jk akipiga stori na mwanafunzi

mwanza baada ya kufungua sekondari ya ilemela leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2007

    What a down to earth president!! Mungu ambariki huyu jamaa kwa kweli anastahili kuwa kiongozi wa nchi. Anachokosea (japo anasameheka) ni kuendelea kuteua mambumbumbu na wapiga porojo kwenye nafasi nyeti.
    Mshaurini...kasi mpya imeshapoa kabisa...hakuna mikimikiki tuliyoitarajia...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2007

    Kaka Michu muambiee Adam Lusekelo Mwakang'ata aandike kuhusu TAHLISO bullshitters! Wewe na Lusekelo ni ma hero wetu huku ughaibuni bila nyie jua halizami akyanani vile Yesu na Mariaaaaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2007

    Mtu wa watu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2007

    hivi ndivyo viongozi wetu walivyo,hawana programu endelevu, at least za nyerere bado twaziona, sasa hivi wanakomalia sekondari wakati vyuoni sasa pananuka, vyuo vyetu vinakuwa ni sekondari zilizokomaa, no international recognition! anyway that how we are!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2007

    photo opportunity!... hii picha inatoa hisia mbali mbali,... "...Inajionyesha kimavazi, huyo binti wazazi wake wana hali ngumu kidogo ya maisha, ndio maana shati lake limefubaa, tena halina vifungo, labda amelirithi toka kwa dada yake au ni la mtumbani, ...Inajionyesha huyo binti kashikilia fagio, kwa maana usafi wa shule ni jukumu la wanafunzi wenyewe, lakini kubwa kuliko yote ni ...Inajionyesha viongozi wanavyojua kutumia nguvu ya kamera na waandishi kuonyesha jinsi wanavyojali hali ya mwanafunzi, binti wa mlalahoi!.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2007

    Michu mpe copy ako katoto ni kumbumbu nzuri sana kwake siku zi jazo japo kwa muda ule alikuwa hajui kinachoendelea alifikiri tu ni ka kaka kanamnyemelea ili akakaseme kwa mwalimu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2007

    Kuteua vilaza...Yes!! Ila kwa nafasi nyingine anafanya kweli!! Anatakiwa sasa aonyeshe u-kasi mpya kwa kuwapa nafasi vijana wadogo wasio na historia kubwa ya chama wala nini....u-DC, RC etc wapewe vijana waliomaliza vyuo vikuu!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2007

    Mtu wa watu ...mtu wa watu , maana yake nini ? Watanzania tuwe serious tuangalie maisha katika mtazamo mkubwa..

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2007

    Safi sana tungejua mengi lakini iinaelekea kakamera kabovu ka Michuzi wamekadhibiti kasiwe kanapiga picha za Raisi na kuziweka kwenye haka kablogu kake.

    Kwa Tanzania Kapiga picha Uchwara Kamichuzi kanakuwa kanajinufaisha eti kwa kutumia kakamera kabovu kalikopewa na umma kujijenga kwenye kablogu kake ambacho ni kinyume na ajira yake tofauti na wengine ambao wanatumia magari ya umma kupeleka hawara zao kusuka nywele saluni.

    Lakini kwa maoni yangu kablogu uchwara ka Michuzi kanafanya mambo makubwa kuliko Daily News.
    Kwa sababu mbili kubwa:

    1.Daily news haifiki nje ya mipaka ya Tanzania wakati haka kablogu kanafika.Hivyo ukitoa habari kwenye kablogu kama hii picha nzuri hapo juu watu wengi wanasoma nje kuzidi kagazeti official ka Daily News ambako mwisho wake kimanzichana na kilabu cha Pombe Mfaranyaki Tanzania.Na wengi wanaosoma hilo gazeti wala hawanunui kwa hela zao wengi hununuliwa maofisini na waajiri wao kutokana na utafiti wa wataalamu wa masoko toka kenya uliofanywa nao wakauwakilisha nchini kwao.Ni kati ya magazeti ambayo hayana wanunuzi mitaani.

    2.Gazeti la Daily News limejaa vituko gazeti lenyewe unaambiwa ni la Kiingereza lakini ukienda ndani unakuta kuna matangazo yameandikwa kiswahili ukurasa mzima au zaidi.Anyway nadhani Daily News siyo gazeti la Kiingereza ila ni la Kiswanglish yaani Kiswahili na kiingereza kwa mpigo.Ukiona kiingereza hujui unaandika Kiswahili msomaji mwenywewe atajijua!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2007

    Huyo mtoto hapo ndio kapendeza hivyo jamani,Maana alijua Rais anakuja.Sasa imagine siku za kawaida.

    Mhhhh kazi ipo.Jk punguza kulipa fadhila weka watu waofanya kazi.Unapoteza uaminifu na imani kwa watanzania.Walikuamini sana.Maintain hicho kitu.Hakuna kitu kikubwa kama hicho walichokupa watanzania...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2007

    jk kwa nini una kalamu tatu mifukoni, tena zote za rangu moja. si ungemgei moja huyo mtoto akaandikie insha?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2007

    JK MIe kiatu chako tu!!!
    Kabila nyuma.....

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2007

    Nasema hivi... hivi ndivyo waheshimiwa wanavyoboresha CV zao, lakini ukweli wa mambo hali ya mlalahoi ndio kama ya huyo binti hapo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2007

    Tanzania dini haijawakolea vizuri hivyo ni heri tu kuchagua mtu kufuatana na uwezo tu.

    Dini Tanzania bado ina nguvu kwa watu maskini lakini kwa matajiri na wasomi na wenye vyeo vya juu bado haijakolea.

