Wewe Michuzi weka hili tangazo la kifo
Especial Announcement Date: Mon, 9 Apr 2007 16:44:56 +0100
From: "Chitenge, Fatima" fchitenge@kpmg.com
Add to Address Book Add Mobile Alert To: info@bongoradio.com
Please If you can make me this anouncement by Radio. I am writing from Angola Luanda to announce the Death of Muhammad Ragabi Mbewla Samgaia from Tanga- Handeni I am looking for his family in Des es salaam the nephew called Ismail Uweji and Abdala Uweji who leaved in Street MagomeniAnd his mother is called Mwajuma Sharehe from Tanga and a brother called Shabani still in Tanga please my phone contact is 244 924126037.
If you can make the announcement in Kiswahili as well. Thanks very much Bongo Radio I am counting on you for this help coz I hear a lot of young people in Tanzania listen to this Radio.
(Iam the wife of this Muhammad)
jamani huu ni utapeli mpya hatujui jamaa anataka kutapeli vipi hakuna cha kufa mtu wala nini wapopo hawa washaanza mbinu mpya...sijui michuzi aliona hili vipi?
ReplyDeleteWewe Anon wa Hapo Juu saa 10:06am , nafikiri umepotoka kidogo. Kwa uzoefu wangu utapeli wa aina hii huwa unahusisha watu wanaotumia email ambazo sio official namaanisha zile ambazo kujua origin yake mpaka uwe mtaalam wa IT. Lakini huyu hapa katumia email ya ofisi, KPMG. Hii ni kampuni kubwa ya ukaguzi duniani. Si rahisi kwa mtu kuingia kwenye mtandao wao na kuanza kufanya utapeli. Maana ni rahisi kuwa kufuatiliwa. Hata hivyo mimi binafsi nimemtumia email na akajibu kuwa kweli huyu jamaa alishawahi ishi Mwanza, Mbeya na Zambia kabla hajahamia Angola. Kwa madai yake kuwa alishawahi kupata ajali ya gari na kupoteza kumbukumbu nyingi. Anasema mara ya mwisho huyu jamaa alirudi Tanzania mwaka 1988. Na kwa mujibu wa huyu dada, jamaa alikuwa na mpango wa kurudi Tanzania mwaka huu kuwaona wazazi wake na akaniambia wazi wazi kuwa jamaa amekufa kwa kusumbuliwa na TB na alikuwa career,sasa sijajua alikuwa career wa ugonjwa gani.
ReplyDeleteKwanza kabisa huyo mtu hana uchungu wowote eti "we michuzi....weka.." then mke gani umekaa na mume usijue kwao hadi afe na huna contacts za ndugu hata mmoja. Kwenda zako wee tapeli usione watanzania wakimya sio wajinga.PUMBAFU!
ReplyDeleteNiliogopa ku comment sababu ni jambo la kifo, lakini najifunza kitu kimoja tu hapa, ukiwa kwenye ndoa uliza mwenzako namba za simu za nduguze.
ReplyDeleteWe anon wa hapo juu uwe unafikiria kwanza kabla ya kucomment. Hivi mtu gani ataweka utapeli wa kufa mtu, halafu huyu hakuomba hela ya mtu kumbuka anataka kuwajulisha ndugu wa mumewe huko bongo. huyo mfiwa si mmbongo, halafu kinachofanya watu ambao tuko up to date kuamini ni kweli ni hiyo mail address. KPMG ni moja ya biggest 4 Auditing firms in the world na wafanya kazi wake si wababaishaji kama unavyodhani wewe. Michuzi jaribu kufuatilia hili suala huyo mjane ana fedha si mbabaishaji huenda atakurefund gharama za matangazo ya radio, Otherwise mungu atakuzidishia kwa kila jema ufanyalo, achana na Comments za kukatisha tamaa.
ReplyDeleteinawezekana akawa mke wa marehemu na asijue hata adress za shemeji zake ?kibaya zaidi hata adress au simu ya mama mkwe wake? sijui labda ni kweli!lakini naona haijatulia hii
ReplyDeleteHili Tangazo sijui ni nani alimtumia Michuzi kwa mara ya pili ili aliweke hapa. Hiyo e-mail ya huyo dada aliyetoa tangazo la kifo aliniandikia mimi kwa mara ya kwanza kupitia Bongo Radio. Nami nilimtumia Michuzi siku ya Jumatatu asubuhi kwa saa za hapa ambapo nyumbani ilikuwa Jioni huko Tanzania, na nia hasa ya kumtumia Michuzi nilijua kuwa ni watu wengi walio nyumbani Tanzania hupitia blog yake kila siku na ingekuwa rahisi kwa watu wanaomjua huyo marehemu kuweza kutoa taarifa kwa ndugu au jamaaa. Lakini Mh Michuzi hakuliweka hili tangazo hapa sasa sikujua kuwa aliona halina umuhimu au labda hakupata hiyo e-mail ingawa ilionyesha e-mail imekwenda bila ya matatizo.
