Bwana Issa Michuzi,
Naona hili Somo la Search Engine Investment halikupita bila kupingwa. Naomba nitoe maelezo machache kuhusu hii Search Engine. kwanza kabisa si Utapeli. hili jambo lipo na search engine bado inajengwa.
Natumaini wana-blog watakumbuka kwamba hapo nyuma Search Engine nyingi zilipelekwa mahakamani na makampuni yaliyotangaza biashara zao humo.kwa nini walipelekwa mahakamani? kwa sababu iligundulika kwamba walikuwa wanatumia automated Machine ambayo ilisetiwa kuwaina-click matangazo kila baada ya sekunde tano ilikuonyesha kwamba watu wanayasoma kumbe uongo natumaini. Google ilipatwa na hii kasheshe kama sikosei.
hawawatu wa search engine hulipwa per view 'pay per view'haka kamtindo kakafa na sasa search engine nyingi zinahitaji watu wa ku-click ndiyo walipwe.
hawa jamaa Agloco ni wapya katika Market hivyo kushindana na Google,Mamma, Monster etc na nyingine nyingi inabidi watumie kila njia kupata watu wa ku-click.
hii search engine ikikua registration ya membership itakuwa yakulipia, amini usiamini. kuhusu kupata data zako(tarehe ya kuzaliwa ) hii ina eleweka sana kwa watu waliosoma marketing, sikatai utapeli wa ki-Nigeria upo sana katika internent. lakini bado kuna ukweli unatendeka.
Umri wako ni kupata kitu kinaitwa consumers' demographic, maana yake nini ? ni kwamba makampuni mengi yana product mbali mbali ambayo yanalenga rika fulani la walaji hivyo ili kujua hasa search engine hii inatumiwa na watu wa rika gani na wanaweza wakanunua nini lazima wapate data kama hizo sisi watu wa business majors tuna elewa hii na mimi nimesoma siwezi kuleta utapeli hapa wa kuwaibia watu identity zao kama wanavyo fanya wa-Nigeria.
Bwana Michuzi,
mimi siwezi kuleta utapeli katika blog yetu hii ambayo ni kiunganisho kwa watanzania wote. Na vilevile hii Search engine wamekuwa registered katika Nasdaq stock market hapa USA. nitaangalia share zao kuona wanaanzia na dola ngapi, nitatuma kwako ili watanzania wanunue share, na hii huhitaji kuwa hapa Marekani, una weza ukawa Tanzania na sehemu yoyote ile, jamani ee ina maana hata kwenye Nasdaq kuna Matapeli?.
Wale wananiita tapeli na siku ooo! sikusoma ni kwamba mimi nimesoma na ndiyo maana nina chunguza utapeli na ukweli. Swali kwamba watu watalipwaje mimi sijui cash au nini sijui, mimi mwenyewe sija pata hata senti tano. Na lini watalipwa mimi sijui.
Asante sana Michuzi. Anayependa anaweza kujiunga hapa Na vile vile Wana blog nitawatumia stock zao ziko kiasi gani kwa sasa..katika stock Market.
vinginevyo jiungeni kwa anaependa http://www.agloco.com/r/BBDY1555

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2007

    acha utapeli weka simu yako tukupigie ofisini, na email yako ya ofisini (sio yahoo au hotmail au hiyo agloco) ndio tutaamini. Ila hivi hivi watu tumekulia town, humuuzii mtu mbuzi kwenye mfuko wa salfeti hapa.!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2007

    Michuzi hivi mbona unatumia nguvu nyingi sana kuwaliza wabongo? au na wewe unapata cha juu nini? utafurahi nini wabongo wakiliwa hela au wakipoteza muda kumtajirisha baniani mmoja
    kila mtu kabumbuluka na mtego mtoto bado unakuja kutushurutisha.
    We all know where to find stock information NYSE is free for public and stock infor doesnt have nothing to do with huu mchanga wa macho overall the truth is we have stepped umande huyu jamaa mwambie akatafute site za wakenya labda anaweza kuwapata. si wabongo so mafala

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2007

    Ndugu Mdau wa AGLOCO wewe ndio aina ya mtu ninayemtafuta. Nakuomba tuongee chemba kidogo.

