Home
Unlabelled
gurumo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
MIKATABA MIBOVU: Rais kasema kweli, je atafanya kweli?
ReplyDeleteHabari za hivi karibuni kama zilivyoripotiwa na Mwandishi Msaidizi wa Rais Bi. Maura Mwingira kuwa kwa mujibu wa Rais Kikwete, Tanzania imeingia kwenye mikataba mibovu kutokana na kutokuwa na wataalamu wenye ujuzi wa majadiliano ya biashara za kimataifa, ni habari za kusikitisha na kukatisha tamaa. Kama aliyosema Rais ni kweli (na sina sababu kuhisi vinginevyo) basi ndugu zangu watanzania tumeliwa!! Kama wale ambao wamesoma katika vyuo vyetu vya sheria na wengine nje ya nchi na wakapewa dhamana ya kusimamia maslahi ya Taifa ilhali waliowapa dhamana hiyo wanajuwa kuwa watu hao wanauwezo mdogo ni jambo la kutia hofu, kutetemesha na kutufanya wote tubakie midomo wazi huku tukitikisa vichwa! Hizi si habari nzuri hata chembe.
Ukweli wa mambo ni kuwa tatizo walilonalo watu hao ambao Rais amedai wana “uwezo mdogo” ni zaidi ya uwezo mdogo! Ni tatizo kubwa ambalo kama kweli Rais anataka kulitafutia utatuzi basi ni lazima tatizo hilo liwekwe wazi na bayana. Nakusudia kumrahishia Bw. Kikwete kazi hiyo.
Ndugu zangu katika kufuatilia mambo mbalimbali ambayo yanaendelea Tanzania na hususan suala la mikataba mibovu, swali moja ambalo nimekuwa nikijiuliza ni kitu gani katika mikataba hii yote kinalinganga, na ni watu gani wanahusika katika mikataba hii yote?. Jibu langu halitawashangaza wengi lakini wakati umefika wa kuita uovu kwa jina lake. Mikataba yote ambayo imelalamikiwa ilikuwa na kitu kimoja kinacholingana. Rais amesema ni tatizo la wataalamu kukosa uwezo wa kujadiliana. Mimi nasema ni zaidi ya hilo. Na sikubali kuwa hawana uwezo ila wametumia uwezo na ujuzi wao vibaya na kuliingiza taifa letu kwenye mikataba ya hasara.
Je mikataba yote ambayo imelalamikiwa na Watanzania ina vitu gani vinavyolinganga? Kwanza, wahusika wakuu karibu ni wale wale na pili wahusika hao wamehakikisha kuwa ni vigumu kujitoa kwenye mikataba hiyo (lack of escape clauses). Mkataba wa IPTL ulikuwa ni vigumu kujitoa kwa sababu hiyo ya kukosa kipengele thabiti kinacholinda maslahi ya Taifa na ambacho kinaweka utaratibu usioadhibi sana pale serikali inapojitoa. Jambo hilo ni kweli pia kwenye mikataba ya madini, mkataba wa Richmond, mkataba wa Tanesco, DAWASO, Songas, Rada n.k
Wahusika katika Mikataba yote hiyo ni karibu watu wale wale wa ofisi moja! Ofisi hiyo si nyingine bali ni ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania. Kwa mujibu wa Katiba yetu:
Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo,
atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli
nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria
zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza,
na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa
kwake na Katiba hii au na sheria yoyote. Ibara 59:3
Kwa vile yeye ni mshauri mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa mujibu wa sheria ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni lazima ipitie mikataba yote inayoingiwa na serikali hiyo na kuhakikisha haina utata, basi katika suala zima la mikataba hiyo tunayoilalamikia jukumu la kwanza linaangukia ofisi hiyo. Ni hawa ambao kwa kutumia ujuzi wao wa kisheria wameliingiza Taifa letu kwenye songombingo hili mikataba mibovu. Kusema kuwa “wana uwezo mdogo” ni kuwapa utetezi wasioastahili. Kwa kusema kuwa hawana uwezo, Rais Kikwete ameshtaki vyuo vyetu kuwa havitoi wataalamu wa kisheria wanaostahili. Jambo hili silikubali hata kidogo. Hao wanasheria wanawakilisha hayo makampuni makubwa wao wamesomea wapi? Ina maana serikali imeajiri wanasheria wa kiwango cha chini na kuwataka wawawakilishe mbele ya wanasheria wenye uwezo mkubwa na kutarajia wana ubavu wa kusimama?
