
dogo sande a.k.a makinyonga (15) akicheza na vinyonga jana huko ei taun. sande amekuwa akicheza na vinyonga kwa kuwaweka mdomoni kwa takriban sekunde kumi kisha kuwatoa. pia amekuwa akiielimisha jamii kuhusu imani potofu juu ya vinyonga. na kwamba hata kama akikaa kichwani unaweza kumtoa wewe mwenyewe na kwamba si viumbe vya kutisha kama inavyoelezwa na wengi wenye imani za kishirikina…
duh, dogo balaa. Sasa si aanzishe mazinga umbwe, nakumbuka enzi za majani ya mkaratusi kugezwa biskuti na akina Power mabula kuzuia magari kwa mkono mmoja. MIM Hongera kwa kutuletea picha za dogo
ReplyDeletemmh! usituxingue we dogo, huo ni uchawi tu!
ReplyDeleteDogo mwanga. Du, mtoto mdogo unakuwa mwanga je ukizeeka itakuwaje?
ReplyDeleteanon Friday, March 02, 2007 12:36:00, huyu dogo sio mwanga jamani, amezoea kuwa karibu na wadudu kinyonga ni mdudu kama wengine tu tena mpole sana unaweza kumfanya pet wako, cha kushangaza hapo kipi? na wanaocheza na nyoka utawadefine vipi maana nyoka ni hatari zaidi ya kinyonga.
ReplyDeleteHuu ni ukatili dhidi ya wanyama! Anatakiwa awarudishe hao vinyonga ktk makazi yao......
ReplyDelete