mwalimu akiwa na baraza lake la kwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2007

    Inabidi tuanzishe uchunguzi kujua ni namna gani Kassim Abdallah Hanga,Abdul-Aziz Twala,Othman Shariff,Idriss Abdallah Majura,Mzee Mohammed Mbaba,Maalim Harun Ustadh,Seyyid Abdul-Muttalib Hashim, Seyyid Ali Asghar, Haj Abdul-Husain Tejani,Babu Haji,Mohammmed Salim Jinja,Amour Zahor, Said Kombanyongo,Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed,

    Jaha Ubwa,Mdungi Usi,Juma Maulidi (Jimmy Ringo),Khamis Masoud,Aboud Nadhif,Salim Ahmed Busaidi,Abdalla Suleiman Riyami,Othman Soud,Azizi Bualy,Hemed Said,Mohammed Juma,Mohammed Hamza,Musa Ali,Said Hamoud,Saleh Saadalla,na wengine maelfu "WALIVYOPOTEA" ktk mikono ya serikali baada ya mapinduzi ya Zanzibar!

    Tukifanikiwa kuyatibu makovu ya kabla na baada ya mapinduzi basi hata hutu tu-mgogoro wa CCM-CUF Zanzibar nao utaisha wiki moja tu badala ya kutumia mabilioni kwa vikao vya muafaka kila siku!

    Unaweza kutembelea hapa kwa habari zaidi: http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli12.html

    Michuzi kaka yangu tafadhali usiyatupe maoni haya!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2007

    Haya kwa waliokuwa wakisema Nyerere alikuwa mdini... hesabuni majina ya waislaam ktk kabineti hiyo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2007

    Hao waliopotea unataka ajibu nani? Siyo kazi ya serikali ya Muungano iulizeni serikali ya Zanzibar.

    Wapemba mna matatizo tumeyachoka mambo yenu. Mkikumbwa na matatizo serikali ya muungano mnaitaka na kuipenda sana na mnataka itoe maelezo na iwasaidie. Mnataka kufaidi huku na huku,Kukiwa na raha (mfano kuna mafuta yawe yamegunduliwa Pemba) mnataka serikali huru ya Zanzibar yenye sauti huko na ushirikishi wa wapemba wengi wa CUF kwenye serikali.

    Hao waliopotea mngemwuliza Seif Sharriff Hamad alipokuwa waziri kiongozi wa juu sana kwenye serikali ya Zanzibar awaeleze walipotelea wapi.Mbona hamukumwuliza wakati huo akiwa serikalini awape majibu huyo mpemba mwenzenu? Mnakaa kupiga umbeya kwenye blogu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2007

    bro michu
    hivi huyu idriss abdallah majura aliotajwa hapa ana uhusiano wowote na abdallah majura wa bbc.
    halafu hii orodha mbona ndefu in maana hawa watu walipotea tu bila kujulikana wako wapi. haiwezekani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2007

    Jamani waacheni wapemba midomo kazi yao,wanapenda sana kuongea vitendo ziiiiiii,halafu ni vigeugeu hao mara wajifanye waarabu wa oman hawataki uhusiano na wabara au mara waukane utanzania na sasa ndio hao wanapiga kelele za dual citizenship,Can you imagine mi msukuma wa shinyanga hio d/citizenship ya nini hata kama nina passport nyekundu lakini inajulikana kwetu ni bariadi.kelele nyingi ni za wapemba bwana vigeugeu sana watu hawa.Sasa unamwuliza Bro.Michu watu ambao wamekufa hata yeye hajazaliwa ili iweje?Mwulize maalim Seif,atakuwa na jibu.Sisi wabara tuacheni tutulie mambo yetu na nyie na yenu.MICHU USIJIBU KITU WATU WAMEKUFA HATA WEWE HUJAZALIWA,AWAULIZE MAALIM SEIF NA WENZAKE WATAMPATIA JIBU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2007

    Anon wa 9:28:00 mimi sio mpemba na wala hata sijawahi kufika Unguja wala Pemba; mimi ni mtu wa Bara tena sina uhusiano wa damu au hata wa ndoa au wa namna nyingine yeyote ile na mtanzania visiwani yeyote. Uhusiano wangu na watu wa Tanzania visiwani ni kupitia UTANZANIA!

