
waziri wa habarti, utamaduni na michezo mh. muhhamed seif khatib akipokea kombe la hisani la jkm toka kwa keith masters rais wa tanzania youth sports charity organisation (tysco) ofisini kwake. kulia ni makamu wa rais wa tysco ulaya david palmer nyuma ya waziri ni mkurugenzi mkuu wa tysco allan kalinga shoto ni mratibu wa tysco vicent kinyange akifuatuwa na afisa mipango wa tysco victor mgoya. tayari yanga na simba wameshakubali kucheza na timu ya middlesex wanderers toka uingereza mwezi wa sita mwanzoni kwa mualiko wa tysco ambayo imeamua kufungua vituo 24 vya kuandaa vijana kucheza kabumbu nchi nzima pamoja na ungua na pemba. kombe hilo litashindaniwa kama charity shield ya fa na mapato yataenda kusaidia maendeleo ya soka la vijana nchini.
kombe jepesiiiiii
ReplyDeleteKama mpango huu tutaushikilia kwa makini wabongo basi soka yetu itapanda sana, bongo kuna vipaji vya soka lakini huwa tunakumbuka kuvishikia vinapokuwa above miaka 25 hilo ni tatizo kwa kweli eheh
ReplyDeleteah afadhali mmeturudishia umiseta .kila la kheri
ReplyDelete