siku mjomba'angu akimalizia kujenga rosheni yake hii kule kibiti nitawaalika kwenye ufunguzi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hiyo ghorofa kali sana, hapo simba ataishia kunusa tu chini, jamaa wanakula mbafu ghorofani. Misupu mpe hai sana huyo anko wako "injinia" wa maghorofa.

    ReplyDelete
  2. 20% analo kali kushinda hili la anko wako,lake kalijengea huko Kimanzichana. expaya deti yake inakuwa siku mchwa wakimaliza kula miti yote iliyotumika kujengea

    ReplyDelete
  3. Hii ndiyo nyumba ya BILL GATE wa kibiti.Magorofa hayako new york au Nairobi tu.Tanzania hadi vijijini yako na ghorofa kama hii gharama yake kuanzia vifaa hadi labor charge haizidi dola 200.Ubahili tu watanzania wengi unawasumbua wangeweza kujenga magorofa kibao vijijini.

    ReplyDelete
  4. Mmmmhhh... Hilo ghorofa kweli lina "structural integrity"? Injinia alihusika? Humo mimi siingii hata kwa dawa.

    Lakini nawatakia "good luck" wakazi wa hapo wakae salama bila kuporomoka.

    ReplyDelete
  5. hawajamloga lakini?manake kuwa na rishen namna hii si mchezo

    ReplyDelete
  6. Jamani tuache utani..Hii ndo halisi halisi ya kwetu!! HIMA HIMA TUONDOKE TUKASIDIE kwetu..Jamani Kweli JK ana kazi..wote hawa ni wapiga kura wake! Imagine!!!! Jamani safari bado ipo!!!!

    ReplyDelete
  7. wachaga bwana kwa sifa! basi tu ili watu wamsifie ana ghorofa. "aisee babangu mi najenga ghorofa halafu unanletea mchezo ntakutoa roho, usilete mchezo na hela yangu..."

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa kujenga bila kupoteza muda kusubiri wataalamu wa ujenzi waliojazana mijini na ulaya na marekani ambao hawataki kwenda vijijini kushauri wanavijiji juu ya ujenzi wa nyumba bora.

    Ikikuangukia hiyo ghorofa wanasiasa na wataalamu ujenzi watakutukana kuwa ulijenga nyumba mbovu bila ushauri wa kitaalamu wa wataalamu ambao hawakuwepo na wala hawana mpango wa kuja kukuona kukushauri kabla na wakati wa kujenga.

    Namkumbuka Nyerere aliyejali watu aliawahi kusema "Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote kwa faida ya wote" Sasa hivi watu wengi wanajielimisha sana kwa faida yao binafsi hawana mpango wa kuwasaidia wengine kama mwanakijiji huyu mwenye ghorofa ya udongo.

    Wasomi wa fani za ujenzi wako tayari hata kubaki marekani na ulaya wakijitwika mabox na wasomi wa ujenzi Tanzania wako tayari kuanzisha viosk vya juice na maduka ya kuuza mitumba au unga wa mahindi kilo moja moja kuliko kurudi vijijini kusaidia watu kama huyu mwanakijiji katika ujenzi wa nyumba bora.

    Elimu ya ulaya,marekani na vyuo vikuu vya Afrika ni kama upuuzi mtupu mbele ya mwanakijiji maana haigusi maisha ya kila siku ya asilimia 80 ya watu waishio vijijini.Watu waishio vijijini bado kujua hasa kazi ya mtu aliyesoma ni nini hasa katika maendeleo ya watu wa vijijini.

    Mfano kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa maendeleo ya Tanzania kimeshikiliwa na kuendeshwa na watu ambao elimu yao ya juu ni darasa la saba nchini Tanzania.Hao ndio wanaoendesha uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii.

    Nyerere aliwahi kusema kilimo cha nchi hii kitabadilika pale wasomi watakapojitosa katika kilimo.Bila wasomi kujitosa kwenye kilimo.Tutapiga kelele za kukuza kilimo na itakuwa ni kama kumpigia gita mbuzi.Wahindi wanatuzidi kwenye biashara sababu wengi wao wasomi,Kenya wametuzidi upande wa kilimo na biashara sababu wasomi wao wengi wako kwenye sekta ya biashara na kilimo.Hapa kwetu wasomi wako tele serikalini na mashirika ya umma.Tuna maofisa biashara na kilimo wasomi wengi.Wakati hatuna wafanyabiashara na wakulima wasomi wengi.

    Tanzania haihitaji maofisa kilimo wengi wasomi inahitaji wakulima wasomi wengi ndipo tutakapo jikwamua kilimo duni.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...