Bunge la Bongo Bubu?
Na Paschal Mayala,
Ubungo Plaza,
sasa hivi
Bunge la Tanzania limeelezewa kuwa ni Bunge butu katika suala zima la udhibiti matumizi ya serikali kama yanavyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ukilinganisha na Bunge la Nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa Upinzani katika Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kenya la Hesabu za Serikali, Mhe. Uhuru Kenyatta wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha Mada ya kuhusu Kamati ya Bunge la Kenya na Udhibiti wa Fedha za serikali.
Bw. Kenyatta amesema Kamati ya Hesabu za Serikali za Bunge la Kenya limeunda Kamati ndogo ya ufuatiliaji utekelezaji wa Mapendekezo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali mara baada ya kuwasilishwa na kujadiliwa na Bunge la Kenya ambapo kabla ya bajeti inayofuata kupitishwa, serikali lazima ijibu imechukua hatua gani kukabiliana na ubadhirifu wa fedha za Umma na bajeti hiyo itapita pale tuu Bunge la Kenya linaporidhika ya matumizi ya serikali ya mwaka uliotangualia.
Kwa Upande wa Tanzania, Baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali kuwasilishwa Bungeni, inajadiliwa na shughuli hiyo inaishia hapo, kwani hakuna utaratibu wa Bunge kuwajibisha serikali ama kuishurutisha itekeleze mapendekezo ya Ripoti ya Mdhibiti Mkuu.
Akizunguamzia Bunge la Tanzania, Spika wa Bunge, Mh.Samwel Sitta amesema hata hivyo Bunge lake limepiga hatua kubwa sana ukilinganisha na huko nyuma kwani hii ni mara ya kwanza kwa Bunge kuipokea ripoti hiyo na kuijadili. Hapo nyuma ripoti hiyo ilikuwa inapokelewa na biashara inaishia hapo.
Spika Sitta amesema, Bunge lake linaendelea kupiga hatua kwa hatua katika kuidhibiti serikali na akasisitiza kadri siku zinavyokwenda na ndivyo wanavyozidi kulipoboresha Bunge katika majukumu yake ya kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu Bunge la Tanzania ya Hesabu za Serikali, Mhe. John Cheyo, amesema kamati yake huwa inatoa mapendekezo makali sana katika matumizi mabaya ya serikali, hata hivyo mapendekezo hayo huwa yanatupwa kapuni na serikali kwa hisia kuwa kwa vile kamati hiyo inaongozwa mtu toka upinzani, hata mapendekezo yake yanaonekana kama mapendekezo ya wapinzani.
Mhe. Cheyo amesema kwenye kamati za Bunge, hakuna uchama wala siasa za vyama na kusisitiza kuwa wao wanatekeleza majukumu yao kwa kuweka maslahi ya taifa mbele na bila kuchanganya siasa za vyama na kazi za Bunge.
Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Marten Lumbanga, ameipongeza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali kwa kuandaa mkutano huo muhimu ambao watautumia kubadilishana uzoefu ili kuboresha matumizi ya serikali kwa maendeleo ya taifa.
Mkutano huo unamalizika kesho jioni kwa Mada zitakazoendeshwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, zitawasilishwa na Mhadhiri Mwandamizi, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ayoub Rioba, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda na Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Deogratias Mushi wa Daily News.
Mkutano huo wa siku 3, ulioandaliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, unashirikisha maofisa Masuhuli (Wahasibu) na Maofisa Wakaguzi wa Hesabu za Serikali toka mataifa 12 ya Afrika na Ulaya
Bunge la Tanzania limeelezewa kuwa ni Bunge butu katika suala zima la udhibiti matumizi ya serikali kama yanavyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ukilinganisha na Bunge la Nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa Upinzani katika Bunge la Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kenya la Hesabu za Serikali, Mhe. Uhuru Kenyatta wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha Mada ya kuhusu Kamati ya Bunge la Kenya na Udhibiti wa Fedha za serikali.
