Home
Unlabelled
bongo neshno dei
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hizi party zilizozuka kimtindo mtindo hazina mana wala manufaa zaidi ya kuchukuliana wake wa watu na umebea wa kibongo,na kuwapa watu chakula kibovu na pombe zilizo pitwa na muda.Wenzetu kama wa gahana na nigerians wanakutana kila mwisho wa mwezi au miezi mitatu kupeana deal maana wengi ni watu wa nafasi za juu,ila wabongo hatuna moyo wa kusaidiana bali kutambiana mara mimi nina nyumba nambili mara nina range rover na Bmw X5 sasa ukiangalia hatusaidiani kabisa ila ujinga tu,na kushindana kuvaa designer cloth wakati wanapiga box.Tukibadilika tuna nafasi ya kuwa mbele sana ila ndio hivyo wa tz
ReplyDeleteSasa hapa ndio mtakapojua kwa nini maharage na nyama zote zina viburudisho vya protini, ila bei zinatofautiana!! Mwenyekiti wetu mpya ndio muandaaji mkuu, Balozi ndie mlezi kaka Abuu mungu akupe nini!!Piga bao,, ukitilia maanani viongozi wako ndani ya kamati, baadhi yao ni hoe hae..mhhhhhh Mangi nyurraaaa!!!
ReplyDeleteHongereni Watanzania wa uk kwa kuandaa sherehe hii kubwa ya taifa , tuanawaunga mkono....
ReplyDeleteNakubaliana na anon wa kwanza kwa mawazo yake. Watanzania maneno mengi na ujinga ujinga tu wanawake, majigambo ukiangalia hawana mbele wala nyuma. Hiyo kamati ya Watanzania mbona walishachaguana Tangu zamani wewe utakuwa fulani na wewe fulani uchaguzi ilikuwa tu kujifanya democrasi imetumika. Umefika wakati sasa watu waache uupuzi wakue hii kamati ni upuuzi mtupu. Tunataka maendeleo lakini hawawezi kutuletea kwani yao yanawashinda. Watu wakijifanya nao wanamtandao ndio yale yale makundi makundi tutafika kweli?
ReplyDeletemuda?? time mbona hakuna?
ReplyDeleteKweli anon hapo juu bahati mbaya sisi watanzania ni wanafiki sana. Hatupendani wala nini. tunajifanya wakarimu wema lkn chini chini tuna chimbana. Tunafurahia matatizo ya wengine, wala hatusaidiani kama mataifa mengine ya kiaafrika ndoo maana wengi hatuendelei, wachache walio fanikiwa kazi kutamba, ushamba huo wenzetu waafrika wengine waliotajirika zamani wala si limbukeni, tumejaa wivu, umbea, kuchonga, uzushi vyote ni vyetu. Kazi ngono kuimbiana tu (baada ya SA tanzania tunakufa sana na ukimwi) bado tuko mbali sana!
ReplyDeleteAnyway tufanyeje, next time nitaomba nizaliwe mwaafrika lkn sio mtanzania!
Hata hivyo sina budi kusema:
Mungu ibariki Tanzania, viongozi na hasa hasa watu wake
Kila sherehe Tottenham.Badilisheni sehemu wote wanuafaike
ReplyDeleteNakubaliana na annoy hapo juu. Watanzania kwa vijimaneno na ubishoo wa kitoto hatuachi kabisa na hutupeleki popote.
ReplyDeleteIngawaje tuko so proud kusema kuwa "lucky we" nchi yetu hatuna ukabila lakini ni heri tungekuwa nao. Labda tungekuwa si wanafiki na mambo ya kimaficho ficho tu.
Tuparty tunakuaga vyaki ajabu ajabu na mashow off yakijinga kama kwamba vile hatukui. Hatusaidiani kimawazo na mikakakati ni mashindano tu.
Asili yetu ya umbea, wivu na majungu sijui tutaiachia wapi.
Kweli kabisa anon hapo juu,watz wamezidi majigambo,badala ya kufanya mambo ya maendeleo wanaishia kufanya pati zisizokuwa na maana,wanaishia kubeba boksi tu na huko bongo familia zao zinaishi maisha mabovu ila hapa wanajikweza tu na majigambo mengi!
