mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu leo imemhukumu justine kasusura (pichani) kwenda jela miaka 35 baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa dola milioni 2 kwa kutumia nguvu miaka minne ilopita. wenzie wanne akiwemo mwanamke mmoja wote wameachiwa huru. atatumikia miaka 30 na nafasi ya kukata rufaa kapewa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Bila shaka imefikia hukumu baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo.Lakini jambo moja la msingi ambalo tunahitaji kulisemea sasa zaidi kuliko kufungwa kwa Kasusura ni kurudishwa kazini kwa askari waliofukuzwa kazi kwa kuhusishwa na kesi hiyo.Mahakama iliwaona askari hao hawana makosa yoyote katika kujihusisha na kesi hiyo.

    Tunawaomba wanasheria waliobebea nchini kulishikia bango.Ili askari hao warudishwe kazini na kulipwa haki zao.

    ReplyDelete
  2. Duh balaa na hiyo miaka aliyokaa na hii mvua 30 aliyopigwa si balaa lakini sijui mweneywe hizo hela atakuwa amezihifadhi wapi labda baadae akitoka zitamsaidia lakini hiyo mvua 30 hadi aje atoke duh si mchezo nina mpa pole sana.

    ReplyDelete
  3. Anafanana na yule jamaa aliyeshinda oscar mwaka huu !

    ReplyDelete
  4. Wizi sio kitendo kizuri kabisa, ndio maana hata wengine huchukua sheria mkononi. Sasa Kasusura anakwenda kusota ndani miaka 30! kama Mungu atampa maisha ina maana atatoka akiwa na zaidi ya miaka 70. Sasa si anawaletea shida watoto wake tu (kama anao) waliokuwa wanamtegemea. Ila kwa walioachiwa huru, pole zao. Ukiangalia miaka waliyokaa ndani, waliyokuwa wanasumbuka kumbe hawana hatia? Hapo ndipo sheria inatakiwa iangaliwe ili watu kama hao wawe wanafidiwa kwa hasara ambayo wamepata ya kukosa kipato na kudhalilika katika jamii pale wanapoachiwa. Miaka 5 ndani hivi hivi tu? Kwa kweli inauma sana.

    ReplyDelete
  5. duuuuuuuuuuuuu!inamaana jamaa alikuwa man alone kwenye hiyo deal? kweli mahakama yeetu kiboko!

    ReplyDelete
  6. hatimae haki imetendeka dooh! jamaa katesa mtaani i hope atabeba vaseline au ky manake jamaa wanausongo nae kumgeuza. Aminia kasusura!

    ReplyDelete
  7. Kesi ya huyu Jamaa ndio iliibua wimbi jipya la style ya Ujambazi. Ktk tukio lake Kasusura alitumia pesa aliyoiba kutoroka kwa kuhonga Mapolisi waliotaka kumkamata.

    Hapa ndio mapolisi wa kibongo ndio walipoanza kuunda urafiki wa karibu na Majambazi kwa kuwalinda baada ya matukio ya ujambazi.

    Baada ya tukio la kasusura ndio style ya Majambazi kupora CASH MONEY iliibuka kama uyoga na kutamalaki bongo.

    Yawezekana mchezo huu ulikuwa ukifanywa toka awali lakini tukio hili ndio liliibua soo lote...

    Hivi wale askari waliodaiwa kumlinda na kumpa escort nao ni kati ya hao watu waliochiwa huru? Michuzi naomba tufahamishe...

    R.I.P Justine Kasusura

    ReplyDelete
  8. this is useful news for us huku ughaibuni..du msela ndo hivyo tena anakwenda kunyea debe...ni noma..

    ReplyDelete
  9. C'mon now, give him a break. miaka 30 kisa mil 2, how bout the killer dito ambae ameachwa akitesa mtaani? na yeye hukumu yake tutaisikia lini? this is bullsh** if you know what am saying.

