mdau maria sarungi-tsehai katushushia hii apdeti sasa hivi...

Hi everybody!

Kwanza nashukuru sana kwa support yenu ya nguvu. Bwana awabariki watanzania wote kwa moyo wenu wa upendo. Nawatumia update nyingine!

Presentation show au Preliminary show ilifanyika jana usiku (23 May). Kabla
ya show hii kulikuwa na interview ya warembo na majaji. Show hii iliwashindanisha warembo katika nyanja nyingine 2 - swimsuit na evening gown. Flavia alivaa nguo ambayo ilikuwa designed na Jamilla Swai.
Kwa kweli mrembo wetu alipendeza sana, lakini cha muhimu zaidi watu wa Mexico walimshangilia sana. Hii ilinipa faraja kwani nilikuwa mtanzania pekee yangu. Lakini nimebeba bendera kubwa ya Tanzania na ninajua nitaipeperusha juu! Mungu yupo....

Umuhimu wa show hii ni kuwa majaji hapa wanawatafuta 15 bora ambao watatangazwa siku y fainali.
Fainali itafanyika tarehe mei 28 ambapo warembo wote wataingia mwanzoni na mara moja wanawatangaza 15 bora na wao ndio wanaendelea kushindana hivyo ni muhimu sana Flavia aingie 15 bora.

Pia kuna award ya Miss Photogenic ambayo nawaomba watanzania waendelee kumpigia! Waende
www.missuniverse.com na kuclick kwenye 'Vote for Miss Photogenic"
pichani ni flaviana katika evening gown na picha ingine toka kushoto ni Yoanna Henry, Miss St. Lucia 2007; Christa Rigozzi, Miss Switzerland 2007; Flaviana Matata, Miss Tanzania 2007; Lyudmyla Bikmullina, Miss Ukraine 2007; Saneita Barbara Been, Miss Turks & Caicos 2007, and Farung Yuthithum, Miss Thailand 2007, pose in their Tadashi dresses and Nina Shoes during the 2007 Miss Universe Presentation Show at Auditorio Nacional in Mexico City, Mexico on May 23rd, 2007.
During the Presentation Show, each Miss Universe 2007 contestant will be judged by a preliminary panel of judges in individual interview, swimsuit and evening gown categories. The scores will be tallied and the top 15 contestants will be announced during the LIVE NBC broadcast of the 56th annual Miss Universe competition from Mexico City, Mexico on May 28th, 2007 at 9PM (ET/delayed PT). ho/Miss Universe L.P., LLLP
mpigie kura flaviana kupitia yahoo news pia. maskini hana kula nyingi pale; wakati wengine wana kura 425 na zaidi. yeye ndo kwanza yangu imemfikishia tisa. tumpeni tafu jamani. popote wanapotaka kupiga kura, tupigeni tu. Ushindi naimani ni wetu mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2007

    tunapigaje kura?? mana sielewi nikishafungua hiyo yahoo window..

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2007

    Ina maana kumpigia kura ya photogenic ni hadi uwe mkazi wa US? mbona tunashindwa kumpigia huku uswazi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2007

    Binti ukirudi bongo usisikilize kabisa hao masugar daddy. Wasije wakakupoteza. You have a big bright future ahead of you.

    Keep your inner beauty up and don't let them loser fans.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2007

    Anon wa kwanza ukibofya hiyo address zitakuja picha za hao warembo. Picha ya Flaviana ni ya 6 click kwenye RECOMMEND THIS PHOTO kuna nyota 5 click kwenye ile ya tano 'highly recommended', utaingia kwenye sign in ya Yahoo. Kama una yahoo ID basi ingia hapo kama huna basi create 1. Ukishamaliza kusign in automatically inajiongeza kwenye idadi ya kura.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2007

    Mie pia nilihangaika, but nimegundua jinsi ya kufanya Maria alisahau kutuelekeza. Bofya HAPA halafu chini ya maelezo ya picha, kuna nyota nyekundu. kushoto kwa nyota hizi nyekundu kuna nyota nyeupe, RECOMMEND THIS PHOTO. Chagua 5 STARS, yaani unarecommend highly. Nimefanya na sasa ana vote 59. na ana rank 4/5.

    ReplyDelete
  6. BRAZA MICHU KUMPIGIA KURA FLAVIANA MATATA NI RAHISI, unachofanya nenda www.missuniverse.com utaona sehemu imeandikwa VOTE FOR MISS PHOTOGENIC utaclick hapo baadae itatokea window yenye picha za warembo hao halafu utaona sehemu imeandikwa AMERICA,AFRICA,EUROPE,ASIA/AUSTRALIA then click sehemu iliyoandikwa AFRICA halafu zitatokea picha za warembo sita ambao ni ANGOLA,EGYPT,MAURITIUS,NIGERIA SOUTH AFRICA,TANZANIA juu kuna maelezo yanasema VOTE FOR THE TOP THREE CHOICES ili kumpa mrembo wetu kura nyingi itabidi uaanze kwa kuchagua picha yake kwanza halafu picha ikiisha tokea chini yake utaona pameandikwa SELECT THIS DELEGATE then uta select usipofanya hivyo utakuwa bado hujampigia kura kisha utachagua warembo wengine wawili utakaoona wanafaa ili kukamilisha top three halafu uta submit your vote kisha itatokea sehemu ambayo inahitajika ujaze FIRST NAME,LAST NAME,STREET,CITY,BIRTH DATE,STATE/COUNTRY,ZIP/POSTAL,EMAIL,CONFIRM EMAIL,GENDER utajaza vyote,kwenye sehemu ya STATE OR COUNTRY ukiclick pale patokea majimbo ya marekani halafu utaona pia pameandikwa INTERNATIONAL kwahiyo kwa vile wewe sio residence wa US itabidi uclick sehemu ya INTERNATIONAL ili kura ya ko iende vizuri halafu uta submit your vote na hapo utakuwa umempigia kura mrembo wetu na itatokea sehemu inasema THANK YOU FOR YOUR VOTE ikimaanisha umefanikiwa kumpigia kura kumbuka kuwa unaweza ukatumia mail nyingi kadri uwezavyo au kama kuna mtu unafahamu mail yake na hajapiga kura unaweza kuitumia kwani hakuna haja ya kuweka password wala kujua siku halisi ya kuzaliwa mtu i hope tutakuwa tumeweza kumpigia kura nyingi na kumuweka katika hali ya kushinda na kuwa MISS PHOTOGENIC.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2007

    Duuuh unajua mie nina address 5 za yahoo, basi zote nimempatia huyu mtoto.Mungu amjalie ashinde,wabongo tuko nae bega kwa bega.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2007

    Duh umeona pose ya top 15 finalist iliyochukuliwa leo huko mehico. Mtoto anazidi kupendeza..


    http://news.yahoo.com/photos/ss/events//en/051007missuniverse/im:/070525/ids_photos_en/r3728023131.jpg;_ylt=AjqJg9OsTRJQKqQhbUIELzB.KcMA

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2007

    Mh hii tarehe ya hili shindano itabidi tukaazime TIVO mbona long weekend itatuharibia

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 25, 2007

    Jamani wameweka picha nyingine kwenye Yahoo. Wengine wameshakua recomanded more than 53 already na yeye ana tatu tu. Nimempa email accounts zangu zote mpaka m=nimerun out.

    Help out guys.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...