    E-mail yangu ni dar.millionaire@gmail.com

    Na kwa wabongo ushauri wangu ni kwamba ukiona kampuni inayoanzishwa ujue hapo ndio kuna uwezekano wa kupata ulaji mnono kwa hiyo msilaze damu. Kama una kiasi ambacho hata kikipotea hutaathirika kiuchumi nunua hisa. Najua wengi mnaomponda Bwana AGLOCO si kwamba mnaponda kweli ila ni staili tu ya kumhimiza atoe maelezo ya kina kama alivyofanya.

    Bwana AGLOCO naomba tuongee chemba - dar.millionaire@gmail.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2007

    usitupotezee muda,

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2007

    Bwana michu, please ninakuomba ili tuwe na uwaminifu na wewe uwe unafanya reseach ya vitu kabla ujaweka kwenye website yako (blog) maana watu waliosoma watakuona kama pia na wewe ni tapeli kwa sababu wewe ni mtaalamu wa picha sizani kama utaweza kuweka picha ya mtu kama unakika wake sasa hihi kuhusu AGLOCO ni utapeli kwanza mtu mwenye analazimia watu. pia serch engine zote or uwa company inayomilika website ndio wanaolipiwa na companies zinazoweka advert zao kwenye website au unavyo pitia kwenye website zao
    Sasa hawa jamaa wanaweza kulipa watu wangapi kama watu wanaweza kubrowers AGLOCO karibu 10 million na halafu kila mtu alipe £1 . je anazo 10 million au ndio mpaka watu waingia kwenye AGLOCO yako au ndio namna ya kuiba ID za wato sory mate.. please Bwana michu tuletea habari za kweli zenye mambo ya maana sio utapeli kama huu...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2007

    Nyiyi wabongo mnaomponda AGLOCO nafikiri hata hamjasoma vizuri kujua anachosema. Kwa ufupi hajaomba hela ya mtu. Kakuomba tu ujiunge na hiyo promotion ya search engine mpya.

    Sasa kama hujajiunga utajuaje kilichomo? Na kama hujajua kilichomo sijui unaponda nini?

    Jamani kuna watu wagumu kuelewa dunia hii, we acha tu. Yaani hivyo vichwa sijui ni miti iliyokauka?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2007

    Huyu jamaa anataka kupata commission kwa kuonekana ameregister watu wengi; ndiyo maana anataka watu waregister kwa kutumia hiyo link ambayo ID yake yeye mwenyewe ni "BBDY1555;" kwa hiyo ukigonga link hiyo ya http://www.agloco.com/r/BBDY1555 unakuwa umewafahamisha hao jamaa agloco kuwa umetumwa pale na yeye mwenyewe na hivyo kumwongezea points za commission. Hiyo siyo vibaya, tatizo anataka kututumia sisi kama vile ni wajinga, badala ya kusema ukweli. Mtu anaweza kuregister mwenyewe kwa kwenda http://www.agloco.com na kufuata maagizo pale na hivyo kutotumiwa kama commission ya mtu mwingine.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2007

    michuzi ungekuwa ughaibuni haki ya nani tungetajirikia kwako.
    mi ningejiunga nao nawapa bank infor zangu naacha wanaiba halafu na-file lawsuit against michuzi sababu ndo site niliopatia information. naweka lawyer mzuri ulaji safiiiiiiiiii
    nawaachia hata wale $1000 lakini nahakikisha ntayopata itakuwa angalau na sifuri ya ziada
    michuzi watch your back home boy, give us ginuine new and pic if there's some you're not sure with seek advice or put disclaimer to back yourself up.
    I like illiterate people like you! but honestly dont want to see you going down for some dumb like this

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2007

    BWANA MICHUZI WABONGO SISI NI WABISHI NA WENGI SHULE NI NYEMBAMBA NA HILI NI TATIZO LA WOTE WENGI. BADALA YA KUTUKANA NA KUKANDIA NAOMBA MFANYE UCHUNGUZI ZAIDI HATA MIMI MTOA MAADA SINA HAKIKA WATALIPA BEI GANI ILA NIMEFANYA UCHUNZI-ANAYETAKA AJAZE ASIYE TAKA ACHA..MTOA MAADA.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2007