Bw. Kenyatta amesema Kamati ya Hesabu za Serikali za Bunge la Kenya limeunda Kamati ndogo ya ufuatiliaji utekelezaji wa Mapendekezo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali mara baada ya kuwasilishwa na kujadiliwa na Bunge la Kenya ambapo kabla ya bajeti inayofuata kupitishwa, serikali lazima ijibu imechukua hatua gani kukabiliana na ubadhirifu wa fedha za Umma na bajeti hiyo itapita pale tuu Bunge la Kenya linaporidhika ya matumizi ya serikali ya mwaka uliotangualia.
Kwa Upande wa Tanzania, Baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali kuwasilishwa Bungeni, inajadiliwa na shughuli hiyo inaishia hapo, kwani hakuna utaratibu wa Bunge kuwajibisha serikali ama kuishurutisha itekeleze mapendekezo ya Ripoti ya Mdhibiti Mkuu.
Akizunguamzia Bunge la Tanzania, Spika wa Bunge, Mh.Samwel Sitta amesema hata hivyo Bunge lake limepiga hatua kubwa sana ukilinganisha na huko nyuma kwani hii ni mara ya kwanza kwa Bunge kuipokea ripoti hiyo na kuijadili. Hapo nyuma ripoti hiyo ilikuwa inapokelewa na biashara inaishia hapo.
Spika Sitta amesema, Bunge lake linaendelea kupiga hatua kwa hatua katika kuidhibiti serikali na akasisitiza kadri siku zinavyokwenda na ndivyo wanavyozidi kulipoboresha Bunge katika majukumu yake ya kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu Bunge la Tanzania ya Hesabu za Serikali, Mhe. John Cheyo, amesema kamati yake huwa inatoa mapendekezo makali sana katika matumizi mabaya ya serikali, hata hivyo mapendekezo hayo huwa yanatupwa kapuni na serikali kwa hisia kuwa kwa vile kamati hiyo inaongozwa mtu toka upinzani, hata mapendekezo yake yanaonekana kama mapendekezo ya wapinzani.
Mhe. Cheyo amesema kwenye kamati za Bunge, hakuna uchama wala siasa za vyama na kusisitiza kuwa wao wanatekeleza majukumu yao kwa kuweka maslahi ya taifa mbele na bila kuchanganya siasa za vyama na kazi za Bunge.
Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Marten Lumbanga, ameipongeza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali kwa kuandaa mkutano huo muhimu ambao watautumia kubadilishana uzoefu ili kuboresha matumizi ya serikali kwa maendeleo ya taifa.
Mkutano huo unamalizika kesho jioni kwa Mada zitakazoendeshwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, zitawasilishwa na Mhadhiri Mwandamizi, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ayoub Rioba, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda na Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Deogratias Mushi wa Daily News.
Mkutano huo wa siku 3, ulioandaliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, unashirikisha maofisa Masuhuli (Wahasibu) na Maofisa Wakaguzi wa Hesabu za Serikali toka mataifa 12 ya Afrika na Ulaya


Michuzi na huyo Paschal Mayalla, jaribu kutoa habari zenye usahihi kwani uhandishi wa habari wenu tusije tilia mashaka.
ReplyDeleteKwenye hii taarifa mnasema " Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Marten Lumbanga, ameipongeza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali kwa kuandaa mkutano huo muhimu ambao watautumia kubadilishana uzoefu ili kuboresha matumizi ya serikali kwa maendeleo ya taifa.
Nafikiri Katibu mkuu kiongozi sio Marten Lumbanga tena, labda kama mlitaka kusema Katibu mkuu kiongozi mstaafu au aliyekuwa---jamani Michuzi fanya editing na wewe au chuja kama unavyofanya kwa watoa maoni.
Marten Lumbanga bado Katibu Kiongozi? Huu ndio tunazungumzia uandishi wa habari wa kishabi. Taaluma haifutwi kabisa. Sasa na wewe Michuzi kabla hujaweka hii habari hapa, je hukuisoma hii habari na kumsahihisha huyo Pascal Mayala? Mie nimeshawahi kukutana na kuongea na huyu Pascal Mayala niona ni mtu makini kumbe hakuna lolote.
