waziri mkuu mh. el akisalimiana na rais jaques chirac wa ufaransa katika mkutano wa siku mbili wa viongozi wakuu wa nchi za afrika na ufaransa ulioanza jijini nice juzi. mh. el alimwakilisha jk katika mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Angalau wadau wakiona kuwa JK aliwakilishwa watapumua maana kelele kelele, kelele, kelele zilishazidi.

    ReplyDelete
  2. mhm, chirac anaongea french, lowassa anaongea kiswahili na kingereza, sasa sijui hapo walikuwa wanaongea nini !!!!

    ReplyDelete
  3. Kingereza ni lugha ya kimataifa,nadhani chirac atakuwa anafahamu kidogo kingereza, kwa hiyo nadhani walikuwa wanaongea kingereza au kama sio kingereza walikuwa wanatumia lugha ambayo wanaifahamu wote vingenevyo tungeona mkarimani pembeni.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. Kwa taarifa yenu, chirac anajua kiingereza. jamani, tufikiri kabla ya kuropoka. Yaani unafikiri kweli viongozi wanaweza kupigwa picha pamoja wakiongea lakini sio lugha ya kuelewana? Ngoja nifikiri kidogo...chirac anaongea kifaransa, lowassa anaongea kiingereza... ahhh....ndio, wanaelewana sana hawa, ndio maana wanapigwa picha pembeni wakiongea. Mawazo mengine ni ya kipumbavu.

    ReplyDelete
  6. Kwani nyie nani kawaambia kuwa Lowassa hapandishi Kifaransa?

    ReplyDelete
  7. Chirac Namjua anaongea kiingereza kibovu.Mswahili akiongea kingereza kibovu mnamzomea na kusema shule haipandi amesomea chini ya miembe. Mbona Chirac hamumzomei? Bali mnampiga picha na kumvunmilia hivyo hivyo na kumtetea kwenye hii.Oh siyo luhga yake.Mimi kiingereza ni lugha yangu ya tatu baada ya kindengereko na kiswahili.Baada ya kunipongeza kuwa najitahidi kuongea kiingereza hata hata kama ni kibovu, mnanizomea.Mnataka nilingane na Tony Blair au George Bush ambaye lugha yake ya kuzaliwa na kusomea ni moja tu kiingereza. Wanga wakubwa nyie wabeba mabox wa UK, USA pamoja na Michuzi wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...