NAOMBA IDHINI YENU WADAU NITANGAZE RASMI KWAMBA HATIMAYE NIMEFIKISHA WAGENI MILIONI MOJA (SASA NA USHEE. SIKUWEZA KUSHUHUDIA HUYO MGENI WA MILIONI MOJA KWANI NILIKUWA SEHEMU AMBAYO MTANDAO NI NOTI RICHEBO) NA NAMSHUKURU MDAU DK. GERALD MISINZO WA UBELGIJI AMBAYE AMENITHIBITISHIA KUWA YEYE NDO ALIKUWA MGENI HUYO WA MILIONI MOJA. NAAMUA KUMPA ZAWADI YA PICHA AITAKAYO INGAWA HII HAIKUWA SHINDANO. PICHANI NI POSTI YA MILIONI MOJA ALONITUMIA KUWEKA MAMBO SAWA.
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KWA MARA INGINE KUWASHUKURU WADAU WOTE MNAONITEMBELEA NA KUAHIDI KWAMBA NITAJITAHIDI KWA KADRI YA UWEZO WANGO KUENDELEZA HILI LIBENEKE. ASANTENI SANA, MUNGU AWAJAALIE...

HAPA CHINI KUNA UJUMBE WA MDAU DK. MISINZO WA UBELGIJI ALIYEIBUKA MGENI WANGU WA MILIONI MOJA KAMILI. NAMPONGEZA NA KUMSHUKURU SANA SANA KWA USHIRIKIANO WAKE. NAMWOMBA PIA DAKTARI HUYU ASEME PICHA GANI AITAKAYO NA KAMA NIIWEKE HUMU AMA NIMTUMIE BINAFSI, KWANGU VYOTE SAWA....


Michuzi,
Mie ndo nilikuwa visitor wako wa milioni moja. Nakuambatanishia file 'MillioniMoja.jpg' ambayo ni picha toka kwa file 'OneMillion.pdf'. Hili file 'OneMillion.pdf' nilisave blog yako ilivyokua inaonekana muda huo.
Nawasilisha.


BE WA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. ...first of all i would like to thank cynthia masasi, she contributed about 10% of that...

    ReplyDelete
  2. We michuzi!...huyo mdau wa milioni moja yuko Ubelgiji!!

    ReplyDelete
  3. Dr. Misinzo wasalimie Ubeligiji

    ReplyDelete
  4. HONGERA MHESHIMIWA MICHUZI.
    ILA NAOMBA NISHAURI KAMA NIONAVYO MARA KWA MARA WADAU WANALALAMIKA KUWA HUTOI MAONI YAO, UNACHAGUA.
    TAFADHALI KUWA KAMA KWELI WA KIMATAIFA, KAMA NCHI ZA WENZETU, TOA MAONI KAMA YALIVYO, ILA TU PANAPO NA LUGHA CHAFU AU MATUSI HAYO MAONI BASI NI HAKI USIYATOE. LAKINI VINGINEVYO, NDIO MAANA YA HIZI BLOG WATU WANAJITOKEZA NA TAARIFA MBALI MBALI, AMBAZO ZINAFUNGUA WATU MACHO, NA TUNAJIFUNZA MENGI. NA SIO KAMA UNAOGOPA, KWANI HUWEZILAUMIWA WEWE, SIO WEWE UNAYEANDIKA MAONI.
    HUU NI USHAURI WANGU TU.
    AHSANTE, NA HONGERA MHESHIMIWA, KUFIKIA MILIONI SIO MCHEZO.

    ReplyDelete
  5. Michuzi,

    Hongera kwa kufikia Milestone ya one million visitors! Ukifikisha two million lazima ufanye Party!

    ReplyDelete
  6. Hongera Kaka Michuzi......Juhudi zako zinaonekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...