Home
Unlabelled
jengo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
INJI INAWENYEWE WALIO JUU YA SHERIA.
ReplyDeleteWakati Dito apata dhamana...
Polisi wawakong'ota waandishi wa habari
Apitishiwa mlango wa majaji
Jaji akerwa, ataka
Tibaigana atoe maelezo
Na Ester Bulaya
HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ditopile Mzuzuri (58) ameachiwa kwa dhamana, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi mitatu.
Wakati Dito akipata dhamana, katika hali ya kushangaza, polisi waliwasaidia ndugu na jamaa zake, kuwapiga waandishi wa habari na wapigapicha ili kuwazuia wasifanye kazi.
Hayo yalijitokeza jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakati Ditopile alipofikishwa kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana katika kesi ya kuua bila kukusudia.
Ditopile alipata dhamana hiyo mbele ya Jaji Agustine Mwarija wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kusikiliza ombi hilo lililowasilishwa na mawakili wa mshitakiwa huyo.
Vitendo hivyo vya polisi, vilisababisha eneo la Mahakama hiyo, kugeuka 'uwanja wa vita' kwa kuchochea vurugu badala ya kutuliza, kitendo kilicholeta hisia kwa baadhi ya watu kuwa kulikuwa na mazingira yasiyoeleweka na yaliyo kinyume na maadili.
Purukushani hizo, zilianza kujitokeza saa 2.54 asubuhi baada ya polisi wapatao 15, kumsukuma mlinzi Kulwa Mkola na kumpitisha kwa nguvu mshitakiwa Ditopile katika mlango maalumu ambao hutumiwa na majaji.
Katika sakata hilo, askari hao pia walimpiga mpiga picha wa gazeti la The Citizen aliyekuwa eneo hilo kwa ajili ya kupiga picha.
Kitendo cha kumpitisha Ditopile katika mlango huo, kilizua manung'uniko kwa baadhi ya watendaji wa mahakama hiyo, huku wengine wakihoji kwa nini wamekuwa wakimficha wakati washitakiwa wengine wanapitishwa kama kawaida.
"Hivi hawa polisi vipi, yaani walivyomzunguka kama... hii yote kumzuia kaka wa watu asipige picha mpaka wamempiga na kitako cha bunduki, hii siyo haki, amefika hapa ni mshitakiwa kama wengine.
"Tangu nianze kazi sijawahi kuona kesi kama hii, huu mlango hauruhusiwi watu kupita siyo sisi wafanyakazi wala mawakili, huu mlango ni kwa ajili ya majaji tu," alisema moja wa makarani wa mahakama hiyo.
Akizungumzia tukio hilo, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo, alisema mahakama imechukizwa na kitendo hicho na kuwashangaa askari hao kwa kukiuka taratibu za mahakama huku wakijua hawaruhusiwi kupitisha washitakiwa katika mlango wa majaji.
Lyimo alisema wamelifikisha suala hilo kwa Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana kwa hatua zaidi.
Alisema kiutendaji, Mahakama haina taratibu za kubagua washitakiwa na kwamba wote wanatakiwa kupitishiwa sehemu moja.
Lyimo alisema askari hao waliamua kuvunja sheria makusudi kwa kumpitisha mshitakiwa kwa nguvu huku wakimsukuma mlinzi aliyekuwa akiwazuia.
Aliongeza kuwa mahakama kwa upande wake, itachukua hatua baada ya kupata maelezo kutoka kwa Kamanda Tibaigana ili iwe fundisho.
"Kwa kweli tumekasirika sana, sijuwi walipewa nini, maana katika hali ya kawaida hawawezi kufanya hivyo. Haijawahi kutokea hapa, nimemwambia Tibaigana awabane polisi wake na wamueleze kwa nini wamefanya hivyo," alisema msajili Lyimo.
"Wakati kesi itakapofika muda wa kusikilizwa, tumeshatoa amri apitishwe sehemu za wazi kama wavyopitishwa watuhumiwa wengine, sisi hatuna mtu maalumu, sheria ipo kwa watu wote hivyo lazima ifuatwe,"alisema.
Hata hivyo, wakati Ditopile anaingizwa mahakamani saa 4.50 asubuhi, kupitia 'korido' za kawaida kama washitakiwa wengine, polisi waliendelea kuwazuia waandishi kufanya kazi yao huku wengine wakiwapiga kwa kutumia vitako vya bunduki.
