kp akila rhumba....




wadau kunradhi. kuna mdau anaitwa steve bonzy kanitumia hii sasa hivi. nawasilisha..


Ndugu Michuzi,
Mimi ni mpenzi sana wa blog yako na haipiti siku pasipo kupitia blog yako zaidi ya mara moja.

Kinachonishangaza na kunisikitisha ni lugha unayoitumia ambayo kwa mtazamo wangu ni ya kihuni na inayopotosha. Nimekuta UK ikigeuzwa ukerewe na maneno chungu mbovu ambayo kamwe hayaendani na aiba na busara yako.

Ningependa kukumbusha tu kwamba blog yako inasomwa na watu wa rika mbalimbali na wenye nia ya kupata habari za nyumbani kadhalika kujifunza lugha yetu. Lugha unayoitumia ni miongoni mwa ujumbe unaoambatana na picha zako. Hivyo basi, tunakuomba utumie lugha ambayo (a) inaeleweka na wote (b) lugha inayotunza maadili yetu (b) lugha inayoelimisha badala ya ile inayokifukia kiswahili kwenye lugha nyingine.

Hitimisho: Tunataka tukuone wewe kwenye picha na lugha....kwa hali ilivyosasa, wewe unaonekana kwenye picha tu,,,,anayeonekana kwenye lugha ni muhuni.

Kazi mzuri Ndugu Michuzi, endeleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ewe mheshimiwa naomba niseme yafuatayo - blogsite ya Michuzi ni yake binafsi na kama blogsite zilivyo ni mwente kuimiliki anayeamua mtindo wa blog yake utakavyokuwa.Hapa ni kama kijiweni tu sema uzuru wa kijiwe hiki ni kwamba kiawakutanisha watu duniani kote kubadilishana mawazo.Lugha ya Michuzi haina uhuni wowote zaidi ya watu kudhani tu kwamba lugha ya mtaani huwa haiandikwi,kama si lugha chafu ubaya uko wapi?
    Ukiangalia hata picha anazoziweka nyingine ni za matukio ya kufurahisha na kuchekesha kama lugha yenyewe ilivyo na wengi tunapenda style hii ya lugha na picha.
    Mtu atakayekuja kwenye blog hii kwa nia ya kujifunza lugha ya kiswahili atakuwa anaumia tu mwenyewe kwa sababu hata wewe unajua kuwa Kiswahili sanifu hakifundishwi kijiweni.
    In other words this blogsite is entirely slang-oriented because in its nature it's not an official website.You've got to have a certain depth of linguistic flexibility to enjoy this blogsite Sir!

    ReplyDelete
  2. Ok, kwa namna moja namuelewa huyu jamaa kwa kuwa watu wa rika tofauti wanatazama blog yako bwana michuzi na si wote wanaweza kuelewa maana yake, LAKINI pia hatutaki kuona tu picha bila funny descriptions, which we also enjoy very much!! Mimi nina miaka 60 lakini ninasoma descriptions zako za picha kama 'Ukerewe', na hata kama sizielewi maana yake papo hapo, zinaeleweka baada ya muda mfupi tu. Kwa hiyo Michuzi ningeshauri uendelee hivyo hivyo, otherwise picha tu pekee yake bila descpriptions zako tulizozoea za kuchekesha zitafanya blog yako ianze kutuboa...... Na wengi wa watu hawajawa na tatizo nazo.

    ReplyDelete
  3. hey hivi nyiyi watu sometimes mna matatizo wee anzisha globu yako ya kufundisha maadili au lugha.Hii ni yake michuzi so watever yeye anataka kuandika ni yake kama unaona ya kihuni usiingie basi kwani lazima wee nani kwani???

