
niko mbele ya nyumba ya zamani ya mwalimu butiama. nilitegemea kwamba kwa vile kuna nyumba mpya hii ingegeuzwa kuwa makumbusho badala ya jengo lingine tofauti lililojengwa kama makumbusho ya mwalimu. nilipotembela humu alikuwa haishi mtu hivyo hali yake ilikuwa sio nzuri sana. natoa rai makumbusho ya mwalimu yaletwe humu na lile jengo la makumbusho yake ligeuzwe aidha shule ya watoto kwani sikuona sababu hii iachwe tupu kwani wageni wangefurahi zaidi kuona sio vitu tu bali pia mahali halisi alipoishi baba wa taifa


Wazo lako ndugu Michuzi ni zuri sana. Hebu ongea na hao waheshimiwa ninatumaini watalifanyia kazi.
ReplyDeleteNahisi hapa nyumbani (nyumba mpya) patakuwa pana upweke sana baada ya Mwalimu kuiaga dunia, hata idadi ya wageni wanaotembelea hapa itakuwa imepungua sana, ukichukulia kwamba wengi walikuwa wanakuja kwa ajili ya Mwalimu na sasa hayupo duniani
ReplyDeleteWazo lako ni zuri kwani sana litaongeza watu wanaotembelea hii makumbusho ndogo na kupunguza upweke