ReplyDeleteKweli kabisa,watz wamezidi kwa majigambo,badala ya kufanya mambo ya maendeleo wanaishia kufanya pati zisikuwa na maana.Wengi wao wanaishi kwa box tu na familia zao huko bongo zinaishi maisha mabovu ila kwa kujikweza ndio wenyewe!
ReplyDeleteWABONGO KWA KWELI MNABOA. KUNA JAMAA HUKO NYUMA (NADHANI ALIKUWA MICHUZI MWENYEWE) ALIPATA KUFANANISHA WABONGO NA SENENE. YAANI WADUDU HAWA HUNA HAJA YA KUFUNIKA KIKAPU ULICHOWAWEKA KWANI HAKUNA ATAERUKA KWANI KILA MMOJA ANAMKAMATA MWENZIE ANAETAKA KUTOKA. HIVYO WOTE WANABAKIA KAPUNI NA KUISHIA KWENYE KARAI LA MAFUTA YA KUPIKIA.
ReplyDeleteHAKIKA WABONGO WENGI, HASA MLIO NJE, MNABOA. HIVI HAMNA JEMAAAAA??? KILA KITU KUSAGIA UTAFIKIRI NYIE NI MALAIKA AMA MIUNGU WATU. WENZENU WAKIJARIBU KUFANYA KITU MNAKUWA KAMA SENENE. ACHENI HIZO. USHAMBA HUO, SIO UJANJA. WE KAMA HUTAKI KUJIUNGA NA WENZAKO KAMA WAFANYAVYO WAKENYA NA WAGANDA AMA WAAFRIKA WENGINE SHARAAAAP! AH, MNAKERA JAMANI. NI LINI MTAJIFUNZA KU-APPRECIATE SOME LITTLE EFFORTS FOR A GOOD CAUSE (IN THIS INSTANCE TO BRING ABOUT UNITY AMONG BONGOLANDERS IN DIASPORA)LIKE THIS ONE ABOU AND CO. ARE ENGAGED IN? ONENI HAYA WENZETU WANATUCHEKA KWA UJUAJI WA KUTOJUA KITU.
ABOU ACHANA NAO HAO WABONGO AMBAO WENGI WAMEJILIPUA BILA MPANGO NA SASA WANATAKA KUKATISHA TAMAA NYIE MLIO CLEAN. DAMN ALL HATERS!!
Labda hii inaonyesha jinsi gani huu uongozi mpya uliochaguliwa una kazi kubwa ya kuwaunganisha hawa Watanzania. Ila ni lazia kwamba watu wakumbuke kwamba huko siku za nyuma ubalozi wetu hapa UK haukuwa mstari wa mbele kuhamasisha umoja na jumuiya kama hii, tushukuru Mungu kwamba Mh. Mama Maajar anajitahdi sana katika swala hili la kuwaunganisha Watanzania hadi sasa wana jumuiya yao rasmi ambayo inatambulika kisheria.
ReplyDeleteKwa wale wote wanaosema kwamba watu huenda kujionyesha wakati wanabeba box, nadhani wewe unachotakiwa ni kujali mambo yako, ukichunguza sana mambo ya wengine ndio unaishia kuongea kama wewe.
Mbona wa-Nigeria wengine wanaendesha mabenz na wanakaa watano kwenye one bedroom flat and life goes on, mbona hao hao wapopo ndio wanaoongoza kwa kujisifia na kuonyeshana walivyonavyo and still life goes on, mbona hao hao ndio wanoongoza kwa kuchomeana home office and life still goes on?
Msitake kuongea vitu ambavyo hata hamvijui kwamba Watanzania ndio wabaya sana UK. Mbona wa_nigeria hao hao pia wanabeba sana box, makolokoloni, na watoza fine za parking tickets? ingawa nakubali pia kwamba wapo wengi pia ambao wana kazi nzuri.
Historia ya Tanzania haiwezi kuwa kama ya Nigeria, Kenya au Uganda hata siku moja. wenzetu wamekuja huku siku nyingi wakikimbia vita, mapigano, udikteta uliokithiri na pia waliokuja kutafuta maisha na kazi ambao ndio kama wabongo wengi.