    ReplyDelete
  10. Jamaa anachekelea kwenda jela huyo

    ReplyDelete
  11. Ni sh ngapi vile? ,million 130 eti?

    ReplyDelete
  12. du!huyu kaiba tu hela tuduchu kafungwa miaka 35,je ditopile aliyeua bila ya KUKUSUDIA itakuaje?
    ni hapo watanzania tutakapobaki midomo wazi mkiambiwa kwamba hajapatikana na hatia,alikuwa anajitetea.
    au kama mtadanganywa kafungwa miaka mitano,basi atakuwa tayari kishatafutiwa makazi yakujificha ukerewe.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  13. Wana blogu hapo juu mnaombwa kuwa mnasoma habari kwa makini, na sio kuanza kuparamia mambo bila kuwa na uhakika. Nani kati yenu au hata wazazi wenu anaweza kusema kwamba U$2,000,000.00 (sio hela za madafu hizo) ni hela ndogo? au mnaongea tuu......

    Kitu labda cha kusikitisha ni kwamba upelelezi wa kesi hii ulimalizika miaka kadhaa iliyopita lakini hukumu ndio imetolewa leo, na hiyo yote inawaumiza zaidi wale ambao hawakukutwa na hatia (naongelea kisheria) kwani kuna watu wanadai humu ndani kwamba hata hao mapolisi walioachiwa pia nao walihusika.

    Kwa ajili ya kuwaelewesha wasioelewa hizo fedha ni sawa na Tshs. 2,600,000,000/- or (2.6bil/-), na wala si ajabu ukikuta watu binafsi wenye fedha hizi taslim (cash) hawazidi 100 Tanzania nzima.

    Hayo maelezo yote ya hapo juu ni katiuka kuwaelezea muweze kujua ni kiasi gani cha fedha kinaongelewa hapa.

    concomitant13

    ReplyDelete
  14. tz inabidi ipunguze vifungo vya mda mrefu ndio maana watu wanarundikana jela kuwahudumia tatizo practical 30 ni 15 maana usiku na mchana ni 2 days,ila pia amekaa rumande sana,pole sana kwa zombe maana yee ndio ataozea jela.

    ReplyDelete
  15. wewe anony wa 8:21:00 usiwe mjinga na kuzarau wanablogu wote usifikirie kwamba hii blogu ya michuzi inasomwa na watu kama wewe tuu, usizarau watu na kuanza kusema vitu visivyo vya maana hapa kwenye blog huoni mtu unasoma tu maandishi kwa hiyo usijaji watu usiowajua kama wewe au wazazi wako hamna dolla million mbili usifikiri kwamba hakuna watanzania walo nazo, hizo mbona ni ndogo kwa baadhi ya watanzania wenye pesa? jitahidi mshkaji na usitukane watu usiowajua na wazazi wao.