Mbali na kiongozi wa askari hao, Inspekta David kuitwa na kuulizwa kuhusiana na suala hilo, polisi waliendelea kutoa kipigo kwa waandishi na wapiga picha.
Hali hiyo, ilijirudia saa 8.30 mchana wakati Ditopile alipokuwa akiondoka eneo la mahakama, ambapo polisi waliendelea kuwapiga na kuwazuia waandishi wa habari.
Wakati vurugu hizo zikiendelea, baadhi ya polisi walikuwa katika harakati za kumzuia Ditopile asipigwe picha.
Katika kufanikisha hilo, baadhi ya askari walimwagia maji kamera zilizokuwa zikimpiga Dito baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Vurugu hizo, zilisababisha kuvunjika kwa kioo cha gari lenye namba za usajili T. 723 AFD, ambalo lilimchukua mshitakiwa huyo.
Mbali na kuwapiga waandishi, ndugu na jamaa wa Ditopile walikuwa wakitoa maneno ya kashfa huku wakitamba kwamba lazima ndugu yao ataachiwa tu.
Kwa upande wake, mlinzi Kulwa alisema polisi waliomsukuma na kumpitisha Ditopile kwenye mlango wa majaji, walitumia nguvu kwa kumpiga kikumbo na kupita haraka huku akishuhudia wakimpiga mpiga picha.
"Kwanza sikujua kama huyu ndiyo Dito, labda angevaa kofia kwa sababu huwa anavaa kofia anayopenda mahakamani. Niligundua kuwa ni Dito baada ya kumuona mpigapicha huku wakipita kwa kasi baada ya kunipiga kikumbo," alisema Kulwa.
Alisema walipofika juu, walikutana na mmoja wa majaji akitoka mahakamani ndipo alipowarudisha na kumtaka atoe maelezo kwa nini aliwaruhusu kupita hapo.
Baada ya kudhaminiwa Ditopile aliondoka Mahakamani hapo saa 9.15 mchana akiwa kwenye gari aina ya Toyota 'Baloon' huku akifuatiwa na polisi waliokuwa kwenye Landrover Defender.
Jaji Mwarija alitoa dhamana saa nane mchana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakao saini bondi ya sh. milioni 20 na mwenyewe Ditopile.
Mbali na hilo, pia anatakiwa kuwasilisha hati zote zinazomwezesha kusafiri ikiwepo pasipoti kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Ditopile pia anatakiwa kutosafiri nje ya mkoa bila kibali cha Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Akitoa dhamana, Jaji Mwarija alisema mahakama imeitoa kwa mshitakiwa kwa kuwa hakukuwa na kizuizi cha dhamana kwani shitaka husika linadhaminika.
Alisema mbali na kuwa kosa hilo lina dhamana, mahakama imefikia uamuzi huo, kwa kuwa mshitakiwa huyo hawezi kutoroka na vile vile atafika mahakamani pale atakapohitajika.
Jaji Mwarija alisema uamuzi huo umezingatia kuwa hakuna dalili za yeye kuharibu ushahidi kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika na kwamba kwa upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili Vicent Tango, hauna pingamizi.
Mapema, wakiwasilisha ombi hilo, mawakili wa mshitakiwa, Dk. Ringo Tenga, Cathbert Tenga wakiongozwa na Profesa Jwani Mwaikyusa, walidai shitaka linalomkabili mteja wao linadhaminika kisheria.
Profesa Mwaikyusa alidai wana uhakika mteja wao akiwa nje kwa dhamana, hawezi kutoroka kwa kuwa ni mtu maarufu na alishawahi kuwa kiongozi hivyo popote atakapokwenda ni rahisi kukamatwa.
Kuhusu kuingilia upelelezi, alisema hilo haliwezi kutokea kwani tayari umekamilika.
Naye wakili wa serikali Tango, aliiambia mahakama kuwa hawana pingamizi la dhamana, bali mahakama itoe dhamana kwa misingi kuwa mshitakiwa anastahili dhamana na siyo kwa sababu ni mtu maarufu.
Ombi hilo la Dhamana lilianza kusikilizwa saa tano asubuhi mpaka saa sita na nusu mchana ambapo Jaji Mwarija aliahirisha shauri hilo kwa muda wa saa moja na nusu na kutoa uamuzi wake saa 8.30.