    Ukiona msomi au tajiri au mtu wa cheo kikubwa Tanzania kashikilia dini sana ujue ana frustration,anatafuta kura kwa watu wa dini,anataka kutapeli anaumwa ukimwi, maradhi sugu,ana kesi,au ana matatizo ya maisha,ofisini katika biashara au ni jambazi, jitu lila rushwa,au lililopata mali kwa dhuluma,ujambazi au umalaya sasa limeamua kutulia na kujifanya jitu la swala baada ya maasi mengi na kuliza watu wengi wasio na hatia au linajifanya jitu la sawla watu walione lizuri walipe mwanya litapeli au liwaibie.

    Kwa Tanzania Dini bado.Pamoja na katiba ya nchi kusema Serikali haina dini lakini watu wake wana dini. siamini.Nadhani ni vizuri kusema serikali ya Tanzania haina dini na watu wake hawana dini ni makafiri wa kutupwa!!

    ReplyDelete
  15. Michuzi mbona hujatoa komenti yangu niliosema Kikwete anajifanya anampenda huyo mtoto sasa ivi lakini mara huyo mtoto atapofika chuo kikuu watamfukuza shule akiwakumbusha ya kwamba ni vyema kama serikali imsaidie kulipa karo ya shule!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2007

    Wewe unayesema, "Daily news haifiki nje ya mipaka ya Tanzania wakati haka kablogu kanafika," ACHA UWONGO! Umbumbumbu (ignorance)wako does not makit it right!

    Fungua website hii: dailynews-tsn.com

    Utapata Daily News na Habarzi Leo online!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 05, 2007

    Nimekubali Daily News linafika hadi nje ya nchi.Thank you for educating me.Hamjitangazi ndio maana wengine hata hatujui kama mko online.

    Mpaka mtu ufanye utafiti ndio ujue! Walahi tafiti zitatuua nchi hii.Utafiti choo cha umma kiko wapi mjini (maana hawana vibao vinavyoelekeza vyoo vya umma viliko viliko),utafiti Daily news ofisi zake ziko wapi na utafiki kama wako online au la! Makubwa haya.

    Anyway,Ila bado soko la ndani Gazeti lenu halina mitaani Tanzania.

    Michuzi uwaombe unaowapiga picha wanunue hilo gazeti lenu pia. Shauri yako iko siku utaenda bila mshahara.Sijui kama Utakula blog ukikosa mshahara mwanga mkubwa wewe!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 07, 2007

    Hapa hakuna cha down-to-earth. labda kama huna akili ya uchambuzi, au ndio umekutana na JK hapa. Anapenda kujionyesha, na kusifiwa. Down-to-earth na mtu wa watu anayelea mikataba ainaya Richmond inayowaibia watuhao hao mabilioni na kuzidisha umaskini wao; asiyejali elimu ya watoto wetu; anayefuja pesa za kodi zao kwa safari nje ya nchi na matumizi ya trilioni moja kwa miezi mitatu (ikumbukwe bajeti ya serikali ni trilioni 3); anayewakumbatia kina Lowassa na Rostam Azizi na klinda uozo wao, hawezi kuwa down-to-earth kwa kupiga picha na mtoto wa maskini.

    Hata ukiwatazama, unaona kwamba JK anamtumia mtoto kujijengea sifa ya kisiasa. Lakini mtoto hakombolewi kutoka ujinga wala umaskini. Wakati mwingine, hata kwa mtoto, picha kama hii ni kejeli na laana. Si ya kujisifia,kama ninavyoona mtu mmoja anadokeza hapa.

    Jk ni mweupe, amesifiwa na kujisifu mno, lakini sasa mambo yamekwamba. Nyie bado mnaimba mtu wa watu? Kwani wengine ni watu wa nani? Tuache ushabiki wa kitoto!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 07, 2007

    Sir Issa..vipi Utaadhi...LUGHA YA PICHA.."RAISI WETU ANAFAA..ANAPENDA "..WANAFUNZI NA ELIMU KWA UJUMLA.."..INAELEKEA ANATOA USHAURI MZURI HAPO...ILI HUYO BINTI AJITAHIDI NA MASOMO KWA BIDII NA MAARIFA AHITIMU .."..CHUO KIKUU.."

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2007

    Nice picture, picture opportunity etc.
    True it's easier to play around with people's emotions, ask the advertisers they will tell you that.
    Not being critical of the president but our society as whole. The poor child represents the actual situation of the education system in Tanzania and Africa in general. While kids in other countries have a better environment to educate themselves, we continue to suffer with the old type of system. Now tell me the kid is carrying a broom used to sweep the school ground etc and forsake that precious time for studying. Oh yes it creates manners and prepares the child for the future is what we say. Prepare the child to sweep the streets it what we are preparing her for. Come on who are we kidding?
    Our education system is not adequate enough; our governments, past and present have failed to address this issue properly! Jk maybe a down to earth person, but he is our leader and let him use this picture as a motivation to develop our crumbling education system.
    For those of us not living in Tanzania, I believe we don't need dual citizenship to help the government in this cause. Simple step such as organizing ourselves and buy books, second hand computers, etc and present them to Tanzanian embassies and consulates near to us. And about worrying that they will end up in the wrong hands, we can always use Mr. Issa Michuzi blog to highlight our contribution, I bet JK goes through it too once in a while! And I believe JK has a website where we can send the details of our contribution and even to the parliament.
    Lets all come up with something to elevate our nation’s poor education system.
    LG

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...