ReplyDeleteWanafunzi Chuo Kikuu UDSM basi
ReplyDelete*Utawala wasisitiza masharti yapo pale pale
*Barua zao kutotazamwa kama hawatalipia
*Hatma yao sasa kujadiliwa Septemba
*Mmoja wa wana Tashiso abainika Katibu Mwenezi wa CCM
Na Waandishi Wetu (http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari0.asp)
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambao wamefukuzwa chuoni hapo wako katika hatari ya kupoteza hadhi yao ya uanafunzi, kama utawala wa chuo hicho utaendea na msimamo wake wa kutaka warejee baada ya kutimiza masharti yote.
Taarifa iliyotolewa na Utawala wa UDSM kwa vyombo vya habari jana, imebainisha hatari hiyo, hasa kwa watoto wa maskini, ambao hawataweza kupata fedha za kulipia ada na masomo ya vitendo kwa asilimia 40 (kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza) na fedha za matibabu Sh100,000 kwa wanafunzi wote wa shahada za kwanza.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini hali ngumu ya kifedha inayowakabili wanafunzi wa UDSM, ambao wengi wapo jijini hapa. Inaonekana wazi kuwa, utawala wa UDSM kwa kusimamia masharti yake, unatangaza kuwafukuza wanafunzi maskini, ambao hata hiyo wako mitaani wakihaha bila kufahamu majaliwa yao ya siku zijazo.
Mwananchi lilipata fursa ya kuzungumza na mwanafunzi mmoja wa kike na akalieleza kuwa; "kaka yangu mimi nina Sh120,000 tu hadi sasa. Ndizo zilizobaki na kama nikitoa Sh100,000 za matibabu nitabaki na Sh20,000, sasa nitawezaje kuishi nikirejea chuoni?" alizungumza binti huyo huku akidondokwa machozi.
Mwanafunzi huyo anawakilisha wengine wengi ambao walilazimika kubakia jijini Dar es Salaam, wakijibanza kwa ndugu au kwa marafiki huku wakijitegemea kwa huduma nyingine. Wengi wa wanafunzi hao, wanapendekeza ungekuwepo utaratibu wa kuwarejesha bila masharti na kisha kunyimwa matokeo yao hadi watakapolipa fedha hizo, kuliko inavyotakiwa kufanywa sasa na utawala wa UDSM.
Taarifa inayofuta matumaini kwa wanafunzi wengi ambao hali yao kifedha ni duni sambamba na familia wanazotoka ni ile isemayo; "Ni kwa wanafunzi wale tu ambao majina yao yatachapishwa kwenye magazeti tarehe 12 Mei, 2007 ndio watakaotakiwa kuripoti chuoni kwa ajili ya kuanza masomo."
Nyingine ikisema; "barua za maombi ya kurejeshwa tena chuoni ambazo zitatumwa baada ya Mei 9, 2007 hazitashughulikiwa hadi mwaka ujao wa masomo."
Katika taarifa hiyo pia kuna angalizo lisemalo; "barua ambazo hazitakuwa na viambatanisho vya risiti za malipo ya fedha ambazo mwanafunzi anadaiwa hazitashughulikiwa."
Kwa mujibu wa hali halisi ilivyo kwa wanafunzi wa chuo hicho, ni jambo lililo wazi kuwa, wanafunzi wengi wako katika hatari ya kupoteza nafasi zao chuoni kwani ni vigumu kupata fedha hizo kwa sasa na kisha wakaweza kurejea chuoni hapo kusoma na kumudu gharama za maisha ya kila siku.
Gharama za vyakula chuoni hapo ziko juu kulinganisha na sehemu nyingine na kipindi cha kuelekea mwisho wa semista, wanafunzi wengi hushindia mlo mmoja kutokana na ukata.
Maamuzi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, kusimamia masharti hayo, yanaweza kuwa yanashinikizwa na hali halisi ya kifedha serikalini. Kuna taarifa za ongezeko la matumizi ya serikali sambamba na kupungua kwa makusanyo kunakoathiri wizara mbalimbali.