ReplyDeleteHatimaye jana nikaamua kutoa matangazo kwenye websites nyingine za kitanzania hapa USA ambapo nadhani kuna mtu akaliona na kulituma tena kwa Michuzi na ndio hatimaye akaliweka hapa.
Kwa Waridi usiongee mambo usiyoyajua yaani unataka kumlaumu mwanamke wa watu ambaye hata si Mtanzania. Jamani tuwe na utu leo tatizo kwa mwingine na kesho litakutokea wewe.
Anon wa 7:07,
ReplyDeleteWewe huyo mnugu wako anajuwa anwani ya huko kwenu BK--Moro milimani--hata kama ni Dar-- kama sio anajuwa you are from Africa and you say, "mambo," to say Hi. Achana na maswali ya ajabu. Michuzi msilize mama--wewe unauwezo wa kuamua kama ni tapeli au la. Laknii kwa asilimia kubwa wa africa hatuna tabia ya kutania kuhusu vifo.
Picha ya Marehemu Mohammed Rajab Mbelwa Semgaya imebandikwa hapa http://www.bongoradio.com/discussion/viewtopic.php?t=751 Kwa yeyote ambaye anamujua marehemu atoe taarifa kwa ndugu au jamaa.
ReplyDeleteNa mahojiano na Mke wa Marehemu yatarushwa na Mwanakijiji kupitia KLH News leo baadae au kesho asubuhi.
Nafikiri la maana ni kusaidia kuhusu hizi habari ndugu wa marehemu wanauwezo wa kutuambia kama ni tapeli ama la si wakati wa kulaumiana na kumlaumu mama wa watu na angeweza kuzika huko na kukaa kimya ni wangwapi tulioko nje na tuna mahusiano bila kutoa habari kamili za wapi utokako? si afadhali huyu hana namba ila anajua mume wake anatoka mahala gani, haya tupo tunaojulikana Warundi, Wasomali, Wazimb, nak je tukifa huku tupelekwe Burundi? acheni kujifanya mu wasafi kama hujui kaaa kimya si lazima uchangie mbona zipo picha nyingi zenye mjadala wazi jamani?
ReplyDeleteKaka Michu hongera kwa matangazo kama haya.
kutokana na maoni kuwa hakuna uhakika kama ni kifo kweli au vipi, ni bora huyu mke aende ubalozi wa Tanzania huko alipo na ubalozi utachukua hatua za kumtafuta ndugu za marehemu na utatoa uhakika kuwa kweli kama huyu mtu emefariki au ni utapeli
ReplyDeleteNie mnao nisonga hapo juu nikomeni hayo ni maoni yangu. Siku hizi kuna utapeli wa kila aina, mpende msipende something is not clear, kwa mfano kuna anon hapo juu kasema point, tunao ubalozi Angola ni kitu cha kwanza huyo mama angefanya ni kwenda ubalozini,Huyo mtanzania nadhani alijiandikisha ubalozini?! kwahiyo hakuna hata haja ya kutangaza hapa.
ReplyDeleteKwa wale wanakaa na wake wa mataifa mengine halafu hawasemi ukweli waliko toka kuna mambo ya kuficha lakini sio your roots! be serious folks!
Waridi
Michuzi kaweka tangazo hili lililomfikia kwake kutoka moja ya comments kwenye picha aloibatiza TAYANA. Sioni haja ya Geeque kulalama. Inaelekea kuna ukweli ndani ya kifo hiki. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.
ReplyDeleteWaridi nakubaliana na wewe, utapeli ni wa aina nyingi. Na wanaosema utapeli si katika mambo ya kifo si kweli, kwani nani hajapata e-mail kuwa Sani Abacha alikufa na nduguze wanatafuta pa kuweka hela. Waridi alitoa comment wa kwanza, kabla ya picha ya marehemu (ambayo ni scanned from archives, maana imekwaruzika haswa), labda katika kuonyesha alivyokuwa zamani, maana kwikwi kasema alipata TB na alikuwa career. Maoni ya Waridi ilikuwa kabla ya mahojiano ya mfiwa na Radio Mwanakijiji. Upande mwingine naona mtu huyu kweli kafa, maana Fatima Chitenge katumia address ya kpmg.com, ni ya kazini. Tunalotakiwa ni kujifunza tu hapa, toa walau namba moja ya simu kwa mpenzio. Mpenzio azihifadhi namba hizi kwa njia tofauti, ili kuepuka yalompata Fatima, kupoteza namba baada ya ajali. Namba walau moja kariri. Turudi home pia afya zikiyumba au pia tukiwa bhukheri wa afya.
