Home
Unlabelled
sisi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Bro. Michuzi jina la hilo kabila ni "Mwera" kwahiyo wao ni "wamwera". Ni kabila kubwa zaidi ktk mkoa wa Lindi.Lapatikana hasa wilaya za Nachingwea,Ruangwa,Lindi(vijijini),Lindi mjini(kidogo),Liwale(kidogo) na pia Kilwa(kidogo).
ReplyDeleteAsili yao ni kaskazini magharibi kwa Msumbiji na inasemekana waliingia Tanganyika kati ya karne ya 12 na 16 wakimkimbia kiongozi wao aliyekuwa katili sana,Sultan Sadala.Wamwera,Wanyasa,Wamakua,Wayao na Wachewa walikuwa na utamaduni wa kuwa na kiongozi mmoja.
Kuna kabila wilayani Kilwa (kabila kuu huko) laitwa "Matumbi".Hawa waliitwa hivyo na Wamwera.Kwa Kimwera wamatumbi ina maana ya watu wa milimani.Uwanja wa soka Lindi mjini unaitwa Ilulu stadium kuenzi milima ya Ilulu iliyopo Nachingwea ambapo Wamwera waliitumia vizuri sana ktk vita vya Majimaji kuwaporomoshea mawe na mishale askari wa Kijerumani.
Walikimbilia milimani baada ya kuteketeza mali,majumba na mashamba ya wazungu ikiwamo kituo cha misheni Ndanda (1906).Jina Lindi kwa kimwera lina maana ya shimo (la choo).Kama ukienda kutokea Dar au Mtwara au Masasi utaona dhahiri unaingia ktk very low altitude above sea level.Ndio maana Lindi kuna joto sana zaidi ya Tanga,Dar na Mtwara.
Baadhi ya watu (mashuhuri) kutoka kabila hilo ni pamoja na Edgar Maokola Majogo, Phillip Magani (1st former CRDB Managing Director,Ruangwa MP and currently the chairman of Roads Fund Board) and Mathias Chikawe.
Samahani kwa kuwaboa ila nimeona kuna habari inahusisha wamwera then nikaona niunganishe na hii.Kama likitajwa kabila jingine nitachangia as well.
Historian man!
Ah,ndugu hapo juu asante sana ,maana nimeshawaeleza watu kibao kama mimi ni mmwera,na wala si mmwela.maana watu wengi waingia hapa watajua sasa.
ReplyDeleteSio siri umenikumbusha kumui(nyumbani),bwana wewe.
Ila kwa kweli Ukimtaja Majogo roho yaniuma ,umeona Nachingwea lakini,hajatusaidia kwa lolote na uchu wake wa madaraka, na huo tu ndio umaarufu wake.Na Hilo wengi wanachingwea Original twalifahamu.Zaidi ya miaka ishirini bungeni hatuna lolote kwetu.Lol wamwera tubadilike Huyu Chikawe naye akituwekea usiku tumpe nafasi mtu mwingine.Tusiogope vitisho vyao.Wilaya ni yetu wote.
Tafadhali michuzi nitolee hii comment ,maana unaniminyia sana !!!!
Historian Man,
ReplyDeleteAsante kwa historia hii.Ni muhimu sana kukumbushana historia zetu katika maandishi ambayo sote tunaweza kuyaelewa kirahisi.
Mwanahistoria wala hujakosea kwani BLOG hii inasaidia mambo mengi licha ya kushushuana pia inafundisha na kutoa macho tusiojua asili ya makabila mengine.
ReplyDeleteHapo pia utakua umemkuna MISOUP kwani maeneo ya huko ndiyo kwake. Mkataa kwao mtumwa MISOUP!
Pia kuna habari kwamba Wambulu wana asili ya Kitusi ambao nao asili yao ni Ethiopia. Sina hakika sana na hilo naomba tuchambulie na hilo mwana HISTORIAAAA.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Membe, naye ni miongoni mwa watu wanaotoka Mkoa wa Lindi.
ReplyDeleteNa mimi naomba kuuliza wagweno ni kabila lingine au ni wapare tu lakini wnalugha nyingine? Watu wa pale ugweno ni wapare au wa chagga? Kwa vile wako milima ya upareni lakini hawaongei kipare. Na ukishuka chini ndio unaanza maeneo ya wachagga. Na katika makabila yaliyopo TZ na lugha zilipo TZ sijaiona hiyo lugha.
