hii picha ya watoto wakicheza chandimu na maelezo hapa chini pia vimeingia toka kwa mdau joji alieko huko kameruni...

Kaka Michuzi nakuja tena kuelezea kwa kifupi sana kuhusu jambo hili,pengine nitapata maoni ya wadau wengine katika suala hili.

Kwa upeo wangu mdogo nimegundua kua baadhi yetu sisi watanzania tunafikiri ili tuendelee kisoka basi tunahitaji kua na utajiri au serikali ifanye kila kitu kuhakikisha kua tunafanikiwa,ndiyo serikali kwa upande wake inatakiwa kuhakikisha kua tunafanikiwa lakini pia tusisahau kua mbali na kuwa na resources za kutosha kama fedha na vitu vingine, tunatakiwa pia kuwa na vipaji vya soka miongoni mwa wachezaji wetu; sisemi kuwa hatuna vipaji la hasha.

Sasa turudi kwenye point yangu,nimejaribu kufuatilia hawa wachezaji wa kameruni kwa mfano etoo na wengineo,na nimepata nyepesi kua etoo ni kihiyo…… hawa watu walikotoka kwa kweli inashangaza.

Wameanzia kucheza soka sijui tuiteje,angalia hii picha ya kitongoji kimoja cha douala hapo juu kisha uniambie tupaiteje hapo mahali, je uswahilini, mchangani au wapi ?

Hivi ndivyo hali halisi ilivyo ni vipaji vyao tu ndivyo vilivyowafikisha pale walipo sio kitu kingine,kwahiyo ndugu zangu watanzania wenzangu tunaopenda kuendeleza soka letu,tujitahidi sisi wenyewe tusisubiri serikali au mtu fulani aje atoe pesa yake ili tuendelee kisoka,tukaze buti hivyo hivyo mchangani mwishowe tutakua kama kina etoo fis…….

Merci

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2007

    nimeelewa uliyetoa habari hii lakini watoto wanaocheza cha ndimu kama hao wapo kila kona ya nchi yetu tatizo lipo kwa wazazi na walimu wakiona mtoto anacheza hivyo watamdescourage ili azingatie masomo ambalo naona ni sawa kama mtoto anaonyesha dalili za kutoshikilia masomo kabisa ila lazima tujue kama alivyosema wmenzetu hapa kila lenye mwisho lina mwanzo vipaji lazima viangaliwe tangu utotoni na kuhakikisha vinalelewa kama dhahabu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...