    ReplyDelete
  4. blogging ni mchezo na mchezo ni sanaa.hii ni lugha ya sanaa ambayo sioni uhuni wake.lugha inakuwa ndio maana hata ofisini kwa Tony Blair kunaitwa no.10,kwenye hii blog ukiona ukerewe elewa ni UK.ukishindwa kuelewa uliza,wadau watakujibu.lazima tutambue kuwa michuzi halipwi na mtu kublog anafanya kwa sababu anaenjoy kublog sasa tukimlimit bila sababu za msingi hataenjoy na sisi tutakuwa hatuko fair.

    ReplyDelete
  5. Ndugu Steve,
    Tumesikia malalamiko yako. Mimi kama msomaji wa blogu hii kila siku, ninajibu malalamiko yako kama ifuatavyo.

    1. Blogu hii inawapa watu wanachotaka, ni vigumu kuzuia maneno yanayotumika humu kwanindio utandawazi huo. Lugha inayotumika siyo ya kihuni ni lugha ya kisasa na ndio inayofanya blogu iwe na muojo tofauti. Kama kuna watu wanasoma kwa kujifunza Kiswahili, mimi ninafikiri hapa sio mahali pake ni vyema ungewashauri watafute shule ya Kiswahili au sehemu nyingine ambayo watajikifunza zaidi. Nafikiri asilimilia kubwa ya wanablogu hii watakubaliana na mimi
    2. Suala la sehemu kama Uk kuitwa Ukerewe mimi sio tatizo kubwa. Kwani asilimia kubwa ya wanablogu wanaelewa kinasemwa nini. Nafikiri Michuzi ana busara si kama unavyofikiria. Nionavyo mimi amejaribu kulinganisha baadhi ya majina(Herufi)au madhari ya miji yetu Tanzania na kuipa majina ya miji mikubwa mingine duniani.
    3. Suala la kuelimisha nafikiri katika blogu hii hakuna, nionavyo mimi michuzi anatukumbusha matukio ambayo yaliyotokea au yanayotokea nyumbani na kutupa nafasi ya kutoa maoni. Kama ujuavyo kila mtu ana kichwa chake hivyo sidhani kama michuzi anaweza kulizuia sana hili.
    4. Suala la maadili ni kweli ninakubaliana na wewe. Ni vizuri sisi wanblogu tusitumie matusi au lugha ya kukashifu mtu katika kutoa maoni. Ninafikiri sisi wanablogu tutumie NGUVU YA HOJA ZAIDI NA WASI SI HOJA YA NGUVU. Ni vyema tukumbuke kuwa kila mtu anasitahili kuheshimiwa. Tusipende kuhukumu wakati hatujui upande mwingine wa shillingi.

    Mwisho ningependa ufahamu kuwa Dunia ya sasa imebadilika hasa kipindi hiki cha utandawazi, dunia sasa ni kijiji kimoja. Na ukumbuke kuwa “Penye wengi pana mengi”

    Wasalaamu
    KITCO

    ReplyDelete
  6. Mwambie kama kijiwe kinamshinda atafute pale dukani kwa mchagga wanakijiwe chao nao. Hapa ni kijweni the only difference is that kijiwe hiki kiko high tech.

    ReplyDelete
  7. Achana na huyo mmbwiga, kakimbia kwao siku nyingi hata lugha haelewi tena. Si unaona kaandika "aiba" badala ya "Haiba" kajilipua huyo msameheni bure.

    ReplyDelete
  8. Humu sijaona tatizo lolote kwenye lugha, kwa sababu hapa sio shule. maneno kama (barabara ya Mandela road) hii kwa kitaalamu inaitwa repetition wataalamu wa mashairi wanaijua vizuri zaidi. UK kuitwa ukerewe ni sawatu, mfano Tanga (kunani) Zanzibar (zenji)morogoro (mji kasoro bahari)Tabora (tabu bora) Tanzania (bongo) ndege (pipa)n.k Michuzi endelea kutupa vitu

    ReplyDelete
  9. Kakam michusi anatumia lugha mbofu mbofu na anapata wateja basi hiyo yuko creative.To fetch people`s atention these days is not that easy my friend ndiyo maana michusi kaja na style yake ya peke yake.Wazee wa Boston juzi mlisikia sakata la Turner right?Kufikisha ujumbe kwa watu wengi sio kitu rahisi jamani.Muchusi mi naona amewafetch ile mbaya,we kama hapa unaona hapakufai katafute sehemu inayoendana na what you you won maadili ga damet.