Tena kunaonekana kuwepo baadhi ya wanafunzi wanaolipa na gazeti hili lilifanikiwa kuwaona wazazi wa wanafunzi kadhaa wakiwashika mikono vijana wao katika benki ili walipe fedha hizo kabla ya kurejea chuoni.
Taarifa ya kuwa utawala wa UDSM kuwa umekuwa ukipata shinikizo kutoka serikalini iliwahi kupingwa na utawala huo. Lakini kupingwa huku kunaelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni hali ya kisiasa inayotanuka sasa chuoni hapo kama ilivyo katika sekta nyingine za serikali.
Kiongozi mmoja wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu (Daruso) aliliambia gazeti hili kuwa; "Hali ni kama mnavyoiona, hapa kuna makundi na hasa wazazi walio na uwezo wa kifedha. Ukitumia mfano huu unaweza kudhani kuwa wanafunzi wanafanana, lakini ukweli unabaki pale pale, wanafunzi wengi wataumia na hali hii."
Chuo hicho pia kimetangaza kuongeza muda wa wanafunzi kutuma maombi ya kurejeshwa chuoni kwa sababu ya msongamano na mlolongo mrefu kwenye matawi ya benki ya NBC na ofisi za Posta.
Sababu hii si halisi sana ila kubwa iliyosababisha zoezi hili kufanyika, inaelezwa na chanzo chetu kuwa, kuona kama kuna hali ya kulipa kufuatia kauli za vitisho za kufukuzwa jumla kwa wanafunzi ambao hawatalipa.
Sasa barua zitapokelewa hadi Mei 9 badala ya Mei 4 na kipindi hiki kitaambatana na uchunguzi wa waliokuwa viongozi wa mgomo huu, japokuwa kwa UDSM inafahamika wazi kuwa Bunge la wanafunzi liliridhia mgomo huo.
Kwa sasa utawala utawaita wanafunzi kupitia njia ya magazeti. Inaelezwa kuwa, majina ya wanafunzi watakaoonekana hawana hatia baada ya kufanyiwa mchujo, yatachapishwa kwenye magazeti ya Mei 12 mwaka huu.
"Ni kwa wanafunzi wale tu ambao majina yatachapishwa kwenye magazeti tarehe 12, Mei 2007 ndio wanatakiwa kuripoti chuoni kwa ajili ya kuanza masomo saa 3.00 asubuni kwenye kampasi zao," ilieleza taarifa hiyo.
Uongozi wa UDSM uliwasimamisha masomo wanafuzi wa shahada ya kwanza baada ya kugoma kuingia madarasani Aprili 16 wakilalamikia hatua ya serikali kupunguza mkopo wa mafunzo kwa vitendo na ada kwa asilimia 40.
Baada ya kuwafukuza, Uongozi huo ulitoa masharti tisa kwa wanafunzi wanaotaka kurejea na masomo likiwemo la kulipa fedha zote wanazodaiwa kabla ya kuruhusiwa kuanza masomo.
Katika hatua nyingine, Makamu Mkuu wa Chuo hicho aliliambia gazeti hili kwa simu kuwa tayari barua za baadhi ya wanafunzi zimeshaanza kupokelewa kutokea Posta.
Mkandala alisema japokuwa bado takwimu halisi za idadi na asilimia ya barua hizo zilizopokelewa kufikia jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho kabla ya kuongezewa muda haijafahamika, bado uongozi wa chuo hicho unajiandaa na utaratibu wa zoezi hilo.
Wakati huo huo Muhibu Said anaripoti kuwa
Chowo, ambaye ni Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria, anadaiwa pia kuwa si Kamishna halali wa Tahliso kama alivyojitambulisha katika mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam, Jumatano wiki hii na kutoa tamko hilo.
Mbali na wadhifa huo ndani ya CCM, Chowo pia ni mfanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na Chowo mwenyewe, zinaeleza kuwa, wadhifa huo ndani ya CCM amekuwa nao kwa muda mrefu na anaendelea kushikilia hadi sasa.
"Hivyo, hatukushangazwa sana na ujumbe ule kutoa tamko kama lile dhidi ya vyama vya upinzani," alisema mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Sehemu ya Mlimani, Michael Doyo.
