wadau msione kimya leo. nimekwama eapoti yadumila toka asubuhi kwani kuna ndege toka bangladeshi imekula mzunga wakati ikitua na kuua shughuli zote za hapa uwanjani na ndege karibu zote leo kanseled hadi kesho. hivyo naomba tuvumiliane hadi nitapopata mawasiliano ya uhakika baadeni. halafu hawa jamaa wa imarati noma kweli, ati kwa vile ajali ile haiwahusu na hivyo waliosababisha abiria woote tutajiju. ah! ndo maana yao inafungwa! sijui nifanyeje nami nshamaliza mfuko wote. ingekuwa bongo ningeenda kulala ccm....


kwa habari zaidi bofya hapa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. mshkaji pole sana!!angalia tu wasikusachi masafuru ya shemeji!!mungu akujalie urudi salama.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, naingilia mtiriko wa mapicha yako, huko dumila, kwa kukuomba, bila kubagua, utundike habari hii muhimu kwa Tanzania yetu, ili wana-blog wasome habari hii inayozungumzia mwenendo wa usawa mbele ya sheria kulingana na the “rule of law”:

    Dito shakani:Kufunguliwa kesi upya, mahabusu leo wagoma - 2007-03-12 15:52:42 Na Emmanuel Lengwa, Jijini

    Siku chache tu baada ya kuachiwa kwa dhamana na Korti Kuu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri, yuko shakani kufunguliwa kesi nyingine mpya inayohusiana na ile inayomkabili sasa ya kumuua dereva wa daladala bila ya kukusudia.

    Hofu juu ya kufunguliwa upya kwa kesi hiyo ambayo sasa ingali ikiendelea Kortri Kuu inatokana na tishio linalotolewa sasa na kiongozi wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila…

    Namunga mkono Mchungaji Christopher Mtikila kwa kujaribu kuleta usawa mbele ya sheria kulingana na the “rule of law”.
    Nawaunga mkono mahabusu hao waliogoma, kutokana na “preferential treatment” upendeleo mbele ya sheria!

    Polisi haina sheria ya kubadili kesi iliyofunguliwa, kutoka “mauaji” kuwa “mauaji bila kukusudia” Polisi ingempeleka Dito mbele ya mahakama, as an innocent person until proven beyond any reasonable doubt kuwa ni guilty.

    Katika kesi ya Dito, kwa polisi kubatilisha msimamo huo wa sheria, ni kuusaidia upande wa watetezi. Polisi ni mshitaki hawezi kuwa mtetezi wa Dito.

    Tusipoangalia umuhimu wa sheria katika kesi hii, tutajikuta watetezi wa Dito wanatumia hiyo nguvu ya polisi kuushambulia upande wa mashitaka kuwa tayari Dito kesha hukumiwa.

    Hii itauwezesha upande wa utetezi kushinda kesi hii kwa legal technicality, na kuomba mahakama iitupilie mbali kesi ya Dito.

    Proper legal or judiciary procedures must be followed, otherwise, kesi ya Dito itajakuwa kama ya Mkuu wa Polisi wa zamani Hamza Aziz.

    Hamza Aziz alishutumiwa kwa kumgonga kwa gari na kumwua pedestrian mmoja usiku huko huko Barabara ya Bagamoyo.

    Ili Hamza Aziz afunguliwe mashitaka hayo, serikali iliamua uchunguzi (inquest) rasmi ufanywe ili kuwepo sababu za kuridhisha kuwa kweli Hamza Azizi kahusika.

    Mwenyekiti wa “inquest” hiyo alikuwa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Mkate. Katika kutoa taarifa yake, Hakimu Mkazi Mkate alitamka kuwa Hamza Aziz alimwua huyo jamaa!

    Upande wa utetezi ulikuja juu na kuishambulia taarifa hiyo, on legal technicality, kuwa kwa kuamua na kutamka kuwa Hamza Aziz aliua, “Inquest” ilikuwa inachukua madaraka ya jaji wa mahakama.

    Hamza Aziz aliachiliwa huru, kaondolewa kutoka polisi kwenda kuwa mshauri wa kisiasa kwenye ofisi ya ubalozi wetu Amerika.

    ReplyDelete
  3. Pole sana Michuzi kwa kukwama eapoti na imarati wamekukaushia hata msosi si ajabu hakuna!

    Nimetoka sasa hivi eapoti ya Dar kumpokea mgeni wangu toka Canada na nimeona kwenye ubao wa matangazo ya ndege zinazowasili kwamba Emirates imekuwa kanselidi....Sikujua sababu, but at least umenifumbua macho hapa !

    ReplyDelete
  4. "kawia ufike...!", labda ulisahau ule msemo "safari ni hatua, na akiba haiozi!" pole khaakhaaaa...

