
Ustaaazi Sheikh Issa Michuzi,
nakuomba sana utoe hiliduku duku langu la katabia ambako sasa kamajitokezasana hapa Marekani katika jumuia ya kitanzania.
Katabia kenyewe ni haka: siku hizi watu wanapo takakuoana hutuma kadi za michango ya harusi ambazo zinamasharti magumu na kwangu mimi naona zinapotezamwelekeo wote wa kusaidia wana ndoa katika kufanikishasherehe yao.
Jambo lenyewe ni kwamba wana ndoa wanaviwango na masharti kwamba iwapo huta toa kiwango hikicha pesa basi usije na girlfriend wako. Hii tabia nimbaya sana na imepoteza maana yote ya kuwaalika watukatika harusi yako. utakuta kadi ina sema dolla 100 niwewe tu na kama utakuja wewe na girlfriend au rafikiongeza dollah 50 au 100 vinginevyo huigi nae .
Mimi kwa maoni yangu hii ni sawa na kumuuzia mtu mwaliko waharusi wala si hiali ya kusaidia wana ndoa kufanikishashughuli yao ya kuoana.
Maneno mengi sana yamesemwa mara baada ya ndoa kufungwa ambayo ni masimango kwawana ndoa..ooh uona sasa michango ya harusi tuliyotoandyo wametumia kuweka down payment ya morgage na onasasa wana endesha Lexus New Model hizo pesa wamepatawapi ghafla tu baada ya kuoana na mambo menginemengine mengi tu.
Na hii huwezi uka walaumi,kwa sababuwatu waliuziwa michango hawa kutoa kwa upendo wakusidia wenzetu wanao funga ndoa..na kibaya zaidiwanapo kuja kwenye harusi wakakuta maandalizi hayalingani na pesa walizo toa ndiyo hasa matusi mitaani yanazidi.
sikatai kwamba wana ndoa wanataka watu walio toa michango tu ndiyo waje lakini kusema kweliutamu wa kusaidi harusi kwa kuambiwa usije na girlfriend wako kwa sababu umeshindwa kutoa $ 150 siwa kiungwana na furaha yote ya harusi ina poteakabisa.
Watu wengine wana penda sana kuja kuona fulaniana owa au kuolewa lakini hawana uwezo mkubwa au wanapenda kusiadia lakini si kwa kiwango hicho sasa jewasitoe walicho nacho? hii tabia naomba sana wana blogtuishambulie na kuikemea.
Michango ya harusi iwe yahiali na upendo najua watasema hatutaki wazamiajikwenye harusi yetu.!Lakini maana yote ya harusi inapotea kabisa unapo uza mialiko ya harusi hata wazungu hawafanyi hivyo wao wana chukua mikopo benki nakualika watu tu marafiki huleta zawadi kwa upendo wao.
week moja baada ya harusi watu wana waona wana ndoa wanaendesha lexus new model mpya tukachongaumetumia pesa zetu utaanza kununa tena ?ndiyo Sababu umetuuzia michango ya harusi hatukutoa kwa hiari zetu.
michango ya harusi iwe hiari. wana blog Please Comment on this....
Mwakipesile_USA


Kaka Michu umechanganya vitu viwili hapa. Yowe za ndugu yangu mchoyo (kwani kuna ubaya gani kuambiwa kiasi fulani ndicho kinatosha uje na umpendaze, si ndo gharama halisi?) Na hiyo RISITI. the receipt is the best joke I hv read for a while...Mganga anatoa maelezo mgonjwa anaumwa nini...aaah this is funny!!! Kwa kasi hii Afrika itazishinda ulaya na Marekani kwa fani ya TIBA! Traditional Knowledge TK yetu inatisha sema wachawi ndo wana iharibu...
ReplyDeletepole yako !!!! hivi hata usa bado wanaomba michango???? nilijua tz tu heee basi wafuate tbia za wenzetu ndoa mnagaramia wenyewe marafiki na ndugu watakusaidia kulipa kwa kupitia zawadi kwishaaaaaaaaaa
ReplyDeletekwani umelazimishwa kutoa? si usitoe tu huo mchango? Kwanza tabia ya kuchangishana mtoni ni tabia gani? kama mmeamua kuonana si muweke hela zenu wenyewe? mie sielewi kwanini unakuja kulalamika hapa kama umelazimshwa vile. Mie ukiniletea hiyo kadi na nikaona hayo masharti ambayo siyapendi basi kadi inaishia kwenye mfuko wa takataka.
