kuna mdau kaniletea ujumbe huu sasa hivi. naomba kuwasilisha....
Ndugu michuzi,
Samahani kama ninakusumbua. Nilikuwa nime tuma waraka huu kwako wiki iliyopita. Nimekuwa nikitembelea blogu yako kama kawaida yangu nikitaraji kuwa utakuwa umenitolea ili umma uweze kujuwa wanyonge wanavyonyanyaswa na wenye mamlaka. Tafadhali blogu hii ni msaada kwa wasio na sauti. Ahsante.
Nakuomba unitolee haya machache ninayoyaandika kwa niaba ya kikundi cha sanaa za maonesho cha MACHOZI THEATRE GROUP Chenye makao yake makuu CHAN'GOMBE- TEMEKE.
Hiki kikundi kinaundwa na vijana ambao hawakubahatika kupata elimu inayostahili kuwawezesha kupata kazi za kuajiliwa katika sekta rasmi. Kwa msaada wa watu mbali mbali ikiwa ni pamoja na mimi tuliwasaidia kuunda kikundi chao ili waweze kuondokana na vishawishi vya mitaani. Walionyesha kuipenda kazi yao ya sanaa za maonesho kiasi kwamba katika kipindi kifupi wamekuwa wanatoa ushindani mkubwa kwa vikundi vyenye uzoefu mkubwa.
Cha kusikitisha ni kwamba mwezi uliopita ( April) Wizara ya utamaduni ilipata ombi kutoka Zambia kuwa wanahitaji vikundi vya ngoma kutoka TZ.
Wao kama kawaida wakawapa jukumu hilo shirikisho la wasanii Tanzania (SHIWATA) ili waweze kuwapata wawakilishi. Shiwata waliandaa mashindano na kualika vikundi mbali mbali katika fani za muziki wa kiasili, muziki wa kisasa, ngoma za kiasili na sarakasi.
Fainali zilifanyika ukumbi wa DDC Kariakoo. Washindi wa kwanza katika muziki wa kiasili walikuwa MACHOZI THEATRE GROUP.
Baada ya matokeo hayo waandaaji waliwaambia kuwa wanahitaji kupata hati za kusafiria ili waweze kwenda Zambia tayari kwa maonesho yatakayo fanyika mwishoni mwa mwezi huu.Bila kuchoka, walitumia muda mwingine tena, zaidi ya ule wa mazoezi ya kujiandaa kwa mashindano, kupata hati za kusafiria.
Cha ajabu ni kwamba mtu aliyetakiwa kuwapa barua ya kuthibitisha kuwa kweli walikuwa wakihitaji pasi alianza kuwazungusha. Hatimaye waliipata tarehe 25/4. Tarehe 27/4 wakazipata pasi. Walipokwenda kwenye kikao tarehe 28/4 wakaambiwa kuwa wamechelewa kupata pasi na hawataenda tena, ingawa wakati huo walikuwa na pasi tayari.
Waliambiwa kuwa badala yao kikundi cha MANDELA DANCE TROUPE cha Mzee Janagala kitakwenda. Kikundi hiki hakikushinda chochote. Kwa ujumla ni kwamba vikundi vyote vilivyoshinda siku ya fainali vimeambiwa haviendi na wamechukuliwa wengine.
Hao wengine waliochukuliwa nao wanahangaika kutafuta pasi hadi hivi ninavyoongea!
Milangoni, hawa waandaaji walikusanya viingilio na kuwaahidi washiriki kuwa wata pata kiasi fulani kwa ajili ya maandalizi ya safari.
Kwa vile wameambiwa hawatakwenda basi hawapati kitu chochote. Wameingia hasara ya pesa na muda wa maandalizi na kutafuta pasi kisha wametupwa nje. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu na pia kwa maoni yangu hapa kuna harufu ya RUSHWA.
Nimeambiwa kuwa viongozi walikuwa wakishinikiza vikundi vilivyoshinda vipunguze idadi ya wasanii ili waende baadhi yao. Huenda wana makubaliano yasiyo kuwa wazi na vikundi vilivyo bandikwa hapa. Hawa watu wanataka kuifanya bendera ya Tanzania kama kitu rahisi namna hii kiasi cha kuwapa watu wasio stahili!!. Wametoa malalamiko yao BASATA lakini kwa kuwa kila kitu kilitokea wizarani basi BASATA haina nguvu sana.
Vijana hawa Michuzi ni wachapa kazi wazuri na sifa zao utakuwa ulisha zisikia. Naomba wadau wengine washirikiane nami katika kuwapa moyo. Wasije wakarudi nyuma waliko toka bali wasonge mbele. Wanyonge kama hawa wanahitaji watu au mtu wa kuwafuta machozi. PCB mko wapi?
Milangoni, hawa waandaaji walikusanya viingilio na kuwaahidi washiriki kuwa wata pata kiasi fulani kwa ajili ya maandalizi ya safari. Kwa vile wameambiwa hawatakwenda basi hawapati kitu chochote. Wameingia hasara ya pesa na muda wa maandalizi na kutafuta pasi kisha wametupwa nje.
Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu na pia kwa maoni yangu hapa kuna harufu ya RUSHWA. Nimeambiwa kuwa viongozi walikuwa wakishinikiza vikundi vilivyoshinda vipunguze idadi ya wasanii ili waende baadhi yao. Huenda wana makubaliano yasiyo kuwa wazi na vikundi vilivyo bandikwa hapa.
Hawa watu wanataka kuifanya bendera ya Tanzania kama kitu rahisi namna hii kiasi cha kuwapa watu wasio stahili!!. Wametoa malalamiko yao BASATA lakini kwa kuwa kila kitu kilitokea wizarani basi BASATA haina nguvu sana.
Vijana hawa Michuzi ni wachapa kazi wazuri na sifa zao utakuwa ulisha zisikia. Naomba wadau wengine washirikiane nami katika kuwapa moyo. Wasije wakarudi nyuma waliko toka bali wasonge mbele. Wanyonge kama hawa wanahitaji watu au mtu wa kuwafuta machozi. PCB mko wapi?Naishia hapa.
CHIFU M.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2007