    Lakini uelewe kwamba hao "waliopotea" ni watanzania kama mimi na wewe ndio maana nauliza. Hata dereva wa daladala alivyouliwa kwa risasi Dar (Nov. 2006) na kiongozi wa serikali nimeuliza sana na bado naendelea kuuliza;hanijui simjui ila utanzania wetu ndio unatuunganisha.

    Mimi siamini ktk dhana za "hao wapemba", "hao waunguja" au "hao wabara"; naamini ktk "utanzania". Hata nawe pia "ukipotezwa" nitahoji kwa sababu ni mtanzania mwenzangu.Sina kadi ya chama chochote cha siasa na sitarajii kuwa na mwanachama kabisa maishani mwangu;sitaki kufungwa mawazo na vyama vya siasa-mimi ni mtu huru natoa maoni yangu kama hivi.

    Napenda nikufahamishe kuwa usalama wa raia/mambo ya ndani ni jukumu la serikali ya muungano na sio seriakali ya Zanzibar.Tuna idara moja ya polisi/usalama wa raia nchi nzima;tuna IGP mmoja tu.Kwahiyo ukisema iulizwe serikali ya Zanzibar unakuwa unakosea.

    Halafu nashangaa kwanini unakuwa "Party-sensitive" kiasi hicho,au kuna chama kilihusika na upotevu wao? Au wewe una husika pia? Tuelezane.Au watu wenye itikadi tofauti na wewe "wakipotea" basi hujali? Hapa nimesema tu tuchunguze hawa watu waliopotea ila wewe unakuja na vyama vya siasa na habari za mafuta;sikuelewi.

    Hawa watu walipotea baada ya mapinduzi ya Zanzibar (kati ya 1964 na 1970);sasa Seif Shariff Hamad anaingiaje hapo? Nadhani huyu Seif kawa Waziri Kiongozi mwaka 1985-88 tu.CUF nayo imeundwa miaka ya 1990 tu (tena baada ya vyama kama NCCR-Mageuzi na UMD kuwa tayari vimeshaundwa).


    Hata kama tunataka "kufukia" kuhusu hawa watu lakini tujue kuna siku "tuatafukua" tu. Katika umri wangu wa miaka 28 sikuwa najua lolote kuhusu hawa watu hadi miaka kama minne au mitano iliyopita wakati Abdallah Idriss Majura anatoa ushuhuda wake BBC Swahili kuhusu SIKU ANYOYOIKUMBUKA (alivyokutana tena na mama yake baada ya miongo kadhaa).

    Baada ya hapo ndio nikaanza utafiti wangu binafsi.Lazma serikali ya muungano ndio ijibu kwasababu baadhi ya hao watu walitolewa bara na kupelekwa Zanzibar walikopotelea.Pia ni watanzania;hakuna utaifa wa Zanzibar! Wengine waliopotea wapo ktk hii picha kama Kassim Abdallah Hanga ambaye hadi wakati "anapotea" alikuwa Makamu wa Rais huko Zanzibar,enzi ya Rais Abeid Amaan Karume!

    Pia watanzania wengine walipotea walikuwa mawaziri ktk serikali ya Karume kama Othman Shariff na Abul-Aziz Twala.

    Tuache chuki wandugu;mtanzania ni mtanzania tu hata kama hana rangi,kabila au dini yako au hamtoki eneo moja;WOTE TU-WATANZANIA.

    Naomba nafasi tena Michuzi!

    Hoja kwa hoja!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2007

    Wewe anon wa May 4:43:00 udini haupimwi na uwepo wa uwingi au uchache wa watu wa dini flan ktk serikali.Inawezekana kabisa ktk serikali kusiwe na watu wa dini fulani lakini wtu wa hiyo dini husika(isiyowakilishwa) watendewe haki kama wengine.

