyo kazi aiifanye vizuri maana ndoo contribution yake kwa taifa, that is what I ment.
Tuwe na majadiliano constructive lkn kama tu nikuonyeshana vidole hatujafanya kitu.
Leo hata tukibadili viongozi au mm na ww tukipewa madaraka tutaiba tu huo ndoo ugonjwa wa mwaafrika sio mtanzania tu.
Watanzania hatujiamini ndoo ubaya wenyewe, we are capable! tuna wenye "vichwa" kuna mabadiliko positive mengi tu tz ukilinganisha na miaka iliyopita...so "It can be donne we should all play our parts".....Nyerere said!
Aurely
Anon wa 10:16 AM umetoa points nzuri sana, maelezo yako yanafaa kupewa hiyo tuzo ya Michuzi. Na Michuzi asingeharakisha kutoa tuzo wakati maoni yaliyotolewa ni matatu tu, it doesn't work that way [najua Michuzi anamjua huyo jamaa vizuri sana]. Katika kitabu changu, hiyo sio fair play hata kama mimi niko against huyu Ngombale.
ReplyDeleteUlichosema hapo ni 100% UKWELI MTUPU mpaka baadhi ya watoto wa hao vigogo wamekubali lakini hawawezi ku-betray wazazi wao.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteHuyu Isaac-Us, ni memba ambaye mawazo yake ni ya kitoto hana point, ingekuwa tanzania bado ipo chini ya wakoloni angekuwa bado anawashabikia wakoloni, akili yake ni ya mtoto miaka 12
ReplyDeleteJamani hapa ni Masiwani Tanga nini?Nakumbuka wakati huo Ngombale alikuwa Mkuu wa Mkoa.Yaani ilikuwa ni gwaride na halaiki mtindo mmoja!!
ReplyDeleteNatumaini watoto wa sasa wanasoma zaidi kuliko kwenda kwenye gwaride na halaiki,maana hata hao waChina wenyewe yanawashinda sasa!!
Hapo juu kuna wale wanaojidanganya na kuona kuwa viongozi wetu hawastahili kukosolewa na kuwa kila kitu kinakwenda vyema.Halafu kina wale wasiojidanganya wanaoona mambo yalivyo Bongo na kuwa upo umuhimu wa kukosoa uongozi wa baadhi ya viongozi wetu.
ReplyDeleteWale wanaokosoa wanafanya hivyo kwa ajili ya upendo na uchungu kwa nchi yetu,ni sio kwa ajili ya kashfa au dharau.
Ni heri tukosoe mambo ya nchi yetu sisi wenyewe kuliko kusikia wageni wakikosoa.