hii ngoma imeingia hivi punde...

Hello Mzee Michuzi,

Naomba unitolee hii barua kwenye blog yako. Ahsante.
Napenda kutangaza kilio changu chenye uchungu mwingi. Mimi ni m-Tanzanianiishiye Uingereza (ukerewe kama uitavyo). Nimekuwa nikiwatumia ndugu namarafiki zangu vifurushi kwa njia ya posta lakini vinapotea. Kila nikifuatilia, naambiwa viliondoka huku salama na kama ni upotevu, basivitakuwa vimepotelea Tanzania.Inaonesha kuwa kuna baadhi ya wafanya kazi posta zetu ambao siwaaminifu. Wao hudhani kila kitu kitokacho ughaibuni ni mali sana nawangeweza kujipatia pesa za bila jasho.
Ukweli ni kwamba wamekuwa wakiniudhi kwani wakati fulani wanaiba hadi picha za familia. Si kwambanalalamika kwa kuwa nimegharamia sana, la, bali ni usumbufu unaokujamara uliyemtumia mzigo anapo usubiri kwa zaidi ya mwezi na nusu na kishaukaambiwa hajapata kabisa.Hii ni aibu. Wanatudhalilisha hata sisi tulioko huku. Kila ukienda postaunaulizwa mzigo ulikuwa unakwenda wapi, unasema Tanzania, tunaonekanawezi pia.
Yaani huku walishaanza kusema wataongeza bima kwa vifurushi vinavyokwenda kwenye nchi zilizo ajili wezi (baadhi ya wafanya kazi) posta kamaTanzania. Kuanzia sasa sintatuma mizigo yangu kwa kupitia posta zetu,nimechoka, nitatumia kampuni za wageni, uzalendo umenishinda.
Naomba wengine wote waliowahi kupoteza vifaa vyao kuacha kutumia postazetu hadi suala hili lipatiwe ufumbuzi.
Kwa yule mwizi, sina chakukuambia zaidi ya kusema mungu atakuzawadia kulingana na matendo yako.

Chifunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. pole ndugu ila ndio **UAMINIFU** kwa wa tz wengi ni sifuri,,hatuna hatuna kabisaaaa uaminifu yani ni wizi tu,, tumezidi,,,

    pole sana ndugu kwa kuibiwa vifurushi vyako, nadhani ni vema ukavikusanya vikawa vingi ugharamie tu DHL vitafika kwa walengwa,,ila posta tz hamna kitu uababaishaji mwingi,,

    ReplyDelete
  2. Unajua like father like sone. nchi viongozi wala rushwa na waizi wengi. sasa wafanyakazi wa posta ni kama watoto wakiona baba anishia bila kufikiri maslahi ya mtoto nao wanaona ni heri wajichukuliw chao mapema.

    Lakini it is not fair kwa sababu hata picha wanaiba. Sijui wanaenda kuwaonyesha ndugu zao na kusema huyu na mfahamu. Picha za mwanangu zimeshapotea kama mara mbili.

    ReplyDelete
  3. Pole sana ndugu kwani ni biashara na faida. Watapata bad reputaion, watakosa wateja, biashara itafungwa na hao wezi sijui watakimbilia wapi.

    Siku hizi kuna mashindano ya biashara na wateja wana haki ya kuchagua nani wafanye nae biashara. Waache waendelee kuishi maisha ya SU, watanunuliwa na kufukuzwa kazi.

    ReplyDelete
  4. Duuh! Mijizi hii inaiba mpaka picha!!! Mimi sithubutu kupeleka chochote Tanzania kwa kupitia posta zetu. Mara nyingi kama siendi mwenyewe basi nitatafuta mtu anayekwenda ili nimuombe anipeleke mzigo wangu. Vinginevyo sithubutu kupitisha chochote hapo kulipojaa wakwapuzi.

    ReplyDelete
  5. Chifunda na Kwame, ndio uaminifu ni mdogo, lakini kabla hamjapigilia msumari, hebu tuangalie ukweli, umesema UMEAMBIWA, je huko kuna tracking systems zilizotumika kukuhakikishia zimeondoka? Kwani kuna unpriviledged wangapi wanaobeba vifurushi na kuvipanga kwenye POSTA za huko? You got to have evidence rather than just kuambiwa kuwa vimeondoka huko. Mbona sisi tunatuma vifurushi kwa ndugu zetu na vinafika salama usalimini? Au wewe hutumi ila unatumia nyanja hii kudanganya ndugu zako kuwa kila ukituma vinapotea? Acheni hizo bwana..... huo ni ushamba kutukuza huko na kufikiri wasio waaminifu ni nyumbani tu. Be real, we know how it goes man....