Alisema, katika mkutano wao wa Maelezo, Chowo alizungumza kama Kamishna wa Tahliso wakati si kweli.
Alidai Chowo si kamishna halali wa umoja huo, lakini wanashangaa kuona anang'anga'nia cheo hicho licha ya muda wake kuisha.
"Siku ile Maelezo (Idara ya Habari) alizungumza kama kamishna wa Tahliso cheo ambacho ameking'ang'ania kwa miaka mitatu wakati katiba inasema ni cha mwaka mmoja," alisema Doyo.
Kiongozi mwingine wa Tahliso aliyezungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari na kutoa tamko hilo, ni Mwenyekiti wa umoja huo, Bruno Ng'ingo.
Alipoulizwa, Chowo alikiri kuwa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kigoma na pia ni mfanyakazi wa Tanesco, lakini akasema vitu hivyo havihusiani na uongozi wa wanafunzi.
"Ni kweli mimi ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kigoma na pia ni mfanyakazi wa Tanesco. Lakini hayo hayahusiani na uongozi wa wanafunzi," alisema Chowo.
Alikiri muda wake wa ukamishna wa Tahliso kuisha mwaka jana, lakini akasema aliteuliwa tena baada ya mwenyekiti mpya wa umoja huo, Ng'ingo, kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika kisiwani Zanzibar mwaka huu.
"Nilimaliza muda wangu wa ukamishna chini ya uenyekiti wa Sufiani Robert mwaka jana, lakini baada ya Bruno (Ng'ingo) kuchaguliwa Zanzibar, niliteuliwa tena mwaka huu. Sikumbuki tarehe, muulize Bruno," alisema Chowo.
Madai dhidi hayo ya Chowo, yametolewa siku chache baada ya mwanafunzi huyo kushiriki kikamilifu katika ujumbe wa viongozi awa Tahliso kumwandikia
Hatua hiyo ilikwenda sambamba na ujumbe huo kutoa tamko wakisema kuwa Siku moja baada ya Tahliso kutoa tamko hilo, Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) ilipinga tamko hilo ikafuatiwa na SUASO ya Chuo Kikuu cha Sokoine na Daruso Mkwawa, ambapo Waziri Mkuu wa Mkwawa Safari Lawrence alisema wamefedheheshwa na kauli ya viongozi hao wa Tahliso.
hata kama uhuni huo umegundulika lakini hakuna kitakachotokea! hakuna atakayekumbuka chochote kwan hili swal ni zito na linahusu maswahi, linagusa sehemu nyeti kabisa ya uozo wa vyombo vyetu, siku zote ni bora liende! bora bajeti ipite! bora maslahi yapatikane! this is terrible!
ReplyDeleteEee bwana Michu Hebu toa Ufafanuzi kuhusu katibu mkuu kiongozi Ni MARTEN LUMBANGA Au PHILEMON LUHANJO?, Maana hapo kwenye riport ya mayala inasema katibu mkuu ni Marten Lumbanga, Tusije sikia baadae kuwa na Rais ni Benjamin Mkapa?
ReplyDeleteHivi Nyerere aliwezaje kusomesha watu bure?
ReplyDeleteMakwaia wa Kuhenga (http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/4/makala1.php)
HIVI rais wa kwanza wa nchi hii, aliwezaje kusomesha vijana bure au kwa karo nafuu sana mpaka elimu ya Chuo Kikuu wakati uchumi wa nchi hii sana sana ulitegemea korosho, tumbaku au pamba?
Tunashindwaje leo hii kusomesha vijana wetu wakati nchi hii inasifika kwa utajiri mkubwa wa madini ya kila aina na mengine hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani ila Tanzania pekee?
Haya ndiyo maswali mimi, nadhani na watu wengi tu wamekuwa wakijiuliza baada ya fukuza-fukuza ya maelfu ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wengine kutoka matawi ya chuo hicho.
Yapo maswali mengine pia ambayo watu wamekuwa wakijiuliza. Toka lini mtoto wa shule akakopeshwa? Unayemkopesha ni nani hasa; mtoto au baba yake? Na unapomkopesha mwanafunzi, atalipa namna gani deni lake wakati ajira yenyewe baada ya masomo si jambo la uhakika?
