kutokana na maombi ya wengi nimejichovya kwenye kutoa huduma za mtandao nikiwa na wadau wa bombadesigns. mengi utayapaya ukibofya http://www.bombadesigns.com/ na vile vile tunatengeneza mambo mengine mazuri kibao ya harusi kupitia www.harusiyangu.com ambayo ipo kwenye matayarisho na itazinduliwa hivi karibuni www.michuzinet.com itayosheheni habri motomoto na za saa hiyo hiyo kwa picha, maandishi na video nayo iko njiani ingawa bado haijakamilika.

stei tyuund na tunakaribisha maoni, ushauri, kosoo jenzi na vitu vingine kama hivyo. azma ni kuonesha umma kwamba mengi yanawezekana bongo na nyie mlio ughaibuni mkae mkao wa kula kwani majibu ya maswali yenu mengi yatajibika humo...
ILANI: UKIKIONDOA www.bombadesigns.com MITANDAO www.harusiyangu.com NA www.michuzinet.com IKO KWENYE MATENGENEZO NA BADO KUZINDULIWA. HIVYO HITILAFU YOYOTE UTAYOKUTA BAADA YA KUBOFYA INA MAANA HIYO - MAMBO BADO NA YAKIWA TAYARI MUDA SI MREFU UJAO MTAJULISHWA. HII ILIKUWA NI KAMA PASHA MOTO NA KUWAFANYA WADAU MKAE MKAO WA KULA. NAWASHUKURU WADAU WOTE WALIONITUMIA UJUMBE KUNITONYA KUHUSU HITILAFU FULANI KWENYE HIYO MITANDAO. ASANTENI KWA KUNIELEWA NA KUNIVUMILIA KWA MUDA. MAMBO YATAJIPA KARIBUNI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Nampenda Mh. Zitto Kabwe (Mb.)
    Huyu bwana wakati wa kampeni alipata kusema "nimegombea ubunge kwa sababu naupenda na ili niwatetee wananchi"

    Nilitegemea Misupu ungesema ninaanzisha hii tovuti ili nifanye biashara na si kusema watu wamenishauri. Haya mambo ya siasa mpaka kwenye mambo ya binafsi? Kazi kweli2!!!

    ReplyDelete
  2. nimeamini kuwa wewe ni mzee wa liverpool kwa huo uzi ulionitilia.

    ReplyDelete
  3. Baada ya kuvungua links kadhaa katika Harusi yangu nimekutana na ujumbe huu

    :Warning: mysql_pconnect(): User harusi_harusi has already more than 'max_user_connections' active connections in /hsphere/local/home/harusi/harusiyangu.com/Connections/wedding.php on line 9

    Fatal error: User harusi_harusi has already more than 'max_user_connections' active connections in /hsphere/local/home/harusi/harusiyangu.com/Connections/wedding.php on line 9

    Mshtue huyo webmaster

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. NI vyema kuthamini vitu vinavyotutambulisha kuwa sisi ni watanzania. ktk cyber space, ukiona domain ni .tz then unajua hii domain ni toka TZ.
    makampuni mengi(ya nchini na ya kigeni) hivi sasa hapa nyumbani yameanza kuona hili na kuanza kubadili domain names to .co.tz or .or.tz na nyinginezo za .tz

    Naona bado michuzi na team yako mnaendelea kutumia .com domain names.
    Tubadilike na tuenzi .tz domain names. zinatupa utambulisho wa kitanzania.....

    nakumbuka hii ilikuwa hot debate katika forum ya eThinkTank TZ...

    ReplyDelete
  6. Kijana Mugasa na Sausi hongereni sana.Hii inaonyesha ni kiasi gani vijana mlivyo wagunduzi na kujaribu kujikwamua kuliko kutegemea tu mishahara ya waajiri. Kitu harusiyangu kimetulia pamoja na kwamba ndiyo bado kipo kwenye matengenezo. Hii inatoa hamasa kwa vijana kuwa innovative. Michuzi endelea kuchannel vijana kupitia blog yako kwa mambo mazuri kama haya ya ugunduzi.

    Big uuuupp!!
    Mallya EM

    ReplyDelete
  7. Aisee vijana mmetulia, hii idea ni nzuri sana ila nawashauri mpopulate hizo categories with lots of information. I imagine a one stop shop for my wedding, hii itaua vikao vikao hivi ambavyo trend inavyoonesha watu wanakuwa wagumu kuhudhuria. Yani hii safi sana. Ila kweli ndo hivyo kitu kipikwe kiive ndio kiwekwe mezani au sio? Mimi nafagilia sana innovative ideas zinavyotoka home kama hivi. I'm so proud of you guys and I will spread the word.
    So long

    ReplyDelete
  8. Vijana naona mko juu, kazi nzuri, nimeppreciate ubunifu, you make us proud. Yani kama naona vile, harusiyangu ikisimama sasa vikao vya nini, manake siku hizi kuwapata watu mzozo. Safi sana, I cant wait for the whole thing jinsi itakavyokua, ingekuwa bomba sana kama hii kitu ingewekwa mezani ikiwa imeiva.
    Ngoja nibofye bofye nitarudi na ushauri wangu.

    ReplyDelete
  9. ..michuzi ongeza bidii na hii blog yetu ya picha maana ndio ita survive kuliko zote hizo...this blog is like a diamond na asije mtu akakudanganya ...brother keep doing what your doing maana ndio siri ya mafanikio yako ila jaribu kuweka na picha za mikoani kidogo especially kama kuna matukio muhimu huko itafurahisha zaidi...vipi na VIDEO ukiongeza unaonaje?

    ReplyDelete
  10. ...hivi kweli Bother Michuzi umeshindwa kutuwekea kabisa picha za Dar Star search? au ni usanii wako tuu...sasa naanaza kuamini mtu aliyesema una beef na IPP

    ReplyDelete
  11. wadau mimi nilikuwa mtumiaji mzuri tu wa Website ya Harusiyangu.com ila kuanzia jana nashindwa kabisa kuingia ktk hiyo website..nitype www.harusiyangu.com inakuja website nyingine ya mambo ya travel to TZ na kenya sasa sijii tatizo naomba mshitue administrator wa Harusiyangu.com kwa niaba yangu..nashukuru

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...