    ReplyDelete
  5. Ooh pole sana kaka Michuzi,sasa duu sijui itakuaje hapo itabidi tu ujibanze japo kwenye benchi mpk asbh.

    ReplyDelete
  6. Ooh pole sana kaka Michuzi,sasa duu sijui itakuaje hapo itabidi tu ujibanze japo kwenye benchi mpk asbh.

    ReplyDelete
  7. Basi Mzee Michuzi hizo picha za Dumila zimetosha!!!Ni nyingi sana.Tupe michapo mingine,nasikia Lowassa anataka kuanzisha Trams(treni za mjini) hapo Dar.Mungu aibariki bongo!

    ReplyDelete
  8. Eh! Michuzi!
    Pole sana, bora salama na safari njema!
    /maggid

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli mi-soup hapa unataka tucheke tu! Umenifurahisha sana sana!. Sasa hao Wabangladesh wamepona? Mbona hiyo habari haimo kwenye web zote leo?

    Pole sana. Ndo maana hata ndege zao hao waarabu wote ni nauli ni rahisi tu. Huwa hawajali vitu serious kama hivyo! Hata kwa issues zingine hawako serious sana Waarabu.

    Pole sana na karibu sana bongo.

    ReplyDelete
  10. Pole mzee mzima. Mpe hi huyo demu anayepiga simu hapo.

    ReplyDelete
  11. POLE SANE MICHUZI!

    Michuzi mimi ninakushauri uanzishe utaratibu wa "GUEST BLOGGER." Yaani mtu au watu unawaachia blogu ikiwa wewe mwenyewe uko bize au uko sehemu sehemu wakusaidie kuweka mavituz.

    Kwa mfano wakati uko Dumila ungemuachia Majjid Mjengwa naye awe anaweka vitu hapa au Chemi Chem-Mponda au wanablogu nyingine.

    Hii itakusaidia usiwe na presha ya kublogu ukienda likizo au sehemu ambazo mawasiliano ni kwa mbinde.

    Haya ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  12. Pole sana MIM kwa kukwama dumila, ishu ni pale kama ulikuwa haujaaga kwa mwajiri wako ukijua kuwa unaingia ofisini mapema siku ya jumatatu, imekuwa hola.

    Usijali haya ndo mambo ya usafiri. Kumbuka msafiri kafiri, itabidi ulalale tu popote pale.

    Wewe anon wa 12 March saa 3:00pm , unaonekana ni fala tu, yaani ndege moja ya Bangladesh kupata hitilafu unajenerolaizi waarabu wote, kama sio chuki binafsi ni nini. Tumeshaona madege ya wasio waarabu yakianguka na haukusema , wewe paka tu. Ndege za France, na nchi nyingine zisizo za kiarabu zimekuwa zinaanguka na hatusemi kuwa ni wazembe. ATC yenyewe kuna siku ilishindwa kutoa matairi,ikazunguka masaa mawili hewani nayo ni ya waarabu?

    Vitu kama hivi vinahitaji takwimu, sio kujiropokea tu kwa wajinga kama nyie msiokuwa na kazi, kama hauna cha kuandika kaa kimya, hakuna atakayekuuliza. Tumechoka na pumba zenu.

    ReplyDelete
  13. Sasa Issa,wewe mwenyewe unaiharibu hii Blogu yako.Yaani tangu wiki hii yote ni picha hizo hizo.Please snap out of that!

    ReplyDelete
  14. Mkiambiwa mlipie travel insurance hamtaki. Na kam ndio ticket za ofa kasheshe

    ReplyDelete
  15. michuzi pole! ila unakampani ya kutosha huyo dada hapo pembeni kila siku upo naye ulivyokuwa zanzibar ulikuwa naye, ukaenda kumnunulia Flat screen dubai wakati mnachagua alikuwepo inaonekana ni my small wife wako michuzi usibishe!
    Ila pole na safari msafiri kafirii.

    ReplyDelete
  16. Eh! Michuzi wenyeji wako wapi. Au huko hamna wabongo wenyeji? Au ndio hivyo tena simu hazipokelewi?

    Dubai msituangushe bwana. Msimfanyie mishuzi mkausho...
    Michuzi anaonyesha poa tu hata kama mnaishi kumi kwenye nyumba mnampa warning tu. First camera yake iwe off alll the time...yaani hamna kupiga picha. Second atakaloliona humo, atakalolisikia humo aliachie humo humo ndani kwenu.

    ReplyDelete
  17. I am glad unaenda bongo kwasababu tumechoka habari za dubai.
    Huwezi amini home sweet home especially kwa watu walio nje nchi najua wanaelewa what I mean. Tunamiss story za bongo.