    ReplyDelete
  16. Hapa hukunu imetuchanganya hasa pale inaposemekana kuwa kiasi cha feza kilichoibiwa katika sakata hilo hakijulikani! Kwa hiyo achana na habari ya dola milioni 2 make haijulikani kinachoendelea hapo. sasa huyo bwana katiwa hatiani kwa kosa lipi kama hata hizo hela anazotuhumiwa kuiba hazijulikani? Ni basis ipi iliyoleta ushahidi hapo Kisutu wa milioni 2 na ilijulikana lini kuwa hazikuwa milioni mbili kama ilivyodhaniwa hapo awali? Nadhani kuna kitu hapa ambacho badhi ya wachangiaji hawakijui, pengine kwa kuwa hii ni incidence ya siku nyingi kidogo. Katika maelezo ya msingi, huyu bwana alidai kuwa mnamo tarehe 2 Aug. 2001 huyu bwana akiwa mtumishi wa kampuni moja binafsi ya ulinzi jijini Dar aliagizwa kufuata mzigo (Parcel) airport. Akiwa njiani anarudi alitekwa/alivamiwa na watu wasiojulikana ambao walimwamuru kushuka ndani ya gari alilokuwemo na kumpeleka kusikojulikana.Katika harakati hizo huyo bwana alipelekwa ktk maeneo mbalimbali chini ya ulinzi wa watekaji nyara hao ikiwemo Dar, Tanga, Arusha na hatimaye Mbeya ambao walikuwa wamemwekea ulinzi wa kutosha kwa masaa 24.Wakati taarifa inatoka kuwa huyu bwana anatuhumiwa kuiba akiwa kazini na kuwa anatafutwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari hasa TV na Magazeti ambako picha yake ilisambazwa karibu kila sehemu huyu bwana hakuwa na taarifa yoyote sababu ya mazingira ya ulinzi aliyokuwa amewekewa na watekaji nyara wake.
    Kwa sababu hii tayari vyombo vya usalama vilikuwa kazini tayari kumsaka mtu huyu kwa udi na uvumba kwa kutumia mbinu zote. Mtu huyu alipelekwa mjini Mbeya katika nyumba moja ya kulala wageni ambako alitelekezwa na watekaji nyara wake baada ya kugundulika wanafuatiliwa na polisi.Hivi ndivyo Justine Kasusura alivyokamatwa kwa mara ya kwanza.
    Akiwa mwenye furaha akidhania kuwa sasa yu huru mikononi mwa dola kwani kaokolewa kwa watu ambao haikujulikana hatima yake kwao ilikuwa ni nini alishangaa alipoanza kupewa sekeseke na kutakiwa aeleze wapi zilipo dola milioni 2 za kimarekani alituhumiwa kuiba akitokea aiport alikotumwa mzigo. huo mali ya benki moja ya kigeni, Citibank. Alidai kuwa katika harakati hizo aliteswa sana na mapolisi akiwemo aliyekuwa mheshimiwa ZOMBE akilazimishwa kusema ziko wapi hela na alishirikiana na nani. Alikiri kusema mambo mengi katika kunusuru uhai wake kutokana na mateso ailyokuwa akipata kutoka kwa wanausalama wa nchi hii, hali iliyopelekea kuhusishwa hata maofisa mbalimbali wa usalama wa geshi hili la polisi ambao hata hivyo baadaye waliachiwa huru baada ya kuona mazingira hayawahusishi kabisa na kashfa hii.
    Kwa mantiki hiyo basi, hapa kuna mambo ya msingi ambayo yalipaswa yafuatiliwe kwa kina baada ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hii. Si rahisi kwa Kasusura na profile aliyokuwa nayo kazini kwake kujua kuwa alichotumwa kilikuwa ni hela. This should be between some bank officials na wakuu wa kampuni ya ulinzi aliyokuwa akiifanyia kazi Kasusura ambao watakuwa ndio walio organize mpango mzima wa kumteka na kumpora Kasusura na hatimaye kumtelekeza Mbeya. Sina uhakika kama kuna mtu/ofisa hata mmoja toka taasisi hizo mbili (Benki na Kampuni ya ulinzi) ambao wamehusishwa na tukio hilo hadi mwisho au ktk wakati fulani kwenye kipindi chote hiki tofauti na matukio sawa na hayo ambayo karibu yote yamewahusisha maofisa wa taasisi husika (mabenki) jambo linaloonyesha kuwa na walakini ktk utendekaji wa haki na sheria katika kesi ya Kasusura. Ni kama ametolewa kafara huyu na wahusika wakuu wa mpango huo kwa sababu hadi mwisho tunamwona yeye ndiye anayepanda karandinga kuelekea Segerea kutumikia miaka 30 huku kukiwa hakuna mlalamikaji wala ushahidi wa kutosha tofauti na mazingira ambayo yanaonekana yametengenezwa makusudi!
    Kwa ufupi haya ndiyo yaliyojiri ktk kesi hii ya huyu bwana.
    Hawezi kuwa na milki ya dola milioni 2 mfukoni huyu bwana akaamua kukaa gesti ya uswahilini huko Mbeya kama kweli alikuwa timamu badala ya kutafuta njia yoyote ya panya na kutokomea ujiranini. KUNA JAMBO HAPA, LAKINI NDIO NCHI YETU HII..Wahusika ni watu muhimu na wanainfluence kwenye judicial system tokana na uwezo wao kwa hiyo hatushangai kwa kilichotokea kwa MHANGA huyu..