Pia ipo lugha ambayo imekuwa ikitumiwa na serikali za awamu mbili baada ya Mwalimu Nyerere, lugha ya “kuchangia” gharama ya kusomesha. Serikali hizi zimekuwa zikisema: “Sisi serikali tutatoa asilimia 60 ya gharama ya masomo na nyie wanafunzi asilimia 40.”
Na ndani ya lugha hiyo hiyo, si wanafunzi wote ambao wamekuwa na sifa ya “kuchangiwa” na serikali. Ni wale walioshinda mitihani yao tu kwa madaraja mawili ya kwanza, ndio ambao wamekuwa wakichangiwa na serikali.
Ni katika sura hii ya “kukopesha” au “kuchangia” gharama za elimu, ndiyo sasa tunaona kuzuka kwa rabsha vyuoni; wanafunzi wanagoma kuingia madarasani kwa msingi kwamba wao wenyewe au wazazi wao hawakopesheki kutokana na hali yao ya umasikini uliokithiri.
Kutokana na mabango yao, wanafunzi wanasema serikali inaweza kabisa kulipa gharama hizo kama ingepunguza gharama za uendeshaji wa serikali yenyewe na matumizi ya kimatanuzi ya safari za nje ya nchi, karibuni kila wiki.
Wanasema kwa kuwa nchi sasa ina utajiri mkubwa wa madini, basi ingehakikisha inaambulia chochote cha maana katika uchimbaji wa madini; mali ambayo sasa inakwenda nje ya nchi.
Hali ilivyo, ni mfano mtu mwenye shamba la mihogo, anakuja mgeni kutoka mbali anamwambia atampa jembe zuri zaidi kulimia. Mavuno yakishapatikana, yule mwenye jembe anadai asilimia 97 ya mavuno ya shamba hilo!
Yaani katika mihogo 100, mgeni anachukua 97, mwenye shamba anabaki na mitatu tu! Ndiyo hapo nchi hii ilipofikishwa. Wageni wanachukua asilimia 97 ya madini yetu na sisi asilimia tatu wakati kila kitu ni chetu, kuanzia ardhi mpaka madini yenyewe!
Sasa kapo ka wimbo ambako wanafunzi hao waliofukuzwa na wenzao huwa wakipenda kuimba wanapofanya maandamano au mikutano yao: “Kama si juhudi zako Nyerere, huyo… angeibukia wapi?”
Maana ya wimbo huu ni kwamba, viongozi wa sasa na wa jana wa nchi hii, wote walisomeshwa karibuni bure na serikali ya kwanza ya Mwalimu Nyerere na ndiyo maana wamefika hapo walipofika!
Sasa tutazame kitu gani kimetokea hapa katikati mpaka mambo kuharibika kiasi hiki na kwa nini serikali ya kwanza baada ya uhuru wa nchi hii ilijitahidi kusomesha watu bure mpaka kiwango cha chuo kikuu.
Ukweli ni kwamba serikali ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilikuwa inachukulia jukumu la kukidhi haja za lazima za watu kama vile elimu na tiba kama ni wajibu na jukumu la lazima la serikali.
Ulikuwa wajibu wa serikali kutenga kiwango maradufu cha bajeti kukidhi haja hizi mbili kupitia utozaji kodi na mali inayotokana na rasilimali za nchi ambazo wakati ule zilikuwa chini ya udhibiti wa serikali. Na kwa kuwa serikali za wakati ule zilikuwa zikiundwa na chama kilichoanzishwa chini ya misingi ya kijamaa na usawa wa binadamu, jukumu la kusomesha watu lilikuwa wajibu wa dola kwa niaba ya wananchi.
Hapa tunaona watu wengi mashuhuri na viongozi wa juu wa leo ambao ni watoto wa wakulima na wafanyakazi masikini wakiwa wamepata elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakiwapo viongozi mbalimbali wa sasa wa nchi hii.