    Naomba nikuulize,ktk kipindi hicho ambacho waislamu walikuwa wengi ktk Cabinet je wengine walikuwa wanalalamika?

    Kwahiyo kama kuna watu wanalalamikia udini nadhani tuangalie vigezo vyote na sio kimoja tu kwasababu hata wakati wa Mwinyi bado waislamu walilalamika kuhusu udini.

    Sioni vibaya mtu akilalamika kama anayo madai ya msingi ingawa najua watu wengi (watanzania) hawapendi mtu (mtanzania mwingine) alalamike.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2007

    Hivi watu wanawachukia "wapemba" namna hii kwa kosa gani walilowafanyia? Sitoki Pemba wala Unguja ila sina chuki na mtu yeyote kwasababu ya eneo atokalo, dini, rangi, itikadi ya siasa au kabila!

    Tanzania ni nchi ya mikoa 26 kwahiyo huwezi ukajiita mtanzania wakati unaitenga baadhi ya mikoa au watu wake. Leo "tutawatoa" "wapemba", kesho "waunguja", keshokutwa? Tutaanza kumega "wakagera", "wakigoma", "waruvuma", "wamtwara", "waarusha", wakilimanjaro", n.k Nini na nani atabaki?

    TAN+ZAN+I+A=TANGANYIKA+ZANZIBAR(UNGUJA+PEMBA)

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2007

    Enzi za Mwalimu ilikuwa mwiko kutaja hayo majina!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2007

    Tanzanians, Ugandans, and Zimbabweans have been taken hostage by the elites. For Tanzanians you can't let CCM abuse the economy of your country by few people who preach to you amani na utulivu while you don't even know when your nest meal will come from. Most of Tanzanians are living below poverty line of less than $1/month. Instead of fighting against corruption and nepotism, you are fighting about, with all due respect (the dead). Come on people! Stop the madness and wake up!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2007

    Kama kuna watu walikuwa na bahati ya mtende basi ni Salim Ahmed Salim na marehemu Prof. Abdulrahaman Babu. Kwa vile walikuwa vipenzi vya Mchongameno basi akawatoroshea bara na baadae ng'ambo ili nao "wasijepotezwa". Pia marehemu Oscar Kambona nae alicheza kama Pele pale marehemu Mchongameno alipojaribu "kumpoteza"; akakimbilia zake Uingereza!

    Inasemekana "upotoaji" wa watu hao ulifanya kwa condonation au connivance ya marehemu Mchongameno! Inachosikitisha sana ni kwamba hata CIA nao walikuwa nyuma ya "upoteaji" wa wanasiasa hao vijana waliokuwa na mawazo ya kisoshalisti lakini ambao ndio WALIPANGA NA KUONGOZA Mapinduzi kabla marehemu A.A.K na chache chake "hawajayapora" Mapinduzi!

    Yaani acha; wenzetu Visiwani wameonja joto ya jiwe si kitoto mazee!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2007

    Wapemba acheni ujinga. Majina yote yawe ya Wapemba kisha udai wewe Mbara!.. hakuna mbara hata mmoja anayefahamu list hiyo!... wewe Mpemba. Nyerere hauwaua watu wenu. Mmewaua wenyewe kwa sababu kama kweli angetaka kuwaua basi Salim na Babu wangekuwa wa kwanza kuuawa maanake wao ndio walikuwa shina la Ukomunisti Unguja!.
    Na ilikuwaje Nyerere mwenyewe awe mkomunisti kama aliwachukia wakomunisti?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2007

    Wapemba acheni ujinga leo mnajifanya mnataka UTANZANIA!!!!si kila siku nyie ndo mnadai muungano ufe ili mkimbilie kuomba misaada kwa babu zenu waarabu,Nyie wenyewe mmeuana msilete haya mambo yenu huku bara sie tuna matatizo yetu kibao yanatusubiri.Juzi tetesi za mafuta mnataka kuukana utanzani na muungano ndo zenu hizo.Kwa taarifa yenu visiwa vyenu sie wabara tunaona ni mzigo tu kwa Tanganyika.Mabilioni ya shilingi mpaka leo Tanesco wanawadai uwezo wa kulipa hamna.Hao uliowataja wameuawa jiulizeni wenyewe huko kwani hilo si SUALA LA MUUNGANO.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2007

    Anon wa 3:32:00 am kwa taarifa yako mi si "mpemba" na sina uhusiano wowote na Zanzibar zaidi ya UTANZANIA wangu. Kama uko UK sema tuonane wapi na lini. Lakini hata hao "wapemba" nao ni WATANZANIA kama wewe (labda nawe ni mtanzania); wao kuwa "wapemba" SI DHAMBI.