    ReplyDelete
  17. WEWE MICHUZI NI MNAFIKI SANA UMEWEKA PICHA YA KISUSURA NA MAANDISHI MAKUBWA MBONA HUKUFANYA HIVYO KWA DITOPILE ULIKUWA CAREFUL SANA NA COMMENTS ZAKE. LAKINI HUYU BWANA UMEANDIKA KWA MAELEZO MAKUBWA HUU UNAONESHA NI USHAMBA NA ULIMBUKENI MKUBWA NA KWA AIBU HUTA POST HII COMMENT!

    ReplyDelete
  18. UKWELI NAWAAMBIA HUYU JAMAA KESI ATAMALIZA NA ATAKATA RUFAA NA ATASHINDA ULIONA WAPI MWIZI WA HELA NYINGI AKAFUNGWA? WANAPOTEZA USHAHIDI UTANIAMBIA HUYU ATAKATA RUFAA NA ATASHINDA KWANI HELA YA KUMALIZA KESI IPO.HUONI MWENYEWE ANACHEKA TUU

    ReplyDelete
  19. MICHUZI,
    NIMEHISI KITU FULANI. WEWE UNA MADA UNAZIWEKA HAPA KWA LENGO FULANI. MFANO HII YA KASUSURA SIJUI ULITAKA UPATE MAONI GANI, MAANA NILITOA JANA MAONI NA NILIKUWA NASUBIRI TU UWEKE YASOMWE NA WENGINE. INAONEKANA HUKUPENDEZWA NAYO. SASA NAHISI 'Anony' WENGI WANAOJIANDIKA KATIKA UKURASA WAKO, UNAWEZA KUWA NI WEWE MWENYEWE, ILIMRADI TU UNAWAPA WATU MAWAZO UNAYOPENDA WEWE. SAWA, HAMNA SHIDA BWANA. KISA UNAMILIKI WEBSITE? AU SABABU UNAPIGA PICHA ZA VIONGOZI WAKUU, NA UNAPANDA NDEGE? Ahhhhhhh, panga safari zako mwenyewe bwana. Wakibadili viongozi ina maana husafiri tena? Mshukuru sana JK.

    NIMEJISIKIA OVYO KWA TARATIBU NA BAADHI YA MIENENDO YAKO HUMU.

    ReplyDelete
  20. Anon wa hapo juu nakubaliana na wewe kuwa Blogger yupo bised na baadhi ya maoni, Ila nakupinga kwa kusema anony wengi ni yeye, mimi nimetumamaoni mengi sana kayatoa kama yalivyo na maoni mengi kayatrash vile vile. huende uslitumia lugha ambayo haifahamu kama kichina hivi au...

    ReplyDelete
  21. Anon wa saa 8:21am ukitumia exchange rate ya sasa unakuwa wrong, tumia ya 2001 inakuwa Tsh 1.8 Bil.

    Kumbuka time value of money, inflation na depreciation of Tshs.

    ReplyDelete
  22. Msomaji mmoja ametoa interesting views:
    kama usiku na mchana ni siku 2;
    amekaa ndani miaka 6 = miaka 12;
    amehukumiwa miaka 30 = miaka 15;

    kwa hiyo atatumikia kifungo cha miaka(15 'minus' 12) = miaka 3 (ya kimagereza)

    kwa hiyo basi, mwaka 2010 Kasusura atakuwa mitaani au sio......

    ReplyDelete
  23. Hapa ndio sheria zinaponichanganya! Yule mwalimu aliyeforge milioni 4 Moshi kafungwa miaka 58!! Fundisho...Ukiiba iba 'vijisenti' sio vijihela!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...