mwandishi wa bbc saidi yakub akiuliza swali kwa jk jana wakati wa mkutano wa rais na wabongo waishio ukerewe. yaliyojiri soma chini
‘MKIJILIPUA’ HAMTAPATA PASI MPYA ZA KUSAFIRIA - JK
Na Maura Mwingira
18/2/2007
London
Rais Jakaya Kikwete amesema, serikali haitakuwa tayari kuwapatia pasi za kusafiria Watanzania ambao kwa makusudi waliamua kuziharibu pasi walizokuwa nazo kwa lengo la kuukata uraia wao na nchi yao .
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi) na jijini London , Uingereza wakati alipokuwa akijibu maswali ya Watanzania wanaoishi na kuendesha shughuli zao nchini hapa.
Rais alilazimika kuyasema hayo, baada ya baaadhi ya Watanzania wenye asili ya Zanzibar kumtaka rais atoe tamko litakalo ruhusu Watanzania hao kupewa pasipoti mpya zitakazowawezesha kupata kibali halali cha kuishi nchini Uingereza.
Wengi wa Wazanzibar hao ambao wamekwama kupata pasi za Tanzania, ni wale waliokimbilia Uingereza kati ya mwaka 1996 na 96, wakaomba hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa kwa kisingizio cha hali mbaya ya kisiasa visiwani Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.
“ Kama kuna anayejiita mkimbizi bila shaka aliingia hapa akiwa na pasipoti ya Tanzania, na kama alipanda ndege hakuna ndege utakayopanda bila kuonyesha pasipoti, sasa nataka nipate ufafanuzi tatizo liko wapi, kama pasi imekwisha muda wake basi si aende tu akaongezewe muda ” akahoji Rais
Na kuongeza “ kama kuna mtu aliyeikana Tanzania akasema nchi gani ile hata kuishi haifai mimi nataka kuishi hapa (London) kama kuna mtu aliichana pasipoti yake, akaiponda Tanzania, ‘akajilipua’ sasa ametubu kwamba amekosa anataka apewe pasi yake ya Tanzania naye atueleze hapa ili na mimi nijue nianzie wapi” .
Rais alisema serikali haiwezi kutoa pasi kwa watu ambao waliamua kuzichana pasi zao kwa kisingizio chochote kile, na hawana karatasi zozote za kuwatambulisha wao ni nani. Na kuongeza kuwa pasi hazitatolewa kwa kutumia kivuli cha pasipoti halisi (photocopy) kwa kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kufanya hivyo.
Alisema kama wanataka pasipoti za Kitanzania basi waende wakachukue pasipoti zao zilizochukuliwa na serikali ya Uingereza ili ziwarahisishie kupata pasi mpya.
Alibainisha kuwa yeye hawezi kutoa tamko lolote la kuwafanya Wazanzibar hao kupata pasi mpya kwa kile alichosema kufanya hivyo ni kujitafutia sifa ambazo hazina maana yoyote kwake.
Alisema kuwa atamshangaa afisa yoyote wa uhamiaji au ubalozi wowote wa Tanzania, atakayempatia mtu pasipoti kwa kutumia kivuli cha pasi yake badala ya pasi yenyewe.
Kwa mujibu wa Wazanzibar hao, wanadai kwamba serikali ya Uingereza ilichukua pasipoti zao na kuwapa nakala na sasa inawataka kuonyesha pasi halali za Kitanzania ili iweze kuwatambua na kuwapatia hati kamili za kuishi nchini humo
Aidha serikali hiyo ya Uingereza ilikataa kuwapa hadhi ya ukimbizi Wazanzibar hao kwa kile ilichodai kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa haki za binadamu nchini Tanzania wala machafuko ya kisiasa kiasi cha kuzalisha wakimbizi. Na badala yake, ilidai kwamba Wazanzibar hao walikuwa wanakimbia hali mbaya ya uchumi, kwa hiyo walikuwa ni wakimbizi wa kiuchumi.
Ni kutoka na wimbi la Wazanzibar hao kukimbilia Uingereza kwa kisingizo cha hali mbaya ya kisiasa, ndipo serikali ya Uingereza ililazimika kuanzisha utaratibu wa viza kwa kila Mtanzania anayeingia Uingereza pamoja na kwamba Tanzania kama mwanachama wa Jumuia ya Madola haikustahili kutozwa viza kuingia nchini humo.