ReplyDeleteMtume, kumbe huko nako kuna michango ya HARUSI:- Huko basi siji, kwani nilikuwa nataka kuikimbia hapa Bongo! Haya watu wa majuu!!
ReplyDeleteI agree 100%. Kama huna hela ya kufanya harusi, do what you can...or nenda kafanyie Vegas! other than that, people shouldn't try to do a BIG Wedding that they can not afford. Also, isiwe just kwasababu watu wana kuchangia, then you as the wedding party you don't have to come up with anything...that's not fair..ndio maana ndugu zetu wa hapa marekani they plan a wedding for a year ili wakusanye pesa ya harusi...Watanzania, tuacheni mambo ya kuchangisha!! michnago kwakweli imezidi, hasa ukiwekewa kiwango...LET'S TRY TO BE REAL...sio mambo ya kusema it's our culture kuchangisha...hayo mambo yamepitwa na wakati...changisha when it is really necessary...kwa kitu kama kilio au ugonjwa.
ReplyDeleteGood point. The fact is this, the whole concept of wedding has been distorted, especially within the Tanzanian community. I have had this question for years in my life and could never find an answer, only to come to the understanding that these are Swahili people, with swahili culture and primitive folklores. First,Why should i contribute money for your own wedding? If i contribute something into your wedding, then i deserve to share your wife. Second, why a contribution tag? Third, when you invite me to your wedding, i'm doing you a favour,i don't lose anything if i don't show up to your wedding. This is one fact that i got from my school research...In the whole world, only Tanzanians have this futile culture of wedding contribution.I wonder when will the mentality of a Swahili man change!
ReplyDelete....................
MY SWAHILI TRANSLATION
Mjadala mzuri. ukweli ni kwamba, hii kitu yote ya kuhusu ndoa na harusu imechafuliwa, sanasana kwenye jamii ya watanzania.Nimekuwa na hili swali muda mwingi bila ya kupata jibu, mbali na kujua kwamba hawa watu ni waswahili, wenye mila za kiswahili na desturi za kiswahili.Kwanza, kwa nini nikuchangie fedha kwenye harusi ambayo ni yako? Pili, hata kama nachanga, kwa nini uweke kiwango? Tatu, kama ukinialika kwenye harusi yako, inabidi unishukuru kwamba nimekuja kufanikisha harusi yako, na sipotezi chochote iwapo sitakuja.Katika uchunguzi wangu niliofanya, ukweli ni kwamba ni Watanzania pekee yao Duniani wenye tabia hii ya kuchangia harusi. Sijui ni lini watu watabadilika!
Habari zenu kwa ujumla,mimi nadhani nyie wenzetu wa USA mnajitakia haya masuala mengine kwa kweli shauri kiutu suala la mchango wa harusi ni hiari na si jambo la kupangiwa kiasi maana ni uwezo wako.Sisi wenzenu wa Europe tunaamini ni kuwa kutoa mchango ni kuongezea msaada wa dharura maana waoanao wanatakiwa wawe wamejiandaa vya kutosha kifedha kabla hajatangaza hiyo ndoa,hivyo hata ikitangazwa watu watatoa mchango ule wanaoweza kujitolea ni si kupangiana viwango vikubwa vya pesa,maana kila mtu aishie ulaya ana majukumu makubwa ya familia hapo alipo na nyumbani kwa wazee pia,sasa kuchangia mtu harusi hakutaweza kuharibu bajeti ya mtu ya maisha tu shauri wanaoana.jaribuni kubana matumizi na kuishi kama watanzania,itawasaidia sana.