    ReplyDelete
  6. KWELI HII NI AIBU SANA.HATA MIMI WANANIBOAGA SANA.

    KWA VILE WAMEJISHUSHIA HADHI WENYEWE NI VYEMA KUACHANA NAO TU.

    TUMIA KAMPUNI ZINGINE,ACHANA NA WEZI.

    ReplyDelete
  7. wewe unayesema hapo kwa vile hayajakukuta. Siku ukituma kitu cha muhimu ndio utakapojua uchungu wake ni nini ukiambiwa hakijafika.
    Wewe uwadanganye TZ kuwa umewatumia hata picha tu itakusaidia nini?
    Underpriviledge wako unaowasema ni nchi gani? Kwa vile USA post office is a Govt Job na inalipa vizuri sana kuliko hata ualimu. Na mambo ya ugaidi yalivyoingia ndio usiseme..wako very careful. Hata barua yako ipotee miaka mingapi hapa mara kuna siku inaletwa kwanza inawekwa kwenye mfuko vizuri na maelezo kuwa imepatikana wapi na lini.

    Tuache kutetea vitu vinavyoonekana. Ila kwa vile monopoly imekwisha sasa tutatuma kwa kupitia njia nyingine na wao watakosa kazi.

    ReplyDelete
  8. Jamani, yani ni jana tu nimetoka kupokea kamzigo toka kwa besti yangu Ukerewe..Mama yake ndio alioupokea posta..Huyu besti alishatuma mzigo mwingine before huu wa jana, ukapotelea posta.

    Huyu mama ni mpelelezi, akamchimba mtu flani pale posta akasema huwa wanachomoa vitu na kuacha either box au bahasha tupu, so ushahidi kuwa vitu vinachomolewa upo..

    Mi naona ni kiasi cha kujipanga watu wachache, tukaivamia posta section ya parcels na kuongea na bosi wao, watimshwe watu kazi, waje watu wapya and clean..FAGIO LA CHUMA lipitishwe!

    Kweli inachosha sana, mtu anajitolea hela yake kutuma mzigo, unabaki kuibiwa, yani wanaiba hadi picha na nguo za watoto. Kenge hawa!

    ReplyDelete
  9. Aisee, THIS is REAL, niko ubelgiji, nimemtumia mtu CD tatu zenye nyimbo azipendazo na USB drive ya SONY microvault 2GB, ni ndogo kama ukucha, tangu January hadi leo havikufika. Kazini Tanzania wakanitumia makaratasi ya kujaza, yalifika ndani ya siku 7 tu. Kama vili sijakoma, ndugu yangu akaninunulia mashati ya batiki manne na kuyatuma kwa njia ya posta kwa gharama ya shs 47.000 Tshs, ni tangu february mpaka leo. Wanaboa mno. Nilituma dawa za mgonjwa last year zilifika, ila ilibidi niandike juu, usiibe ni dawa ya mgonjwa mahututi, OKOA maisha. Kwa kweli hata mie situmi kwa posta tena, washindwe na walegee! Nimetumiwa risiti za utumaji za huko Tanzania, wazungu hapa wananitolea macho havijafika vitu hivyo, na hakuna jinsi ya kutrack package huko Tanzania. nilidhani ni mie tu ndo naibiwa.

    ReplyDelete
  10. couldn't agree with you more. Posta yawezekana baadhi ya wafanyakazi ni wezi ambapo wanaharibia sifa ya shirika pamoja na wale wasio wezi.
    anayekataa kwamba hujafanya research (anonymous 7:55) ni yule ambaye hataki ukweli, unless hajaishi bongo. Airport yenyewe wanakuibia iwe perfume, viatu or anything kadogodogo they will try to steal from you while your within airport waiting for your mizigo, sasa kama wao wanaweza, walio posta ambao hata wewe haupo, ndugu zako hawajui lini mizigo inaingia ndio wataacha kuiba? let's be realistic here.

    ReplyDelete
  11. Halafu we anonymous wa Friday, March 16, 2007 7:55:00 AM kama wewe ni mmoja wapo wa hao watu wa posta kaa kimya maana tunakuja huko kuwa-sort out and put you into your place...

    Kama watu ni wezi na kuna watu kibao wanalalamika kuhusu the same thing, wewe unawatetea wa nini? Weweeee, acha hiyo wewe!