    Hivi nikuambia historia ya ukoloni wa Uingereza huko Marekani na ya baada ya uhuru na kuwataja watu mashurhuri wa Marekani ktk miaka (lets say) mia 2 basi mimi nakuwa Mmarekani? Nikukutolea habari za kina Kanyama Chiume, Ngwazi Dr Hastings Kamuzu Banda na wengineo basi nakuwa Mmalawi? THINK TWICE.

    Hayo mambo yalikuwa yanafichwa zamani ila siku hizi kila kitu kipo hadharani na ndio maana nimesema unaweza pita shemu kama hizi ukaone ushahidi: http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli7.html

    Lakini kama unabisha sio kweli kwamba hawa watu hawakuaawa basi TUAMBIE "UKWELI" wewe,wako wapi au walikufa vp? Au nenda kamuulize Abdallah Idriss Majura (nae "mpemba"?) akueleza jinsi BABA YAKE MZAZI yake alivyouwawa kisiri na kinyama huko Zanzibar.

    Kama unaijua historia ya Tanzania basi utakuwa unajua hata Muungano "ulichagizwa" na Marekani kwa kuhofia wakomunisti wasije igeuza Zanzibar ngome yao. Pia pia "kijijini" kwa Mjengwa "ukafumbue macho" ndugu yangu: http://maggidmjengwa.blogspot.com/2007_01_01_archive.html

    Hivi umewhi kujiuliza kwanini baada ya mapinduzi ya Zanzibar majina ya kikomunisti yalianza Zanzibar? Haya ni kama vile Fidel Castro school, Lumumba school, Mao Zedong stadium, n.k Haikuwa kwa bahati mbaya.Inatokana na wa-Cuba amabao ndio "masterminders" wa mapinduzi yale.Nenda WIKIPIDEA halafu tafuta Salim Ahmed Salim;alikuwa wapi mwaka 1961/62 wakati Zanzibar yatawaliwa?

    Pia uelewe Nyerere hakuwa mjamaa hadi baada ya 1967 (Azimio la Arusha lilipoanzishwa) na "upoteaji" wa watu hawa ulifanyika sana kati ya 1964-1967 ingawa inasemekana uliendelea baada ya hapo.Babu na Salim walitaka "kupotezwa" BAADA ya kifo cha Karume mwaka 1972 (wakati Nyerere tayari kawa mjamaa).

    Pia ujue kuwa Babu na Salimu walikuwa "vipenzi" vya Nyerere; an exception to the general rule.

    Tupo pamoja hadi hapo? Kama una chochote cha kubisha hapa basi tuambie wewe ukweli ni upi.Usibishe tu (HAPANA,HAPANA) toa hoja za kukanusha existence ya watu hawa na pia disappearance yao. Mfano Kassim Hanga yupo hata hapo pichani,sasa "alikufa" vp?

    Nasisitiza tena MIMI SI MNZAZIBARI.Hata ukisikia jina langu utashangaa sana;tena natokea Kilimnjaro.Lakini napenda sana kutafuta maarifa na taarifa toka sehemu mbalimbali.Nina vitabu vingi kama vya Kenyatta (burning spear), Ndabaningi Sithole, Mandela, n.k

    Nafuatilia sana historia za watu/nchi mbalimbali za Afrika na hata nje ya Afrika.Kwahiyo ufahamu wangu wa habarizi za Zanzibar SIO dhambi KABISA.Nayajua na nayafuatilia mambo ya Bara na Visiwani kwasababu ni zote sehumu za Tanzania.