    ReplyDelete
  18. Duu Bola Misupu Urudi Huko Dumila Maana Kaa Umeenda Kuoa!!!! Picha Kibao Inatosha Rudi Tupate Za Uswazi Nazo

    ReplyDelete
  19. kuna plastiki inayotolewa na mabenki inayoitwa credit card. Kama wewe ni msafiri wa siku nyingi na mfanyabiashara, jaribu kuomba benki wakutengenezee, wewe sasa ni tajiri.

    ReplyDelete
  20. Misupu ! Ulibeba kande za safari ?

    ReplyDelete
  21. We anon March 12 10:15 nadhani hukuelewa. Niliposema Waarabu ni wazembe nilikuwa siongelei ndege ya Bangladesh kuanguka wala Bangaladesh siyo nchi ya Kiarabu.

    Nilikuwa namaananisha management ya Uwanja na pia ile ya Emirates ambazo ni za Kiarabu. KWa sababu, airport zingine na airlines zingine kama kukitokwa problems za namna ile Abiria kama mme-check in mnapelekwa sehemu ambako mnapata huduma zote free of charge.

    Sas Michuzi anasema Emirates walijitoa kwa sababu eti hawakusababisha ajali hiyo.

    Ndo maana nilisema, this is common to Arabic World. Uzembe na kurahisha mambo. Problems zote zinazotokea huwa wanapenda sana kurahisha na kuchukulia issues kirahisi tu.

    Kama wewe ni Mwarabu, I am sorry, but that is the FACT. I have been to most Arab Countries. Ya Michuzi ni ndogo tu hiyo. Kuna vitu vya ajabu sana.

    ReplyDelete
  22. Wewe annoy hapo juu omba msamaha yaishi. Kwanza ujue hata kama umecheck in kama tatizo halijasababishwa na shirika la hiyo ndege uliyonunua ticket wao hawahusiki kabisa na kukulea.

    In the US watu walikaa kwenye runaway masaa 8 bila kutake off na bado hawakulipwa anything. The only thing hiyo ndege ilikua blamed ni kwa kutowarusha watu uwanja wa ndege kusubiri weather iwe cleared.

    Ndio maana ukinunua ticket angalia bill of right ya hiyo shhirika la ndege au tumia credit card zenye insurance and some benefits. Ticket zilizo kwenye sales most of them hazina guarantee.
    kwa hiyo wewe kusema waarabu wanafanya mambo kiurahisi sio vizuri. Mimi sio muarabu lakini ukishaishi nchi za nje unaelewa au una jua how it feels ukisiskia mtu anakusema au ana judge people of your color, your originality, your continent or your gender. It is not easy.

    ReplyDelete
  23. Makaburu wanataka sana waitwe waafrika hawataki kuitwa makaburu (boers).Wanasema bara la Afrika lina watu wa makabila mbalimbali kama waarabu,watu weusi wa makabila mbalimbali,na wazungu wa Afrika ya kusini.Wote hawa ni waafrika.

    Ajabu nchi hii wahindi na waarabu hawataki kuji-identify kama waafrika tofauti na makaburu ambao wanaendesha kampeni ya hali ya juu kimataifa wajulikane kama waafrika.

    Waarabu wa Afrika kama akina Ghadafi wanajifanya waarabu zaidi kuliko waafrika na wanafanya makubwa kwenye jumuiya ya nchi za kiarabu kuliko jumuiya ya nchi za kiafrika.

    As long as waarabu wa Afrika hawapendi kujiona kama part and parcel of Africa mtaendelea kuonekana kama watu wakuja na kupondwa na waswahili muwe Tanzania au nje ya Tanzania.Mtabaguliwa sababu mnabagua.Wahindi wanabaguliwa sababu na wao wabaguzi.Lazima mvune mnachopanda.Ukibagua mswahili lazima akubague.

    ReplyDelete
  24. Nashukuru kama umeelewa. Mimi nilikuwa naongelea hali halisi ya Middle East kwa ujumla. Middle East huwezi ongelea bila ya kutaja UARABU. Kuongelea haya kunasaidia wengine ambao wana nina ya kwenda huko kujua nini cha kufanya au kujiandaa nacho kabla ya safari.

    Hii Blog ni ya kuelimishana na si kuweka na hisia za kibaguzi. Njia rahisi ya kufanya kama una hisia za kibaguzi, ni kuacha kutembelea hii blog. Hakuna hata mmoja ambaye ni Mtanzania halisi mwenye hisia za kibaguzi.

    Tuweke issues na si kutukana matusi kama pale juu (March 12: 10:15). KWa sababu ukitukana namana hii unakuwa una-overshoot kiasi kwamba hata ideas zako hazieleweki! Nguvu hoja zaidi na si hoja ya NGUVU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...