    Ah hapa Bongo mambo haya yapo sana,once inapotokea chance kama hiyo basi waliopo madarakani always wanafikiria kuwaweka watu wao,, hapo kwa kweli kama swala hili lina ukweli mimi ningewashauri mlipeleke PCB maana hapo lazima kutakuwa na RUSHWA tu sio bure na hapo ndo tutaona kazi ya hao PCB maana some times mi naona kama ni wababaishaji tu, hakuna wanalolifanya kazi kukamata wala rushwa wadogo wadogo hatujaona wakitangaza kukamata wale wala Rushwa wakubwa zaidi zaidi ya kukomalia kesi ya balozi Mahalu aliyekuwa Itally sasa waende hapo waanzie hapo wizarani then wawahoji hao kina jangala waliwezaje kupewa chance ya kwenda huko Zambia while hawakushinda?? Then issue ya pasport kwa hapa bongo kwa kweli si yakuzungushana kama wakati ule,, sasa hivi unalipia passport leo after two days unaenda kuchukua pass yako sasa iweje hawa vijana wazungushwe?? hivi kweli leo watanzania mmefikia mahali pa kuwanyanyasa weusi wenzenu kwa kudai haki yao?? Tunajenga Taifa la namna gani hapa yani hata kwa hao maofisa wa uhamiaji mnatia aibu sana ukienda imigration office hapo ni aibu tupo yani ukiona muhindi anavyoshughulikiwa haraka haraka na onother side mswahili anazungushwa pasipo sababu za maana ah,, inauma sana badilikini watanzania punguzeni tamaa....( IWEJE WATU WENYE ASILI YA KIASIA MUWAHANGAIKIE NA KUWAELEKEZA KA UFASAHA NA MUWAACHE HAWA WEUSI WENZENU??? UHAMIAJI MNABOA SANA) Na mnapenda sana kupokea chochote na cha kusikitisha ni wote mpaka vibinti na vyenyewe vinataka chochote hapo uhamiaji badilikeni ili tuendande na hii kasi mpya ya mheshimiwa Raisi out of that mtakuwa mnadidimiza taifa letu,, na kumbukeni Passport ni haki ya kila Mtanzania...... Peace to you all.... Keep it up brother Issa wa Michuzi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2007

    Unajua hutakiwi kukaa kimya andika mlalamiko yako wapelekee Wizara ya KAzi mheshimiwa Bendera namsifu anajitahidi na atalifatilia mwenyewe kaka anafatilia sana ajira ya vijana, Pili mngewaandikia pia haoi waandaaji na kuwapa gharama zenu za maandalizi kwa jinsi uliyoeleza inasikitisha sana kwa kweli. Huu ni uozo jamani System iko Corupt na Viongozi kadhalika nao wako corupt Kama walijua kuna akina Janala kwa nini waliitisha mashindno?
    Kaka linatatulika ila wape pole sana wasife moyo ndio nchi yetu tena.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2007

    Wakienda PCB watafanikiwa kwani issue yao ni ya kilo moja ya mchele na shingo ya kuku, watajifanya kijisafisha baada ya kuisafisha ile issue ya magunia ya mchele ya ngombe wasiohesabiak ya RICHMOND, Sasa mtikils a amelishikilia ukweli utajulikana maana hata mmiliki wa RICHMOND PCB hawamjui ama wamemficha. Hapa jamani mtawini ndugu zangu wa MACHOZI Kwani mtakuwa ndio kafara yaani sehemu ya kujisafisha na hili genge la kulinda MAgunia na kufichua robo kilos

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2007

    upuuzi kama huo TZ ni kama order of the day na ndio vinavyorudisha nyuma kila kitu...dawa yao ni kuwasema kama hapa uliyeandika hapa kwa michuzi nina uhakika wanasoma na tafadhari taja majina ya hao waandaaji waliowadhulumu hao vijana...safi sana uliyepost hii barua na yule aliyepost ile ya upuuzi wa POSTA safi sana na kuna jamaa insider wa posta kaniambia wakubwa wameipata na kuitana vikao tayari msiwe na wasi ujumbe wanapata ila tuongeze kasi ya kuwaweka hapa na kwenye mitandao mingine na ikiwezekana kuwashauri wafanye nini

