wadau msiboreke na maandishi kibao. ni katika kuendeleza libeneke la shirika letu la posta ambapo wadau wamekiri kupokea vifurushi vyao salama salimini. kwa niaba yenu naomba niwape pongezi posta na pia mama bujiku ambaye yupo kuhakikisha mambo yote yanakwenda mswano. waraka huu ni mmoja wa mingi iliyonifikia na yenye kueleza kwamba mambo si mabaya kama inmavyodhaniwa...
Kaka Michuzi,
Nakushukuru kwani kifurushi changu kimepatikana baada ya kuwasiliana na Mrs Bujiku na alikuwa akinitumia mail kuni update na leo katuma kuwa kimepatikana nashukuru sana kwani nilikuwa mmoja wa walalamikaji. Na hii ni email toka kwa Mrs Bujiku
Habari Bw. Pius,

Nimefuatilia kifurushi chako inaonekana kimeingia TANZANIA tangu tarehe 24/2/2007. Kifurushi kipo na tayari nimeshawasiliana na No 754 283251 amesema atakuja kuchukua jumatatu ataje NO AM 633 aje na kitambulisho cha kadi ya posta ya sanduku hilo au passport au kitambulisho cha mpiga kura Nimegundua kuwa:

1.BOX 33909 linatumika na watu/ makampuni mengi ikiwemo Giraffe Oceanic View Hotel, Mkahe Trading Company, United Pharmacy ya Masaki,n.k
2.Pia linatumiwa na Rahel Nanyaki, Somebody Thobiasi na wengine.
Inawezekana uchelewesho umetokea kwa sababu sanduku linatumika na watu wengi hivyo inakuwa ngumu kama calling note hiyo imepita mikono mingi, kuna uwezekano wa mtu kusahau kufikisha ujumbe kwa mhusika kwa sababu ya kawaida ya ubinadamu. Anachofanya mmiliki wa box hiyo kuruhusu kutumika na makampuni zaidi ya moja si sahihi. kila kampuni linapaswa kuwa na sanduku lake.
Ada ya sanduku la 'small business' ni Tshs 30,000/= pamoja na VAT kwa mwaka.
Tunashukuru kwa kuwa kifurushi hicho kimeonekana na pole sana kwa usumbufu ulioupata.

Tafadhali naomba uendelee kutumia posta katika kutuma barua na vifurushi vyako.

J. Bujiku (Mrs)

Pius Pius Mikongoti
C-13A-6 Ken Damansara Condominium-217
Jalan SS 2/72,
Poste Code: 47400
P J, Kuala Lumpur
Malaysia
Mobile:+60176452510

----------- OR ------------
The United Republic of Tanzania
Ministry of Foreign Affairs and International CooperationsCentre For Foreign Relations (CFR)
Box 2824,
Dar Es Salaam,
Tanzania,
East Africa
Office: Fax/Phone: +255 22 2851007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2007

    yaani kifurushi kilikua dar toka mwezi wa pili. mbona kazi...basi vingi viko tu hap vimekaa. kwani a calling notice inatoka mara ngapi? wakisend mara moja basi? walikua wanasby time mwisho kingepotea kabisa.
    thanks god to the blog umepata mzigo wako

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2007

    MICHUZI BLOG YAKO INA BARAKA SANA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2007

    Inamaana angu mwezi wa pili wamekaa naho sasa hiyo calling notes wanatoa mara moja tuu? Box kutumika na Makampuni mengi si hoja yote si ya mtu mmoja tatizo liko wapi? wao waseme wazembe basi!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2007

    Juhudi za Posta inabidi zitambuliwe na kupongezwa hasa ktk suala hili. Hii ni pamoja na wao (posta) kukubali mapungufu yaliyotokea kwa upande wao. Na huyo mteja nae inabidi akubali mapungufu yake; hasa kwa kuruhusu box (lake?) kutumiwa na kampuni; tena zaidi ya moja kitu ambacho ni kinyume na taratibu, na analikosesha shirika la posta mapato!!! (Maana kila kampuni inayotumia hilo sanduku la posta imekwepa kulipia sh.30,000 kwa mwaka kwa ajili ya huduma ya sanduku!)
    Penye ukweli watu tusikwepe na kujivua uwajibikaji. Posta wana wajibu wao, nasi wateja tuna wajibu wetu. Tutafanikiwa iwapo kila upande utatimiza wajibu wake kikamilifu.
    Hongera sana posta na nawaombeni mwendelee kuwajali na kuwaelemisha wateja. matatizo mengi yaweza kuepukika kwa utaratibu huu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2007

    Michuzi,mi naona watanzania tuache kulalamika lalamika kila siku wakati na sisi tuna matatizo!!! hao posta wameonyesha ustarabu sana,imefika wakati tujifunze kuwa na ma box yetu binafsi tuache kudandia dandia ya watu.hilo suala hata mimi nimeliona mara nyingi ofcn kwetu,unapokea calling notice ya mtu hujawahi kumsikia kumbe ni ndugu ya ndugu na jirani na mfanyakazi mwenzio!!!! hapo unategemea nini!!! unatafuta muhusika mpaka unachoka unaishia kurudisha hiyo kadi posta!!

    Bravo posta!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2007

    SAWASAWA KABISA MIZIGO HAIWAFIKII WAHUSIKA KWA KUWA HAWANA ANUANI KAMILI YA KUWASILISHA WARAKA WA KUMWITA MWENYE KIFURUSHI AFUATE POSTA HUSIKA
    INGEKUWA VIZURI HAO WANAOLALAMA PIA WAONGEZEWE GHARAMA ZA UWEKAJI NA UTUNZAJI WA VIFURUSHI VYAO HAPO POSTA KWANI WANAZUIA NAFASI YA KUJAZA VIFURUSHI AMBAVYO VISINGEKAA HAPO POSTA MUDA MREFU.
    ILA SUALA LA KUTOWAJIBIKA POSTA NA HASA POSTA KUU, HILO LAZIMA LIANGALIWE SANA. BI BUJIKU FANYA UWEZALO KUHAKIKISHA UNASAFISHA HIYO OFISI NA IKIWEZEKA PUNGUZA WATU INGIZA KOMPYUTA ILI UWE NA WATENDAJI WACHACHE NA ULETE UFANISI KAZINI. ahsante, mtumiaji wa posta

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...