nembo mpya ya kundi la wanaume halisi linaloongozwa na sir juma nature baada ya kujitenga kutoka wanaume tmk. kundi hili tayari limeshakamilisha albamu yenye nyimbo 14 na wako katika harakati ya kuizindua kwa maonesho ya mikoa kadhaa hivi karibuni.
hapa chini kuna ujumbe ambao kuna mdau katutumia tuusome na kuujadili
Bwana michuzi naomba sana uitoe hii katika glob yako

Imetokea baadhi ya Watanzania kutumia vibaya IT development kwa mfano cellphone zenye camera. Nasema wanazitumia vibaya kwa sababu wanawapiga picha kina dada wa Kitanzania walio maarufu (eg dancers, waigizaji etc) wakiwa uchi pale wanapokuwa nao faragha na kisha kuzitoa kwenye magazeti na sasa hata tulio nje ya nchi tunazipata kwenye emails.Tena wanawapiga bila ridhaa yao.
Nasema bila ridhaa yao kwani kwa kuziangalia (bwana Michuzi naweza kukutumia E-mail za kina dada hao maarufu wawili ila usiziweke hadharani maana ni aibu) hizo picha, utaona kuwa either wamelewa, au wamelala na hawajajiandaa kupiga picha.
Hivyo ni possible kabisa kwa simu zetu za kisasa mtu akajifanya anasoma msg kumbe anamchukua mtu picha. Huu sio ustaarabu hata kidogo. Sijajua kama huwa wanaziuza kwenye magazeti na kwa kiasi gani ambacho unakuwa tayari kumdhalilisha mtu namna hiyo.
Hata kama amekupiga chini sio dawa kumdhalilisha. Na hata kama hawa kina dada wana tabia mbaya, sio njia za kuwarekebisha, instead tunawaharibu zaidi. Na mwisho tukumbuke kuwa hata mmoja wetu (hata ndugu yako)anaweza kuwa victim wa huu ujinga unaoenea.
Nashauri kwa wanaofanya kamchezo haka ka kishamba waache, na hao kina dada wa kiTZ wasimwaamini kila mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Nature nimekukubali!hiyo nembo si mchezo,inaizidi hata ile uliyoibuni mwanzo Ya TMK wanaume (yenye shoka).kweli wewe kichwa.

    Kuhusu picha,its true huu si mchezo mzuri.Cha ajabu ni kuwa kwanini hawa akina dada wanau intertain?au wanapenda.Nakumbuka mmoja (Nora, i guess)alipotolewa ktk gazeti vyombo mbalimbali vilijitolea kumsaidia kisheria,hata waziri wa wanawake nae alisema aende akamwone ili amsaidie wamshtaki huyo mtu,maana Msichana alisema,anamjua,ni ex boyfriend!.Lakini sijasikia huyo binti akichukua hatua yoyote,mpaka nimesafiri sijui huko nyuma.Kwa hiyo labda(sina hakika) wasichana nao wanajitakia.mwisho,i think na dada zetu wawe makini,si kila anaekusifia na kukununulia bia,na kukupa lifti ni mtu mzuri wa kwenda kulala nae!

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa nakubaliana na aliyetoa ujumbe huu,hata mimi nilipata hiyo e-mail za picha za hao wadada.
    Kilichonishangaza ilivyowekwa kwamba ni 'aibu kubwa kumbe wasanii maarufu tunaowafahau ni makahaba'. Nachojua mimi wanawake hawafanyi ukahaba wenyewe tu,mbona hao waliopiga picha hawakuweka sura na uchi wao kwenye picha?kwamba tuwaone na wao.Shenzi zao.
    Tabia mbaya sana,wala hawajafanikiwa kutuconvience watz kwamba hao wadada ni makahaba,maana kama nora alikuwa amelala kabisa.Waache utoto,wafanye mambo ya maana.
    Asanteni.

    ReplyDelete
  3. Nawaunga mkono wote hapo juu kuhusiana na picha za udhalilishaji kwa hao kina dada wawili, kweli it is not fair mambo ya faragha kumwagwa hadharani, in short ni ushenzi!

    Kuhusu nembo ya TMK sijaifurahia kwa vile inaonyesha majani ya bhangi, je Tanzania tumehalilisha uvutaji wa bhangi. Wasanii ni kama role model/kioo cha jamii, vijana wengi wanawaangalia wao. TMK wanapoonekana kufagilia bhangi hiyo inakuwa sio sawa kabisa!

