
askari wa kikosi maalumu cha kuzuia ujambazi wakikusanya magamba ya risasi yalokutwa leo sehemu ya kurasini mivinjeni jijini dar baada ya greda linalofanya kazi ya upanuzi na ujenzi wa barabara ya kilwa rodi kuyafukua. polisi bado hawajatoa taarifa rasmi ya kukutwa kwa magamba hayo wala idadi yake na sababu ziliopelekea kuwepo kwake hapo mahali. ujenzi na upanuzi wa barabara hii ya urefu wa kilometa 11 na ushee na ambayo ikiisha itakuwa ya njia mbili kuanzia mbagala umezinduliwa majuzi na jk na inaghalimiwa na serikali ya japan
Michuzi kuna kamchezo hapo maana kuna matukio mengi sana yanafanyika na ushahidi unapotea i mean maganda yanaokotwa watu wanatamabaa na hayo maeneo ya Mivinjeni ndio kwao hao wanaokota maganda sasa watuambie yanawahusu ama?
ReplyDeleteHii issue inanichekesha, mi nilidhani wameokota risasi kumbe maganda!!!, Hayo bwana kuna mtu aliyabeba kutoka maeneo wanayolengea Shabaha kama Kunduchi vile akidhani dili miaka hiyo, akaona uchafu akaya damp hapo sasa leo hii imekuwa uchunguzi, uchunguzi gani hapo hebu waendelee na uchunguzi wa kesi za wafungwa wasipoteze muda buree
ReplyDeleteHawa wachunguzi njaa kweli. ndio maana kesi nyingi hazina ufumbuzi. Iweje risasi zinazoshukiwa ama kitu chochote cha mashaka kuokotwa kama njugu na mikono wazi bila kuwa na glove. Sasa utabainije alama za vidole za wahusika wakati askari kanzu wenyewe walishachafua na vijikono vyao!! Bongo kazi kweli!
ReplyDeleteHizo sio risasi ni maganda ya risasi wanachofanya hao ni kuyazoa wakayatupe dampo ili jamaa waendelee na ujenzi wa bara bara
ReplyDeletehapo kesi atambambikiziwa mlevi aletoka baa usiku kazidiwa kazima karibu hilo eneo mpaka kesho yake, au mtu yeyote tu mwenye ugomvi nao lazima apewe kesi uchunguzi umekamilika
ReplyDelete