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2007

    Kutokana na huu upumbavu ndo maana mimi nikaamua kujilipua mburundi, eti kisa baba yangu hana jina basi siwezi kutendewa au kusikilizwa kokote niendako. Nchi hiyo mimi nimeshachoka nayo kabisa.Na rais wenu wa sasa ndo chanzo mpaka babu Seya kafungwa mambo ni hayo hayo tu,kukomoana. KAMA KUNA MTU ANATAKA KUJIPIGA UINGEREZA SASA HIVI, HILI KUEPUKA HUO UPUMBAVU HAPO TANZANIA. MCHONGO MPYA NI KUJIPIGA kisenge KWASABABU TANZANIA BARA NA VISIWANI UKIJULIKANA WEWE MSENGE UTAENDA JELA NA HIYO IPO KWENYE KATIBA YA NCHI. Tuwaachie hao wenye majina na nchi ya yenye ku over spend billioni 900 kwa mwaka mmoja na INFLATION yao ya asilimia 7, kazi kudanganya watu uchumi unakua.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2007

    kaka michu naomba kuweke hii linki vizuri ili watu waweze kuipata vizuri

    wenzangu m oneni matata anavyojichanganya, inapendeza
    kwelihttp://www.missuniverse.com/backstage/05.06.07-001v.html.

    ReplyDelete
  7. Jamani, mbona habari hizi zinasikitisha. Lakini tumesikia upande moja.

    Hivi hakuna Investigative Reporter Bongo ambaye anaweza kufuatilia habari hizi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 16, 2007

    Jamani, kumbe ni kweli. Nimesikia kuwa hata kikundi cha sanaa za ngoma za kiasili cha JKT Mgulani nao wameachwa katika hali ya kutatanisha ingawa walishinda. Tatizo la watanzania huwa tunaridhika na kusema haya, basi na inaishia hapo. Tunatakiwa kupiga kelele na kudai kilicho chetu. Ikiumbukwe kuwa haki lazima ichukuliwe kwa gharama yoyote ile.
    Kama dada chemi alivyo sema, wako wapi waandishi wa habari waende kutafuta ukweli wa habari hizi kwa manufaa ya wananchi? Uozo umegunduliwa basi uanikeni hadharani ili tufahamu. Kikundi cha machozi kipo, waandaaji wapo, na wengine waliodhurumiwa, wapo. Mnataka nini zaidi kuweza kulifuatilia? Mheshimiwa rais wetu anakemea rushwa mbona hatuoni mabadiliko? ndiyo kusema kuwa kuna baadhi ya watu wanamuona kama anapiga makelele ya bure au ndiyo inamaanisha kuwa anapigana vita ambayo tayari alisha shindwa tena akiwa peke yake na umati wa wapiganaji ambao hawako tayari kupigana?!!!!
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 16, 2007

    Poleni sana,
    Dada Chemi nakupongeza kwa mawazo yako mazuri. Si waandishi tu wanaotakiwa kufuatilia, hata wizara yenyewe ifuatilie ili tuone sura mbili za sarafu.
    Wana blog mnafanya kazi nzuri. Mjaaliwe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 16, 2007

    Hello Mzee michuzi.
    Naomba kuuliza swali. Nafahamu umuhimu wa blog yako kwa wananchi wanao taka na kupenda mabadiliko. Hii ni blog ya kimapinduzi kwani imekuwa ni mdomo wa umma. Acha wanao kataa wakatae, bali huu ndio ukweli. Wewe binafsi na wengine mnao towa kafara muda wenu ili kuuelimisha umma, kwa maoni yangu mnastahili kutambuluwa na kupewa tuzo ya aina fulani kwa mchango wenu.
    Swali lenyewe ni hili, na ningependa ulijibu kwa kutowa ujumbe katika blogu hii. Hivi malalamiko yakitolewa kwa umma wa Watanzania kwa kupitia blogu yako, kwa mfano tatizo la upotevu wa vifurushi na barua posta, je kuna utaratibu wa maksudi wa kuwapelekea wahusika barua iliyo tumwa kwako pamoja na maoni ya wasomaji ili waweze kulifanyia kazi? Kuna malalamiko yanayo jirudia kiasi inaonekana kwamba watu hawa hawasikii kilio kinacho kuja kwa kupitia blogu hii. Ningeshauri kuwa uwe na utaratibu wa kuwajulisha wahusika ili wafahamu kuwa wanacho fanya si kizuri na kama watasemwa sana tunaimani watajirekebisha na utaratibu mzima hautakuwa passive tena.
    Naomba kuwakilisha swali na maoni.
    Ahsante.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 17, 2007

    Sir Issa ...VIPI MZEE WAPE POLE SANA.. MACHOZI.." KAMA SIKOSEI ZAMBIA NI MAJIRANI ZETU, LAKINI HATA HAPO KWENDA TU MWALIKO LAZIMA MTU AJENGE NYUMBA...JE KUJA HUKU...."....HII NI DILI AU DHULUMA..."..Samahani Wizara husika kama nimekosea...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...