    Naomba nafasi kaka Michuzi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2007

    Nataka kukuuliza wewe anon(3:32:00 am) "ujinga" ni nini? Nadhani hao waliotoa hoja sio wajinga kwasababu hayo yaliyo tajwa yapo na yametokea.Nadhani mjinga ni yule ambaye hajui na hajui kwamba hajui.Hivi akitokea mtu toka Unguja akaanza kukueleza stori za kina Rumanyika na Omukama basi anakuwa "mhaya" au "mkagera"? Kila mtu anaweza kuwa anawafahamu kitu chochote hata kama yeye hatoki huko.

    Vitabu,Internet,televisions,radio,newspapers,magazines,journals,etc vinaweza kumafanya hata mtu wa kutoka Chad akaijua vizuri historia ya Tanzania kuliko mtanzania mwenyewe.Kama hauna interest ya kutafuta knowledge unaweza kudhani watu wengine "wachawi" au "wapemba" kwasababu wao watakuwa wanajua mengi kuliko wewe;mwishowe utaishia kuwatukana tu,kisa wao wanajua jambo ambalo wewe hulijui.

    Wewe ambaye si mtanzania (maana hauamini kama Pemba ni Tanzania au kama "wapemba" ni watanzania au wana haki ya kutoa maoni tofauti na yako,KINYUME na katiba ya Tanzania)huenda hata hamjui Mputa Maseko, Songea Mbano, Zwangendaba, n.k na huenda mtu akikutajia majina ukamuita "mruvuma", "msongea" au "mngoni".

    Mi nadhani kama kuna watu wanatoa hoja basi ukitaka kuwakanusha uinabidi uende kwa hoja;sema tu hilo ni la uwongo na hili hapa ndio ukweli.Babaake Majura alikuwa "mpemba" au "mzanzibari"? Watu karibu wote hapo wana asili ya Unguja,kwa taarifa yako.

    Lakini hata ukisachi ktk Internet haya mambo mbona yapo tu nje nje!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2007

    HAO WATU KAMA MAITI,WAZIMA AU WAPO NJE YA NCHI HAKUNA AJUAYE ZAIDI ABEID KARUME. JIBU ZURI NI KWAMBA KWA NINI ALIUAWA HUKO IKULU ZANZIBAR.
    SIKU HIZI KUNA UHURU KAMA UNAVYODAI. NAKUSHAURI NENDA IKULU ZENJI UKAULIZE HAKUNA MJADALA WA WALIOKUFA KWA KUKUBALI AU KUTOKUBALI MUUNGANO.
    MAMBO YA KUDAI IGP MMOJA, JESHI LA POLISI MOJA AU WMN MOJA, NANI HAJUI HAYO. mzenji

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2007

    Anon 10:11:00 pm hakuna STATE/REPUBLIC inayoitwa Zenj wala Zanzibar ila kuna STATE inayoitwa TANZANIA/REPUBLIC.YOU SHOULD EVERY CRIME COMMITTED WITHIN TANZANIAN BORDERS IS DONE AGAINST THE REPUBLIC/STATE OF TANZANIA;WHO ELSE SHOULD BE ANSWERABLE THAN THE SEAT OF THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA?

    HAVE YOU EVER STUDIED CONSTITUTIONAL LAW OR SOMETHING OF THAT SORT? JISOMEE MWENYEWE HATA LEO.PIA PITIA MTANDAO WA BUNGE UKAISOME KATIBA.UKIUA ZANZIBAR AU UKIUA RUKWA UTASHTAKIWA NA JAMHURI YA MUUNGANO NA SIO SERIKALI YA MKOA WA RUKWA AU YA "MKOA" WA ZANZIBAR.

    WATU WAMEDAI VIFURUSHI VYAO "VILIVYOPOTEA" POSTA TANZANIA(SEHEMU AMBAYO HAINA UGUMU WA NAMNA YEYOTE KWENDA TOFAUTI NA WIZARANI NA IKULU) ILA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYESEMA WAENDE DAR (POSTA)WAKAULIZE.NA POSTA WAMEJIBU.HII INA MAANA WAKUBWA WANASOMA HAPA NA UJUMBE UNAWAFIKIA.

