makatibu wakuu wa ccm na cuf, luteni mstaafu yusuf makamba (shoto) na maalim seif shariff hamad wakiongea leo juu ya mkutano wa muafaka wa kisiasa zanzibar kwenye hoteli ya courtyard, dar. nadhani sura zao zinaonesha nini kinaendelea kwenya mkutano huo muhimu wenye lengo la kuudumisha muungano wetu, hasa ikizingatiwa kesho ni siku ya kumkumbuka mmoja wa waasasisi wa muungano, hayati abeid amani karume - ama karume dei.
habari za uhakika zinasema mazungumzo hayo yatafikia tamati mwisho wa mwezi huu na kutangazwa, na kwamba suluhisho la mpasuko wa kisiasa la zenj linaelekea kupatikana na kwamba pande zote mbili zitaibuika kidedea na watanzania watafurahi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mungu Ibariki Tanzania kweli lakini hizo sura zinaonyehs mambo bado ni magumu, Hamad hayupo kabisaa hapo kwenye huo mkutano,anafikiria watu wake Pemba!! wakati Makamba anacheka kuweka tu mambo sawa lakini rohoni anajua kinachoendelea! Mungu ibariki Tanzania na Africa kwa ujumla!

    ReplyDelete
  2. Maalim Seif hana ujanja tena zaidi ya kuongea kwa upole na CCM. sasa maalim kesha pewa mafao yake yote kama waziri kiongozi(waziri mkuu zanzibar) sasa atafanya nini tena wakati paymaster wake ni CCM? wana-CUF-wafuasi walie tu..wao ndio walio baki na njaa kali. Maalim ana peta sawa na viongozi wa CCM waliostaafu.Hivyo wana CUF rudini CCM maalim tayari amekwisha rudi..kama nyie mnaendelea kupigana na majambia mtabaki peke yenu na njaa kali. RUDINI CCM hakuna cha CUF wala upinzani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...