    ReplyDelete
  12. Nakubali kuwa wizi upo, lakini si kila mtu pale posta ni mwizi. Mimi nina experience tofauti, kwani nimekuwa nikituma vitu kama viatu, nguo, picha na vyote vimekuwa vikiwafikia. Cha maana kama mzigo umetumwa REJISTA na BIMA pia. Lakini ukituma kama unatuma peremende, basi wenye njaa wanaukomba!! Vile vile na ndugu zetu hapa Ulaya wanatabia ya kutumia hii faida ya umaskini wetu Bongo kutudanganya kuwa mzigo walituma! Kama kweli wametuma wakupe evidence za kutumwa kwa MZIGO huo, wewe uliwalipa wao na wala si POSTA TZ!! Laiti kama ukisema kuwa mzigo umefika home, lakini CONTENT ndani ndo zinakasoro, hapo kuna jambo!!! KUWENI makini WANDUGU.

    ReplyDelete
  13. Tanzania ni nchi yetu wote tupende tusipende kila mmoja anakupenda nyumbani kivyake.

    Hakuna kitu duniani kinachopita kusema ukweli pale panapo hitajika. Kuna ukweli watu wanaiba sana posta watu wengi yamewakuta lkn sema tu wanaona hata wakisema hakuna follow up bac wanaacha tu.

    Zaidi ya hapo watanzania wengi tu ndugu au rafiki wanadanganya wenzao walioko nje ya nchi kwa transactions za kila aina kujenga nyumba, biashara, nk. Hayo yanatokea so palipo ukweli usemwe sio kwavile wewe hayajakukuta ndoo useme ni uongo au eti ni sababu ya kudanganya nndugu...

    Kama alivyo sema anon mmoja hapo juu malipo ya maoovo yote yapo soon or later. Hakuna cha mbabe au nani. Acheni wizi na uongo hautufanani watanzania!

    Mungu ibariki Tanzania, viongozi na hasa hasa watu wake!

    ReplyDelete
  14. ni kweli poster bongo ni wezi,hata mimi yamenikuta,huku ukituna kwe register au recorded huo mzigo unakuwa chini ya uangalizi mpaka unapofika bongo.tena huku ukiuliza unaambiwa mpaka siku ulipofika bongo.ila hawana wezo wa kufuatilia ndani ya tanzania,ila wanachofanya wao ni kukulipa kupitia insuarence yako.sasa waneiba picha ,hata wakulipe pound ngapi ni kazi bure tu,post bongo jirekebisheni

    ReplyDelete
  15. Tatizo posta bado wafanyakazi wao wengi ni wale wa miaka ya 47.Wagumu kubadilika na shule wengi hawajaenda ni wale waliofeli form 4,form 6 na darasa la saba

    Shirika la POSTA inaelekea halijali sana kuingiza damu mpya ya vijana wasomi wenye mawazo mapya wala kuhamasisha upandaji wa viwango vya elimu kwa wafanyakazi wake hasa wale wanaohudumia wateja moja kwa moja mfano kaunta,kwenye mizigo na vifurushi n.k

    Posta kunahitajika mabadiliko ya uongozi na wafanyakazi kuanzia chini kabisa hadi juu kabisa.

    ReplyDelete
  16. Anonymous ulietuma dawa umenichekesha sana...Yani hawa watu wa posta hawana dini, ni laana tupu!..

    Basi na mimi ntamwambia besti yangu Ukerewe aandike hii parcel ina mapepo, ole wako ufungue..Maana waTZ kwa kuogopa mapopobawa!..

    ReplyDelete
  17. Hii ni kweli---Sep/06 nilikuwa bongo, wakati wa kurudi huku nikajisahahu nikaondoka na 20000/=(shilingi)---- X-mas nikaamua nimuwekee mshkaji kwenye X-mas kadi--hadi leo hiyo kadi haijafika---at the same time nikamtumia mshkaji $50 kwenye kadi--likewise hadi leo haijafika----maana kwenda western Union kutuma $50---unaona hata noma--I guess I have learned my lesson well. Ndipo hapo nikakumbuka tulipokuwa sec school---washenzi walikuwa wanachukua barua na kuingiza pini katikati, ikigoma kidogo wanajuwa kuna chapaa na kamwe hutaiona---this is verry unethical. Michuzi hivi bongo somo la Ethics linafundishwa at any level????

    ReplyDelete
  18. Revd. EVM nakubaliana nawe kabisa. Tujaribu kuwafuatilia hao wazungu wetu kwani huenda mzigo wa mafara sisi hawaipeleki au ikija hawaipokei kwa kuogapa kuwa hayo mabatiki yenu yana upele na ukurutu.