    KAMA WEWE NDIO ULIOHUSIKA "KUWAPOTOTEZA" HAO WATU BASI POLE SANA KWA KIHORO ILA LENGO HAPA NI KUWAPA UJUMBE WAHUSIKA/SERIKALI NA WATU WENYE MAWAZO CHANYA;SAMAHANI KWA KUKUPA PRESHA NDUGU YANGU,LAKINI KWANINI "ULIWAPOTEZA" AU JAMAA ZAKO "WALIWAPOTEZA" HAWA WATU?
    MLIKOSEANA NINI?

    HAUJAULIZWA WEWE AMABYE HAKUNA UJUALO ZAIDI YA KWENDA KIBARUANI KUPINDA MGONGO UPATE MLO WAKO NA JIONI UENDE CLUB.HII NI CHANGAMOTO KWA WATU WENYE "BONGO" NA "WANAOFIKIRI".

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2007

    hivi hii ni haki kweli kumwambia mtu akaulize kuhusu watu waliouliwa kwa mtu amabye baba yake (mzazi?) ndiye "aliyewapoteza" watu hao?

    pia mambo ya maisha au vifo ni ya seriakli ya muungano.ZANZIBAR/ZENJI SIO NCHI(DOLA).Kwahiyo Z'bar "haina" watu;watu wote ni wa Tanzania.

    Pia inadaiwa walipotea kwasababu ya imani zao za kijamaa na sio mambo ya muungano.

    nadhani hapa ni sehumu muafaka ya kutoa mawazo huwezi mpangia mtu wape aende atoe mawazo yake.Ni Michuzi tu ndie anaweza kumzuia mtu ila sio MPAMBE yeyote amabe hana anachomiliki hapa.

    Mbona watu kila leo wanatoa mawazo yao kuhusu Kikwete,Posta,Lowassa,Seriakli,n.k na hakuna anayewaambia waende Dar/Tanzania wakaulize huko? Wewe hili lakuumiza nini? Au ulihusika nalo? Acha kujifanya MICHUZI hii sio blog yako.

    Kama Michuzi ameruhusu maoni wewe kinakuwashia nini? Au nyie ndio mnanufaika vitendo vya wengine "kupotezwa" au kuchafuliwa majina ili jamaa/wazazi/ndugu zenu wakae madarakani milele mnufaike?

    Pilipili usioila yakuwashiani?

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2007

    Wapemba ndio walioharibu nchi hii.
    Kama mjuavyo wanablog Nyerere alisomea nchi ya kibepari(Uingereza) Kwake Ujamaa ni kitu alichokuwa hakijui kabisa.Sasa baada ya kupata uhuru hakujua afuate siasa gani.Bahati mbaya akamchagua Mpemba Abdulahaman Babu kuwa waziri wa mipango ya uchumi.

    Huyu mpemba alisomea na alikuwa mkomunisti wa kutupwa.Ndiye aliyekuwa mwalimu wa Nyerere wa Siasa ya Ujamaa.Nyerere akamwamini mno na akawa anamsikiliza sana.Kila jioni Babu alikuwa akimfundisha Nyerere na kumpelekea vitabu vya akina Lenin na upuuzi wa Akina Che Guavera.Akapandikiza upuuzi wake kwenye kichwa cha Nyerere na Nyerere akakubali mawazo ya Babu nchi ikaanza kuelekea ujamaa wa Kikomunisti.

