mdau wa blogu za picha maggid mjengwa akila pozi na katibu mkuu wa ccm mgosi makamba huko iringa majuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nakushukuru sana Michuzi kwa kutuwekea picha ya Mzee Makamba.
    last week, JK aliwaasa viongozi wetu kukubali kukosolewa au kuambiwa ukweli kuhusu utendaji wao. kwani kwa kufanya hivyo, JK anaamini kwamba kutaboresha utendaji na uwajibika kwa hawa waheshimiwa na kwa serikali yake kwa ujumla. Ni jambo zuri likitekelezwa na ifahamike wakosoaji wenyewe ni sisi wananchi na si viongozi wenyewe.

    Mimi naomba nianzishe mjadala kuhusu huyu mzee makamba.Na nitazungumzia utendaji wake kipindi alichukua Mkuu wa Mkoa wa Dar, na sio nafasi yake ya sasa kwani sina mengi ya kuzungumzia kuhusu ukatibu mkuu wake.

    Kwangu mimi Mzee Makamba (alipokuwa RC wa Dar) alikuwa ni mtu wa kelele nyingi mbele ya vyombo vya habari au anapoongozana na viongozi wa juu yake. Matendo yake yalikuwa ni katika kulinda heshima yake ni si katika kutekeleza majukumua au kuhudumia wananchi.
    Yeye mwenyewe Alianzisha mambo mengi ambayo alishindwa kuyatekeleza. Swala wa machinga alilizungumzia sana, little was done. huduma mbovu za afya alizungumzia sana, again little was done than said. Uchakavu wa barabara, hapa ndio tulishuhudia kandarasi bomu zikipewa kazi na barabara kuanza kuharibika kabla hata ya kukamilika kwa ujenzi.

    kwa kifupi Mzee huyu alikuwa ni mtu wa kupiga sana domo na utendaji mchache. A typicall nature ya watu wa pwani (hata wakwere nao wanaweza kuingia humu pia kama hawabadiliki).

    Wadau wenzangu mnasemaje kuhusu hili?

    ni mtizamo tu na ni haki yenu kuichambua kauli yangu au kuuchambua tendaji wa Mhe Makamba alipokuwa RC wa Dar.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana kabisa na uwepo wa mjadala kuhusu Makamba.Mimi nina mashaka sana na JK kama yuko serious kama tunavyodhani. Kumteua mtu wa porojo kama Makamba kuwa SG wa chama kikongwe na kilichopoteza mwelekeo kama CCM ktk dunia ya sasa ni maajabu makubwa. DSM aliishindwa akabaki kujipendekeza kwa kila mkubwa aliyepita karibu yake mpaka ikawa AIBU. Kifupi DSM hakuwa RC bali msaani na ameongeza matatizo badala ya kuyaondoa kama alivyopaswa kufanya kwa madaraka aliyokuwa amepewa.

    ReplyDelete
  3. Anahitaji tiba haraka afya yake si nzuri atumie hayo madaraka aende nje kutibiwa hiyo sukari,sijui presha na sasa naona ana nundu kichwani...sijui tumor ile au?

    ReplyDelete
  4. nadhan tungeanza na elimu yake kisha tukaenda mbele baada ya hapo au mnasemaje mlioanzisha mjadla?

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani Mheshimiwa hajafanya makosa kumuweka Makamba kwa sababu na yeye ni mtu wa polojo sana kuliko utendaji, kwa hiyo angemuweka mtu wa kazi angefunikwa kama yule Jamaa wa Burundi aliyefunikwa na katibu pia siasa za Hapa kwetu Bongo ni polojo tu na wananchi tumeishazoea hivyo kama mtu hajatupigia porojo hatumchagui. Hapo kwa kweli CCM nawakubali na itachukua muda sana kubadilisha wananchi,

    ReplyDelete
  6. Mimi nadhani Mheshimiwa hajafanya makosa kumuweka Makamba kwa sababu na yeye ni mtu wa polojo sana kuliko utendaji, kwa hiyo angemuweka mtu wa kazi angefunikwa kama yule Jamaa wa Burundi aliyefunikwa na katibu pia siasa za Hapa kwetu Bongo ni polojo tu na wananchi tumeishazoea hivyo kama mtu hajatupigia porojo hatumchagui. Hapo kwa kweli CCM nawakubali na itachukua muda sana kubadilisha wananchi,

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  8. Nilijua Michuzi hutoweka ile comment yangu juu ya ungozi wa juu wa nchi yetu. Sikutukana wala kutumia lugha chafu. Nilisema ukweli na kwakuwa Watanzania tunaogopa kusema ukweli na kuishia kusifiana kijinga ndio maana tunakuwa duni. Kujipendekeza tu....

    Comments za webgine hadi matusi yapo lakini kwa kuwa hazimlengi Rais na mawaziri wake unaziruhusu tu. Acha hizo Michuzi. Tunaposema kweli juu ya uoza wa nchi yetu tunataka habari ziwafike wahusika wabadilike!

    ReplyDelete
  9. mzee ukitaka siasa kuikosoa ccm ni hapa http://www.jamboforums.com ingia siasa pale

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...