So wao ilikuwa ni rahisi kuji-establish hapa Uk ofcourse ukichukulia ukweli kwamba wana ujanja fulani ukilinganisha na watanzania.
Huu ndio muda wa watu kuanza kuwa optimistic na kuacha kulalamika kila siku, fikiria kila Mtanzania akianza kulalamika kama hao jamaa wa hapo juu, JUMUIYA hii ambayo ni changa itafika wapi. Mimi naomba wale ambao wanaona kwamba hakuna umuhimu wa watu kukutana waendelee na maisha yao waache wale wanaotaka umoja waendelee kukutana na itakuwa ni somo zuri kwa wasiopenda ushirikiano.
Hongera sana CHOMBEZA kwani hata kabla ya jumuiya hii mlijaitahidi sana kufanya sherehe kama hizi za uhuru, muungano na mapinduzi, keep it up.
Pia kwa balozi wetu na uongozi mpya wa wabongo UK tunawaomba msikatishwe tamaa na watu wasiopenda maendeleo.
Kila kitu kina mwanzo na huu ndio mwanzo wetu. Tutakuja kwa wingi tu......... Idumu Tanzania
Anko Michudhi tunajua una uwezo wa kutrace ISP address za watu, na kujua nani kasema nini humu bloguni mwako. Hembu mwanike mmoja wa hao washamba tumchambue kama ulivyomfanyia yule jamaa wa New York mbaye hadi leo hana hamu. La kama huwezi tupe sie hizo ISP zao tukusaidie, maana hawa shetani wakatishaji tamaa sasa wamezidi. Ama la piga panga maoni yao ya kishenzi shenzi taipu hao. Kwako wewe Faraji wala usiwajali hao habithi. Endelezeni juhudi za kutuunganisha raia wema ambao tuko safi, na mpe salamu Mh. Maajar mwambie tuko pamoja naye na tutakuja kwa wingi hiyo siku hadi washangae hao baradhuli.washindwe kwa jina la Yesu na Muhammad S.A.W!!!!
ReplyDeletehahahaha, wabongo bwana sasa we hata hujui kuwa hiyo ni ip address utamtrace nani? eti ISP address???? WHAT THE HECK IS ISP ADDRESS? punguzeni box jamani wabongo wa uk kanyageni umande kidogo
ReplyDeleteku ping mtu sio rahisi especially kwa marekani ndugu yangu. Watu wanatumia library, school na pia blueberry zina internet service. Na nyngi hazina permanet Ip address
ReplyDeletecha kujua atajua tu kuwa ni usa, uk au wapi lakini pin point tabu...
waachie tu watu waseme walitakalo just know that sticks and stones may break bones but words will never hurt
Mimi ni mmojawapo wa anons niliyesema tabia mbaya ya watanzania. IP address ya nini? hajatukanwa mtu hapa, kwanza mi naweza weka na email yangu hapa kabisa sijali sijaua mtu nasema ukweli ulivyo, mbona kila leo tuna chambua mabaya viongozi wetu wanayo fanya iweje sisi wenyewe?
ReplyDeleteIssue sio mabox au maisha private ya mtu nadhani wengi hapo juu tunapiga vita ile tabia ya kuto pendana kulinganisha na mataifa mengine wao wengi wana ushirikiano sana. Watanzania tuna chunguzana mambo madogo madogo sana badala ya kufanya ya muhimu.
Hatuja mkataa aliyechaguliwa wala kuja kwenye mkutano/party lkn ili kazi yake iwe rahisi lazima kuwe na umoja wa kweli! kati ya watanzania kuliko kutambiana.
Lazima tuseme ukweli pale ambapo tunaona hapaendi vizuri ndoo tusonge mbele. Tunapoficha tunaendeleza unafiki tu.
Folks tubadilike tupandishe think/reasoning level yetu let us be more mature mentaly and spiritually
Asante anon hapo juu, tatizo la watanzania wengi shule ipo midomoni mwao wakati wakijigamba lakini wengi wanazitumia kuwasaidia kuendelea kuishi huko UK ndio maana huyo jamaa kashindwa kutofautisha IP address na ISP(Internet Service Provider)mfano AOL, ndugu usiandike mambo usiyoelewa,hayo ndio majigambo yenyewe tunayozungumzia tunaomba watanzania myapunguze na mfanye maendeleo binafsi na ya taifa!