    ReplyDelete
  10. halooooo....pele limepata mwenye kucha....mzee steve eeee!!! mi nadhani hauko sawa japo lalamoko lako ni la msingi

    ......mi nadhani hii kuandika ukerewe ni kama style ya michuzi aliyoichagua kufanya ni moja ya kivutio katika hii blog zaidi ya picha sababu kuna picha inaweza isikuguse na usione kwanini michuzi kaiweka, baada ya kusoma alivyoielezea ukapata hata cha kuchangia.

    ......unajua kwanini nakwambia lalamiko lako ni la msingi....kama kaka michuzi anakumbuka mie mwenyewe nilishamwambia kuwa mwanzoni alikuwa ananipa taabu sana na lugha aliyotumia kama kuita uk = ukerewe.... dada aliyeolewa kuitwa my wife...lakini baada ya kuendelea kuzuru kijiweni nilimuelewa na naenjoy kichiziiii.

    Kuhusiana na wewe kutaka kujifunza lugha kupitia hapa itakuwa ngumu....nadhan ndo maana kuna ippmedia,majira, mwanachi nk...kule utaweza jifunza maneno kibao ya kiswahili fasaha.....darhotwire.....mh!! nadhan ndo hao hao kina michuzi coz wana hadi slang za mtaani...huko usiguse kabisa kama hapa panakubore

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  11. du HIYO MI INSHA KAMA MMETUMWA???

    ReplyDelete
  12. Hata mimi sikubaliani na huyu mdau kama wengine walivyoeleza hapo juu.

    Kutumia "lugha ya kihuni" ni moja ya staili na vivutio vya hii blogu.
    Inaleta ladha ya aina yake na kuwafurahisha wasomaji.

    Kwa hiyo ningeshauri michuzi aendelee hivyo hivyo kwa kadri anavyoona inafaa.

    ReplyDelete
  13. Kaka Issa,
    Bila shaka umeyapata ya wadau wako endeleza makamuzi. Huyo Steve kila siku yeye ni kulalamika lugha lugha tu halafu iweje. Na wewe zeze acha kutuzingua hapa ati lalamiko lake la msingi wakati huko dahotiwaya ndiyo lugha inayotumika, sasa wewe ilikuwaje tena upate taabu na lugha ambayo ndiyo mwanzilishi wake

    ReplyDelete
  14. Hapa siyo darasa la kiswahili sanifu tafadhali!! mwishowe mtahoji hata hata hiyo sentensi kwenye katuni "anakula rhumba" kuwa ni ya kihuni, sijui KP angeandika "anacheza muziki", which is boring na haina ladha, mahanjubati kwenye lugha muhimu bwana!

    ReplyDelete
  15. Wenye kupenda lugha chafu ndio manapandisha idadi ya kufungua ukurasa wa blog hii. Ni aslai kwa Michuzi ambaye sasa anajivuna kuwa kuna blog karibu itafunguliwa ,ara milioni moja!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 03, 2008

    Baba Michuzi, kanyaga twende mwanangu!! Mambo ndo kama hivyo, ukileta za busara kivile anavyotaka Steve, mtabaki wawili tu. Hebu firikira 'demu bomba kinoma' inandikwe 'msichana mzuri sana'! Hahahahaaa hapa hasomi mtu, utabaki peke yako. Ila unachoniboa ni pala unapoita UK ni Ukerewe wakati UK ni Ukinga yaani Makete kule wanakotokea mabilionea wengi kuliko sehemu yoyote bongo! Habari ndo hiyo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...