    ReplyDelete
  19. mi nilikuwa nawatumia picha ndugu zangu mpaka nikachoka, hawazipati??!! hata nikawa naandika "no money inside" bado hazifiki. duh bongo!
    nikatuma kibox uzuri nikakinunulia insurance, nikawapa number ndugu zangu mwaka mzima wanaenda posta hawakipati. baada ya mwaka nika-file insurance, mwezi baada ya kufile insurance kibox kikarudi eti kimekosa wa kuki-claim wakati nimeweka phone number, physical address na mwenye ku-claim alienda posta mara kibao kufatilia. sasa hivi situmi hata barua posta wana njaa sana pumbafu zao

    ReplyDelete
  20. Pole kwa matatizo ndugu siku nyingine kuwa mwangalifu unapotaka kutuma vitu ukiwa ulaya hasa UK ukienda posta kuna kitu kinajulikana kama Datapost bongo wanaita EMS jaribu kuulizia service hiyo na uhakika ukitumia Datapost mizigo itafika salama salimini, Good luck!

    slimdel@hotmail.com

    ReplyDelete
  21. Mimi nakataa kabisa watu wanaosema mizigo isiyokuwa trackable inapotelea wakati mwingine huku huku.
    Mfano halisi. Nina cousin Kenya na kuna siku nilituma package mbili. Moja iende kwake Kenya na nyingine iende TZ. Ya kwake ilifika within 7 days. Hiyo ya bongo haijafika mpaka leo. kwa hiyo mnataka kuniambia kuwa jawa wazungu wana hold mizigo ya bongo tu?

    Na jingine linalokera hata huo mzigo ukifika wanacharge ushuru twice the price of the content. Na risit hawakupi.

    Wangewekewa camera kila mahali toka mzigo unavyoingia kwenye facilities zao mpaka unavyomfikia mteja.

    ReplyDelete
  22. ndugu ukituma mzigo hakikisha iko insured na utume kwa registered au recorded basi itafika salama mimi nimetuma mingi na sija pata matatizo yeyote yote imefika

    ReplyDelete
  23. Nyie mnaosema vifurushi vinaibiwa posta za Tanzania.Jaribuni kutuma vifurushi posta za Nigeria.Ninaapa mbele ya Mungu mtalitangaza Shirika la Posta Tanzania kuwa ni shirika la wacha Mungu watupu ambao hata kama wana dhambi, dhambi zao ni ndogo mno kiasi kuwa Mungu hawezi hata zitilia maanani hata mkimshitakia.

    ReplyDelete
  24. Jamani mbona mie niko ukerewe na kila siku natuma nguo naweka na mobile phones mbili au tatu,nakatia na bima havipotei vinafika salama salimini.msiikandie bongo ni nchi yetu na wote mmetoka huko au kwa vile leo mmekuwa warundi mnaisaga?east west home is best!MKUMBUKE MDHARAU KWAO NI MTUMWA SO ARE U JAMAICANS OR INDIANS AMBAO HAWAKUMBUKI KWAO?

    ReplyDelete
  25. Jamani tuipende chi yetu!!!! If you sending money then use appropriate ways the same goes to parcels!!! insure them.... achana na mambo ya tz watu wana njaa, mizigo inafika. For once lets say something positive about our motherland........god watu wengine bwana!!!!! oh ukerewe ukerewe

    ReplyDelete
  26. Hata mimi nimetuma picha kwa ndugu na marafiki Tanzania na hazikufika! Hata greeting cards zimeibiwa.

    Huo mchezo wa kuiba mizigo ni ya miaka mingi. Dawa waweke hidden cameras na wafanyakazi wakikamatwa wafukuzwe na wafunguliwe mashitaka.

    Kwa kweli inaudhi sana huo wizi!

    ReplyDelete
  27. Nyie mnaosema tuseme something positive about our country, kama nimeibiwa mizigo niseme tu ehe...post wanaiba lakini ni wachapa kazi bora?

    Watu wanaosema wengine tuwaongo hapa tu ni wale hawajawahi kutuma anything back home since they left the country. Lakini mwenye mazoea ya kutuma kitu mar kwa mara unalern. Weka insurance na tumia DHL.
    Uwongo sifichi mara nilivyoona wanacharge ushuru kama nini. Na guarantee ya mzigo kufika ni 25%. Nimehamia DHL na ni nzuri sana kwa package kubwa na unamalize mambo yote hapa hapa. Huko wanapokea tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...