
mkuu wa shule ya sekondari ya makongo ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la michezo afande iddi kipingu akiwa na rais wa global scouting bureau james gamble na wachezaji nyota wa zamani uingereza hivi majuzi. afande kipingu anasifika kwa kuvumbua, kukuza na kulea vipaji vingi vya soka nchini na sasa kwa kushirikiana na gsb ameanzisha akademi ya soka kule makongo.
Hahah. Michuzi thanks kwa kupost Picha ya HeadMaster wangu(KIPINGU). Its been Long time.
ReplyDeleteKumbe Kipingu ni mshamba tuu kama wewe Michuzi. Milebo mikubwaaaaaaaa.
ReplyDeleteWith this trend you people need a serious intervention.
ama kweli bongo hakuna anayelala njaa
ReplyDeleteYaani Msafiri kupigwa bomba Canada na sasa hivi kashapata mchongo mwingine na nasikia hata huo uislam kaucha kwa mbwebwe
safi sana
hayo ndiyo mambo ngugu yangu
mwendo mdundo tuuu
Mimi kama mpenda michezo mahiri, nawashukuru sana Jack Pemba na bosi wake kwa kuamua kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi na kuwafungulia milango ya uwezekano wa kucheza katika za Ulaya nagharibi ambapo viwango vya mcheo huu huu wa mpira wa miguu viko juu sana.
ReplyDeleteIla kuna kitu ambacho watanzania na hasa wanahabari (vyombo vya habari) mnapaswa kuvifanyia kazi. Msione kwa kuwa wachezaji nyota wa zamani wameletwa Tanzania basi kila mwananchi anawaamini hawa jamaa, hii ni kazi rahisi sana kufanya ukiwa uko ulaya na kwenye charity organisations ambazo zinashughulikia michezo.
USHAURI WANGU KWA WANAHABARI:
Fanyeni mahojiano na uchunguzi wa kina kuhusu shughuli za hawa jamaa huko Uingereza na kujua chanzo cha fedha zao. Mimi siamini kwamba Jack Pemba ambaye anakaa Tanzania karibu muda wake wote analipwa kwa kazi ambayo mie hata siioni, wakati kuna vipaji kibao viko africa magharibi ambavyo ni ready made na wangechukua kwa jina la kampuni yao na kutengeneza hela nyingi (they seem too good to be true. Pia waseme au watoe majina ya wachezaji wa kutoka nchi nyingine ambao tayari kampuni yao (GSB) imeshawapatia mikataba na timu kubwa za ulaya magharibi. Nisingependa kuingilia tabia binafsi za watu, lakini watu wanao mjua ndugu yetu Jack wanaweza kukubaliana na mimi kwamba kama ni uongo na majisifa atakua ameacha basi ni jana, hivyo ukweli halisi sidhani kama unajulikana, isije kuwa kama mambo ya Kajumulo hapa.
Waandishi wa habari wetu ni lazima muwe investigative na msikubali vitu hivi hivi tu (accept things at face value).
Kama kuna mwana habari ambaye kweli yuko makini na jambo hili, mie naweza kutoa msaada wa kufanya utafiti wa mambo fulani fulani kuhusu hawa watu na hasa vyanzo vyao vya pesa mpaka wakaamua kukuza vipaji Tanzania.
Wasiliana nami kwenye immigrscando@yahoo.com