    Kwa mambo yote hayo mawili vyombo sheria vyetu ziko wapi?

    ReplyDelete
  4. NI KWELI KABISA SI USTAARABU KUMPIGA PICHA MTU UCHI NA KUZISAMBAZA , KAMA ALIKUWA MPENZI WAKO NA AMEKUPIGA CHINI YA NINI KUMVIZIA NA KUMPIGA PICHA UCHI KISHA UKAZISAMBAZA KENYE ENTERNET? NAOMBA MPIGE VITA HIVI VITENDO KWANI NI KINYUME NA UBINAADAMU NA PIA KWA WATANZANIA,

    ReplyDelete
  5. Huyo Dada AISHA mimi nilimtaka ili nioe kabisa lakini bado wamekuwa na kasumba za kutaka watu wanaowanunulia chips na pombe tu ona sasa,lakini bado ana nafasi njoo mimi niko majuu huku mbona usikii,michuzi nisaidie jamani.namba yangu ataipata toka kwako

    ReplyDelete
  6. Hao akina dada nao wasiwe wanajiachia ovyo!

    Hivi serikali si ilipiga marufuku matumizi ya hiyo alama ya jani? Hio yote ni kushabikia BANGE tu.

    ReplyDelete
  7. wanaotumia simu kwa picha hizo ni sahihi kabisa.wanatuonyesha upande mwingine wa shilingi ilivyo.tusitake kuona mazuri tu ya hao hata mabaya pia!

    Kila mtu ajali usalama wake na mahala alipo na ajue ana mtu wa namna gani ambaye wamekwenda naye huko alikoenda.Hii ni tathmini yao wenyewe!.

    kama ni maarufu basi watambue wanazungukwa na athari gani? kama waoa hawatambui wewe ndiye unatambua???!

    Akina dada hao waatmbue kitu kinaitwa "risk assessmnet",analysis of vulnerability na Countermeasures za kuwa maarufu.

    Huo ndio ushauri wangu na maoni yangu.

    ReplyDelete
  8. Hawa akina dada mimi siwaonei huruma, sababu sheria zipo kama hizo picha za Nora na Aisha MAdinda zilipigwa bila ridhaa yao wangefika kwa pilato muda mrefu. Hivyo nafikiri hizi picha kwa njia moja au nyingine wamekubaliana nazo, jamani msiwasemehe acha waseme wenyewe na pakusemea ni kwa pilato. Kwanza picha zenyewe zinatia kinyaaaaaa. Vipo vituo vinatoa msaada wa kisheria, kwanini wasiende wakasaidiwa? Labda ni tabia yao na biashara yao.

    ReplyDelete
  9. Hao jamaa si waungwana kabisa.
    EBU NI FOWARDIE kwenye hii email hapa chini.
    maddidy@hotmail.co.uk

    ReplyDelete
  10. Habari WaTZ wenzangu, Ni kweli kabisa nimi pianakubailana na watoa mada tajwa. Hiyo email mwenyewe niliipata. Kweli hii ni aibu, kwa mwanaume mzima na akili zako kufanya mambo ya kishamba kama hayo. Kwa mtindo huo hatuwajengi hao akina dada bali tunawaharibu mbele ya macho ya washibiki wao, na kama wakiwa makahaba kweli, sisi wenyewe ndiyo tunakuwa wa kwanza kulalamika. Wajinga sana hao "SHENZI TYPE"

    ReplyDelete
  11. Nembo imetulia mzee wa ugali ,kandamiza tu kwa sana mpaka watie akili sie wa mbali bado tuna kukumbuka usizisahau zile biti zako za kama kwa mzee MANDELA

    ReplyDelete
  12. Ninyi wa kabila la Rasta, nembo ama subliminal advertising ya joint, njaga, ganja, bangi? Au wenye Bendi hiyo ni watumizi wa hiyo bangi?

    Nimemwuliza mmoja wapo wa Rasta kweli anavyofikiria nembo ya namna hiyo, kanifungulia:

    O man, dont be bomba plast! That is holiweed! We smoke it! We chew it! Good medicine for pains, bones and stomach! Many plants grow meyard! It go well a mango, man!