    Kama kuna mtu wa kulaumiwa kwa nchi hii kukwama ni Mpemba Abdulhaman Babu ambaye ni architect wa siasa za ujamaa Tanzania.Ndio maana nasema wapemba wamehusika kuharibu nchi yetu.Aliiharibu halafu akakimbilia London Mwanga mkubwa.Akatuachia nchi yenye siasa mbovu alizoanzisha na baadaye na wapemba wenzie wa CUF wakaanza kushambulia kuwa nchi toka uhuru haijafanya chochote.Wapemba hovyo.Ukiwaweka mahali wao kazi yao kubwa kubuni mbinu za kukuangusha kama siyo mpemba mwenzao.Ndiyo maana Karume aliwalimba makofi! Wakatorokea huku bara kuuza PWEZA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 22, 2007

    Anon wa 5:22:00 pm unanipa raha sana tu.Umeacha kucheza mpira (hoja) sasa unapiga viatu (ukabila/umajimbo);raha kweli kweli.

    Hapa ndipo tunaweza hata kufahamu uelewa,upeo,akili,busara na elimu ya mtu.Hoja kwa hoja sio hoja kwa "uzushi","matusi","ukabila",n.k

    Nasubiri hoja zako."Wapemba" wako wapi na wanafanya nini (ilmardi hawavunji/hawavunjiwi sheria) WALA HALINIHUSU kwasababu kwetu SIENDI KWA BOTI BALI KWA BASI;Kilimajireeee!

    Kitu kingine kinachonipa raha mi kwamba mi si "mpemba" (mpemba ni nani kwani au ni dhambi kuwa mpemba?)na wala sina hata ujamaa nao wa aina yoyote.Kwetu kuna barafu juu ya mlima milele na milele labda iishe karne hii tu.Kama huamini tukutane live Michuzi akiwa mkutanishi.Hahahahahahahaha!

    Na nina hakika habari hii hapa niliyoipost hata hao "wapemba" au "wazinzibari" (kwani nao si watanzania?) wala hawana data nayo.Ni utundu wangu wa kusaka elimu na ufahamu nje ya ile yangu ya darasani (i mean my LL.M degree of which I'm thankful to God and proud of).

    Website mmewekewa hapo juu,mbona hamtaki kuisoma?

    Ukitaka kumjua mbongo tena yule ambaye ni shuleless basi hoja zake zinajaa uzushi,mambo ya kufirika tena bila kusadikika,Hoja za kutunga na ambazo hazina hata credibility,authenticity,foundation,authority,reasonability wala reliability.Hahahahahahahahahahah!

    Eti Babu alimshawishi Nyerere afuate Ujamaa! Leta evidence basi.Dunia nzima inajua Nyerere aliuleta ujamaa Tanzania kutoka China wewe leo unatuambia Babu ndie "alimshawishi";hahahahahahaha!

    Toa data basini vipi Babu alimshawishi,wapi,lini,kivipi na halafu utuambie wapi umetoa habari hizo.Hapa ni hoja kwa hoja;hatugombani,hatupigani na wala hatutukanani;amani tu watanzania! Nyerere anajulikana alikuwa mtu wa misimamo na asiyeyumbishwa na ambaye mambo mengi aliyoyateleza i yale aliyoyaamini (sikiliza hata hotuba zake anayasema haya) tena hata vitabu kuhusu ujamaa aliandika.

    http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/441768.stm

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 22, 2007

    Wapemba hawafai kwa muungano wowote ule uwe wa Zanzibar,Tanzania au Afrika mashariki.Muungano waujuao wao na kuutambua,kuupenda kuuheshimu na kuujali ni wa wapemba kwa wapemba unaoongozwa na mpemba.

    Ndiyo maana hata ni vigumu kupata Raisi wa Tanzania Toka Pemba wale utaifa hawana.Kutwa kucha wanawaza Pemba na hatima za Wapemba.Utaifa (UTANZANIA) vichwani mwao hauko kabisa.Iwe kwa kauli au vitendo.

    Halafu wametuchafulia sifa ya nchi.Mhusika mkuu wa kulipua ubalozi wa Marekani Tanzania ni mpemba.Ndiyo maana hata mayowe yao kimataifa sasa hivi hayatiliwi maanani.Nchi nyingi zimeanza kuwashtukia kuwa mpemba kumeanza kuwa nuksi na si sifa tena.

