
Kikosi cha F.C.BONGO Helsinki. kabla ya mechi na wakameruni katika mashindano ya kimataifa ya HELISNKI PREVENTION CUP 2006.
Toka shoto waliosimama: ALI NYOKA , NAMAN, ZAKARIA , KEVIN , SULO , MAPINDUZI, ALI APEPE, MARCELO, MIKE, OJUKU, ERICK ABDULI , ZULU , BOB NA EZZA.
Chini toka shoto: JOHARI , BEN , HENRY , EDWARD , CHRISPIN , NJAU , MZEE MATARUMA (nyuma ya kipa) AHMADA (kipa), EDDY NA NGASA.
Mashindano ya PREVENTION CUP yanafanyika kila mwaka wakati wa summer jijini Helsinki yakishirikisha timu za mataifa mbali mbali, timu ya Wabongo waishio Finland (F.C.BONGO HELSINKI) imeshiriki katika mashindano hayo kwa miaka minne mfululizo, miaka mitatu ya kwanza timu hii ya watanzania haikuweza kufanikisha kuvuka katika michuano ya awali (First Rounds) lakini mwaka jana 2006 walfanikiwa kufika nusu fainali na kuwa mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wagiriki goli sita bila na kupokea medali za shaba.
Mataifa yalioshindana katika mashindano hao ni:Finland Wenyeji na mabingwa (GOLD MEDAL)Nigeria (SILVER MEDAL) na Bongo(BRONZE MEDAL)
Timu zingine ni Greece, Cameroon, CongoSarkus (Midle east United), Mundial (South America United)Ghana, Somalia, Vietnam, Algeria, Angola, Russia
Bofya hii http://www.youtube.com/watch?v=1GHFEHudqnw uone Bongo FC wakipokea medali
Baaab Kubwa FC Bongo... Hapana shaka mwaka huu mtafika Fainali...!!
ReplyDeletedu abdala ezza na ,ojuku bado mnajikumbushia enzi zetu za kisarawe na kidonge chenkundu ispokuwa huko naona mnavaa jezi lkn pale gerezani tulikuwa vifua wazi naomba msimnyime namba na ,kimbweru,jerry lkn sasa hivi jerry kishakuwa mtumzima duh nimekumbuka mbali masikini marehemu ,matido sijui km bado mnamkumbuka ,ispokuwa mbona rumi simuoni ,pamoja nakaboteka au walikuwa kazini ???? kiasi nimefurahi kuwaona kwani ni mda mrefu atujaonana karibuni holland
ReplyDeletewazee wa kazi mwaka huu mpaka fainali
ReplyDeletewanastahili sifa sana, habari hizi zingefaa zitolewe magazetini wabongo wote wawatambue hawa mashujaa.
ReplyDeleteMzee Mataruma nakukumbuka enzi zako midfielder la nguvu na chama yako ya akina wagadugu,tostao na ngereza pale mwadui,nisalimie finland.
ReplyDelete