ReplyDeleteNataka kujiandikisha kwenye jumuia hii.Naomba contacts
ReplyDeleteTembelea hapa
ReplyDeletewww.empapulazakakobe.co.uk
Jamani watanzania wenzangu naaombeni mnisaidie kuhusiana na bendera yetu. Hivi rangi gani huwa juu is it kijani ama blue kwani nimeisha ona bendera ikigeuzwa mara blu iko juu na mara kijani. najua rangi zinamaana. M
ReplyDeleteLakini WaTanzania wote wanaoishi wako hivyo?au wa Uk na USA tu?vipi kuhusu WaTanzania wanaoishi nchi za Nordic kama Sweden,Finland,Denmark,Norway na Iceland?
ReplyDeleteJe ni bad experience ya mtu anaamua kutafsiri wote wako hivyo?Je ni tabia za kiTanzania hizo umbea,kupenda kulaumu kila kitu,wagumu kusifia,wajuaji ndio wao,kudharau wengine?
Kwa mtazamo wangu wakuingia humu kwenye blog za KiTanzania,naona kuna watu wana mapungufu mengi( bila shaka kila mtu ana mapungufu yake).Watu wako wepesi sana kukosoa na kulaumu na kukatishana moyo.Labda hili linawafanya baadhi ya Wabongo wa huko Uk kuwa wagumu na kufanya umoja na kujichanganya pamoja.
Kuchukulia picha linatumwa humu na Michuzi kuhusu wadau wa 'Ukerewe wahusika wake wengi wanakubwa na kukashifiwa. wengine wanapitiliza na kusahau kila mtu ana uhuru wa kuwa anavyotaka kuwa na hamna wenye haki ya kumuingilia kwa hilo.Kashfa kama huyu mtu kashoka n.k.kila mtu anavaa kutokana na taste yake,wote hatuwezi kuvaa kama Wamarekani weusi n.k.
Huu ni mfano mmoja wapo inavyooneakana baadhi ya watu walivyokuwa na mawazo finyu,no wonder unakuta nchi bado iko nyuma ,(ukiangalia jambo ktk pande tofauti) kama hiyo ni utashi wa watu.
Maneno yatakuwepo maana huko UK hizi association zina karuzuku kidogo
ReplyDeletekwa wale wooooote ambao mnakandia sisi Watanzania napend kuwaambia ya kwamba Ndio wabongo kila siku tunaambiana hatuna mpango but at the end of the day I AM PROUD TO BE MTANZANIA. mtu ni kwao na mjaa asili haachi, na mwenyezi mungu ndio alijaalia mimi nafsi yangu idondokee bongo , hakufanya makosa kwani kazi yake haina makosa. sas nyie mnao jitia tia hapo juu sijui vipi tenaa haswa wewe ulioomba in your next life usiwe mtanzania, sijui nikwambia , huna next life na hii ndio life yako so make the most of it ! tena shame on you. Mimi koko niliko nitajivunia asili yangu, mijitu inayokataa asili yao ndio inakuwa miserable na haifanikiwi maishani ng'atu. Nyinyi mnaowasema wanaigeria na waghana kama mnawajua sana , sas kwa taarifa yene hawa wenzetu mafanikio yao makubwa yanatokana na kwamba WANAIPENDA NA HAWAJASAHAU ASILI YAO na HAWAIGI IGI hovyo mila na desturi za watu wengine. Sio kama mataifa mengina hawasengenyani ama hakuna watu wasion na mpango ! la hasha mimi nikakofanya kazi hapa ukerewe na maproffesional wa nchi tofauti za afrika na hawana tofauti na watanzania !!! La msingi ni kwamba tuwe PROUD na asili yetu na hapo ndio mapenzi ya dhati kati yetu yatakuwepo, of course na unafiki hautakosekana kwani hiyo no hulka ya kibinaadamu, mimi nakwambia huwa nashangaa watu waaojitia eti mimi uswahili sitaki naishi maisha ya kizungu , !! hehehe ungejua hakuna mtu mnafiki kama mzungu !!! tena yuko miserable na madeni kibao !!!!!!! Basi kwa tarifa yako Uswahili ndio uliokuzaa na uliokukuza na umo kwenye damu yako so get over it , wewe ni mtanzania instead of kujishaua na kujifanya wewe different