    Naungana na aliyesema wapemba wametuharibia sifa ya nchi yetu.Kitendo cha Mpemba mwenzao kulipua ubalozi wa Marekani Dar es salaam kimetuchafulia sifa yetu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 22, 2007

    ukitaka kuangalia nani kaharibu wapi? basi yapo mengi. kama sasa hivi Zanzibar kuna majambazi wengi na kati ya hao wengi wao ni wabara na wachache sana ndio wazanzibari. kwa hiyo tunaweza kusema kuwa wabara wanawaharibu wazanzibari na zanzibar yenyewe? wapemba ni binaadamu kama wengine, nyinyi mkiwachukia wapemba na wao watawachukia na kuwaita wanyamwezi. na bado inashangaza huku zanzibar kuna watu wabara kibao wanafanya kazi kwa hao hao wapemba. hata pemba kwenyewe pia wapo. inakuwaje baniani mbaya kiatu chake dawa.
    katika blogs mkitia mambo ya siasa na dini tutaijharibu

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 22, 2007

    Kwenye hiyo picha namtambua Mzee Kawawa, na Mzee Bhoke Munanka kama watu ambao wako hai leo hii (kama wengine sijawatambua naomba radhi). Sasa nani kati ya hao wawili mnataka awajibike kwa matukio ambayo mnasema yametokea zaidi ya miaka 40 iliyopita? Na pengine wao hawahusiki.

    Mimi ningefikiri kuwa sasa hivi ingekuwa muhimu zaidi kufikiria kesho nitapata vipi chakula cha kunishibisha mimi na familia yangu, kuliko kutaka kufahamu Nyerere au Karume walifanya kitu gani kabla sijazaliwa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 22, 2007

    Aon wa May 22, 2007 4:10:00 PM hivi kwanini unaadhimisha siku yako ya kuzaliwa wakati ni tukio lililopita miaka mingi? Kwanini twaadhimisha siku za uhuru,muungano,n.k? Kwanini unakumbuka 1st and 2nd world wars? Kwanini hata ulaya na marekani bado serikali zao zaadhimisha kumbukumbu za biashara ya utumwa? Kwanini vyama vya kutetea haki za binabamu vinataka nchi zilizoshiriki biashara hiyo (karne 4 zilizopita) zilipe reparations leo?

    Kovu la leo limetokana na maumivi ya jana.Yaliyotokea jana yana athari leo na hata kesho.Huwezi ukajenga kesho bila leo na jana.Serikali yetu inatumia mamilioni kila baada ya uchaguzi Z'bar kwa ajili ya mazungumzo ya muafaka yasiyo na mbele wala nyuma.Kwanini? Kwasababu wanaangalia tatizo la leo bila ya kujua kwamba limesabishwa na tatizo la jana.

    Pia ujue accountability ipo kwa serikali na sio kwa mtu binafsi hadi ionekane uhusika wake na tukio ulizidi mamlaka yake ya kiserikali.Kwahiyo hayo ya kina Kawawa na Munanka uliyoyaandika hayana maana.

    Maanon wengine hapo juu majibu yenu yapo ktk comments za juu zaidi;naona mlipenda tu kuandika nanyi mtoe hasira zenu za mabox.

    ReplyDelete
  25. uzuri ni kwamba wabongo wengi wana akili, wenye kusisitiza amani na utulivu ndiyo wenye maslahi/wizi, kuna watu hapa hawataki watu tulalamike kwa sababu wana kasumba za nyerere, leo bongo watu wakisema kitu kupinga serikali bado wanafungwa na kupigwa na polisi. believe me these things still happens although we have free press, but we still don't understand freedom of speech, wadaku wa ccm wanasema eti unaharibu amani.power corrupts, mtu hata kama ana nia nzuri bado anakuwa corrupted by it.we have to have mechanism to make ccm accountable to the people, utulivu na amani hautaendelea milele kama wananchi maskini, angalia kenya watu wamechoka sasa ndio wamekuwa wanyama, bongo tutafika tu!!! kama unavyojua nyerere katurudisha nyuma miaka ishirini, 2028 tuta kuwa kama kenya leo kuchinjana barabarani, you can bet on that!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...