ReplyDeletekama hamna uwezo wa kufanya sherehe si basi lazima kushangishana jamani? mtu anajikuna napopata mambo ya ufahari yamepitwa na wakati
ReplyDeleteMimi nilichosema hapa ni kwamba hii tabia si ya kiTanzania ni tabia ambayo sijui niite jina gani labda ni ya ki-shetani. Bwana MICHUZI, mimi ninavyo jua ni kwamba watu wanapo taka kuoana wanakuwa na kiwango fulani cha pesa kama budget yao na wanapo fanya gharama za harusi wakaona kuna upunguzi ndiyo hutoa ombi la michango kutoka kwa marafiki na ndugu ili kufanikisha harusi yao na baada ya kupata kiwango wanacho kitaka ndiyo hutoa mialiko kwa watu wote wanao penda wao kuja kwenye harusi yao bila kujari huyo alitoa kiasi gani cha pesa au aje na nani! Lakini hapa Marekani siyo hivyo tena wewe kama hukutoa kiasi kilicho semwa kwenye kuuziwa kadi huji labda umwache girlfriend wako nje kama pesa haikutosha. Na kibaya zaidi Kuna ma-arusi yamekuwa yana fanyika ni yakishteni kwa lugha yangu na maoni yangu kwa nini nina sema hivyo, ni kwa sababu yana kataza kuja na watoto -jamani matokeo ya harusi huwa ni nini kama si watoto ? watoto si ndiyo baraka za harusi au ni michango ya kuamuriwa ndiyo baraka za harusi? au kwa sababu watoto hawakutoa michango ya harusi? jamani tuna elekea wapi, utamaduni wetu wa kitanzania ukowapi? na upendo wote wa kidungu uko wapi? mbona tumekuwa mashetani..sababu ni nini? Iwapo kweli wana ndoa na kamati zao za harusi zina taka ku-control wazamiaji basi wafanye hivi acheni kuomba kuomba michango ya masharti nendeni benki mkachukue kitu ina itwa signature Loans - hii unapata mpaka dolla 20,000.00 kwa kuwa na credit nzuri tu na kazi ya kudumu na kusaini jina lako baada ya hapo andaeni harusi na kualika watu mnao wataka nyie waje na siku ya harusi kaeni na hayo majina mlangoni kama mnavyo fanya siku hizi, hao walio kuja kwenye harusi wataleta michango yao kama zawadi si tena michango ila zawadi narudia. Basi kitakacho patikana hapo kitasaidia kulipa huo mkopo na maarusi nao watalipia kidogo kidogo .Lakini kama wanataka wana jumuia ya kitanzania wawa fanyie harusi basi acheni hayo matabia ya kishetani na uchoyo mapaka watoto hamtaki waje kwenye harusi sababu hawakutoa michango -vitoto vina kula sana vitaongeza gharama..jamani hii kweli ndiyo maana ya harusi , mbona wazungu hawafanyi hivyo? sisi wote hapa marekani tuna fanya kazi na wazungu ikiwa wanaoa huwa wanatoa mialiko tu na haina masharti yoyote, 'children are blessings' na utaona watoto wapo. Lakini sisi watanzania sijui hii tabia imeanzia wapi. Na ndiyo maana matusi na masimango baada ya harusi ni mengi sana ooh una ona wamenunua nyumba na Lexus mpya matusi matusi -michango yetu hiyo ooo harusi haikufanana na michango yetu pesa ziko wapi.,this is to Much..Please wana blog kemea hii tabia ..Udumu UTanzania wetu Amina.
ReplyDeletekweli hiyo ni kali,kweli hapo nimepata point.Ndio maana mimi kwenye harusi ya ngu nataka niite tu watu waje wale msosi na waende zao sitaki mchango wa mtu yeyote.Hayo mambo mengine ya kuchangisha watu ni kutaka ufahari ambao mtu huna uwezo nao.Je wewe ni edgar mwakipesile au erick mwakipesile?
ReplyDeleteHii tabia ya kuchangishana kwa harusi ni mbaya sana. Huku U.S. wenyeji wenyewe hawachangishani, sasa hawa waTanzania wanaleta uswahili wao huku na juu ya hilo wanatoa condition. Nakubaliana kabisa na huyo jamaa kuwa imefikia mahali kuwa watu wananunua mwaliko. Kuja kwenye harusi SIO LAZIMA. Kwa nini ubaki unachangisha watu kwa harusi yako mwenyewe? Watu inabidi wabadilike. Kama unataka kuoa, jigharamie mwenyewe, kama huna hela, fanya harusi simple. Nenda court house, judge awafungishe ndoa, nendeni zenu Applebees, au Chili's, au TGFriday's mpate chakula chenu wewe na mashahidi wako wawili mambo yamekwisha, kwani taifa zima la U.S. linajua maisha ni magumu na hurusi zana gharama. Ndio maana nawapenda wamerakani, wao wako simple, huwa hawana complications kama za waAfrika. Halafu hao watu wenye kuoana mkiwachangia leo, next week mnawaona wamanunua gari mpya tena gari expensive, au wamenunua nyumba. Kwa maana nyingine wakati wachangaji wanatafuta hela kwa shida, maharusi wanatumia michango hiyo hiyo kufanya shoping spree. NI AIBU, NA TABIA HIYO IKOME KABISA.