ReplyDeleteyawezekana labda ni kweli. hivi Angola wanatumia lugha gani? kama ni kiingereza then alivyosema wife ot this muhamad, lazima ujiulize, au walikuwa katika hali ya kutokuelewana, kama lugha yao sio kiingereza basi yawezekana ni matatizo ya lugha tu.
ReplyDeletekwavile hatujui tutabaki kusema labda.
Ila kama kuna mtu anawafahamu hao nduguzake waliotajwa ni vyema kuwapa taarifa ila wawe makini katika kulishughulikia swala hili. nikiwa na maana wawe na mategemeo yote mawili kwamba ni kweli au ni utapeli.
Wabongo kwa kurukia jambo tu. Kila mtu nyie kwenu tapeli. Watu wanaotumia email zao za kazini chance ya kuwa matapeli ni 0.1%. Think before you write and don't just your comments for the sake of writting
ReplyDeleteNa pia anayemsema huyo mama wa watu kwa kumwambia "wewe michuzi"...kwanza mjue labda hajui kiswahili vizuri na pili mjue kunamakabila mengine lugha yao sio polite kama yetu. Ongea na wakenya, wacameroon kama huwajui utadhania wanakugombeza.
Halafu mjue kuna watu wanasahau kwao sana. Sio kuwa namlaumu marehemu ila kama yeye hajaenda siku zote hizo nyumbani kwao chance ya kuwataja au kumhusisha mkwewe na nyumbani kwao ni ndogo sana.
Najua kuna mambo mengi yanaweza kuwafanya watu wasiende kwao kwa mda mrefu ila pia kuna watu wengine wanajisahau au wanaishi double life wameoa sehemu nyingine na wakienda nchi nyingine pia wanaoa, sasa watamintroduse vipi huyo mke nyumbani kwao?
Huyo mwanamme labda alikua anaficha mambo mengine tu...What a Coincidence or bad lucky awe na amnesia au alikua tu hataki kumjulisha mkewe ndugu zake waliko?
Ni pole sana kwa huyo mjane lakini ni mambo mengi yakujifunza hapa kwa siye tunaoishi nchi za ugenini.
1. Mtu akikwambia alipata ajali akawa hakumbuki his/her past don't get marry him mpaka akumbuke kila kitu.
2.Kama hamtoki nchi moja basi kusanya au toa information ambazo zitakusaidia baadaye.
Kwa wanaoleta utani kwenye jambo hili hebu msikilizeni mjane anachoongea mtagundua kuwa nini kilichomsibu dada wa watu:
ReplyDeletehttp://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2007-04-11T21_15_52-07_00
Jamani angeendaje kwenye ubalozi wakati mkisikiliza anavyosema walikua wanamtafutia passport? Maubalozi yetu haya ya nje hata ukiwa na passiport na bado uko hao wanavyodo kama nini. Sembuse mtu ameshafariki na hana passiport.
ReplyDeleteSi ajabu alishaenda huko na akaona hamna kinachoendelea
Habari zilizopatikana ni kwamba familia ya marehemu imepatikana huko Tanga.
ReplyDeletehehe ni utapali jamani mtakuja kustukia mwisho atawaambie marehemu anadaiwa....nyie chezeni tu....nje kote mgeni anakimbilia ubalozini mwake yeye anakimbilia kwenye net ndio nini sasa amini usiamini ni utapeli na issa usifunge hii hadi tujue mwoisho wake
ReplyDeleteNi kweli familia ya Marehemu Mohammed Rajab Mbelwa Semgaya imepatikana huko Handeni, Tanga kutokana na juhudi kubwa za ndugu yetu Mwanakijiji wa KLH News ambaye pia alipewa ushirikiano wa karibu na Mbunge wa Handeni Dr. Abdallah Kigoda. Binafsi namshukuru pia Mh. Michuzi kwa kuweka hili tangazo hapa ili kuwawezesha Watanzania wengi kujua kilichotokea.
ReplyDeleteNa kwa wale critics wa hii habari nadhani mmeshaona hatima yake kuwa mjane wa marehemu amekutanishwa na familia ya marehemua mumewe kwa njia ya simu. Kwa habari zaidi mnaweza kutembelea KLH News site @http://mwanakijiji.podomatic.com
Mungu Aiweke Roho ya Marehemu Pema Peponi.
Sir Issa mpe pole sana huyo mfiwa, mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.RAMBIRAMBI TUNAPELEKA WAPI KAKA ?
ReplyDelete