    TATIZO LA WENGI WANAPONDA KITU WASICHOELEWA. MNAFIKIRI GOOGLE WANATENGENEZAJE PESA? HII KAMPUNI NI GOOGLE YA SIKU ZA BAADAE.MAELEZO WALIYOTOA NI KWAMBA UNACHOFANYA SASA NI KUJIANDIKISHA NA KUANDIKISHA WENGINE. IDADI NZURI IKITIMIA KAMPUNI INAINGIA KWENYE SOKO LA MITAJI. HAPO NDIO SHARE ZITAPATIKANA. THAMANI YA SHEA ITAPANDA KUTOKANA NA BEI YA SHEA (HISA)NA PERFORMANCE YA KAMPUNI. HAPO NDIO WENYE HISA WATAWEZA KUUZA/KUNUNUA NA KUPATA FAIDA(DIVIDEND+CAPITAL GAIN). KWA SASA HAWAULIZI BANK DETAILS ZAKO. OF COURSE HAKUNA GUARANTEE, ZAIDI YA 80% YA BIASHARA ZOTE ZINAZOANZISHWA DUNIANI KILA MWAKA HUFA KABLA YA MIAKA MITATU. NI JUU YAKO KUWEZA KUBAINI KAMA HII BIASHARA ITAFANIKIWA AU LAA. UKIWA NA UFAHAMU WA MAMBO YA BIASHARA ZA KISASA ZAMTANDAONI, NA UKIWEZA KUSOMA MAELEZO, FORUMS, REPORTS NA INSTRUCTIONS MPAKA KUWEZA KUFANYA UAMUZI, BASI UTAFANIKIWA. TATIZO SI WENGI WANAWEZA KUELEWA MAELEZO YALIYOPO KWENYE WEBSITE KWA UFASAHA KWA SABABU HAWANA UJUZI WA KUTOSHA KUSOMA HAYA MAMBO NA KUYAELEWA.

    HUYO HAPO JUU ALIYESEMA JAMAA LINK YENYE "BBDY1555" NI REFFERAL NUMBER YA MDAU, HAJUI ANACHOSEMA. INAONYESHA HAJAJIANDIKISHA. UKIJIANDIKISHA HIYO NUMBER INAKUJA MARA YA KWANZA, UKICONFIRM UNAPATA "ID" MPYA. HIVYO KILA ATAKAYEJIANDIKISHA ITAKUJA HIYO NYMBER KWANZA. SIWEZI KURUDIA MAELEZO YOTE HAPA, SOMENI MUELEWE KABLA HAMJASEMA.

    MIMI NADHANI HII IPO,ILA ÍNAHITAJI UELEWA WA HALI YA JUU WA HAWA MAMBO, NA WEWE MWENYEWE UWE MAKINI KUJILINDA NA SCAMS NA UWEZEKANO WA KUIBIWA. SI RAHISI KWA MTANZANIA WA KAWAIDA KUFUATILIA HII KWASABABU IPO COMPLICATED, LAKINI NI KWELI.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2007

    mwingine amesema hii ni kama upatu bongo: nasema hapana. tofauti ni kwamba upatu, kama multi-level marketing nyingine, ni pyramid, ambazo ninazikataa sana. katika pyramid, walio wengi wanachanga (chini) na wachache walio juu wanapokea. assumption ni kwamba wachangiaji hawana kikomo, maana wakifikia kikomo,michango mipya itatoka wapi? hii agloco ni wachangiaji wengi(advertisirs, na sio idadi tu bali amounts) na wapokeaji ni wengi pia(wadau). kadri wapokeaji ambao pia ndio wanaosurf the net na kununua baadhi ya bidhaa za advertiser wanavyoongezeka, ndivyo advertisers wanavyoongeza dai kutangaza zaidi.