ReplyDeleteNakubaliana na huyo mtu kweli michango imezidi.
ReplyDeleteHalafu watu hawana aibu card ndani zimeandikwa IN KEEP WITH TRADITION WE ARE REQUESTING so so ....what tradition???
Leo mchango wa harusi, kesho open house, kesho kutwa house warming mara baby shower. It is so hard. na zote wanategemea two hundres and up.
Kila siku nasema fund raising za nini? Maana ya harusi imeondoka kabisa watu wengine wakioana mkienda kwenye harusi yaani hata hiyo hela hamuoni imeenda wapi. Na kama unafunga harusi fanya ya uwezo wako sio ya makuu na kuchangisha watu na hamna viti vya kukaa ukifika kwenye arusi. Nilifika kwenye harusi majuzi viti vya kugombania ilibidi niondoke.
You can do a simple wedding in the US for $10,000 sasa kama mnataka kuoana kweli hamwezi kuweka hiyo $10000 wawili mkamaliza sherehe yenu ndogo? Na hiyo hela ukienda nayo bongo harusi ni babu kubwa kule kam sio mjini basi kule kijijini mpelekee bibi harusi.
ASANTENI SANA WANA BLOG KWA MAONI YENU NA WASHUKURU SANA KWA KUKEMEA KERO HII NA MIMI KWENYE HARUSI YANGU WATU WATAKUJA KUTOA ZAWADI SI MICHANGO NA HAKUNA MASHARTI
ReplyDeleteUDUMU UTANZANIA WETU ALIO TUACHIA BABA WA TAIFA HIKI NDICHO KITU KILICHO BAKI BAADA YA KUFA KWA UJAMAA.
ASANTENI SANA -NDAGA FIJO. JOUNE MWAKIPESILE-USA
Hii tabia mbovu tumeilea wenyewe wabongo. Ukicheki zaidi ya asilimia 90(90%) ya waliowahi kufanya harusi hapa(au harusi za ndugu zao), wamekula michango ya watu(wengine kwa kulazimishia) ili kufanikisha sherehe zao. Wewe sasa unaombwa uchangie mtu mwingine, macho yanakutoka. Mbona hamkukataa michango ya harusi zenu?... acheni unafiki hapa. Ama kweli mkuki kwa nguruwe...
ReplyDeleteWATU WACHANGIE WANACHOWEZA KULAZIMISHANA NI USHAMBA! MI NTACHANGA DOLA 2 NA NAKUJA NA KIJIJI KIZIMA MTANIFANYA NINI?????PUMBAFFFFFFFFF!
ReplyDeleteKuna watu amabao wanachangisa halafu harusi haufanyiki na watu hawarudishiwi pesa zao!
ReplyDeleteHii michango imekuwa kero sasa. na kuweka na viwago ndio wanazidi kufanya kuwa mradi. Mimi nadhani huwa ni hiari ya mtu na uwezo wa mtu, kama watanzania watu wanamatatizo mengi, wanasema wanataka 50,000 ukitoa pungufu wanasema Hupewi kadi. basi usingechukuwa hata hicho kidogo. maana huna thamani kwa wanandoa mpaka utakapo toa mchango. Sio mambo hayo tubadilikeni. Swali. Asipo fikisha kiwango hupewi kadi. Je akitoa zaidi anakuja na majirani? na Akitoa na asipo kuja je?
ReplyDeletemimi kuna ndugu yangu aliweka harusi yake mwezi wa nne mwishoni bado nilikua hata sijamaliza mitihani shuleni. Mimi ninakoishi na yeye ni mbali sana.
ReplyDeleteCan you believe nilivyomwambia unajua hizo tarehe wala sitaweza kufika alichonijibu ni kuwa wala usijali kuja wewe leta mchango tu. I was shocked. My presence was not that important than the money.
Jamani mimi siwaelewi woooooooooooooooote mlioandika komenti kigeni kipi? mnajifanya kama hamjui kuwa utaratibu wa kuchangishana umeanza tangu zamani na pia kuhusu watoto kukataliwa kwenye harusi HAIJAANZA OVER NIGHT IN US tangia zamani tena Dar es salaam madingi wanaalikwa kwenye harusi na kadi zinasema watoto hawaruhusiwi. unless nyie watoa maoni wooooote DAR TRANSIT?????? kuhusu kuchangishana ughaibuni no comment kwasababu siishi huko!
ReplyDelete