just deal with it.Yaani kuna mijitu hapo juu imenitia hasira hapa hata sijui naaandika nini mtajiju, anyway mimi niko ukerewe na nimegundua kitu kimoja labda sisi tulio nje ndio tuna matatizo kwa sababu tuko HOME SICK, basi turudi nyumbani labda itawasaidia wale wenzetu wanaotaka kuukana utanzania wakiwa wanaenda kutembea bongoland mara moja moja ili kukumbukia life ya kwetu, yaani unatoka ndani asubuhi huna kitu na kichwa kimejaani kuwaza utapatia wapi pesa unakutana na konda wa daladala anakuchachafya wewe na abiria wenzio mpaka mnafika mnakokwenda na humo kwenye basi by the time umefika posta mpya kumetokea vituko kama kucheka umecheka mpaka mbavu koi ama unashuka umenunaaaa unaenda kuhadithia mbele ya safari na kila mtu unemwambia anakucheka ( mambo haya ulaya adimu ) yaani wewe kama uko ulaya ujue kama una stress zako za asubuhi utashinda nazo. Jamani namiss nyumbani na nina uhakika hao wanaongea onge hapo juu ni homesick hizi , nendeni mkatembee ama bado travel document hazijatoka !! he he he. In a serious note jamani watanzania wenzangu , TUJIVUNIA KUWA WATANZANIA NA TULINDE ASILI YETU HAPO NDIPO TUTAENDELEA, angalia mfano wa wachina na wahindi ?????!!!!!!!!!! wako wapi ?? na ni kwani wamefika mbali ??? Na hakuna kujilinganisha na wanaigeria, manaigeria kwao ana mafuta kama muarabu mweusi na wezi sana hatuwawezi sisi utapeli wetu cha mtoto kwa hawa watu !!!!!!!!
ReplyDeleteuimbe soote
Tanza nia, tanzania
nakupenda kwa moyo woote
nchi yangu tanzania
jina lako ni tamu saana
nilalapo sikuoti wewe
niamkapo ni heri mama wee
tanzania tanzania
nakupenda kwa moyo woote
KUHUSU UCHAGUZI WA JUMUIYA
kuna anony hapo juu umejitia eti ooh watu wamechaguana , la hasha , kura live zilipigwa na zikahesabiwa, ulikuwa na chance ya kuja na kupiga kura yako sasa kama hukutumia democrasia uliyopewa then acha kuleta unafiki. Bwana Abuu ameshisha kwa kura halali 37 mshindi wa pili akiwa ni Saidi kwa 27 na wametoka pale woote wameridhika na uamuzi ,!! hiloo acha uchochezi.
Mimi kitu kimoja tuu chombeza mngesamehe mapato ya hii siku ya mtanzania mchukue expenses zenu tuu na faida muiache jumuiya ya watanzania ili iweze kuanza shughuli zake kwani bado changa, It would be a good gesture for money is not everything all the time even though it helps to have it so help Umoja wa watz UK to a good start !!!!!!!!
Bwana Mwenykiti Abuu hongera sana kwa ushindi wako na tutakuwa pamoja kuendeleza jamii yetu, na Mama Yetu mpendwa Mama Balozi what can I say about you other than you are a heaven sent, ni kama wale manabii waliokuwa wakitumwa kuja kuokoa jahazi la jamii fulani, tunakuombea kwa mwenyezi mungu afaya njema na uadilifu wa kupambana na kazi yako ngumu!! Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kama waswahili tusemavyo , "Kwa hakika hapa ulicheza" kutuletea Mama Maajar !!!!!!!
Michuzi nimesema saaaaaaanasio lazima watu msomae mie nilikuwa nimejisikia kuandika tuu leo nacheck typing speed yangu mpaka kidole kimeenda upande !!!!!!!!
Wasalaaaam na usiku mwema
Hakuna jipya, kila mtu ana uhuru wa kuandika maoni yake, haina maana kwa kusema ukweli mtu hapendi nchi yake kila mmoja na moyo na anapenda ki vyake acheni magazeti, tunazunguka pale plae tu, point kumbwa ni kwamba tubadilike period!
ReplyDelete