Rais Kikwete ambaye alikutana na Watanzania hao akiwa njiani kuelekea katika nchi za Scandnavia, alibainisha kwamba kila Mtanzania ambaye pasi yake ya kusafiria imemaliza muda wake, anayo haki ya kuongezewa muda, na yule ambaye anahitaji kubadilishiwa pasi yake na kupewa mpya anayo haki ya kupewa hati mpya ilimradi anatimiza masharti yanayohitajika.
Aidha Rais alisema kwa Mtanzania ambaye kwa makusudi kabisa hakwenda kuongeza muda baada ya muda wa pasi yake kumalizika, asikimbilie kuilaumu serikali kwa kuwa ni kosa lake mwenyewe.
Akijibu swali kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na baadhi ya watendaji serikalini, Rais alisema kuwa hakuna mtu mwenye ruksa ya kuondoa maisha ya mtu mwingine, awe katika serikali au nje ya serikali na kwamba atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali yeye ni nani na tayari serikali imekwisha kuanza kuchukua hatua hizo.
Kuhusu suala la ununuzi wa rada ambalo limekuwa gumzo katika vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, Rais alisema kuwa serikali imeiagiza Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) kufanya uchunguzi utakaobaini kama kuna watu wowote ambao walipokea rushwa katika mchakato mzima wa ununuzi wa rada hiyo.
Kuhusu ni lini mazungumzo ya kumaliza mpasuko wa visiwani Zanzibar yatakamilika na endapo maamuzi yatakayotokana na mazungumzo hayo yataheshimiwa na kutekelezwa.
Rais alisema hawezi kusema ni lini mazungumzo hayo ambayo hivi sasa yanaendelea kati ya Makatibu Wakuu wa CCM na CUF yatakwisha kwa kile alichosema kuna tofauti za msingi kati ya CCM na CUF zinazohitajika kufanyiwa kazi.
Kesho Jumatatu Rais Kikwete anaanza ziara yake nchini Sweden, ambako pamoja na mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hiyo.

This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletenashangaa watu wanahangaikia KADI za CCM
ReplyDeleteDawa ni kuwa na British Passport kisha tuone kama kuna kubaguliwa
idadi kubwa ya watanzania walioko Uingereza wanaolilia passport za Tanzania ni kwamba wanatupotezea muda.
ReplyDeletekama waliisaliti Tanzania kwa kukimbilia mikoba ya malikia kwanini sasa wanataka kurudi wakati walijua wazi kufanya hivyo ni kinyume na sheria?
mimi nadhani huo mjadala hauna kichwa wala mkia, waacheni waendelee kuomba visa wanapotaka kwenda katika nchi yao ya zamani - TANZANIA,.
sasa wewe uliona wapi watanzania wana hadhi ya Burundi na Somalia?
haya mambo ya aibu, tena kumwuliza rais kitu kama hicho nadhani ni utovu wa nidhamu.rais ana mambo muhimu ya kufanya jamani, siyo huu upuuzi.
dual-citizenship status, if we agree to legalise it, should only be made available to Tanzanians who have never claimed asylum anywhere in the world, be it Afghanistan or Zanzibar.
dual-citizenship, should be exclusively accorded to persons, who were born in foreign lands where they qualified for nationality, through marriage to other nationals, permanent residence or other non-asylum/refuge claims.
Tanzania kuna amani, ukimbizi umetoka wapi? kama walikimbia vita Tanzania, wabaki huko kwenye amani.
ukweli ni kwamba sisi ndiyo tunasaidia wakimbizi kutoka nchi zote za maziwa makuu.
tunajua hawa ni wakimbizi wa kiuchumi, njaa....siyo siri.lakini waliisaliti Tanzania.hilo ndilo kosa lao, na hawastahili kusamehewa kwa sasa....achana nao na mikoba yao mwekundu.wengine wanaona kama wameongezewa uhai, kumbe ulimbukeni..
WASALITI WA AINA HII KWA NCHI ZA WAJANJA INAKUWA SHUGHULI
Michuzi Huyo Anonymous hapo juu sio Raia
ReplyDeleteCHRISTOPHER COLUMBUS!!!! WAALIKE NAO WAENDE TANZANIA.. KILA SIKU WEWE TUU????