    ReplyDelete
  13. hi wa tz wenzangu, hili ni jambo la aibu kweli lakini tukiangalia kwa undani zaidi hizo picha sio real, mie nimetumiwa hizo attachment pia, huyo aisha ni lini amekuwa mnene kiasi hicho?? na hata norah sura kama ni yeye lakini bado nakataa kabisa kuwa hizo picha ni utaalamu tu,

    kuna kozi nilikuwa nasoma zamani kidogo 2003, tulionyeshwa jinsi hata mtu unavyoweza kubambikiwa kesi ya uongo, teknolojia inakua sana na kila jambo linawezekana siku hizi, hizo ni graphics, animation na mambo kibao kwenye komputa,

    katika hiyo kozi tulionyeshwa kuwa inawezekana kabisa mtu akatoa sura yangu na kubandika sura ya michuzi mfano na ikaonekana mimi ndo nilikuwa nafanya jambo fulani, so inawezekana kabisa utaalamu umefanyika hapo kwa watu kuweka pic za aisha na norah kwenye hiyo miili isiyo na nguo, fungukeni macho jamani, hakuna hata mtu mmoja ameligundua hili,

    watu hapo juu mmeonyesha hisia zenu na hata kuwaita majina hawa wadada, but may be they are innocent, watu wanataka kuharibu majina ya wenzao tuu, kuna vi simpo programs hata mimi naweza fanya hivyo kutoa sura ya mtu mmoja na kubandika ya mtu mwingine, hicho kitu kinawezekana kabisa,

    hapo lazima kuna kamchezo kamechezeka jamani yani sijui nielezeje,michuzi kweli hata wewe hujui kama hili jambo linawezekana, nilifanya jounalism kozi kidogo hata huko nako nilionyeshwa vitu kama hivi,haya mapicha ya utupu mtu anaweza ku download na kuanza kufanya utaalam wake, sasa nyie msio amini mkija kuzikuta sura zenu ndo mtaamini,

    halafu jamani kitu kingine, haya mambo yaku chat online nayo yanamadhara yake, unachat na mtu hata humjui yuko wapi sijui mara unasema mmekuwa marafiki unabadilishana picha matokeo yake ndo hayo, au hata ki picha ulichoweka kwenye msn messenger mtu anaweza kuki copy, na watu wanaotumia website kama hi5.com kuweka picha mle nako zina kopika pia, hata hizi picha za michuzi humu blogoni zinakopika pia, so mtu akiamua kukuchafua anaweza na watu hawawezi kuamini eti mtu kakuchafua inakuwa kama hivi kila mtu anawaona hao wa dada ndo tabia zao,

    tuwe macho teknolojia ina madhara makubwa sana,

    ReplyDelete
  14. Hapa U.S. ukishikwa unapiga picha mwanamke sehemu zake nyeti bila ruhusa yake, polisi wanakukamata, na utamwona judge. Hiyo ni violation ya privacy act. Unakwenda jela.

    ReplyDelete
  15. Jamani nimesoma masikitiko ya watu kuhusu picha za utupu za Norah na Aisha zinazosambazwa kwa email. mimi kwanza ningependa kumwambia huyo mtu kama ni kweli hizo picha ni za hao wadada huyo aliyechukua ni mshamba tu inahusu nini kwenda kuwaanika kwenye internet???? na kwanza cha ajabu kiko wapi maana kama ni uchi kila mtu anao na norah anaonekana kajipumzikia anapunga upepo wake maana dar joto jamani, kwani mtu akiamua kuvua nguo na kunywa maji ni ukahaba? hiyo anayosema sijui condom mimi sijaona kama ndio condom hata kama ndio yenyewe so what? si kaamua mwenyewe bwana yeye ni mtu zaidi ya miaka 18 ana uhuru wa kuamua kufanya chochote na mwili wake, tena kama ni condom namsifu kwa kuonyesha anajali. haya huyo bwana shemeji mbona yeye hakuweka dudu lake tukaliona kuhakikisha hao watu walikuwa wanafanya ngono. hivi anajua maana ya ukahaba huyo? Norah, sha kuleni upepo mtakavyo Dar joto ati, wadada wenyewe bomba. huyo anayesambaza picha hana expore huku ulaya kuna nude beach kila mtu anavua na kula starehe si kwa ajili ya ukahaba tu. unaipa raha kile roho inapenda.
    Cheers

    ReplyDelete
  16. Bangi zinawafanya mazombi!

    ReplyDelete
  17. nature aminia babaake,unawezake kutengeneza nembo ya maana hivi?imetulia,ule mkono kumbe una mk nilikuwa sijagundua mpaka nilipotuliza macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...