????????????

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Haya ndiyo matatizo ya serikali zetu za mitaa. Yaani jiji la Mwanza limeshindwa hata kuitunza hiyo sanamu, check ilivyopauka. Hapo hakuna hata ile maana ya kumuita Nyerere baba wa Taifa, kama sanamu yake haitunzwi. Zumba's

    ReplyDelete
  2. Eee bwana umenikumbusha mbali sana, michu kuhusu hii sanamu. Pale Tabora Community centre kuna sanamu ya Baba wa Taifa kama hiyo yaani copy right. Sanamu ile iliwekwa mwaka 1988 nakumbuka wakati sherehe za CCM kitaifa zilipofanyikia Tabora Tabora, kipindi hicho nikiwa nacheza Gwaride la Chipukizi wa CCM, nikiwa shule ya msingi. Kwa wakati ule sanamu ile ili Cost Tsh 18 Million. Sasa hebu piga factots na inflation na nini utapata gharama zake kwa sasa.

    Kinacho sikitika pamoja na kutumia gharama zote za sanamu baada ya hapo ikatelekezwa haifanyiwi ukarabati. Sasa najiuliza je kama gharama halisi zilikuwa ni zile basi sanamu hizi zina thamani kubwa sana kifedha na kumbukumbu ya baba wa taifa kwa vizazi vijavyo.

    Swali ni je, nani wa kuzihudumia? Serikali ipo wapi mpaka sanamu inapauka hivyo kama imepakwa unga wa ngano usoni, je hawaoni kuwa hii ni kumdhalilisha baba wa taifa?, je hawaoni kuwa hela ya walipa kodi inaangamia kwa kugharamia vitu vikubwa ambavyo hatuwe kuvi maintain.

    pilingu.

    ReplyDelete
  3. Jamani hivi huyu aliyechonga sanam anamjua Mwalimu kweli?mmh hapo pana utata mana hafanani hata chembe.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli nimekuelewa fika kwa kuweka alama kadhaa za kuuliza. Maana ukiangalia bustani inayozunguka sanamu ya "SHUJAA" wa Tanzania, inatunzwa, tena vizuri sana. Lakini sanamu iliyogharimu fedha nyingi sana inaachwa mpaka inakuwa ni "eyesore" kwenye hiyo bustani. Nadhani halitakuwa jambo baya kumwamsha Mtukufu Meya kutoka huko kwenye usingizi mzito aliko... Hii inatia AIBU sana!!!

    ReplyDelete
  5. HIvi hawa hawajabadilisha tu hiyo sanamu kimeo hadi leo, waajabu sana. wana mdhalilisha baba wa taifa

    ReplyDelete
  6. Hii sanamu ililalamikiwa kwamba haifanani na Mwl Nyerere,lakini ipo tu.Kama Sokoine vile...mmh!
    Sasa ilivyopauka ndo kitukoooo!

    ReplyDelete
  7. Nimeangalia picha zote za huu mji zikanifurahisha sana ulivyomsafi. Yaani ni mji msafi sana . Ila kwenye hii sanamu kweli sio vizuri. Inabidi waitake care.
    Wamemsahau mwalimu na kifimbo chake? Atawajia huko maofisini kwao awachape kishenzi

    ReplyDelete
  8. hivi ni lazima pawe na sanamu ya mwl hapo mahali???

    manake wengine hatuelewi vema protokali, kama si lazima bora iondolewe jamani kuliko inavyoonekana sura mbaya afu kama vile Mwl alikuwa anatumia mkorogo inavyoonekana, kwanini kumdhalilisha mzee wa watu lakini? afu mkewe yuko kanda hii hii? bila shaka anapitaga hapo duuh!
    ivi michuzi haya maoni yetu unasaidiaje kuwafikia walegwa, au nikiburudisho cha sisi wachache wenye access ya internet??

    Pilingu na wewe ulikuwa shule ya mshingi afu ukafanikiwa kujua gharama za sanamu tabora??????kwakweli midomo mali yetu

    ReplyDelete
  9. We Anon wa 11:57 Am Wewe inaonekana bado upo mbali kidogo, Gharama anaweza jua hata mtoto wa chekechea provided inatangazwa hadharani na wote mnaisikia, kwa taarifa yako mimi nina kumbukumbu ya mambo yote niliyoyasikia kuanzia nilipofikisha umri wa miaka sita, sasa kama wewe huwa huzingatii unalosikia kila siku basi ndio waleee, mpaka leo mkiulizwa rais wa Tanzania nani mnajibu NYERERE, pole sana.

    ReplyDelete
  10. Sir Issa vipi Mzee huyu MWL Nyerere kweli shujaa...Duu

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli sisi tunoaishi mwanza tukifika eneo hilo,hua tunainamisha vichwa chini kwa aibu.didn,t you notice issa?

    somebody plz get rid of that statue of shame.

    ReplyDelete
  12. Ninahofu hivyo ndivyo uwanja mpya wa taifa utakavyoishia. Watanzania tunajua kutumia hela nyingi kutengeneza kitu halafu tunatelekeza. I really hope it won't happen to the new stadium.

    ReplyDelete
  13. Michuzi usingeitoa hiyo na wewe umefika Mwanza NINGEKUSHANGAA! umbali toka hapo mpaka ofisi ya RC ni kama mita 100 tuu lakini sanamu inachafuliwa,kuchorwa chorwa na hakuna anayejali wala kuona aibu.Tatizo tuna tabia ya kudharau kitu ambacho hakituingizii mshiko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...