    ni kama google tu, ila tofauti ni kwamba idadi ya share za google ni chache(maboss wa google wakiwa na nyingi zaidi) na nyingine hata wewe unaweza kununua sokoni. katika hii agloco, wenye share watakuwa wengi zaidi(ukijiandikisha bure sasa) utazipata bure, lakini baadae zikishafika sokoni basi, itabidi ununue. wakati huo, bei yake itapaa kama ya google sasa, maana advertisers watataka kutangaza kwa hili kundi kubwa la watu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2007

    Nakuunga mkono kabisa wewe mtoa maoni hapo juu.Tunaponda sana bila kuelewa badala ya kufanya uchunguzi, hii huwezi ukawalaumu wa bongo wakulaumu ni shule tu, mtu anavyo toa maoni yake ina onyesha kabisa na shule yake na hili ni tatizo la nchi yetu mpaka serikalini. Fanya uchunguzi, baadaye lete 'argument' ambayo ina saidiwa na ukweli ndivyo wasomi wanavyo fanya Duniani kote.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2007

    tupe NYSE symbol ya hiyi kampuni.. hata u google haikupi kitu. Bado hujmpata mtu hapa, acha utapeli kijana. Tafuta kazi ya uhalali

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2007

    wewe anon wa saa 5.34 ume google kwa kuandika jina la babu yako? au ..andika AGLOCO tu na utaona maelezo yote yana toka..sija kutakana hata kidogo ..wewe Anon mwingine subiri kidogo nitakupa data zote za stock market 'just wait' cha kufanya sasa jiandikishe usije uka nilaumu mimi..

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2007

    share hazitolewi bure we muogopa umande, if company not doing well they do a reverse split to raise the value of their share, giving out free share will ruin the overall market value of the co even an idiot cant think of that??!!
    aisee nabahati mieenda shule sijaspeshalizi kwenye business ila the business requirement classes gave me knowledge of that
    Now i see kwamba elimu ya marekani safi na inatarget kupambana na real life challenges.
    dogo rudi kapige box kwa staili hii umedunda, come back prepared

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2007

    Wewe unayetaka NYSE symbol hujasoma maelezo ya hii kampuni. Haipo sokoni bado, na kama ilivyo kwa kampuni nyingi zinazoanza na kukua taratibu, inatarajiwa kuanzia kwenye AIM.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2007

    Wee mbwiga hapo umeambiwa ni NASDAQ sio NYSE !

    Naona wamefaili IPO prospectus hapa: http://ipo.nasdaq.com/TextSection.asp?cikid=71762&fnid=3262&sec=bd

    Kuna article hii hapa inachambua udhaifu wa business model ya AGLOCO - http://www.tradersnarrative.com/what-everyone-ought-to-know-about-agloco-744.html

    Kuhusu historia ya AGLOCO soma hapa -

    http://en.wikipedia.org/wiki/AllAdvantage

    --- na hapa ---

    http://www.247wallst.com/2007/02/busted_dotcom_i.html

    Kwa ujumla AGLOCO inajadiliwa sana kwenye mtandao. Kama uwekezaji wa aina yoyote ile ni jukumu lako kusoma na kuamua kama ni kampuni inayofaa kuwekeza ama la. Lakini hakuna aliyesema huu ni utapeli. Na eleweni kuwa huyu aliyeleta taarifa kwa Michuzi sio mwajiriwa wa hii kampuni. Yeye ni mwekezaji kama watu wengi tu walioamua kujiunga na kupromoti AGLOCO.

    Kwa hiyo kama mwanahisa wa TBL akikutaarifu kuwa TBL hisa zao ni bomba je utaanza kumuuliza ofisi yake huyo mwanahisa iko wapi? Yeye anakupa taarifa tu, ni juu yako kufuatilia data za TBL na kuamua kama inafaa au la.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 25, 2007

    toeni wizi wenu hapa nyie hamna tofauti na joji kichaka, kaanza na wmd kaishia na ugaidi kama nyie mmekuja na ku-click ads for payments sasa hivi mnataka kuuzia watu share
    hatuna muda wa kujadili wizi michuzi naomba ufunge huu mjadala kimbiza hawa wezi warudi kubeba box

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...