Mambo yamekuja kuharibika awamu zilizofuata baada ya Serikali ya Mwalimu Nyerere na ujio wa uchumi wa soko huria na ubinafsishaji, mifumo ambayo ilitumbukizwa nchini kichwa kichwa na Wazungu kupitia mawakala wao wa ukoloni mamboleo, ndiyo Benki ya Dunia (World Bank) na Shirika la Fedha la kimataifa (IMF).
Sasa elimu ilihesabiwa si tena kama huduma muhimu na ya lazima kwa jamii ambayo inapaswa kutolewa bure na serikali ya wananchi. Sasa elimu ilichukuliwa kama bidhaa (commodity) kama vile nyanya sokoni!
Ndipo sasa serikali zetu hizi zikalazimishwa kuanza kutumia lugha ya kilaghai kama “kuchangia gharama”, “mikopo” na maneno mengi mengine ya “danganya toto” kama hayo. Toka lini mtoto wa shule akakopeshwa? Atalipa na nini?
Hao walioshinikiza serikali zetu kubidhaifisha huduma muhimu kama vile tiba na elimu (ndiyo hao wakala wa ukoloni mamboleo na ubeberu, IMF na World Bank) hawakuingilia kati wakati mashirika ya kimataifa ya madini (multinationals) yalipoingia nchini na kuanza kuchimba madini yetu kama vile dhahabu, almasi, tanzanite na kadhalika.
Badala ya kushauri serikali zetu kukamata hisa (shares) katika umiliki wa mali hizi, mashirika haya yalitazama pembeni wakati kampuni hizi ziliposema zinahitaji kulipa mrahaba (royalty) tu mfano wa mwandishi wa kitabu anavyolipwa na mchapishaji wake mauzo ya kitabu chake!
Ndani ya asilimia mia moja ya mauzo ya rasilimali hii ya nchi ya madini, kampuni hizi za kigeni zinachukua asilimia 97 wakati Tanzania inaambulia asilimia tatu tu! Na hakika si asilimia tatu. Ni asilimia moja unusu. Ile nyingine inachukuliwa na wajanja wengine wanaoletwa ati kufanya ukaguzi wa mauzo ya madini hayo!
Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani wataishtua serikali yetu vipi wakati wanaofaidika ndiyo hizo serikali mama ambako ndiko yalipo makao makuu ya taasisi hizo?
Kama hili hilitoshi, kumezuka hulka ya matanuzi katika serikali zetu, kwenda mwendo wa matumizi makubwa kama vile kununua magari ya kifahari yenye bei ya sh milioni 50 mpaka milioni mia moja, na haya magari kupewa mawaziri ambao sasa wanafika 60, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya na kadhalika.
Hata kama tulitumbukizwa kuingia mfumo huu wa uchumi wa gulio, kubana matumizi kunatushindia nini ili vijana wetu wasome bure?
Ni katika sura hii ndiyo sasa tutazame rabsha hii tuliyonayo ya wanafunzi. Ni dhahiri kuwa fukuza fukuza hii haisaidii kwa sababu ni mfano wa kujikomoa sisi wenyewe kwa sababu tutakaoharibikiwa ni sisi ambao ndio watu wa taifa hili, kupoteza kada ya wasomi.
Tukumbuke kwamba migomo ni jambo la kawaida kwa wanafunzi popote pale. Hata wakati wa Mwalimu Nyerere wanafunzi waligoma!
Moja ya sifa ya kustahili kuwa mwanafunzi ni uwezo wa mwanafunzi huyo kufikiri. Huyo mwanafunzi kama haoni hata haya niliyoandika hapa, ni mwanafunzi wa kabila gani huyo?
Nashauri tuwarudishe shule vijana wetu, tena bila masharti. Wakisharejea, tujikague mwendo wetu kwa maana ya rasilimali zetu na matanuzi yetu. Tujiulize, kwa mwendo huu, tutafika?