Awali, ombi hilo lilipangwa kusikilizwa juzi, lakini mshitakiwa huyo hakuweza kufikishwa mahakamani mapema kutokana na kutokuwepo mawasiliano mazuri kati ya magereza na polisi waliopaswa kumfuata gerezani.
Watu mbali mbali wakiwemo ndugu wa mshitakiwa, makarani, wanasheria walifurika mahakamani hapo kujua hatma ya Ditopile ambaye kesi yake imekuwa na mvuto wa kipekee.
Ditopile aliingia mahakamani akiwa ameinama na kuweka mikono yake kifuani, huku akiwa amevaa suruali ya rangi nyeusi na shati la mistari.
Kama kawaida yake aliendeleza mtindo wake wa kuficha uso kwa kofia nyeusi aina ya pama na alipofika kizimbani kabla ya mahakama kuanza alivua kofia na kusoma gazeti la Rai.
Baada ya kupata dhamana ndugu wa Ditopile na mke wake, walishangilia huku wakikumbatiana na kwenda kuwapa mikono mawakili wake.
Hivi karibuni Ditopile alibadilishiwa shitaka na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutoka ya mauaji hadi kuua bila kukusudia.
Kwa mara ya kwanza, Novemba 6, mwaka jana, alisomewa shitaka la mauaji ya Hassan Mbone (33) aliyekuwa dereva wa Daladala, ambapo anadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 4, mwaka jana, saa 1.30 usiku katika njia panda ya Kawe na Bagamoyo,
jamani,hii ni dar es salaam sehemu gani?du itanibidi nirudi haraka iwezekanavyo,maana sini sababu yakupigwa na baridi huku nilipo wakati kikwete kishaanza kutubadilishia nchi.
ReplyDeleteHilo jengo jinsi lilivyo unganishwa na hiyo stair, linanifanya nipate mandhari nzuri ya University of Dar es Salaam kama ujenzi wake wa kuunganisha Hall 2 na Hall 5 ungemaliziwa kwa ngazi kama hizo, ila ulikatishwa , michu epu tupe picha ya majengo haya mawili ukirudi.
ReplyDeleteJengo kama hili linajengwa Ilala kwa ajili ya wamachinga, litakuwa pembeni ya uwanja wa Karume na makaburi ya karume, hapo kati kati itakuwa inapita barabara ya Kawawa kuelekea chang'ombe
ReplyDeleteNi kweli kabisa kisheria Dito anastahili dhamana kwa jinsi kesi ilivyonyongwanyongwa na kuwa ya kuuwa bila kukusudia. am not happy about this na roho inaniuma utafikiri huyo marehemu dereva nimemzaa mimi. najiuliza maswali mengi na nakosa majibu. Hivi huyu Dito angekuwa amemuuwa mtoto wa kigogo yeyote mzito kwenye system kama vile mtoto wa JK, BWM,PM au mwingine mwenye nguvu hii kesi ingepelekwa hivi?! yaani nahisi kisirani na nimesusa kuandika.. Eti wanadai sheria msumeno....lol
ReplyDeletebongo wajenge hivyo mi sitakatiza kwenye hicho kidaraja ntashuka chini ndo nitembee kwenda jengo lingine, manake ujenzi mifuko ya simenti itakuwa inajazwa mchanga nusu daraja halikawii kudondoka
ReplyDeleteMichuziiii hii ndio mijengo ya kisasa inayopunguza kwanza ajali ya wavuga barabara kwa miguuu pili msongamano wa watu barabarani unatumia tu hizi flying brigde ndio zinavyoitwa huku mamtoni kwa pale bongo tunaziihitaji nyingi sana .Tena hata kwa hizi highways zetu tungeziunganisha kwa hizi flying bridge ingekuwa bomba sana japokuwa sidhani kama hapa bongo tunazo highways or motorways
ReplyDeleteHivi michu umebakiza nchi ngapi? umalize dunia yote kwa utalii wako
ReplyDeleteMchuzi umeificha habari muhimu na ilo jengo ,Ungeiweka ijitegemee .Dito na sheria
ReplyDeleteMichuzi, wacha kubagua maoni! Mtundiko wangu dhidi ya kesi ya Dito wapi?
ReplyDelete