Home
Unlabelled
mengi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Heeee jamani!!! mbona hawa wafanyabiashara ni wahindi tu??? wabongo mko wapi???? hi sasa kali, jamani tutapotea kwenye anga yetu wenyewe.
ReplyDeleteMengi anajaribu kutuonyesha kuwa yeye ni dam dam na hawa majamaa. Keep it up.
ReplyDeleteNi mtu safi sana huyu. Ana akili ya biashara na kaajiri watu wengi. Ana uzalendo. Maskini....ndio tajiri pekee MWEUSI Tanzania. Bahati mbaya WEUSI wenziye wanasiasa hawampendi wanamtosa na kukumbatia GABACHORI watoa rushwa maarufu duniani.
ReplyDeleteACHA UPUUZI WE! WAHINDI HAO WAKO PAMOJA NA NDIO MAANA WANAFANIKIWA.TOFAUTI NA WAFANYABIASHARA WA KIBONGO,KAZI KUCHOMANA TU NA MA BEEF YAKUTOANA UHAI.WAPO WAZAWA WENGI TU WENYE MAPESA ILA WANAJIFICHA AIDHA KUOGOPA USUMBUFU TOKA KWA VIGOGO AU DEALS ZAO NI ZA UNGA WA UDAGA AU NGOZI ZA BINADAMU.
ReplyDeleteroho yangu yote ina-imagine kila mmoja wao angekuwa amenipatia waleti yake kwa muda ule pale waliosimama pale tu, mwenzenu ningekuwa nala kuku kwa mrija ukerewe saa izi.
ReplyDeletenyingi mnaowaita hao MAGABACHORI na kuwatofautisha na WEUSI ama wewe anon mwengine unaouliza mbona wahindi tu, hiyo isikusumbue kitu all in all ni WATANZANIA na tena WAZALENDO sana. Mimi naongea kama MWEUSI na mmoja wa hao MAGABACHORI hapo juu ni practically close family tena nimekua namjua
ReplyDeletekama baba yangu mkubwa kwani amekuwa na baba yangu na wamechezea wote michanga na manati huko mkoani kabla hajashuka bongo kutafuta maisha na mungu akamjaalia uwezo kutokana na kuwa very focused na kufanya kazi kwa bidii. And believe me anon ulioongelea kupata wallets pesa iliopo hapo sio mchezo ni bajeti ya nchi ....... wabongo wengine badala ya kutafuta jinsi ya kujiendeleza personally tumekalia kuangalia rangi za ngozi za wengine IT SHOULD NOT MATTER WHETHER U R ASIAN OR BLACK WE ARE ALL WATANZANIANs...... !!!!!!!!Tutafika kweli ??? Bwana Mengi hongera sana kwa yote anayoifanyia Tanzanian community
wewe anon uliyesema mmoja wa hao wahindi kasoma na baba yako.Sasa baba yako yupo wapi?Ina maana huyo muhindi alikuwa kamzidi akili darasani au???Maana nilidhani baba yako angekuwa pia katika hiyo picha kama mfanyabiashara.
ReplyDeleteJamani hebu tumuunge mkono Mengi.Maana pale wakiamua kuzungumza kihindi Mengi atabaki hana wa kuongea nae.Ahahhhhhhhhh
Mzee mwenyewe wa biashara-BAKHRESA uko wapi???Maana unatambulika nchi nyingi kidogo africa.(TZ,Kenya,Uganda,.....)
ReplyDeleteWewe anony wa 7 March, 12:47:00 am kichwa sana,aminia! leo jioni (hapa UK) nilikuwa naongea na mama mmoja mtu mzima kiasi ambaye ni miongoni mwa maelfu ya watu wenye asili ya India waliotimuliwa na Last King of Scotland (Idd Amin) toka Uganda mwaka 1972.Anaongea kwa uchungu na anaikumbuka sana Uganda na namna walivyopata taabu,usumbufu na hasara kipindi hicho;anaumia sana akisimulia kuwa yeye alikuwa kizazi cha nne cha ukoo wao kuzaliwa Uganda.Baba wa babu yake alizaliwa huko mwaka 1870 (takriban miaka 65 tangu wangoni waingie Tanganyika).Ana uncle wake yuko Mwanza na kawashauri watoto wake wadogo waende Mwanza au Dar wakajaribu maisha ila yeye(huyu mama) anapenda watoto wake waende Uganda na this summer watafanya East African tour.Kuna watanzania wenye aili ya kihindi na kiarabu waliokuja Tanzania mapema tu kabla hapa mabila mengine hayajasogea pale-tunakumbuka Kilwa ilivyojengwa na waajemi na waarabu kati ya karne za 9 na 16 (kabla hawa wanaowaita wenzao majina ya kibaguzi wa rangi hawajafika nchi hii toka misitu ya Kongo au Sudan huko),sasa mabaki yao leo tutayapeleka wapi? Uzalendo hautokani na rangi ila akili ya mtu tu.Napinga sana tabia za kibaguzi kama hizo.Mimi mweusi na ni maskini wa kutupa ila sidhani kama umaskini wangu umechangiwa na rangi ya mtu mwingine.Leo hao wenzetu wanaweza kuja Tanzania bila shilingi moja mfukoni toka kwao ila watachangiana ktk temples zao au miskiti yao na baada ya miaka michache tu wanakuwa matajiri.Lakini mimi nikienda kwa mjomba wangu au jamaa wengine kuwaomba wanichangie pesa ya mtaji watakataa;sanasana watachangia harusi yangu tu ili tunywe na hadi tusaze lakini no cash at all;ndivyo sisi weusi tulivyo.Pia tunakua na kuishi bila malengo makubwa/marefu.Kama unautaka utajiri na unadhani hutaweza kuupata unaweza kuwaandaa watoto wako ili wawe matajiri wa miaka 30 ijayo-ni mambo ya mipango,kujituma,elimu na kutokata tamaa.Tazama watu kama Mengi na wengine wanaoinukia kwa utajiri miongoni mwa weusi wa bongo kama kina Shigongo na huyu jamaa alitolewa hapa anachangia mamilioni ktk elimu mkoani Mara (anamiliki kampuni ya kuuza na kukodisha majumba,nimemsahau jina lake)halafu jaribu kufuatilia historia zao utagundua kuwa walikulia ktk maisha ya kawaida tu ila wamejipanga tu vizuri na sasa wanafanikiwa.Hivi hatuwezi kuamua hapa tukutane kama watu 20 hivi tuchange vipaundi/vidola vyetu twende Morogoro au Tanga au Pwani tuchukue hekta kama 30 hivi za ardhi tupande matunda yaliyo bora na yenye viwango halafu tuwauzie hao Imalaseko, Score au Shoprite kwa USD badala ya wao kuagiza nje? Tukifanikiwa (labda baada ya miaka 7) hatutaweza kuisadia governement yetu kupata mapato na sie pia kujiinua kiuchumi? Tena baade tunaweza kuweka kiwanda kidogo cha kusindika na kukamua hayo matunda na kuuza ndani na nje na pia kuwapa ajira ombaomba wenzetu wa Bongo! Hivi unadhani ni lazma tuwe na milioni 800 moja ili kufanya hivi? Michuzi ametuonyesha njia na wengine pia wanaweza wakafuata kwa mtindo mwingine.Huyu bwana (Issa) anaweza kufa sio tajiri ila nadhani mwanae atakuwa anapo kwa kuanzia ktk maisha yake ya baadae.TUJITUME,TUACHE CHUKI DHIDI YA WENZETU WENYE RANGI TOFAUTI NA SISI.TUFANYE KAZI KWA BIDII NA KWA MALENGO NA USHIRIKIANO,NAAMINI NASI SIKU MOJA,MWENYEZI MUNGU AKITUJAALIA,WACHACHE WETU-KAMA SIO WENGI WETU-WANAWEZA KUWA KTK VIKAO KAMA HIKI ALICHOSHIRIKI MHESHIMIWA MENGI NA MATAJIRI WENZAKE. JK.
ReplyDeleteJamani hawa wafanyabiashara ni ordinary people tena wala hawako conscious na Uhindi wala nini, sisi ndio tuanattach hayo yote juu yao..Kuna huyo wa kwanza kulia, he's a very good man - a friend of my father's too..
ReplyDeleteWale wanaoleta uhindi uhindi wako kariakoo kwenye vibanda hasara wanauza maji ya bakhresa..Hawa watu wana upeo bana, sio wale watanzania wenye asili ya kiasia wanaojiskia wao ndio Miungu...Kenge maji!
Wahindi wanafanikiwa kuliko waswahili kwa sababu zifuatazo:
ReplyDelete1.Mhindi akianzisha biashara ni kitu cha kifamilia (Family business) ambako kila member wa Family anakuwa actively involved katika uendeshaji wake na kila member anakuwa mwaminifu katika biashara wakati mswahili akianzisha biashara kama ni baba au mama au mtoto biashara hiyo ni yake tu na yeye anaficha siri za biashara hiyo utafikiri uchawi.Hahitaji msaada wa family members wengine na hawaamini,na hata akiwaamini watamwibia uaminifu unakuwa sifuri.
2.Wahindi wanaamini ili uendeshe biashara kwa ufanisi unatakiwa uwe msomi waswahili wanaamini kuwa ili uendeshe biashara kwa ufanisi inabidi uwe mshirikina aliyebobea.Kutwa Wanakesha kwa waganga wa kienyeji.Hivyo utakuta wahindi wengi hata awe anauza kashata shule kasoma.Huwezi kukuta mhindi mbumbu kwenye biashara au aliyeishia la saba.
3.Kiwango cha uaminifu kwa wahindi kwa wahindi ni kikubwa mno.Wengi hukopeshana fedha na bidhaa hata bila kuandikiana kwa wanasheria wala kupeana mbele ya mashahidi lakini hawadhulumiani.Tofauti na waswahili ambao ukitaka kumkopesha hata uwe na wanasheria na mashahidi kaa chonjo unaweza ukadhulumiwa vile vile.Ndio maana waswahili kuaminiana kudogo.
4.Wahindi ni wakopaji na walipaji wazuri kwenye vyombo vya fedha kama mabenki.Tofauti na waswahili wengi.Hivyo hata mabenki wanawapenda zaidi wahindi kuliko waswahili si kwa sababu ya rangi zao bali kwa kiwango cha uaminifu wao katika kulipa mikopo.
5.Wahindi hutumia dini zao kuinuana.Dini nyingi wanazosali waswahili kazi huwa ni kusali Usiku na mchana kutwa na kuagana bila kupeana mitaji au mikakati ya kuondokana na ulofa.Wakikusaidia sana sana utagawiwa mtumba au utapewa tende au pilau la bure siku ya sikukuu aende akijamba njia nzima kila mtu ajue kupitia harufu ya ushuzi kuwa kala pilau.
Wewe anony wa 4.35 am hamna kitu, li message lirefuu na tena halina hata paragraph, wewe unadhani kila mtu ana muda wakusoma li message lote hilo? Tumia paragraph ili message zako ziwe na punch.
ReplyDeleteanony wa 4:03:00 pm nadhani ulikosa kazi ya kufanya au maboksi yamekutia hasira ndio ukaamua kuja hapa.topic ya kujadili ipo juu pamoja na picha,jadili hiyo na kama hauna cha kuandika funga matak% yako ulale asubuhi ukajiboksishe tena!
ReplyDeleteAnoni wa March 7, 4:35:00 AM speech very touchy na nimependa idea yako ya kukusanya hivi vipaundi (hapa UK) tukanunue shamba Morogoro, sasa tutawasiliaje tuongee business?achan na wabongo watafuta rangi za watu. mimi anon 12:27:00 AM
ReplyDeleteHey everyone,
ReplyDeletenobody should have to cry about, no jealous, no ration discrimination we are all human being we kama huna hela shauri yako acha kulumbana, oh mara mwingine kaandika mparagraph mrefu, mara nani asome lote hilo, we cha msingi ungemwambia aweke paragraph ujue unasoma kabisa insha. cha muhimu kaza buti tafuta hela uwe kama wazee wazima, kuna aliyezaliwa na mali?
...annony wa 1:55 march 7 point zako nimezikubali. Ulichosema ni sawa kabisa. Ila hapo pa mapilau ya sikukuu na kinachofuata baadaye, umeniacha hoi kabisa kwa kicheko....!!!
ReplyDelete