hassan rehani 'supa stirio' bitchuka na shaaban dede (shoto) wakichengua wapenzi wa sikinde ddc kariakoo. hawa jamaa watapaa mwezi julai kwenda ughaibuni. soma zaidi hapo chini
DDC Mlimani Park Orch "Sikinde ngoma" ndani ya Masala Festival mjini Hannover

Katika hali isiyo ya kawaida muziki wa dansi wa Bongo umevamia majukwaa ya kimataifa kama nyuki wenye hasira na usongo!!!
nchini ujerumani kuna maonyesho makubwa ya muziki zaidi ya nchi yeyote barani ulaya.mojawapo ya maonyesho hayo ni Africa Market yanayo fanyika mjini Hamburg na Masala Festival ya mjini Hannover,
Ambapo mwaka huu mziki wa dansi wa Bongo ndio utakuwa chachu ya kuvutia maelfu ya watu.

Bendi mbili maarufu za Bongo zimelamba bingo kwa kuchaguliwa
kutingisha majukwaa bendi hizo ni The Ngoma Africa Band inayoongozwa na mwanamziki nyota Ebrahim Makunja a.k.a Ras Ebby makunja mwenye makao yake nchi ujerumani.
bendi hiyo maarufu barani ulaya inayo piga mziki wa dansi wa kibongo ambayo imedumu kwenye gemu kwa miaka 14 ndiyo itakayo tingisha jukwaa la mjini Hamburg Juni 2, 2007 katika maonyesho ya Africa market yanayotarajiwa kuudhuriwa na maelfu ya watu.

DDC MLIMANI PARK ORCHESTRE ambayo ni moja ya bendi kongwe za Bongo inatarajiwa kutingisha jukwaa la mjini Hannover julai 4, kwenye Masala Festival.
Bendi ya Sikinde iliishawahi kufanya ziara kama hiyo mwaka 1994 na pamoja kuwa haijafanya maonyesho sana barani ulaya lakini bendi hio mziki wake unajulikana kwani wana album tayari katika lebel ya "Africassete"ya America wakongwe hao wa mziki wa dansi wanasubiliwa kwa hamu mjini Hannover.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2007

    michuzi una uhakika huyo kushoto ni mwanamuziki? au chinga tu kapagawishwa akavamia steji maanake sitegemei mwanamuziki kuvaa hivyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2007

    Hassan Rehani Bitchuka ni mmoja wa waimbaji wakongwe nchini.Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Mkoa wa Kigoma ana sauti nyororo na tungo zake hujielekeza zaidi katika kuiasa jamii kuachana na tabia zisizofaa kama vile uvivu, ulevi na usalitikatika ndoa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2007

    Hat mimi najiuliza mara mbilimbili kama kweli huyo kushoto ni mwanamuziki. achilia mbali mavazi, hapo mkononi kabeba kiroba cha konyagi yuko nacho kwenye stage!!!! mi nachanganyikiwa kabisa na hawa wanamuziki wetu. hivi kwani kazi zingine hazina maadili?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2007

    Oya Shaban Dede yuko kushoto,mwenye kofia nyekundu.Huyo mnayemzungumzia nyie ni mshabiki tu jama mwenye uhuru wa kuwa atakavyo kulingana na haiba na uwezo wake.
    Sasa mmemuona Dede?Michuzi alifikiri wengi tunamjua...kumbe sivyo,aahah ahha.Haya,anafanana na mwanamziki?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2007

    Labda ni yule aliyevaa kofia nyekundu. Kwsababu hata miye huyu wa jersey ya yellow kama part crash vile.

    All in all huyo mwimbaji Bichuka na wengine kama hawa wangetakiwa wawekwe kwenye a hall of fame au a walk of fame star some where in bongo. Waimbaji kama hawa tunatakiwa hata tuwaweke kwenye vitabu vya histiria ya muziki bongo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2007

    Ras Ebby Makunja a.k.a bwana kichwa ngumu,kiongozi na mwimbaji wa watoto nunda The Ngoma Africa !wajamaa hawa ngoma africa wakali ngoma zao kubwa mno,kazeni kamaba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...