Makwaia wa Kuhenga ni mwandishi mwandamizi. E-mail; makwaia@bol.co.tz
wabunge hao hao ndo serikali(mawaziri) watajidhibiti vipi? i think the entire system need to be re-designed
ReplyDeleteUjumbe kutoka Zambia. Tafadhali bonyeza hapa:
ReplyDeletehttp://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/6624547.stm
Achana na Wakenya hao! Hawana hata mpya. Kila kitu chao ni kizuri kuliko cha bongo! Kila nchi ukienda ukikutana nao, wanajikweza sana hawa Wakenya! Watuachie bongo yetu. Iko bomba kuliko yao!
ReplyDeleteWengi wao hawawezi kujenga au hata kufikiria kuganya hivyo. Bongo super kwa hayo mambo. Na vingine vingi!
Tanzania, Serikali ndio mtawala wa mihimili yote miwili iliyobaki.Serikali ndio inatawala mahakama na bunge.Mahakama na Bunge ni kama washauri tu wa serikali ambao serikali ina uhuru wa kuamua kuwasikiliza au kutowasikiliza.Ndio maana Uhuru Kenyata analiita Bunge lisilo na nguvu.Mfano Rais akiligomea bunge nini kinafuata kwenye nchi kama Tanzania?
ReplyDeleteNchi zingine bunge laweza piga kura ya kutokuwa na imani naye na likamtoa au likataka iitishwe kura ya maoni ya wananchi ili aondolewe akishindwa majukumu yake.
Hapa bunge ni kucheka cheka tu bungeni na vichekesho kibao ndani ya bunge utafikiri wako kwenye kijiwe cha kahawa wakati wamo mle kujadili hatima ya maisha ya watu.
Tuna upungufu wa wabunge wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kutoa hoja zenye nguvu zinazoweza tikisa hata vyombo vya habari na kuifanya serikali ikae mguu sawa.Bahati mbaya hata vyama vya upinzani wapinzani nao hawana wajenga hoja wenye nguvu hata waliomo ndani ya bunge.
Maswali mengi yanayoulizwa humo bungeni ni ya ajabu ajabu na ya kupoteza muda tu.Mfano mtu anauliza kwa nini barabara fulani au mradi fulani haujatekelezwa au kwisha jimboni kwake. Swali kama hilo angeuliza hata mkuu wa wilaya kule jimboni kwake angempa jibu badala ya kupoteza muda wa bunge kuuliza waziri ajibu bungeni.Hili bunge lina utoto fulani na upotezaji muda sana Sana.
Mtu unatakiwa uwe na roho ya uvumilivu wa paka kuweza kuwa spika wa hili bunge.
Wengi wao hizo hizo pesa ndizo zilizowapeleka huko.
ReplyDeletewataziojije?
Nani anaweza kujinyoshea kidole?
We acha tu hii nchi inaliwa na wenye meno tu!
Kama huna meno ulie tu!
Unajua watanzania wengi ni wapumbavu sana mkiambiwa ukweli mnajifanya sijui hatutaki kusikiliza kisa kimesemwa na Mkenya. Ukweli uko pale pale Bunge letu ni rubber stamp tu ya Serikali halina sauti, halina nguvu na wala halina uchungu wowote na mali za umma zinavyotafunwa na viongozi wengi ambao ni kama majambazi. Badilikeni Watanzania bila ya hivyo nchi itaendelea kuwa masikini hadi siku ya mwisho parapanda itakapolia.
ReplyDeleteNimekubali makosa, naomba mnisamehe. Hata hivyo nimefurahi kujua mtu aliyenifahamu na kunikubali amegundua mimi si lolote kwa sababu ya kuchemsha jina tuu!.Mind yangu ilikuwa Katibu Mkuu Kiongozi maana yake ni Marten Lumbanga- Hivyo Marten Lumbanga wa sasa ni Philemon Luhanjo, kama ilivyo kwa "Kingunge" Ngombale Mwiru, Kingunge Malechela, Kingunge Makamba na vingunge wengine wa chana na serikali. by the way, I'm sorry lakini wee michuzi wee!. haya...
ReplyDeletePascal Mayala,
ReplyDeletePAtrick Nyelesa Nhigula, Tambaza O level and Nia Sudi....habari za masiku juu ya habari na Uandishi...endeleza kazi nzuri.Tuwasiliane...pnhigula@yahoo.com