jengo pekee la sinema lililo hai. baada ya tv kuingia bongo majumba yote ya sinema yalikufa kifo cha mende

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Bro Michu mie unanikata stima tu hilo anga lilivyo blue yaani nina miezi kadha huku kwa joji kichaka sijaliona anga la namna hiyo, ni mwendo wa mibarafu kwenda mbele sipendi!Aah!wacha nijirudie zangu bongo mie.

    ReplyDelete
  2. Unajua wamiliki wa hizo biashara za sinema bongo hawajui marketing. Wao wanajua kujenga na kusubiri watu waje. Lakini TV sio kikwazo kwa sinema. TV haiwezi kubadili raha ya big screen. May be home cinemas zikianza kusambaa hapo ndio majumba ya cinema itabidi yakuna kichwa.

    ReplyDelete
  3. ...mnh, na kweli; enzi hizo Empire Cinema, jumapili si foleni hiyo kwenda kumwangalia Bruce Lee na Chuck Norris "wanavyozidunda". Yaani ndio kusema kina Empress, Avalon, hata Starlight Cinema kwisha??? ama Bongo... Hapa Ukerewe bado majumba ya Cinema yanapeta, nadhani Marketing na Copyright laws ndio urasimu bongo! Ipo siku hiyo starehe ya kuangalia Cinema kwenye hayo maukumbi yatarudi!... Mnaikumbuka Drive Inn Cinema?... Vijana wa zamani mtakumbuka foleni ya magari kuingia Cinema inaanzia Namanga, watu wanajimwaya mwaya kwenda kuangalia Saturday Night Fever!... Enzi hizo!!! Mambo kwa wakati wake. ~MchongomaMwiba~

    ReplyDelete
  4. Pale mlimani city kuna jumba jipya la cinema linaitwa Cineplex kama sijakosea,limetulia sana.

    ReplyDelete
  5. Hapa ni Avalon Cinema nini?

    ReplyDelete
  6. Unalosema kweli kabisa Anon hapo juu.Kujitangaza ni kitu muhimu sana na new world cinema wako nyuma sana kwa hilo.Ndiyo maana kuna trailers na free preview clips za movie yoyote na ndizo ambazo zinatakiwa zifanyiwe advertisement kwenye TV.Kwenye magazeti pia ni sehemu nzuri ya kupata full timetable.Nilivyotoka bongo sikuwa nimeona haya labda sasa hivi.

    ReplyDelete
  7. Kwani nyie ina maana hamuelewe maana ya kuona movie kwenye cinema au kuona nyumbani kwenye TV???????
    Kwanza jiulizeni kwa nini nchi za maendeleo kila mtu ana TV na mjumba ya cinema, market ndio inazidi!!!!!
    Mnataka kuniambia watanzania hawajui maana ya Cinema mpaka leo wanavifikiri ni TV ya kushare????

    ReplyDelete
  8. SASA MBONA HUJAPIGA PICHA za parking ya, ticket office na mpaka ndani tukaona?

    maana si unajua tunataka tujue kama ni sawa na WARNER VILLAGE au mamabo ya SHOWCASE...kama unanielewa

    hebu rudi kapige tena picha hizo tujue kama kweli wako serious huko Africa au wana bahatisha

    ReplyDelete
  9. Anony wa kawanza pole sana,njoo hapa california usiende bongo kwani anga ni bluuuuuuuuu hata wingu 1 hakuna

    ReplyDelete
  10. Watanzania tunapenda kukosoa jitihada za wenzetu na tumekuwa wagumu kutoa ushauri. Sasa wenzangu mnaoponda jitihada za mwenzenu kuwajengea jumba la sinema mnamaanisha kitu gani. Kinachotakiwa ni kushauri jinsi ya kufanya ili aweze kufikia majumba mengine yaliyo dunia iliyoendelea. Pia usifananishe tanzania na marekani, wao wako mbali zaidi yetu sisi na kuwafikia si kazi ya leo au kesho. Sasa kama huyo Anon anayetaka kufananisha jumba la sinema na Warner village anakosea kabisa. Sifieni jitihada za wenzenu, mnasahau kwamba Tanzania ni kwenu hata ufanye nini wewe ni mtanzania. Elekezeni kipi kifanyike ili na sisi tuwe na majumba mazuri, si uzuri wa jengo bali hata vibwagizo vingine viwe vivutio vya kuwafanya watanzania kwenda kuangalia sinema. Kama Anon mmoja alivyosema waongeze kujitangaza sehemu mbali mbali, japokuwa ninaungana na huyo mmiliki kuwa anajitahidi kujitangaza, kinachotakiwa ni kumshauri njia nyingine ya kujitangaza zaidi. Binafsi nimeona akijitangaza kwenye magazeti, weekly newspapers tena ambazo ni free kwa wasomaji, sasa basi kama watanzania tumsaidie na sio kumkandamiza. Kwenda kuishi ughaibuni isiwe sababu ya kutaka kuona bongo ni hovyo, la hasha! msisahau nyumbani wandugu!!!

    ReplyDelete
  11. Mtuachie tulio bongo tufaidi na New World Cinema letu bwana! Si mnajua watu wengi sasa wanatumia cellphones? Kwa taarifa yenu tu karibu kila celphone company offers ratiba za cinema ndani ya jumba hili! Na sio cinema peke yake bali hata matokeo ya EPL, UEFA games, and other sports and entertainment news, finacial news etc. Vilevile, mtaani machinga wana mabootleg movies za kutoka China, and, contrary to some people waliopo nje, zina good quality and the language you can change if you have a dvd remote control! Ila hazina yale mambo mengine kwenye genuine DVD ya Previews, trailers, deleted scenes, bonus views, etc etc. (Napinga sana ubootleg but, hey!) Wale waliopo Marekani na ni wapenzi wa Jack Bauer's "24" mpo episode ya ngapi? Huku ninapeta tu - kwa mfano, season opening yenu ile ya saa mbili mnaianza huko sisi huko tulikuwa tayari episode ya 4!!! You just have to know some people to get virtually any show za US or UK - Go figure!

    ReplyDelete
  12. Watu mnasema mko 'majuu' lakini uelewa wenu mdogo sana.TV hai affect cinema,kwa sababu hizo movie zinazoonyeshwa kwenye cinema zinachukua zaidi ya mwaka mmoja,au miwili kuonyeshwa kwenye tv.Kawaida zinaenda kwenye dvd kwa nza baada ya kama miezi sita au mwaka saa nyingine,then mwaka again after that kuonyeshwa bure,lakini kama una SKY,unaweza kuona kwenye box office wakati zinatoka kwenye dvd.Hio New World Cinema ni bomba sana,ni kama ya huko tu...sound bomba sana,na movies ni latest.Yes,huyu owner anaonekana hajitangazi sana kama mtu unavyotegemea,lakini wanajitahidi,maana kama una CELTEL 32K,unapata kwenye text moja kwa moja.Kwa mlio nje,sasa hivi inaonyeshwa ROCKY BALBOA,na next week tunacheki DREAM GIRLS...

    ReplyDelete
  13. Mh Misoup jamani hii umenikumbusha mbaliii acha tu,enzi zile na my boyfriend wangu hapa ni mtoko babkubwaaaaaaa!!!!!!!!!!Asante sana misoup.

    ReplyDelete
  14. 1. Hodi?

    2. Karibu?

    1. Wazazi wapo?

    2. Wazazi!

    1. Mawazo ya kitoto! Kwaheri ya Kutoonana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...