leo wadau wangu nawapa insha fupi ya jinsi mechi ya watani wa jadi inavyokuwa. hii ilikuwa mchezo wa ligi kuu bara ilochezea mji kasoro bahari aprili 17, 2005 wakati huo neshno ilikuwa inafanyiwa ukarabati. matokeo simba ilishinda 2-1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ivo, ivo ,Ivo haya bwana!Kauli ya Ivo Mapunda kichekesho

    2007-04-11 16:25:56
    By Mwandishi Wetu, Jijini


    Baada ya kutandikwa mabao tisa ndani ya mwezi mmoja, kipa namba moja wa Yanga na Taifa Stars, Ivo Mapunda, ametoa kauli ya kushangaza kufuatia kuwashauri viongozi wa timu yake kuhonga waamuzi ili kupata ushindi katika mechi za kimataifa.

    Mapunda alifungwa 2-0 na Petro Atletico ya Angola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kabla ya kudunguliwa mabao 4-0 dhidi ya Senegal akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars, katika mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana mwakani.

    Kipa huyo wiki iliyopita alifungwa mabao matatu wakati Yanga ilipocheza na Esperance ya Tunisia katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika wa raundi ya tatu.

    Akizungumza katika kipindi cha Spoti Leo cha Radio One Stereo, Mapunda alisema kuwa hilo ni soka licha ya kufungwa idadi hiyo ya mabao katika kipindi cha mwezi mmoja, lakini alitoa wito kwa viongozi wa timu yake nao kuwanunua waamuzi kama wanataka kupata ushindi akidai kuwa timu zingine hufanya hivyo.

    �- viongozi inabidi sasa nao kununua mechi ili tupate ushindi kwani wenzetu hufanya hivyo, �alidai Mapunda alipoulizwa sababu za yeye kufungwa mabao tisa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

    Hata hivyo, kauli hiyo ya kipa huyo ilipingwa na rais wa Yanga, Francis Kifukwe aliyesema kuwa kinachohitajika ni maandalizi kabambe na sio kuhonga waamuzi.

    �Kwa kweli sijasikia kauli ya Ivo, lakini kinachotakiwa ni maandalizi mazuri na sio kuhonga waamuzi, �alisema Kifukwe baada ya kuulizwa maoni yake kuhusu kauli ya kipa wake (Mapunda) aliyetaka waamuzi wahongwe ili ushindi upatikane.

    Hivi karibuni wadau wa soka walikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari wakihoji uwezo wa Mapunda kufuatia kufungwa mabao hayo katika kipindi kifupi, ambapo baadhi yao walitaka Juma Kaseja naye apewe nafasi ya kuichezea timu ya taifa ili onyeshe uwezo wake.

    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...