ReplyDeleteWengine huku wanajifanya wakimbizi wa Burundi wakati ni watanzania.Siku mtakayolazimishwa kurudishwa Burundi mtajamba cheche mkitua tu uwanja wa ndege! njaa zenu zitakuja waua.Mtaulizwa kama nyie ni wahutu,watusi au watwa mkijiumauma na kujikanyaga watawajambisha saa hiyohiyo kule hawana kuchekacheka kama Kikwete.Hizo Pasipoti mlizozichana mtazikumbuka na kuzililia kama kobe aliyefiwa na mkwewe.
ReplyDeleteJK umenena hasa. Nadhani umewamaliza wote waliokuwa na janja ya nyani ya kutaka passport kwa kivuli (photocopy) ya pass ya zamani ilihali walizichana passport zao walipokuja hapa UK. Unajua Watanzania, hasa hawa Zanzibari, wametuharibia vitu vingi sana Duniani kwa kisingizio cha ukimbizi. Kila sehemu unakoenda ukiwa huku unaulizwa vipi, hawa Wazanzibari ni akina nani? Mbona wanalalamikia kila kitu kilichopo TZ..?!!. Tunaona hata aibu kujibu hilo shwali.
ReplyDeleteTunashangaa sana sana, tena sana wanapomwambia Raisi kuwa wanataka Passport za TZ wakati waliikataa na kuzichana na mpaka sasa wanajiita Wazinzibari na si Watanzania! Safi sana JK kwa jibu lako. Wakae huku huku, kama waliona kunafaa kuliko kule TZ. Pia wengi wapo pale Canada na US. Tutaendelea kuwaangalia. Mtajiju. BOngo bomba sana siku hizi. Hakuna kubeba ma-box wala kusafisha chombo (house-girls/boys). Akili yako tu.
Anoy wa 5:14am,Kama huna cha kuandika just back-off!!Watu wamepata vilema kwa machafuko ya kisiasa ya wakati ule, sasa wewe kama hukudhurika waache alidhurika waongee.
ReplyDeleteHaiyumkiniki kwa wewe kuwaongelea watu, au kutoa comment zisizo na kichwa wala miguu.Nakushauri nenda kwenye maktaba yeyote ya ofisi za haki za binadamu upate referencss.
We annon hapo juu February 19;2:55 huna jipya. Aliyepata kilema au kujunjika mguu au mkono ni uzembe wake tu. Haikuwa sababu ya kuwa wakimbizi kwa kuvunjwa mkono kutoka na uzembe na kushabikia vitu bila kina. Nyie (wewe) mwenyewe mmeutaka ukimbizi. Kaeni huko huko. Mikono bado inavunjwa, kama ndo ilikuwa sababu yako ya kuondoka. Ukileta za kuleta tu, wanavunja mkono na hata mgongo! Baki huko huko! Wenzako tunafanya kazi na ku-enjoy life bongo. Safi sana bongo.
ReplyDeleteZimewanukia!!! Mkome kuringa...mlisahau kuwa nyumbani ni nyumbani mlipoakuwa mnajilipua eeh? Anacheka sana anayecheka mwisho.....Na hizo British passports mpaka uwe na ya kuikabidhi kwao ili wakupe yao..huku wataka na huku wataka.......
ReplyDeletesiku nyingine mkitoa hoja muwe mnaenda mmejiandaa,mngemchezea rais hii video kumuumbua
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=8vTs4Ue2cPs
Anon Feb 20, 2007 1.;45 usitake kuchukulia hizo picha kwenye youtube kama ndo sababu ya wewe kukimbilia Ughaibuni. Wako wengu tu waliotulia siku hiyo nyumbani na hakuna shida. Waangalie watu wako wanaopigwa. Maneno kibao na ubishi bila sababu. Nawe pia uwe makini. Hii picha ya kwenye youtube si kwamba ndo kielelezo tosha cha kukufanya uwe na point za kumuuliza JK kuhusu kukimbia kwako na kuchana passport (kujilipua). Unaweza kwenda nayo pale usiwe na point na ukajikuta wewe ni mmoja wa wajinga kabisa kuwahi kuwepo Duniani! Hiyo ni propaganda ya chama kimoja cha upinzani ili kutafuta huruma ya kimataifa. Bahati mbaya sana kimebandikwa jina baya la Ugaidi ambalo kwalo kamwe hakiwezi pata nafasi kuongoza Zenj. Ni bahati mbaya sana
ReplyDeletePoleni mliovunjika viuno na miguu kwa ujinga wenu.Wale waliowachochea sasa hivi wanakula kuku na kunywa juice kwa mirija Kwenye vikao vya muafaka na CCM huku wakipokea posho za vikao wakigongeana glass wakati huko mnaendeleza kuburuza viuno na miguu mliyogongwa nondo na marungu ya dola.ogopa rungu mwanangu hasa likitua kwenye kiuno,utaimba kwaya hata kama si mwanakwaya.
