mwenyekiti wa wabongo ukerewe aboubaka faraji (tai na koti jeusi) akiwa na kamati yake mpya ya uongozi

Faraji mwenyekiti mpya wa Watanzania Uingereza






Na Mwandishi Maalum, London






Abubakar Faraji juzi aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa na kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Uingereza na kukiongoza chama hicho kwa miaka miwili.




Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Asian Community Centre uliopo katikati ya mji wa Wembley, ulifuatia baada ya kamati ya muda iliyokuwa chini ya Bi Nora Sumari kumaliza muda wake.




Faraji alifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupata kura 37 dhidi ya Said Yakubu aliyepata kura 27, wakati Suzani Mzee alipata kura 22 katika ya kura 86 zilizopigwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Bi Zubeda Mahugu.




Bw.John Lusingu mkazi wa Reading ambaye ni msomi wa anayetarajia kumaliza shahada ya udaktari aliibuka mshindi dhidi ya Bi Nunu Chondoma, wakati Bw. Juma Pinto alichaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa jumuiya hiyo kwa kumshinda Bw. Yahaya Kiomoni.




Bi Lucy Shegikile alipita bila ya kupigwa baada ya kukosa mpinzani katika nafasi yake ya uhazini na wajumbe saba waliochaguliwa ni Bw.Gerald Lusingu,Bw.Almas Kasongo, Bw.Dessa Makoko, Bw.Haruna Mbeyu, Bw.Rehani Ellofy, Bi Zeyana Amour na Bi. Nora Sumari.




Kabla ya Mkutano huo, Balozi wa Tanzania hapa Uingereza, Bi Mwanaidi Senare Maajar aliwataka Watanzania hao kuchagua viongozi ambao wataweza kuwajibika katika kukifanya chama hicho kwenda na wakati.




"Nawaombeni muwe makini ili tuweze kupata watu ambao ntashirikiana nao katika kufanikisha shughuli mbalimbali zinazowahusu Watanzania,wakati wa maneno umepita nawaomba Watanzania wenzangu tuamka," alisemaBalozi Maajar ambae ametokea kuwa kipenzi cha Watanzana wanaoishi hapa Uingereza kwa kufanikisha mambo mbalimbali ambayo huko nyuma yaliyokuwa hayawezekani ikiwemo ili la kuanzisha jumuiya ya Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mbona mwandishi hakutaja wote au hao wengine wanafanya nini huko isipokua huyo Lusingu ambaye anasoma?

    Just curious.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana Wadau wa Uingereza kwa uchaguzi! Pia nawapongeza kwa kumchagua Abu Faraji, mie binafsi namfahamu Abukakar Faraji, akiwa Mwenyekiti wa Shule (HP) ilboru Secondary arusha, alikuwa kiongozi supa!

    Mpeni ushirikiano, atawapeleka mnakotaka.

    Faraji tunaomba ututembelee na sisi wa Ireland! Utuhamisishie tuwe na chama. Pamoja na hayo, mie nakutambua kama kiongozi wetu, kwani tunategemea ubalozi wa London, hivyo na wewe ni kiongozi wetu!

    Mwisho nawapongeza wote waliochaguliwa na uongozi uliopita

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa!
    Mimi Ole Ndukia

    ReplyDelete
  3. Huyo daktari J Lusingu wa Reading mbona sikuona ameshinda na kupata wadhifa gani hapo juu?

    ReplyDelete
  4. Yaani kati ya hao wote; mwenye shughuli inayoeleweka ni John Lusingu peke yake wengine je.... machinga na mama lishe eti? ila ameshinda na kupta cheo/wadhifa upi ...
    (anajipigia debe etieee.. au ana-beep ubunge 2010 tehe tehe tehe heeeee)

    ReplyDelete
  5. Chama cha kazi gani hapa Ukerewe Majungu tu na kutaka nyadhifa zisizo na kichwa wala miguu.

    ReplyDelete
  6. Mwandishi kakosea. Hakuna mtu anayeitwa Bw.Rehani katika hawa viongozi. Huyo aliechaguliwa ni Bi Rehana Ellofy. Anahitaji kuomba radhi.

    ReplyDelete
  7. hi all hongereni kwa moyo mlonao , ila kazi mnayo . watu 86 walipiga kura?kazi mlonayo ni ya kuanza kutukusanya inabidi mtufuate tuliko. kazi mnayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...