ReplyDeleteMume wangu wazazi wake wlitoka ugweno kila siku nabishana naye.
Michuzi, acha uongo. Kama hujui tafsiri za kimwera, acha!! Wala husipime. Jogoo kwa kimwera ni "LIPONGo". na kwa taarifa, kila jogoo ni dume. Hivyo hakuna kitu kinachoitwa jogoo dume, kama ulivyodanganya...tumia blog yako kuelimisha badala ya kupotosha!!
ReplyDeleteAhsanteni wadau na Michuzi,
ReplyDeleteNilisahau kumtaja Bernad Membe,foreign minister wetu,naye pia ni mmwera.anatokea Lindi vijijini ktk tarafa iitwayo Rondo pembezoni mwa barabara kuu itokayo Lindi na Mtwara kuelekea Masasi na Tunduru.
Ni eneo la muinuko kiasi na kwahiyo lina hali nzuri ya hewa na sio ajabu waingereza waliamua kuweka mission ya kanisa ya Kiingereza.
Ukisikia majina kama Livigha,Lyuba,Ng'itu,Mnonjela/Nnonjela,Mwambe,Nnunduma/Mnunduma na Makota basi ujue hao wote ni wamwera.Inakisiwa idadi ya wamwera Tanzania ni kama 450,000 (data:wikipedia.com).
Ahsante Jeff.Nakutana na wewe sana ktk "kijiji" cha Liz ila natokea kivyengine.Nitapita kwako one time,usijali.
Mimi ni mpenzi sana wa historia hadi rafiki zangu nyumbani (TZ) wananitania nina mambo ya "kizee".Wanashangaa nikianza kuwaeleza mambo ya kina Mwanamalundi,Chifu Songea Gama hadi habari za kina Salum Abdallah na Mbaraka Mwinshehe wakati Mbaraka kafa mimi nina miezi miwili tu duniani.
Ninapenda kuchangia kuhusu habari za wapare/wagweno (mzee wangu ni mpare) na wambulu (mchumba wangu atokea Babati) ila nahisi sina taarifa nyingi/nzuri sana.Na naelewa kwamba "no authority,no right to speak";I'm joking!
Lakini tumshauri ndugu yetu Michuzi awe anatoa fursa za watu kujadili makabila na asili zetu.Sio kwamba tuwe wakabila,hapana.Lakini naona ni vema tujuane na tujenge mshikamano na mavumiliano kama watanzania bila kutengana au kukujeliana.
Tupo pamoja wandugu!
Historian man!
Asante Historian man,naona unahabari sana kuhusu hawa wamwera,mi ninawafahamu koo nyingine kama Chinguwile,chikawe,Nyagali,Milanzi Mbunda.Mi hawa watani zangu wajadi .Je unaweza kunitajia watani wengine wa wamwera,mi natoka kwa Che Nkapa.
ReplyDeleteannoy hapo juu ,Ka michuzi hajatudanganya ,somo kule home mi ,nimewasikia wanasema yule mtambala so and so .sasa labda angetueleza tu kwamba tambala pia anafahamika kama lipongo ,ngoja nimuulize bibi kuhusu hili kunachingwea ko.jo jo jo jo jo jo .
ReplyDeleteAnon uliyeuliza kama Wagweno na Wapare ni sawa au vipi nenda kwenye link ugoogle kwenye Ethnologue of language of Tanzania, utapata lugha zote za Tanzania. Kipare kimeainishwa kama Asu, kitaalamu hatuna lugha ya kipare bali Ki asu, Pare ni jina la milima iliyoko huko upareni na imetokea watu wanawaita waishio milimani humo Wapare ila Lugha yao ni Kiasu au Chasu. Wagweno na wapare wana lugha tofauti, ila zinakaribiana. Kwa sababu ya kuwa jirani na waAsu na waChaga, Kigweno kimechukua kwa kiasi kikubwa toka katika hizi lugha mbili jirani, with time inaweza ikaja kuwa mixed language kama hali yake ikiendelea hivyo ila kimsingi KiAsu na KiGweno ni tofauti.
ReplyDeletemichuzi una tabia ya kunibania hoja usibane hii ila Waasu wenzangu nao wapate Historia yao.
Nawasilisha