Hatuwezi kuwaachia watu hawa ambao baadhi yao baada ya “uwezo wao mdogo” leo hii wamepewa nafasi nyingine kubwa na wengine hadi uwaziri!! Inakuwaje ubovu unazawadiwa na uzembwe kuvumiliwa? Haitoshi kwa Rais kutaka kuleta wataalamu toka Sweden kuwafundisha wanasheria wetu na kudhania watabadilika. Serikali inaweza kuleta wataalamu kutoka sayari ya Mars lakini kama watumishi wenye dhamana ya kulinda maslahi ya nchi hawana uzalendo na nia ya kufanya hivyo itakuwa ni kama kumpigia mbuzi ngoma ya lizombe, hachezi!!
Gurumo usistaafu tafadhali...kwa miaka yote hio umekuwa kioo cha wanamuziki wote wa Tanzania....bado tunahitaji mchango wako
ReplyDeletewe anoni wa juu huo ni uselfish kwa nini baba wa watu asistaafu. kama yeye anajiona amechoka muacheni akapumzike i am sure muziki hautakufa ila tu ataacha pengo la jina. tumtakie kila la kheri na kwa upande myingine wa hii picha tunafurahi kumuona mheshimiwa Rais yupo nyumbani ama ana ka-holiday kadogo ??
ReplyDeleteMimi nafikiri suala si uwezo wa kitaalam, bali siasa ni kubwa kuliko utaalamu.
ReplyDeleteTume zote za wasomi ni ripoti chache sana zimefanyiwa kazi,
Watu wote viongozi washitakiwe...
nakumbuka Mungai, alihusika katika mikataba ya Air Tanzania,
Walioleta Netgroup washitakiwe kwa kusababisha hasara serikalini
Nafikili sheria inayomuhukumu Prof.Mahalu(Financial loss to the State..)
Raisi kama CEO wa nchi lazima anapitia mikataba yote, na kama anamwamini mtu(waziri etc) basi kama inatokea tatizo wote wawajibishwe.
AZIMIO LA ARUSHA linasema Fedha isiwe kichochezo cha maendeleo....
Jamani inasikitisha sana na wala hatujifunzi kutokana na makosa.
ReplyDeleteHivi ni mikataba mingapi ime-fail ukiangalia tu suala la umeme??????Ina maana siku zote hizo hatukujua.
Ukiangalia madini,ndio usiseme Tanzania watu wameaanza kuchimba madini lini.Mikataba mingapi imetuletea hasara.
Mungu wewe tumekukosea nini??Hivi ni kweli watanzania hatuna akili hivyo???Hawa wanaosign mikataba hawana akili hivyo????
USHAURI.
Moja ya sheria katika hiyo mikata iwe-mkataba unaweza kuvunjwa pale inapooneka upande mmoja unapata hasara sana.Au mnasemaje jamani???
Hivi hakuna shule inayofundisha kuchambua mikataba???Maana hata mtu ukinunua diesel lita 10 unajua inakupeleka km ngapi.Tutafute njia ya kujua hii mikataba inatupeleka wapi....
Sio kweli. Chanzo kikubwa sio utaalam haba. Kama rais kamaanisha hivyo toka moyoni mwake, basi naye uwezo wake ni duni. Naamini kasema uwongo au kawakoga tu wafadhili wetu. Na si uungwana. Tatizo nio rushwa. PENYE RUSHWA HAKUNA HAKI jamani. Wanaosaini mikataba wanapewa rushwa kubwa sana na kushawishika kutojali madhara yafuatayo. Kama uwezo ni mdogo, kwa nini mikataba ya kuuza mali ya umma iwe SIRI? Kwa nini bunge lisiibariki kwanza kama ilivyo mikataba ya kimataifa? Kwa nini mikataba isichapishwe ktk magazeti UMMA uione? Acheni kutubabaisha.
ReplyDelete'You can fool some people all the time. You can fool all the people sometimes. BUT you CANNOT fool all the people all the time'. Angalia sana handsome boy!
DU JAMANI,MMESIKILIZA MAMBO YA BONJGO HUKU,
ReplyDeleteWAFUNGWA WAMEHOMA BAADA YA HUKUMU YA DITOPILE KUFANYIKA HARAKA,KUNA WAFUNGWA WANALALAMIKA WAMEKAA ZAIDI YA MIAKA KUMI,HADI LEO HAWAJASIKILIZWA WANASOTA TUU,NA TUNAVYOJUA KESI YA MAUAJI HAINA DHAMANA,
KUNA NYINGINE PIA
JANA HUKUMU IMETOLEWA KWA WATU WALIOMUUA JAJI MIAKA KADHAA ILOYOPITA YA KUNYONGWA DUH MI SIONGEI ZAIDI