
nabandika picha hizi za engo tofauti za jengo hili lililopo mtaa wa lumumba jijini dar ambalo lilikuwa kwanza kitivo cha sheria ama darasa la mwanzo kabisa la udsm, kisha elimu ya watu wazima na baadaye makao makuu ya sukita na sasa mna ofisi za wafanyabiashara binafsi.
kwa kusema kweli hali yake ya sasa hairidhishi ikizingatiwa ni jengo la kihistoria katika nyanja ya elimu ya juu bongo. ndani kuna ukumbi mkubwa tu ambao uligeuzwa kuwa duka la bidhaa la sukita, na ambao enzi hizo ulitumika kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na harusi, ndondi na hata mieleka ambapo watu kama kina power mike wa nigeria walikuja kuonesha misuli yao.
hii ni katika kutekeleza ahadi kwa mdau born again pagan ambaye ni mshindi wa tuzo ya maoni bora kwa mwezi huu. samahani born again pagan kwa kuchelewa kukupa zawadi yako kwani nilikuwa nje ya dar kwa muda.
mshindi alipatikana kwa kutoa maoni bora kwa mwezi huu kwenye picha yenye kichwa cha 'gwaride' huko chini.
nakumbusha tena kwamba kuanzia sasa nitakuwa natoa tuzo ya maoni bora kila mwezi ambapo mdau atakayeshinda atapata fursa ya kuomba picha yoyote aitakayo...
Asante sana, Michuzi!
ReplyDeleteMbona nimesikia wataalam wakisema kuwa watu wa ndani ya hizo ofisi inabidi waame na kuwa jengo linafanyiwa ukarabati muda si mrefu? Au?
ReplyDeleteHongera Mzee Mtitu wa QBC- Quality Business Consultant, mtaalam wa maswala ya Clearing and Fowarding. Ndiye aliyefungua kesi mahakama ya kuu ya Biashara Dar, AKIPINGA kwa wateja wote wa bandari ya DAR kuchangia gharama ya SCANNER ambayo TSCAN ilinunua na kufanya ipate ile Tenda.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete