Home
Unlabelled
muchacho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Omar Kopa: Mtunzi na mwimba
ReplyDeletetaarab atakayekumbukwa daima
Na Mwandishi Wetu
MTUNZI na mwimbaji nyota wa taarab wa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Tanzania One Theatre (TOT-Plus), Omar Kopa (26) alifariki dunia jana mjini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo mchana Zanzibar.
Katibu wa TOT Plus, Gasper Tumaini alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Omar alifariki dunia saa 3:00 asubuhi akiwa nyumbani kwa mama yake, Khadija Omar Kopa, Mwananyamala Komakoma, Dar es Salaam.
Kifo cha Omar kimetokea wiki mbili baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mwananyamala, ambako alilazwa kutokana na kusumbuliwa na homa za mara kwa mara.
Taarifa za kifo chake ziliwajaza simanzi kubwa mashabiki wa muziki huo wa Zanzibar, hasa eneo la Kwahani, ambako ndiko alikozaliwa na kukulia. Baadhi ya mashabiki walionekana wakiwa wamekaa vikundi wakipeana taarifa za kifo cha msanii huyo.
Kabla ya kifo chake, uvumi ulikuwa umezagaa Zanzibar siku mbili zilizopita kwamba Omar amefariki. Taarifa hizo ziliwashtua mashabiki wake wengi, ambao walifika nyumbani kwake kuulizia iwapo zilikuwa kweli. Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Omar kuzushiwa kifo.
Katika siku za hivi karibuni, afya ya Omar ilionekana kuzorota. Katika baadhi ya maonyesho ya taarab ya TOT Plus, alishindwa kupanda jukwaani kuimba, hali iliyowapa wasawasi mkubwa wasanii wenzake.
Omar alikuwa mtoto wa malkia wa muziki huo nchini, Khadija Omar Kopa. Enzi za uhai wake, alikuwa mmoja wa wasanii wenye uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo za taarab. Pia alikuwa mahiri wa kupanga mashairi ya nyimbo na kuweka muziki.
Watu wengi walikuwa wakidhani kwamba mama yake ndiye alikuwa chachu kwake kuupenda muziki huo, ama pengine kumpa mafunzo ya kuwa mwimbaji mzuri.
Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa. Katika mahojiano na gazeti la Burudani, ambalo ni gazeti dada la Uhuru, Omar alisema wakati anaanza kujihusisha na muziki huo, hakuna aliyekuwa akifahamu kwa vile hakutaka ndugu zake wajue.
“Baba yangu hakupenda kabisa nijihusishe na muziki kwa sababu wakati ule alikuwa akinisisitizia sana kuhusu masomo,” alisema Omar katika mahojiano hayo yaliyofanyika Februari, mwaka huu.
Ijapokuwa alianza kujihusisha na muziki huo tangu akiwa Zanzibar, marehemu Omar alianza kupata umaarufu baada ya kujiunga na TOT Plus mwaka 2002.
Omar alitunga na kuimba nyimbo nyingi za taarab za TOT Plus, ambazo zilikipandisha chati kikundi hicho. Baadhi ya nyimbo hizo aliimba yeye mwenyewe na nyingine aliwapa wasanii wenzake waimbe, hasa zile zilizotakiwa ziimbwe na waimbaji wa kike.
Baadhi ya nyimbo zilizompatia umaarufu ni pamoja na ‘Tuko beneti’, ‘Nifagilieni’, ‘Sitaki ushambenga’ na ‘Ebwana ndio.’
Nyimbo zingine alizotunga, lakini zimeimbwa na waimbaji wengine ni kama vile ‘Huna mpango’ na ‘Wema haupo’, zilizoimbwa na Mwanamtama Amir na Aziza Mkumba.
Wakati akijiunga na TOT Plus, Omar alikuwa kama Malaika aliyeteremshwa na Mola kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikundi hicho kilichokuwa kimepungua makali yake. Pia alikuwa kama vile ameitwa kwa ajili ya kumuongezea nguvu mama yake Khadija.
Alijiunga vipi na TOT Plus?
Mwaka 2002 alifika Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria harusi ya mama yake. Baada ya harusi kumalizika, alikwenda kwenye onyesho la TOT Plus.
Akiwa ukumbini, kikundi hicho kiliporomosha kibao cha ‘Huyu ni wangu’, ambacho kwa kawaida huimbwa na Abdu Misambano. Omar aliombwa apande jukwaani kuimba kibao hicho.
Baada ya kuimba beti kadhaa za wimbo huo, mashabiki waliohudhuria onyesho hilo walilipuka mayowe ya kumshangilia kutokana na kumudu vyema kuuimba. Ilikuwa vigumu kuitofautisha sauti yake na ya Misambano.
Mara baada ya kumaliza kuimba wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TOT Plus, John Komba alimfuata Omar na kummwagia sifa kemkem, kisha alimuomba ajiunge na kikundi hicho ili awe mmoja wa waimbaji taarab.
Siku chache baada ya kujiunga na kikundi hicho, aliibuka na kibao cha ‘Tuko beneti’. Kibao hicho kilibeba albamu ya kwanza aliyorekodi na kikundi hicho.
Moja ya sifa alizokuwa nazo Omar ni kutunga nyimbo zake kwa kipindi kifupi. Alikuwa na uwezo wa kutunga nyimbo na kuikamilisha kwa siku moja, kitu ambacho kwa kawaida huwa ni kigumu kwa wasanii wengine.
“Kwa mfano, wimbo wangu wa ‘Nipepee’, niliomshirikisha mama yangu, niliutunga kuanzia asubuhi, ilipofika saa 10 jioni, nikaingia studio kuurekodi,” alisema wakati wa uhai wake.
Kipaji cha Omar cha kuimba taarab kilitokana na kufuatilia kwake masomo ya Quraan.
Kabla ya kukutwa na mauti, Omar alikuwa akifanya mipango ya kurekodi albamu yake binafsi ya kwanza ya mahadhi ya mduara yenye nyimbo nne. Nyimbo alizotarajia kuzirekodi ni ‘Raha ya Unguja’, ‘Ngoma ya kinu’, ‘Namuenzi mama’ na ‘Ukweli haufichiki’.
Alitarajia kurekodi albamu hiyo katika studio za Sophia Record kwa kuwashirikisha wasanii Mohamed Mbange, Samuel Mshana, Aziza Abdul, Khadija na Ababuu.
Hakika daima Omar ataendelea kukumbukwa na wapenzi wengi wa taarab.
sabah bado anadia kichizi mashallah, mtoto mtamu sana huyu.
ReplyDeleteaah! pole sana khadija kopa ina lilahi waina illahim rajiun. usiliye sana khadija ni kazi ya mungu. michu nisalimiye sabah mwambiye nampenda sana na namtamani kifuani mwangu.
We anon hapo juu sha anza uzinzi wenu, hapa watu wanaomboleza ka unamtaka sabah si mpigie cm kama hunayo bac ulisha dampiwa zamani waachie wenye nguvu.
ReplyDeleteWatanzania wengine bana washerati sana! Mi thimo!