ReplyDeletenani anaetaka mapassport yenu hayo ya kijani? mnasagia eti vunjika kiuno pumbaff kabisa.
ReplyDeletewadosi wangapi wana passport za kibongo hawajui hata bongo inafanana vipi nyie ndo mnawasagia wazenji? pass ya kijani laki mbili tu unaipata regardless of your citizenship amkeni wabongo!
We anon February 21 7;46 hapo juu unaonekana hata hujijui wewe ni nani! Nyinyi ndiyo hasa tunaowasema. Mmekimbia kwenda shulehapa, ukazamia huko na kuchana passport. Leo sasa passport ya kijani unajifanya uhitaki! Ukoloni na uzuzu umekumaliza. Kama hawaitaki passport ya kijani kwani basi wanalialia mbele JK? Kimewashinda nini kupata hiyo pass ya kijani kwa hizo laki mbili unazodai? Acha ushamba wako na ukoloni kichwani mwako. kama unaonya vyombo, ruudi biongo. Tutakupa kazi nzuri na kukufnaya ujisikie raha ukiwa kwenu. Wenzako hao waliifanyi kazi nchi yao mpaka ikaendelea, ndiyo sababu na wewe unapata sababu ya kufanyia kazi, kuosha vyombo!Kalaga bao huko huko na ushamba wako. Utawalamba mpaka visigino hao.
ReplyDeleteRespigi Peter Kimboi nakuona umejisheheni hapo mbele...
ReplyDeleteachani ushamba ukimbizi sio zambi watu watafuta maisha kwa njia nyingi watu wamegundu ukimbizi ndio njia yakuishi uko uk sasa acheni kuponda wazungu walikuja kuiba kwetu kwa kusingizia kanisa sasa nawao kusingizia ukimbizi tatizo nini watu wana tafuta maisha acheni ujinga mbona wanawaletea tv majiko na mafridge kwa bei nafu amuoni nawao wanachangia maendeleo?
ReplyDeleteWasioelewa kuhusu kujilipua.
ReplyDeleteRais wenu amewapa ticket ya kuweza kuhifadhiwa huko Ulaya bila ya pingamizi yoyote ile kwa haya maoni aliyoyatoa.
By default any refugee whose government has refused to acknowledge his birth rights, has the right to ask for refugee status in any country under the charters of UN.
Passport is one of the elements that is right by birth. Naturalized citizen ahs the same right, however, his/her rights can be dissolved. But not the one who is Born in that country.
Jakaya K. has given these refugee claimants an opportunity of gaining access and have the revoked hearing proced tothe court of amnesty one more time, only this time with a guarantee of winning the hearing under the commission of UNHCR.
Once Un determines you as refugee, there is no country who is a member of UN can distort, or revoke.
Kwa kifupi Kikwete kawapa Mashua, mshipi, nyavu na watakapo rudi bongo kujawatembelea akina fulani, wako chini ya chatters of human right. Akisimamishwa na askari akitoa gamba lake tu lenye Malkia, basi hapo hapo huyo polisi hana ubavu wa kunyanyasa.
Ahsante kikwete mwenye akili isiyozidi pua yako kwa urahisi usio na mfano.. Michuzi ukiamua usiitia kwenye forum yako futa hii post ya mwisho tu sio yote kaka.
Tunaelewa " Usimuuzi mchinja mbuzi, utajakosa mchuzi"
Anonymous wa Friday 23rd hapo juu umemwaga point nzuri sana. Hao Wazanzibari wanaolilia paspoti za kibongo ni baada ya UK kuwanyima haki ya kikimbizi.
ReplyDeleteWanajulikana kuwa wanatoka Tanzania na kwa Kikwete kuwanyima haki ya kurudi Tanzania ni kuwapa haki ya Stateless individuals na wakirudi ofisi ya nyumbani ya UK wanahaki ya kupewa haki ya kikimbizi maana hii ndo nchi ya kwanza waliyofikia na hawana pa kwenda.
Hapo bongo watarudi tu, kuna wazungu wangapi wamekaa miaka hapo bila paspoti ya Kitanzania?